Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Kilichonigusa kunako leo: SO U are from TANZANIA !Do U still kill albinos THERE?

>> Saturday, August 27, 2011

Ni swali ambalo,...
..... nilidungwa leo na MDAU wakati nasubiri msosi kwenye KIMGAHAWA cha WASURINAME /wadau watokao Republic of Suriname hapa mjini Amsterdam na MMAREKANI ambaye akumbukacho kutoka TANZANIA sio SERENGETI wala kuna DHAHABU ,...
.... bali ni kuwa TANZANIA wanaua MAALIBINO,...
.... Uganda wanaua WASENGE,...
.... na Mlima KILIMANJARO uko KENYA.

Naendelea KUWAZISHWA kidogo na SWALA HILI!

Swali:
  • Ushawahi kukutana na SWALI ambalo ukajistukia katika kulijibu UNAJIELEZEA SANA  katika kuelezea HALIHALISI  kuliko  kawaida?
Mambo mengine ila ni SHWARI mitaa hii ,...
.....hasa nikiifananisha na MIJI lukuki MINGINE niliyowahi kuitembelea ULAYA..
...hasa katika kutojali rangi za watu  kitu kifanyacho kirahisi unaweza kujisikia uko nyumba ndogo.:-(


SIKU NJEMA!


Hebu ALBINO FULANI aongezee dozi kwa - Barua Kwa Mama



Au tu Albino Fulani arudie  tu na panga-NAFASI




4 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Anonymous 11:30 pm  

Pole sana Mtakatifu,kwa swali,la kushitukiza.La muhimimu hapa nijinsi hawa watu wa nje wanavyo pende kujumuisha watu wote na kila kitu kinacho tokea katika nchi za afrika.mbona wao kuna mambo mengi tu mabaya yana fanywa ndani ya nchi zao hatuwaulizi kiujumla.mfano,hapo hapo ulipo,hao jamaa waholanzi sindiyo makaburu? au huyo mmarekani si niwabaguzi wa rangi, anyway ningengekuwa mimi nimekutana na maswali kama hayo,tungefika mbali.najuwa uli tumia busara kuwajibu. lakini polesana, Kaka S.

Simon Kitururu 7:43 am  

@KAKA S: Umesema yote yani!:-(

isaackin 11:42 am  

aisee mkuu niliulizwa swali hilo hilo pia hapa,yaani nilichukia mpaka basi,maana najaribu kumwelezea huyo mama jinsi tz kulivyo kuzuri,tuna amani,mbuga za wanyama mwisho namalizia risala yangu jamaa ananiuliza"BUT YOUR KILLING ALBINO THERE"
nikabaki nakodoa macho tu maana iliniuzi kwamba watu wachache washafanya nchi nzima tuonekane wauaji wa albino

Simon Kitururu 12:38 pm  

@Mkuu Isaack:Ni kweli kuna watu wameshaamua sie WATANZANIA WOTE ni waua MAALBINO!:-( Na naona kuna wengi hawasemi tu ila wakistukia tu mtu ni MTANZANIA ndicho wafikiriacho!:-(

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP