MOYO labda WASINGIZIWA mengi na WATU ,....
>> Sunday, August 28, 2011
..... kwa kuwa ni UBONGO hasaa ndio kisa,...
..... watu WAMEJIPENDEA /jifia hata yule umuonaye kuwa ni FALA ,mbaya halafu ananuka ananuka kinyesi pia kwa mbaali!:-(Swali:
- SI inajulikana ni UBONGO ambao ndio wenye mchezo MZIMA karibu kivyote hata katika kuelewa na KUJIELEWA kitu ambacho chaweza kuchangia mpaka kwanini unafikiri NGURUWE ni mzuri ila nyama yake HARAMU?
Ndio ,...
.....labda MOYO wasingiziwa tu,...
.... kwa kuwa akupendaye anaweza akawa anakupenda kwa kutumia UBONGO na sio MOYO,...
.... na UBONGO unastukia POCHI , ufala wa afaaye kuchunwa BUZI mpaka yule atakaye saidia wakati MSAADA hata wakuwa ndugu ya Rais NYERERE kisiasa utakavyo hitajika.
Swali:
- Unabisha?
- Kwani hujui kuna wapendwao na wachukiao matege kama NYUMBA, cheo na MAGARI yao hao walengwao kwa kuambiwa ``WANAPENDWA KWA MOYO WOTE ´´ hao ambao ni wenye MATEGE ?
Ndio,...
... inawezekana hata kwa WATANZANIA,...
...... Tanzania hupendwa kwa akili na sio MOYO,...
.... na ikibidi wataiita AFRIKA MASHARIKI kirahisi tu KIAKILI!:-(
Ni wazo tu hili MHESHIMIWA !
JUMAPILI NJEMA!
Hebu Lupe Fiasco aingilie kati kwa- Daydreamin'
BWANA abadili kidogo kwa-Take It Slow
Au tu Safari Sound Band warudie tu kuturudisha KENYA kusiko na matata kwa ndude - Jambo
3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Mtakatifu, mada yako hii/wazolako hili ni changamoto sana. hapa unaongelea,ubongo na moyo. sitaki niingie sana kwenye taaluma yangu,ila nita sema kidogo.ubongo/akili unamifumo yake inayo wezesha mambo yote yafanyike katika mwili wa binaadam.moyo ni katika viungo muhimu katika mwili wa binaadam. sasa akili inachakachua mambo,moyo kwaimani ya hicho kilicho ina haririwa na kuletwa , ama kutendwa na mwanadamu katika kiwango cha hali yajuu hufananiswa na moyo,ambao huonyesha unyenyekevu wa hali ya juu kiimani,ambapo sasa mimi naita roho badala ya moyo.moyo/roho kwa kupitia ubongo/akili nikweli vya weza kusingiziwa,.maranyingi ni akili ya mtu tu ina mtuma kufanya hivyo.ila moyo/roho ina kataa.kama nijuwavyo kulizungumzia swala hili inabidi ujiweke katika halifulani,ambayo uelewa wako kuhusu saikolojia ya mwanadamu,na mazingira yake yanayo mzunguka hufanya kazi kimahusiano,kijamii,nk. Kaka S.
@Kaka S : Yani hapo ulipoongelea ``.....kulizungumzia swala hili inabidi ujiweke katika halifulani,ambayo uelewa wako kuhusu saikolojia ya mwanadamu,....´´ umemalizia kabisa huku nikikubali yote uliyosema!
Ila nahisi mwanasayansi fulani weye! NABUNIA TU!
Mtakatifu ,wala mi si mwnasayansi.Nilishindwa na sayansi,wakati niko sekondari. mimi,ni msanii wa sanaa za manesho. ila kwa sasa nimejisogeza kidogo, nakuwa Therapist.kwa kbobea katika psychotherapy in dance movement,hapa uk. kaka s.
Post a Comment