Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Kama UNAMAPENGO, kula pipi UOZE meno.

>> Friday, December 12, 2008

Taaluma yako ya kuondoa bikira labda haihitajiki SASA HIVI ikiwa hakuna kibogoyo mwenye bikira.

Lakini...
....labda muda au BAADAYE italeta bikira.
Swali:

  • Hivi si kuna wenye mapengo?

Lakini.....
...Ukisomea kilimo cha umwagiliaji kwenye mvua za kutosha ,LABDA utatuelewesha mahitaji mpaka wafikiriavyo wahitajio umwagililiaji JANGWANI .

Profesa wa mambo ya malaria pasipo malaria, labda ndio aliyechangia kuwepo KLOROKWINI itibuyo wa kwenye malaria kama TU muarobaini.

Swali:
  • Ushajiuliza kwa nini nchi zilizoendelea zina maprofesa wa masomo ya nchi zinazoendelea?

  • Hivi nchi zilizoendelea au ziitwazo za dunia ya kwanza, haziendelei?

  • Hivi kuna dunia ngapi?

Kula pipi ingawa ukizidisha utaoza MAPENGO kama matumizi yenyewe ya mswaki wa mti hayakidhi mahitaji ya pembejeo.

Pembejeo inaweza KUTOONEKANA muhimu kama MAHITAJI ya pembejeo HAYAONEKANI kama tu mkojo wa bata.

Lakini....
... UMUHIMU wa pembejeo UKO PALEPALE kama itakujakumrahisishia atakayekuja tumia au kumhamasisha MTUMIZI awezaye kuponya UKOMA wa KITUKUU chako ,KAMA SIO hata pamoja na jamiii yako ,HATA KAMA ni baadaye kidogo baada ya WEWE , MIMI na YULE kuaga dunia au kwa lugha ya matusi;' KUFA ' ,na kikwapa kugeuka UDONGO.

Ya LEO yanamadhara kesho hata kama hayaonekani LEO.

Labda ...
....ni kweli mpata MIMBA leo hazai LEO.

DUH!
NAACHA!
TOPIKI IMENISHINDA na imeisha !

Lakini, pembeni kidogo ya katikati ya topiki,...
Swali:
  • Ushawahi kumsikia asimuliaye ya mbinguni bila kufika PARADISO?
  • Unafikiri ni raia wangapi wa TANZANIA ambao si mafisadi, wamewahifika IKULU na wanajua labda vyooo vinanuka ?


BWANA na BIBI ASIFIWE!
IJUMAA na wiKIENdi njEMa!

Tulia na Bembeya JAZZ NATIONAL watukumbushe ya WHISKEY SODA...


AU Chakachas watupe JUNGLE FEVER....


Lakini ngojea tu tupate chakacha ituhamasishe wikiendi kutoka kwa...ZUHURA SWALEH alonge ya SHANI.....halafu wengine tupate dhambi.

6 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Unknown 3:40 pm  

Ngoja nikunukuu kwanza.

Swali:

Ushajiuliza kwa nini nchi zilizoendelea zina maprofesa wa masomo ya nchi zinazoendelea?
Mwisho wa kunukuu.

Unajua siku moja nilikutana na dada mmoja wa kizungu kwenye hafla fulani, alijitambulisha kwamba anatokea marekani na alikuja nchini kukamilisha digree yake ya mambo ya tiba pale muhimbili.
Nilimuuliza kwa nini ameamua kuja kusomea huku kwetu, kitu gani kilichomvutia?
Akajibu kuwa kuna baadhi ya maradhi hayapo nchini kwao, yaani wameshayatokomeza tangu zamani ambayo kwa huku Afrika bado yametamalaki, kwa hiyo ni jambo la kuamua tu mtu uende nchi gani hapa afrika.
kwa hiyo tanzania likawa ndio chaguo lake.

Swali:

Je unadhani kwa mtindo huu maradhi yatatoweka Afrika?
je kama yakitoweka hawa wazungu watasomea wapi?

naomba mchango wako.

Simon Kitururu 5:03 pm  

@Ambiere:Maradhi yanaweza toweka.Si tunadai hakuna ugonjwa wa ndui sikuhizi?

Yakitoweka tutayatengeneza katika maabara. Si tunajifunza ya JUPITER wakati tuko duniani?

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa 5:04 pm  

nimeipenda ya mbinguni. hata anayekwambia habari za uzuri wa paradiso, haonekani kuwa na haraka ya kwenda huko.

Anonymous 6:21 pm  

Tuwekee sauti kwenye you tube

Anonymous 6:21 pm  

Tuwekee sauti kwenye you tube

Simon Kitururu 9:01 am  

@Kamala: Kazi kweli kweli!
@Anony:Mbona kuna sauti!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP