Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Sitaki kuwa PUA kama shughuli ni kunusa HARUFU mbaya!

>> Wednesday, August 17, 2011

Lakini PUA,...
.... si ndio inusayo manukato yanukayo VIZURI?


Sitaki kuwa MIKONO,...
.... kama ndiyo itumikayo mpaka KUCHAMBIA yadhaniwayo ni MABAYA.

Lakini si mikono,...
.... ndiyo UKIPENDA ishikiliayo mpaka mtoto MZURI ?


Sitaki kuwa UBONGO,...
.... ufanyayo masaa ishirini na NNE kazi mpaka ile yakutojisikia VIZURI.

Lakini si UBONGO,...
..... ndio siri nyuma ya kujisikia utamu au tu hata ya kumbukumbu ya ulivyowahijisikia VIZURI?

Hatanisipoendelea:
  • Si umestukia usichokitaka kuwa au usicho kitaka tu labda kina zuri lake pia ukikideku kiupande wapili?


Ndio,...
.....labda sitaki kuwa ULIMI pia,...
.... lakini labda vitu vingi ni kama ULIMI,...
..... ambao UKITAKA  unaweza kuichukia kwa  uwezo wake wa kulamba machungu ,...
...... ingawa kwa wapenda utamu bado huohuo ulimi  KUSTUKIWA ni MUHIMU kitu kifanyacho ,...
..... kichukiwacho mara kibao na WANADAMU ambao hata hawaufikirii ULIMIWAO  sio ulimi bali ladha ya KILICHOONJWA!

Swali:
  • Ni marangapi huwa unakumbuka una ulimi?
  • Au wewe ni miongoni mwa watumiao ULIMI ila hata siku moja hujatumia hata dakika mbili kuufikiria ULIMI wako?

Ni wazo tu hili MHESHIMIWA na usikonde!:-(

Hebu CHICCO aingilie kati kwa-Thank You My Friends




Chicco aongezee dozi kwa - G-String



 Ringo aingilie kati kwa - Into Yam





Kabla Jaziel Brothers hawajamalizia kwa- Woza





0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP