Salam,
Ubalozi wa Tanzania Hapa London Leo uliwaalika watanzania wote kutoka madhehebu na dini mbalimbali kuja kupata futari ya pamoja walioandaa ikiwa ni ishara njema ya kuonyesha amani,upendo, ukarimu kwa watanzania wote. Vyakula vya aina mbalimbali viliandaliwa na vilipikwa katika hadhi ya kitanzania.
Naibu Balozi Mh Chabaka aliwashuru wadau wote ambao waliweza kuja na kujumuika na kufuturu kwa pamoja. Aidha Mh Balozi aliahidi kushirikiana na watanzania kwa ukaribu zaidi katika hali na mali pia kuwaomba kutoa ushirikiano wao na ubalozi katika kuboresha mawasiliano na utendaji wa kazi ili kusukuma mbele gurudumu la maendeleo. Aliendelea kwa kusema Ubalozi upo kwa ajili yetu hivyo tuutumie ipasavyo.
Kwa niaba ya URBAN PULSE CREATIVE Tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa ubalozi wetu kwa namna walivyojitolea kutengeneza futari na kuwakaribisha wadau kuja kufuturu.
Asanteni Sana,
MUNGU IBARIKI AFRICA, MUNGU IBARIKI TANZANIA
URBAN PULSE CREATIVE
Picha za tukio:
| Afisa Zamarani akiwakaribisha wadau wote |
| Aziza Ongala( Mtoto wa hayati Remmy Ongala) Akila pozi na Frank |
| Carol kutoka ubalozini(kushoto) akila pozi na jestina George. |
| Freddy Macha katikati akiwa na wadau |
| Futari likikwenda sambamba kwa kupiga stori na kufurahia |
| hata watoto walikuwepo |
| Mh Naibu Balozi kilumanga akitoa shukrani kwa wote walioweza kuja kupata futari |
| muda wa kupata futari ndio huu |
| Mzee Kiondo kutoka Ubalozini akisubiria Futari |
| ustaadhi akiangalia mda kama umefika ili wadau wapate kufuturu |
| wadau wakipata Futari. |
| wakati wa dua |
| zamu ya kina mama sasa. |
0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Post a Comment