Umuhimu wa MTU mmoja utegemeavyo angalau MTU wa PILI hata katika yale ya utunzi wa MIMBA!
>> Sunday, August 28, 2011
Na hata katika swala la ``Kwaniniiii?´´katika MTU MMOJA ,....
........mara nyingi JIBU LAKE labda sio lile ``Kwa sababu´´ ila ni lile mbele ya SABABU za mtu zaidi ya MMOJA!!:-(
Na ya MTU mmoja,....
.... hata kiulevi, udokozi wa mboga ,USHIRIKINA au tu hata ULOKOLE ukiyafuatilia,....
..... unaweza kukutana na yazaidi ya ya MTU mmoja yaliyofanya au KUMJENGA huyo mtu MMOJA,....... kuwa MWALIMU mzuri au hata MCHIMBA makaburi vizuri!.
Swali:
- SI unajua labda wadaio wamejifunza kitu peke yao labda kuna BAADHI ya misifa wamejizidishia tu?
- SI unajua labda kuna sababu inahitajika MIJUSI angalau miwili ili MIMBA YA MJUSI itungwe?
Na kwa kuwa hata katika ya MTU MMOJA yake binafsi,....
.....``UNAJUA?´´ jibu lake ZURI labda sio lile ``NAJUA ´´ au ``SIJUI´´ bila kuhusisha ujuzi wayaliyofunzwa na WATU wengine...
......... labda bado ni lile mbele ya AJUAYE na ASIYEJUA hasa mbele ya neno `` NAJUA au SIJUI,...
.... ambalo laweza kutoasiri hata ya MJUZI mzuri wa hata kupika MAGIMBI ,....
.... unatokana na hata ambacho hakikiri,...
....kile alichostukia kwenye uchemshaji wa MAGIMBI wa WACHEMSHAJI wengine ambao kivyake ni KIBAYA.:-(Swali:
- SI umestukia kirahisi unaweza kuchukulia neno kama ``NAJUA´´ kama ndio ujuzi kikweli wa adaiye KUJUA wakati kujua au kutojua ni zaidi ya NENO na labda hata hilo neno ni matokeo ya kujifunza neno hata hilo ``NAJUA´´ kutoka kwa MTU MWINGINE?
Ndio,...
..... labda jihadhari na adaie haraka anajitegemea katika KUTOJUA au KUJUA,...
.... kwa sababu kuna NENO na kuna TENDO lirahisishalo UMAHIRI wa MTU hata katika yakudai tu ujuaji au tu utojua,................kwa kuwa MTU HUYO hapo inawezekana anajiamini UJUAJI ni kitu ndani ya MTU MMOJA na ndio maana kikujitegemea NENO ni rahisi kutamkwa ,...
Swali:
- SI unajua hata siasa ya KUJITEGEMEA ya RAIS NYERERE ilihitaji uwepo wa zaidi ya MTU MMOJA?
Asanteni wote ambao kwa kuwa UWEPO wenu hata hapa kwenye BLOGU hii,....
.... ndio hasa kisa labda hata UJINGA WANGU kuna ambaye mchango wake ni kustukia,..
.... ee bwana hili lijamaa SIMON KITURURU, ....
.... ee bwana hili lijamaa SIMON KITURURU, ....
......JINGA KWELI!:-(
Ndio,....
.....MKUU labda lakini hata ukuu wako ni kwa sababu kuna zaidi ya mtu MMOJA hapa DUNIANI,.....
.... na ni kweli MTU mmoja ni MUHIMU ila labda hilo haliondoi ukweli ya MMOJA labda huhitaji uwezeshwaji na MTU mwingine!:-(
NI WAZO tu hili MHESHIMIWA!:-(
Hebu twende MSUMBIJI ili TOFO TOFO wacheze muziki kidogo,...
....
Au tu TOFO TOFO waendelee kwa kumfundisha MKE wa JAY Z jinsi MSUMBIJI ngoma inavyochezwa,...
Vitali Maembe arudishe usiriasi wakati akidai-AFRIKA ni SHILINGI TANO
Vitali Maembe amalizie kwa kuongele hizi-Hotuba
Kabla REMMY ONGALA hajadinya tena-CAROLLA
4 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Nikweli kaka wa mimi, kila Mtu anahiji Mtu, mwandishi anahitaji msomaji na biashara inahitaji mteja, nimekusoma sana tuu!!!Vipi leo hukwenda kanisani?J'2 iwe njema kwako.
Katika kila kitu lazima kuwe na mwanzilishi.kwanaza kabisa naomba nikupe tano,kwa kunifumbua mcho kuhusu,mangoma uliyo weka hapa(video/cd za muziki) watu wa msumbiji nawavulia kofia, niwa kali kwa dance/ngoma.niliwahi kuwaambia jamaa zangu wa west afrika kuwa kwa afrika msumbiji ni kiboko/wanaongoza kwa ngoma/dance,wakawa wana bisha.na hasa jamaa wa Jamaika, nao walikuwa wanasifia sana west afrika, nafikiri wameona wao na umenisaidia sana kupigilia msumari.aksante,mtakatifu.pia bwana maembe kwa muziki wake,huyu jamaa namuangalia kwa jicho fulani.anaainayake ya muziki,na ujumbe,hivi ndivo anavyo takiwa kuendelea, kama atapata watu makini.Na kma ulivyo sema umuhimu wa mtu mmoja,kama mwanzilishi unategemea sana mtu wapili.huwezi ukawa wewe tu.na ndiyo maana,wazo la mtu mmoja huzaa kitu kamili.ila wasiwasi wangu juu ya kitu kutoka kwenye umoja kinapo anza kuwa cha wawili,nk huchukua sura tofauti na ilivyo kusudiwa awali,hii ndivyo necha, inavyo tueleza.ndiyo mana kama unakumbuka,usemi huu, kidole kimoja hakivunji chawa. kaka S.
@Dada wa MIMI:
Ila ni rahisi sana kujiamini huhitaji wengine kwa kisingizio cha KUJIWEZA eti!:-(
......yani sijaenda KANISANI , ....wala hata nje ya mlango wa chumba cha HOTEL leo bado!:-(
@KAKA S:Wasumbiji mie huniua sana na ngoma zao!
Rafiki yangu kapitiliza na kudai hata maswala ya SINDIMBA na mpaka ngoma kadhaa BONGO hasa za kusini ukitaka kuzifaidi kiumahiri ,... vuka mpaka hata ambao watu ni waongea lugha ileile kwa upande wa Msumbiji. YEYE anadai alienda kwenye sikukuu moja pande za kule katika kijiji kimoja akakoma ubishi na ingawa alikuwa anajua kucheza sindimba akaogopa hata kudai anajua kitu kwa kushuhudia shughuli inavyowekwa na jinsi jamaa walivyo na stamina na shughuli.
Vitali Maembe nahusudu sana kazi zake na nimebahatika kukutana naye MOROGORO na BAGAMOYO pia ila kifupi kwa hiyo hata sijui sana anavyolenga shughuli .Ila kama ulivyosema : ``...ila wasiwasi wangu juu ya kitu kutoka kwenye umoja kinapo anza kuwa cha wawili,nk huchukua sura tofauti na ilivyo kusudiwa awali`....´´ hicho ndio naombea kwake kisitokee na kufunika kabisa staili yake kama akiwezeshwa na watu wengine.
Maana siku hizi ukisikiliza miziki maarufu kuanzia BONGO mpaka kwa akina Lady GAGA utastukia msanii kafunikwa na sayansi ya nini kinauza tu !:-(
Post a Comment