Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Kuna wakati inasemekana KUKU WA NYAMA afugwaye na BINADAMU husahau kuwa ATAKUFA kabla ya siku zake kisa WANADAMU haohao WAMLISHAO!:-(

>> Saturday, August 20, 2011

Na katika usahaulifu,...
.... yasemekana KUNA WAKATI hata BINADAMU wenyewe husahau kuwa WATAKUFA,....
.....na hilo ni moja ya lisababishalo baadhi ya watu KUJILIMBIKIZIA,...
... utafikiri wakifariki wataondoka na vikorombwezo vyao,...
....halafu WACHOOOOYOOOO kama hata magimbi WALIOJILIMBIKIZIA  watayamaliza vile wenyewe!:-(

Na yasemekana PIA ndio sababu hata WATU wengine huringia wenzao hata kwa kuwa wanamakalio makubwa,...
.... kwa kusahau makalio hayo yanaoza tu kaburini kama ya watu wengine yaliyopigika pasi kama kawaida tu.:-(

Swali:
  • Unabisha?
  • Kwani hujastukia kuna MTUZ zimejisahau kuwa moja ya sifa ya UBINADAMU nikutoishi milele hapa DUNIANI?
  • Hivi unauhakika kuna kitu ROHO na kuwa hizo roho za marehemu lukuki tokea enzi za ADAMU na HAWA kuwa zipo tu  hata kule uchochoroni unakonaniliaga zinakudeku tu maringo yako?

Lakini inasemekana  ingekuwa WATU wanauhakika na ya baada ya KUFA kuwa mambo ni SHWARI,...
..... labda  wengi wasingeogopa KUKUMBUKA  kuwa kama wako hai ,...
....KIFO kipo!:-(

Swali:

  • Si inajulikana asilimia kubwa ya WAJILIPUAO kwa kisingizio cha DINI au hata wajinyongao kisa UHAI wao wanauoanisha na KIBANO ZAIDI  kifanyacho wasiogope kujiua ni imani yao kuwa kuna uahueni baada ya kuzededi?

Ndio,...
.... ni WAZO TU HILI MHESHIMIWA!:-(




Hebu KEM aanzishe upya na kutubadili wazo hilo hapo juu  nyoko kwa-I Can't Stop Loving You



Maxwell arudishe- Lifetime



Maxwell adinye - This Woman's Work



Chico DeBarge arudishe - Virgin



Chico DeBarge arudishe pia na - Iggin' Me




Jon B. aulize - Are U Still Down?



Kabla Toni Braxton hajaingilia kwa - Un-Break My Heart





Halafu Brian McKnight amalizie kwa - Back At One




0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP