Kwa kuwa BINGWA wa UMESENJA atakacho ni UMENEJA !
>> Monday, August 15, 2011
Ingawa kila mtu ni MKALI kwenye KITU fulani ,...
... yasemekana wengi wetu kikushughulika ,....
......hatupendi na hatufanyi yale ambayo kiasili siye ni WAKALI,...
....au IMETOKEA kuwa hatuko kwenye FANI ambazo tungekuwa MABINGWA,...
.......... kitu kifanyacho mengi tushuhudiayo hapa DUNIANI yanafanywa na watu ambao KIUKALI ni vuguvugu ,....... na hata uvuguvugu huo kufikiwa ni kutokana tu na JUHUDI KALI la sivyo mambo yangekuwa ZIRO.:-(
Swali:
- SI inasemekana kuna MADAKTARI ambao labda ubingwa wao ungekuwa wa KIJINIASI kama wangekuwa madereva wa DALADALA?
- Na si kuna WALIMU ambao wangekuwa mabingwa zaidi kama wangekuwa MANESI ?
- Na si kuna MASHUSHUSHU labda wao wangefaa zaidi kuwa waandishi wa magazeti ya UDAKU na wala sio USHUSHUSHU wa mambo ya USALAMA wa TAIFA?
Ndio,...
..... inawezekana hatufanyi yale ambayo kirahisi tungekuwa MABINGWA,...
... kitu kiwezeshacho UVUGUVUGU kama ule usemekanao KUJITOKEZA msenge ajilazimishapo uke, FISADI ajilazimishapo UTU au MALAYA ajilazimishapo tu ULOKOLE.:-(
Swali:
- Unabisha?
Ndio,...
.....labda saa nyingine KATIBU ,....
.... ndiye afaaye UENYEKITI hata kama MWENYEKITI anafikiria anafaa UENYEKITI.
NI wazo tu hili MKUU!
Hebu tena Duke Ellington abadili kwa kurudisha JAZZ katika ndude- The Nutcracker Suite
Duke Ellington ,Billy Taylor na Willie the Lion warudie pia ndude hiihiii katika mkao wa JAZZ ile-Perdido
Seu Jorge aturudishe tena Brazil kwa kurudia-E depois
Au tu Seu Jorge atulize tu zaidi kwa - Burguesinha
0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Post a Comment