Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Swala la ''JIFUNIKE tusikutamani''!

>> Wednesday, December 03, 2008

UKIJIFUNIKA hatuoni, ndio maana kuna waaminio HATUTA TAMANI.

Lakini....
..KIPOFU haoni na ANATAMANI!

UKIJIFUNIKA , wawezakunifanya nifumbe macho nakuona NANIHII nyekundu kama katika NDOTO za alinacha nisivyoona umevaa NANIHII!

Kunavitu ukiviona ndio havitamanishi.
-Unaweza ukachungulia na kujisikia kutapika kidoooogo!

Kuna vitu NI vizuri wakati unavifikiria tu lakini ukiona , kuonjeshwa au kuonyeshwa vina vimavimavi.

Unachoamini , unaweza MPAKA kudhani ndio UKWELI hata kama UKWELI hauhitaji UAMINI.


Tukumbuke...
...binadamu ni mtu wa ndoto na alinacha.
Kabla hajatengeneza ndege wala kuona AIR KIBAHA, alishawaza kupaa kama ndege kwa kumuonea donge KUNGURU.

Binadamu anaweza kutamani vitu ambavyo wenye busara wanadai vifichwe BILA wenye busara kustukia VINATAMANIWA kuonjwa hata visipoonekana kwa sababu VIMEFICHWA.

Swali:

  • Unafikiri toto la kiume na la kike hawatagundua matumizi ya NYENZO au SEBULE za haja ndogo ,kama hawajaona wala kusimuliwa watoto wananunuliwa HOSPITALI?


Lakini...
...binadamu anakinai!
Akiona kila siku harage anaweza akavutiwa na njegere.
Akipika nyama sana , labda ataanza kuvutiwa NA kula mlenda.

Lakini ...
... labda ni kweli mpishi adaie hali, INAWEZEKANA HALI kwa sababu HALI SAHANI NZIMA ingawa nanihii anaonja mara kwa mara na anauwezo wa kukusimulia KAUTAMU kake.

DUH!
Saikoloji nyuma ya ''JIFUNIKE , tusikutamani'' , imenishinda.
NAACHA!
SIKU NJEMA!


Tulia kidogo na POP IDOL katika.....na Barbie Girl

Au tumpate tu MBILIA BEL atulize wakati tunaendeleza...katika AFRICA FEELING

4 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 4:35 pm  

Simon napenda uandishi wako. yote ni kweli kabisa.kazi nzuri endelea hivyo hivyo

Simon Kitururu 1:10 am  

@Yasinta: Asante sana Dada yangu!

MARKUS MPANGALA 6:23 pm  

wakadhani walalapo fofofo hawapata gono ati kwakuwa fofofo inajto basi wakaona wametupa kisogo wakati tunawachungulia. wakanuna kumbe wakasahau kwamba wenyewe wanajichungulia, wakasahau kwamba kibezi chao ni porojo halafu wanakuja staili ya kumaliza mboga. ugali ukasota na maharage hayakunoga kwakuwa wapikaji waligoma kwenda labda mbuzi mwenyewe hakunona ndiyo maana wakaona fofofo ni mtindo wa kupata GONO.
mkuu imenikaba koo

Simon Kitururu 10:46 am  

@Markus: :-)

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP