..... na ndio maana ni moja ya SHUGHULI ihusianishwayo na kazi mpaka afanyazo MUNGU.
Swali:
Si inakumbuka MUNGU huwa hahusianishwi na KUKOSEA?
Hivi kwanini bado kuna wadaio KUMZIMIA Mungu lakini wagumu kumuigilizia MUNGU katika ya KIMUNGU zaidi yale ya KUSAMEHE na kung'ang'ania yale yasemekanayo pia ni ya KIMUNGU ya kutoa ADHABU tu kama Mungu ?
Ndio,....
....pamoja na yote ambayo hufanya kwa mtu KUSAMEHE kuwe kugumu,....
.....BADO yajulikana kusamehe kwa mtu ni bonge la TIBA kwake.:-(
Swali:
Kwani unafikiri ni ALIYESAMEHEWA TU ndiye anufaikaye na kitendo cha KUSAMEHE?
Ndio ,....
....katika kusamehe kuna wafikiriao ni VYEMA kusamehe aliyeomba MSAMAHA TU kwa kuonyesha kastukia alipokosea,....
....ingawa pia kuna WADAIO wenye busara zaidi husamehe hata wasioomba MSAMAHA kwa kuwa labda hata hawajastukia WALIPOKUKOSEA hasa kwa kuwa KIBINADAMU hawastukii kila kitu WAKIGUSACHO kikugusacho ambacho kwako ni MAKOSA,....
.....kwa hiyo,....
....wasamehe tu akina SIMON KITURURU, Babu Seya, Limpenzi lako, NDUGU LAKO, Rais KIWETE ,jamaa tu lililokusonya bila sababu wakati unanunua nyanya na bamia KIGENGENI huku ukimtamani muuza genge kimahaba, .....
......kama tu labda walivyosamehewa akina Mheshimiwa Rais IDI AMIN, Winnie Mandela na Rais Mandela, Mheshimiwa CHENGE na ......,.....,.......,.......
........hata kama BADO hawajisikii kukuomba msamaha,....:-(
...MIYE nawaza tu hapa MHESHIMIWA jamani!:-(
Mimi Simon Kitururu naomba MSAMAHAkwa yote lakini MDAU hasa kama kunamaeneo nimekukwaza KIZEMBE!!:-(
Tubadili wazo kwa kumsikiliza CHUCK BROWN...
Chuck Brown aturudishe enzi hizo kwa-Bustin' Loose
Ask Arubian "Bobby" born, Alfonso Farrell what he wants his music to convey and he replies, " I want my music to make people feel good and to create sweet memories. The energy in my music has no limit; I want people to feel entertained and to hear the love that I have for creating music, translated into my songs."
Bobby's career in music reads like a manual for how to cultivate a perfect marriage of ambition, talent and a splash of Caribbean spice to produce what is a honourable 26 years of making hip shaking music. At 61 years old, his showman ship in music is a far cry away from the young boy who left his home land of Aruba to become a sailor, only to fall upon uncertain conditions on European soils before eventually moving to Germany to pursue a career as a DJ.
Despite the weathering conditions of his former life, his eminent love for music remained present and his growing passion for making people dance is what caught the attention of Katija Wolff, whom at the time, was scouting for performers to front the epic group, Boney M. Having been fully bowed over by his eclectic style and charismatic island charm, in 1974 Bobby was chosen as the single male in the Caribbean collective, Boney M along side fellow group members, Liz Mitchell, Maizie Williams and Marcia Barrette.
By 1979, Boney M had received worldwide recognition with hits such as ‘Daddy Cool', ‘By the Rivers Of Babylon/Brown Girl in the Ring' and ‘Sunny' all of which became instant number one hits across Europe. Boney M played an infinite role in Bobby's music history, moulding him into the class act that he has since then become. Even after the split of the group in 1986, Bobby Farrell's jubilant energy and unyielding love for music has enabled him to spawn a solo career of 15 years, earning himself the title "King of Disco".
Forever reinventing his sound and fuelling his creative engine, it comes as no surprise that Bobby's latest material integrates 70's Disco with multiple different genres, only working with creative like minded individuals on the way to breathe life into his artistic foresight. Always regaining his love for traditional Calypso music, Bobby's fusion of Disco music with Arubian influences also remain as dominant features in his songs, reaffirming his meritable pride in his Caribbean culture.
In 2010, Bobby continues to tour the world, gracing the global stage with his flamboyant style, infectious rhythms and glamorous backing singers, Edna Proctor, Maureen Pengel and Jacqueline Jonkers. "I like to look good on stage and to release all my energy in my shows. I still wear my glitter costumes and my girls always look glamorous along side me"
Currently housed under Swedish Production Company, Roasting house, Bobby's desire to create good music lives on as he readies his untitled new album, due for a late 2010 release.
Read more...
Ilikuwa ASUBUHI isiyotegemewa BAADA YA ya usiku ambayo hayakutegemewa,...
....kidume PASKALI aliamka na KUJINYOSHA huku akitabasamu kwa sana tu bila kujizuia,...
.... kwa kuwa USIKU WA JANA kuna kitu aliingiza kidogo.
Na ilikuwa ASUBUHI nyingine yenye MAMBO MENGINE ingawa kwa ASHURA hayo yalitegemewa,....
....Ashura aliamka kwa haraka na kutupilia BLANKETI kule mbali huku akijamba kidogo kwa sauti kama afanyavyo kila akiwa peke yake kwa UHURU ambao hadharani anajizuia,...
....lakini AKILINI akiirudia mistari ya UJUMBE ambao kuanzia kwa apangacho tu KUVAA hata kabla hajasema kitu atakacho KUSEMA akitoka nje kwenye UMATI anajua nia YA APANGACHO ni HEKIMA na BUSARA hasa katika yale ambayo JAMII kwenye ubongo ingawa ni YA MSAADA watu hawataki kwenye UBONGO kuyaingiza hata angalau KIDOGO.:-(
Swali :
SI labda ni tatizo kwa kuwa BINADAMU hutosheka na KIDOGO kitu kifanyacho waendao shule baada ya MTIHANI kutupa vitabu kwa kuwa kama wamepasi MTIHANI basi yanatosha waliyo ingiza hata kama ni kidogo?
Na labda yote ya AJIVUNAYE kwa kujua ni yale tu ,....
.... ubongoni yaliyoingia tu KIDOGO!:-(
Ni wazo tu MKUU na kutolielewa RUKSA!:-(
Hebu EDDY GRANT atusaidie kurudisha ustaarabu hapa KIJIWENI kwa ndude-Hello AFRICA
EDDY GRANT arudie -War PARTY
Au tu hebu Eddy Grant amalizie tu na -LIVING on the FRONTLINE
Kuna mambo NI KWA MTU MWINGINE TU labda ndio yako wazi,....
...... kuliko idhaniwavyo kuwa NI WAZI kwa kuwa tundu liwazi NI LAZIMA liingizwe MTALIMBO wakati kuna pia WADHANIAO wanajua kwa uhakika KIUHAKIKA kuwa WAO kama tundu li wazi basi hilo tatuzi ni moja tu kuwa hilo tundu LIFUNIKWE!:-(
Swali:
AU?
Na kama ILIVYOWAZI KWA WENGINE ajisaidiaye kwenye CHOO CHA KUKAA na chenye MAJI akimaliza KUJISTAREHESHA kwa kwenda HAJA KUBWA inabidi a-FLUSH mharo tepwetepwe ,...
.... bado kuna waondokao CHOONI na ni WASTAARABU TU kwa mtazamo wa JAMII ambao wakimaliza kunya hung'atuka HUKO maliwatoni bila kuvuta maji kitu ambacho kuna MTU MWINGINE anadhani si kawaida,....
.... kama ishangawavyo na WENGINE kuwa KUNA waondokao NYUMBANI KWA MTU WALIKO ALIKWA na mtu bila KUAGA ,...
.... na kama ishangawapo VILE VILE mpaka kwenye SIASA ilivyo kuwa KUNA wasiotimiziwa ahadi wawezavyo MARA kwa MARA kurudia KUMPIGIA KURA YULEYULE MBUNGE kwa ridhaa yao wenyewe WAMJUAO hana msaada KWAO.:-(
Swali:
Kwani BINADAMU hawakushangazi kwa kupenda kikojoleo wakati hawapendi mkojo?
Ndio,...
.....labda KUNA wote WAONAO tundu,....
...ingawa tumizi la tundu HUTOFAUTIANA kutokana na TAFSIRI tu za watu,....
...ndio maana .kuna BAADHI tu YA WATU HATA KAMA NI WENGI ,....
....ndio wakubalianao tumizi la TUNDU ni lile la goli kuingizwa TU hata kwa TIKITAKA wakati TUNAJUA kunawadhaniao kama GOLIKIPA TU kuwa MATUMIZI MAZURI YA TUNDU LA GOLI ni yale ya TUNDU LA GOLI kulindwa KITU MTALIMBO kisiingie!:-(
Ndio,...
...hili ni WAZO TU hapa MHESHIMIWA!:-(
Hebu tugawiwe MUSTANG SALLY na Wilson Pickett
Au tu hebu tucheki ALBUM version ya hiihii ndude........
[Tahadhari: Nachoandika ni kutokana na tafsiri yangu BINAFSI ya mambo kama Simon Kitururu na mie sio Mwanahistoria wala Aliyesomea DINI ingawa kila siku mambo haya mawili nayaingia kichwakichwa kivyanguvyangu kutokana na VIANZO vyovyote vya TAARIFA nibahatikavyo kuvipata kwa hiyo KUKOSOA mtazamo wangu RUKSA- na bila kusahau MLENGWA hasa wa hii taralila ni Da MIJA!:-( ]
Nafasi ya kiboxi cha maoni kwenye Blogu ya Da MIJA haikunitosha,....
....kuingia kichwakichwa swala HILI lililoanzishwa na Da Mija kutuonyesha PICHA ya ZIZI au MAHALI alipozaliwa YESU kama lionekanavyo siku hizi baada ya Miaka Elfu kadhaa ....
Hebu tupadeku.....
Na chachandu ya kuongelea swala nilijuavyo mimi kama SIMON KITURURU ililetwa na Swali la Da MIJA:
Swali langu ni kwamba kwa nini tunakataa hiyo siyo sehemu alipozaliwa Yesu? ni kwa vile Yesu alizaliwa zamani sana na kumbukumbu ya mahali hapo haiwezi kutunzwa au? na kama hiyo ndio sababu mbona Kaaba kule Mecca inasemekana ilijengwa kwanza na Abrahamu ambaye aliishi miaka mingi tu kabla ya Kristo?
JIBU langu kwa kifupi kwa swali hilo hapo juu kwa wale wapenda NJIA YA MKATO ni :
Si wote wakataao hapo ndipo alipozaliwa Yesu ndio maana kuna watu wanapata ulaji hapo kwa kuwa kuna MTUZ kibao zinaamini ni hapo ndipo palikuwa MATENITE WODI.
Kwa tupingao kuwa swala hilo lina utata wengi wetu ni baada tu ya kufuatilia HISTORIA ya BIBLIA na pia ya eneo lenyewe kitu kifanyacho kama mimi niamini hapo ukweli wa swala hilo misingi yake ni IMANI na sio KWELI kama kweli ya FACTS aka data nyomi ziwezazo kuhakikiwa.:-(
Na kuhusu KAABA bado ni vile vile kama utafuatilia HISTORIA yake utastukia sio watu wote wanaafiki unalo- SUGGEST kuwa kila mtu anaamini hivyo kuwa palijengwa na ABRAHAMU, ingawa asilimia ya wengi wakubalianao na wewe ni WAISLAMU ambapo tutarudi tena katika swala la DINI na imani ambavyo AAMINIYE huo utakuwa ni KWELI TUPU hata kama asiyeamini atakuwa na vigezo vyake. Na kunawatakao kusahihisha kidogo ambao ni WAISLAMU kwa kusema :
Abrahamu na Ishmael kwa KIISLAMU walirudia tu tena KUJENGA katika misingi ya zamani kwa kuwa mtu wa kwanza kuijenga KAABA alikuwa ADAM ,na kuna wengi waaminio HAPA DUNIANI kuwa hapo ndipo kulikuwa na jengo la kwanza DUNIANI.
Hebu tudeku KAABA katika mchoro kabla sijaendeleza kulima N'GWE kitaralila:
KAABA
1 - Black Stone on the south-west corner.
2 - Entry door, on the East wall 2.13 metres above ground level. It is accessed using a set of portable steps.
3 - Rainwater spout made of gold. This was added in the rebuilding of 1627 after rain the previous year caused three of the four walls to collapse.
4 - Gutter, also added in 1627 to protect the foundation from groundwater.
5 - Hatim, a low wall originally part of the Kaaba. Pilgrims do not walk in the area between this wall and the Kaaba. Some believe this area contains the graves of Hagar and Ishmael.
6 - Al-Multazam, the part of the wall between the Black Stone and the entry door.
7 - Post of Abraham. Abraham is said to have stood on this stone during the construction of the upper parts of the Kaaba, raising Ishmael on his shoulders for the uppermost parts.
8 - Corner of the Black Stone (South-East).
9 - Corner of Yemen (South-West). Pilgrims traditionally acknowledge a large vertical stone that forms this corner.
10 - Corner of Syria (North-West).
11 - Corner of Iraq (North-East).
12 - Kiswa, the embroidered covering, replaced annually.
13 - Marble stripe marking the beginning and end of each circumperambulation.
14 - Post of Gabriel
Kabla sijaendelea cheki zaidi BAADHI ya Hoja kama hizi zilizotangulia HAPA kwa DAMIJA :
Anonymous said...
Sista huu uongo usiuvalie njuga na wewe utaonekana mwanamke wa fimbo sio shoka tena! ni uongo mtakatifu waliotudanganya miaka tele na bado wajinga wanaendelea na upuuzi huu mpaka kwa watoto wao??!! jamani hebu tutoke huko, tuwaachie wazungu na fantacy zao, waafrika tuna yetu tulioyadharau, tumebaki kupokea kila kitu... WAKE UP
Blogger nyahbingi worrior. said...
we nani kakwambia?au ndio vitabu vinavosema?kwa habari kama hii naamini vizazi havitokaa kamwe kujuwa ukweli kuhusu 25/dec/...
SIMON KITURURU said...
Binadamu kweli kiboko! Wamegundua Yesu alikuwa ana sura gani ingawa kwa mamia ya miaka inajulikana hakukua hata na mchoro wa sura ya YESU,...
.... na eti siku hizi wanajua mpaka ni zizigani alikozaliwa Yesu ingawa ukisoma BIBLIA utajua ZIZINI alipozaliwa YESU hapawezi kuwa katika hali ambayo kiujengaji ingedumu kiasi hicho ukizingatia kwa mtazamo wa sasa palikuwa ni kakijiji fulani tu!
Anyway,...
X-mas njema!
OOOOOKAY!One two one two Microphone check:
NAANZA kuvamia stage zaidi kidogo KIKIFUPI :
Nianze kwa kusema IMANI ni kitu chaajabu sana na NDIO MAANA ni kwa imani pekee ndio mpaka waaminio Ng'ombe huamini ni kweli Ng'ombe anamchango wake baada ya kifo hata kama wasio na imani hiyo kutoona uhusiano wowote wa Ng'ombe na nguvu za KIUNGU.
Kwa hiyo kabla sijaendelea;...
.....Ningependa kurudia busara za WAUNGWANA wapenda DINI kuwa kama unaamini na unataka kutunza imani yako``Don't let a little KNOWLEDGE wreck your FAITH, kwa kuwa ni FAITH na SIO KNOWLEDGE iaminiwayo KUOKOA MTU hasa kwa kuwa kwa KUJUA unaweza kirahisi kuona katika yote ya imani ni UJINGA na ni FAITH aka IMANI ifanyayo uamini hata KISICHOLETA maana.
And as they say wale waponyaji KIMOSESI KULOLA : ``Imani yako ndio ITAKAYO kuponya hata gono na ukiwa vuguvugu labda mambo yatakuwa madangachee kinoma``.:-(
Niendelee kwa kukumbusha;...
.....Moja ya tatizo la KANISA na WANAHISTORIA,...
....kihistoria ilikuwa ni msuguano wa WANAKANISA kuamini BIBLIA ni kitabu chenye historia sahihi ya ulimwengu na WANAHISTORIA ambao walikuwa wanabunbulua ukweli kuwa Mengi kihistoria yaliyoandikwa kwenye BIBLIA hata ukifuatilia yajulikanayo kuhusu MISRI kutoka kwenye MAPIRAMIDI na maandishi mengine HAYA machi aka HAYAFANANI na ukweli wa FACTS ,......
.....kitu kihakikishiacho wanahistoria kuwa BIBLIA sio kitabu cha HISTORIA kama WAAMINIO BIBLIA wapendavyo kukinukuu kihistoria.
Na nagusia hili kabla SIJACHOKONOA zaidi swala,...
....kwa sababu hili pia HUJITOKEZA kwenye dini nyingine za hapa ULIMWENGUNI za waumini kutaka sana kitabu cha miongozo ya IMANI kiwe ndio jicho la kila kitu KIHISTORIA pia jambo ambalo huleta msuguano hasa ukizingatia KNOWLEDGE and FAITH mara lukuki havishabihiani na mambo mengi katika dini umuhimu wake uko tu KIIMANI na ukiuchokonoa KIHISTORIA matokeo yake moja ya mfano wake ni vita vya WAYAHUDI na WAARABU visivyoisha.:-(
Nanirudi kwenye hoja KWA KURUDIA kuwa;.....
......tukiachana na ya UKRISTO na kwenda mpaka ya UISLAMU mengi misingi yake iko kwenye IMANI na ukifuatilia utastukia kukuta sentensi nyingi zisemazo``INASEMEKANA ´´kwa kuwa ni stori ambazo ni inasemekana na wakati zinapata umaarufu hakuna aliyekuwepo kushuhudia - kwahiyo ndio maana kwenye KAABA katika ile POST of Abraham mara karibu zote sentensi itumikayo ni ``INASEMEKANA hapa ndipo ABRAHAM alisimama wakati KAABA inajengwa sehemu ya juu huku amembeba Ishmael MABEGANI.
Note neno :``INASEMEKANA´´
Nianze kuiingia hoja kutoka ANGLE nyingine:....
.....Ukifuatilia HISTORIA ya mji wa Makkat Al Mukarramah aka MECCA na mpaka KAABA lenyewe ,....
......utakutana na mambo kibao ambayo VYANZO tofauti vya habari vitakueleza kitu kingine.
Kwa mfano ;..
Kuna vyanzo vya habari vidaivyo jiwe BLACK STONE liliwekwa na Nabii Mohammad na kuna vidaivyo ni Abraham na Ishamael waliloliweka. Kuna waaminio kati ya Hatim na KAABA ndiko waliko zikwa Haggar na Ishmael ingawa kuna wakataao hilo. Na kuna wadaio Makkah a.k.aBAKKAHa.k.a Makkat Al Mukarramahau tu MECCA ,....
....ulikuwa MJI muhimu katika BIASHARA kama kazi za Ptolemy zidaivyo mji huo wakati unaitwa Macoraba kitu ambacho wanahistoria na ARCHAEOLOGY kwa ujumla inapinga kwa kuwa kipindi kinukuliwacho hakuna hata andishi au vinyangarakata vyovyote viashiriavyo uwepo wa MECCA ingawa FALME kibao za eneo hilo na miji mingine katika eneo iko kwenye recodi za kihistoria .
Kwa hiyo ukimsoma Wensinck katika Encyclopedia of Islam, halafu ukaja kusoma ya IMOTI adaiye kuwa kipindi hicho kulikuwa na Kaaba nyingi ila hii iliyobaki leo ndio pekee iliyokuwa ya JIWE na kusababisha iwe ya kiania yake , ukaenda kwa Patricia Crone katika Makkan Trade and the Rise of Islam,.......mpaka ukaja kwa akina Karen Armstrong katika Islam: A Short History, ukaenda kwenye majibu ya Dr. Amaal Muhammad Al-Roubi kwenye kitabu cha -A Response to Patrica Crone's book,......
....HADITH , na mpaka ukaja kumaliza na KITABU KITAKATIFU cha KORANI ,....
....unaweza kujikuta kama LAINI KIIMANI umeshaitia uvuguvugu IMANI yako kama tu WATUMIAO akili baada ya KANISA kuruhusu waumini kujisomea wenyewe BIBLIA wapaparikavyo na MADHEHEBU mbalimbali kisa kuna kitu tu KUHUSU MUNGU wanadhani wanajua.:-(
Kuna watakaodai lakini kuwa ,....
....uhakika tu ni kwamba KAABA ni ya zamani zaidi ya dini ya KIISLAMU na kabla ya UISLAMU wapagani washaabudu sana hapo na HUBAL akiwa ni moja wa miungu MAARUFU wasemekanao waliwahi kuwepo hapo ingawa pia kuna wadaio kuwa mpaka sanamu la Yesu na Maria vilishawahi kuwepo hapo kama MASANAMU tu mengine ambayo inadaiwa kunakipindi yalifikia 360 hapo yote yakiabudiwa.
NIKIRUDI kwenye SWALI lako Damija :
Naongea yote haya na LABDA HATA KUTOKA NJE YA ULICHOULIZA yote ikiwa ni kujaribu tu kusema kuwa ;...
.....sio KWELI watu wote wanakubaliana na MECCA na KAABA kama swali lako ninavyoonyesha KUEGEMEA au tu KUSAJESTI.
Na ni rahisi sana kuhakiki hilo kwa kusoma vitabu tofauti tofauti vya historia ya UISLAM au tu hata kwa ku -GOOGLE hili swala kwa kuwa kirahisi TU hata kwa kulisoma pasipo aminika sana kama kwenye WIKIPEDIA na utakuta pamoja na udhaifu wake kama CHANZO CHA HABARI ZA UHAKIKA lakini utastukia kitu kimoja ambacho hakipingiki KIRAHISI kuwa,....
... hata kuhusu KAABA na MECCA kama tu PICHA uliyotuletea ya padaiwapo alizaliwa YESU,... ....ukiutafuta utata kuhusu UKWELI wake utaupata KWA KUWA UTATA UPO,...
...na kwa hiyo labda tuachie IMANI kuongoza katika hili SWALA kwa kuwa ni WENYE imani tu ndio watakuwa na asilimia MIA ya KUAMINI vinenwavyo ni FACT.:-(
NACHOJARIBU KUSEMA pia ni kwamba:
Na kama ilivyo wasio WAISLAMU wengi waaminivyo kuwa kwa kuwa WAISLAMU katika kuswali huelekea KAABA basi hawatofautishi kitendo hicho na cha WAKANISA la KIROMA cha kupigia magoti sanamu ya MARIA ambavyo vyote kwao ni MAKOSA hata kama kwa WAISLAMU KAABA haiko mbele yao kama sanamu ya MAMA Maria ilivyo kwa WAKATOLIKI,....
..... kitu KIJITOKEZACHO TU TENA tena ni jinsi WAHUSIKA WATAFSIRIVYO,...
....na tafsiri za watu KIIMANI ni HATARI kitu ambacho ukicheza nacho kuna maeneo unaweza hata KUKOLIMBWA kwa kuongea wazi wazi mitazamo ambayo huweza kugeuza IMANI za watu kuonekana ni ZA Kibulicheka tu.:-(
Na moja ya DINI ambayo WENGI huogopa kujiingiza waziwazi kuongelea mambo yake ni ya KIISLAMU kwa kuwa ni moja ya DINI ambayo waumini wake hawataki mchezo na TAFSIRI za ajabu ajabu ya wakiaminicho kitu kifanyacho hata kati ya WAISLAMU na WAISLAMU ukiwa MSHIA ujihami na WASUNNI na ukiwa MU- AHAMADIYYA ufuataye mafunzo na TAFSIRI za KORANI za Mīrzā Ghulām Aḥmad,...
...wajikuta unakwepa WASUNNI na WASHIA kwa kuwa wote wanaweza kukukolimba,....
.....kitu kichangiacho pia kuzuia kusikia kwa wengi tafsiri tofauti tofauti watu wazitoazo kwenye KORANI kwa kuwa kuna hofu kama tu ilivyokuwa kwenye UKRISTO zamani ambapo kama unajua kitu kama vile DUNIA HAIKO kama MEZA inabidi ULE TU KOBISI kwa kuwa ukitamka PAPA na TIMU yake wange KUKOLIMBA.:-(
Na tukiachana nahilo ;...
....nukuu muhimu kuhusu SWALA ZIMA hili nashauri soma mwenyewe: Korani.
Au jaribu pia kucheki watu kama :
Hafiz Ghulam Sarwar's -Muhammad The Holy Prophet
Wensinck, A. J; Ka`ba- Encyclopaedia of Islam
Diane Morgan 's Essential Islam: A Comprehensive Guide to Belief and Practice
Na kwa kuwa siku hizi GoogleIPO, basi jaribu pia kutafiti mwenyewe VITABU na SITES unazofikiria zina aminika zaidi hasa ukizingatia:
1. Chunguza mwandishi ni nani na hakuna hila za kisiri katika aandikacho.
2.Zingatia kuwa WENGI waandikao wanaweza wakawa wameathiriwa tayari MTAZAMO -nanafikiri unatambua kuwa ni kawaida KITABU alicho andika MSABATO kuhusu kanisa la KIROMA kwa kawaida huwa tofauti na ALICHOANDIKA Padre wa kanisa la Roma kuhusu Kanisa la Roman Katholiki kuhusu swala hilo hilo.
3.Na wategemeao WIKIPEDIA kunukuu wakumbuke katika WIKIPEDIA hujui ni nani kaandika na anania gani katika hili kuwa ni moja ya UDHAIFU wa kuitegemea kama kweli tupu ingwa inaweza kukupa mwanga kidogo hasa kukupa pia majina kadhaa ya VYANZO vya waliotafiti HABARI hii ukawatafuta na kuwanukuuu moja kwa moja katika mkao wa nani unapenda kuamiani asemacho ndicho kiko karibu zaidi na ukweli.
Na narudia :
SWALA HILI ni la KIIMANI zaidi na umuhimu wa UKWELI utategemea zaidiIMANI YA MTU kwa hiyo cheza nalo KIUANGALIFU la sivyo unawezajikuta umekuwa MPAGANI hivihivi!:-(
Kumbuka inasemekana katika IMANI:
.....A little knowledge is a dangerous thing ,...
...DON'T LET A LITTLE knowledge wreck YOUR FAITH kwa kuwa kunauwezekano- YOU are JUSTIFIED by FAITH alone!:-(
Na kama HITIMISHO:...
....DaMIJA kuhusu swali lako BILA kutaka kuchezea sana zaidi IMANI za watu kwa kuongea sana mpaka nikwaze zaidi mtu NALIACHIA hapa:-(
Tubadili swala kwa kwenda BRAZIL kukutana na Carlinhos Brown arudie-Ashansu
.... kwa kujifunza mwenyewe UYAJUAYO hata kama kwako ni USTAARABU na juhudi zako za kuyajua zinahitaji KUPIGIWA MAKOFI,...
.... kwa wakuangaliao kwa pembeni wasiofuata ustaarabu wako wanaweza kukuona weye MWANAHARAMU TU!
Swali:
Si unajua moja ya kwanini WENYE MYWELE za RASTA kama ZANGU Simon KITURURU hawaheshimiki sana na baadhi ya watu DUNIANI kwa kuwa kwa USTAARABU wao hawajawahi kukutana na kuona MWENYE NYWELE ZA RASTA astahilie KUHESHIMIWA hasa kutokana na misingi ya USTAARABU wao kutofautiana kitu kiwezacho kuwafanya wafikiri kuwa ni kweli yeyote MWENYE Rasta labda SIO MCHAFU, hatumii madawa ya KULEVYA au tu SIO MVIVU wa mambo mengine yoyote ya kujenga jamii KISTAARABU kama yafanywao na wenye VIPARA na BONGE la kitambi hata kisicho cha uvivu wa kwenda haja KUBWA?
Ndio,...
...wenye VIPARA na vitambi wana wawakilishi katika wadhaniwao ni WASTAARABU,....
... kama tu watembeao uchi KISTAARABU kwa kuwa jamii inakubali ustaarabu wa KUUZA SURA KI-UMISSI KARIAKOO,...
....na kwa hiyo kionekanacho kama CHUPI kikiitwa ni nguo ya KUOGELEA kwa wastaabu hawatakiona ni chupi hasa kama mayoyanyoya ya sehemu za siri ya KIMWANA yalikatwa kabla hajatembea kwa mwendo wa MARINGO mbele ya MAJAJI akitingisha vitako vidogo VIPENDWAVYO katika ustaarabu wa UMISSI NANIHII,....
...na kwa hilo na MAMBO kama HAYO JAMII ndio hupata ustaarabu na WASTAARABU wa kuwaigilizia KATIKA JAMII.:-(
Swali:
AU?
Kwani huna MAFISADI wakupao hamu ya kuwaigilizia USTAARABU wao wa KIFISADI wakati ndio WAHESHIMIWAO kwenye jamii?
Ndio,....
..... kuna MADHARA ya kukosa wa kumuigilizia,....
... na moja la MADHARA yake yasemekana ni kuweza MPAKA kumgeuza KIJANA ASIYE MSENGE mwenye hamu ya kujua YA UKUBWA wafanyayo WAKUBWA FARAGHANI kugeuka BASHA ili ale JICHO la KALIO LA MWANAMUME MWENZAKE wakati MADEMU wapo na mgao wa embe dodo nzuri tu iliyotuna na ISIYO HARAMU kisa wameigilizia kusikofaa KUIGILIZIWA!
Ndio,...
....PAMOJA na mapungufu yake HILI NI WAZO TU MHESHIMIWA na usikonde!:-(
Hebu UB40 katika kubadili MKAO hapa kijiweni warudie-Tell Me - Is It True ?
Au tu SHAGGY abadili zaidi kitoweo kwa PAMBIO iitwayo- Boombastic
... ndio maana ASILIMIA kubwa ya WATU huogopa bila hata kuchunguza KIOGOPWACHO kina madhara kweli YAWATISHAYO matokeo yake unaweza kukuta kuna WAOGOPAO mende , FISI au tu MBWA kuliko BINADAMU WENZIO wajulikanao kwa kuua WATU hata kuliko MBWA na fisi na kufanya hivyo hata BILA za maana sababu.:-(
Swali:
AU?
Na TIBA ya woga wa MENDE,....
..... labda ni kumkabili MENDE na katika kuchunguza na kuukabili woga kitu kiwezacho kuwa tiba kwakuwa kwa kumkabili MENDE unaye muogopa unaweza kustukia katika kupigana NGUMI kwa mtu na mende kirahisi sio MENDE atashinda!:-(
Na ukichunguza yote yaogopwayo kama GIZA na sio mende,...
....unaweza kugundua karibu WOGA wote hutokana na kutofikiria hasa nini kinaweza kuwa gizani huko chumbani kwako ambako mwenye funguo ni wewe tu mwenyewe na ukastukia kunauwezekano vyote viogopwavyo MTU hana sababu za kuviogopa kihivyo kwa kuwa labda kitishacho NI HIYO TU HOFU kuliko kitu chenyewe KISABABISHACHO HOFU aka WOGA hasa kwa kuwa ukweli uko pale pale UKIKABILIANA nacho kuna uwezo mkubwa tu ni weye utakayeshinda.
Swali:
Hivi leo unakumbuka UNACHOOGOPA ni nini na umekibingilisha kucheki kuwa kina sababu kweli ya kuogopwa au unaogopa tu?
SI nasikia mtu aogope asiogope HATA KUTETWA siku ya siku ikifika hata ufanye nini utajikuta umewekwa kati ukisutwa hata umbeya wa enzi za BIBI na MASHOGA zake enzi hizo wakisukana mabutu?
Na hata ukiogopa si siku ya siku KUFA kuko palepale tu hata kama kwa kumuogopa MENDE umefanikia kumkwepa maishani mwako yote?
Ndio,...
...KWA BAHATI MBAYA,....
.... labda MENGI yastahiliyo TUYAOGOPE ndio HATUYAOGOPI na yale ambayo tulihitaji kutotishika nayo ndio YANATUTISHA,...
... kitu kifanyacho yale yastahiliyo KUKUMBATIWA ndio tunatoka baruti kuyakwepa na YALE YASTAHILIYO kuogopa ndio twayaingia mpaka chumvini kwa kutoogopa na kulamba visivyolambwa kama ICECREAM aka AISHIKIRIMU vile-LOH!:-(
Na nimelikatiza hili WAZO Mheshimiwa nisije KUPITILIZA bure likazidi utamu!:-(
Hebu MZEE Yusuf na Zanzibar Stars waingilie kati kwa -Najiamini
James Brown aseme-I'm BLACK and I'm Proud
Herbie Hancock aturudishe mwaka 1975 katika kitu-Chameleon
Au tumcheki tu Lenny Kravitz asipokuwa mbele ya kipaza sauti akiimba na badala yake awe kwenye Drums katika wimbo huuhuu wa Herbie Hancock ujulikanao kama -Chameleon
...... kuanzia majoho ya MAASKOFU na WACHUNGAJI makanisani,....
..... mpaka mwendo wao katika kutaka kuonekana ni watakatifu zaidi labda NI MAIGIZO tu kwa kuwa MUONEKANO wao hauna uhusiano na neno waumini walilolifuata lile la MUNGU.:-(
Hebu mchungulie PAPA BENNY kabla hajaanza kuongea KITU katika mavazi na UTEMBEAJI wake na uniambie kifanyikacho hapa hakina uhusiano na VIFANYWAVYO na akina Mzee Jangala katika kudaka watazamaji ki-THEATRICAL a.k.a kimaigizo....
Ndio,...
....naamini MENGI yafanywayo na WAHUBIRI katika sehemu za DINI karibu zote nizijuazo,....
....hayana tofauti sana na yafanyikayo kwa WAGANGA wa kienyeji katika kufanya vituko KUCHEZA MAIGIZO ili kukuweka mkao wa KUINGIZWA mkenge ,...
......kwa kuwa vingi ni vituko vya MAIGIZO TU ambavyo kwa mfano MAKANISANI havina uhusiano na NENO la MUNGU na kwa mganga wa KIENYEJI huwa wala havihusiani na tiba utakayo pewa ni kwanini MGANGA anatoa sauti za ajabu na kukuvalia mafuvu ya BUNDI au kibwaya cha ajabu ajabu katika MAIGIZO ya kukufanya uamini afanyacho kina ukweli kwa kuwa kinakufanya ukae KISAIKOLOJIA mkao wakutishika au kujisikia unashuhudia kikweli NGUVU za KILICHO na nguvu zaidi yako.:-(
Swali:
AU?
Unafikiri MAJOHO ya WAHUBIRI neno la MUNGU pamoja na sauti zao walizojifunza kutolea NENO LA MUNGU vina uhusiano na nini hasa MUNGU anataka kusema?
Tukiachana nahilo,....
...... na tukiangalia wafanyayo WANAJESHI kwenye magwaride ya KIJESHI mpaka ya KUPIGA KWATA mpaka VIATU VINACHAKAA SIKU MOJA kama sio mpaka kuruka juu mbele ya JUKWAA LA WAHESHIMIWA,...
.....hasa wakati wa AMANI ,....
....unafikiri sio MAIGIZO tu wafanyayo na YUNIFOMU zao ili WANANCHI waingie mkenge kuwa mpaka TANZANIA inaweza kulidindishia hata jeshi la Africa Kusini kama likileta KIBEZI tu kama cha JESHI la MAREKANI,...
.....kitu ambacho inaweza kuwa ni ALINACHA ukizingatia hata RADAR yenyewe mtumba wajanja walio kula dili kuna uwezekano ni moja ya pambo tu kama mapambo mengine ya uwanja wa MAIGIZO kabla MZEE JANGALA hajaingia kuigiza?
CHeki tisha toto za wanajeshi KOREA KUSINI.....
Tukiachana na hilo.....
..... bado nadhani kuna atakaye kubaliana nami kuwa,....
...... kuna watu wana mwendo wa MITAANI kama ilivyo kuwa kuna nguo wazivaazo tu MITAANI kwa kuwa wanategemea kuangaliwa na watu kama tu walivyo wenye nguo maalumu CHUMBANI na vitendo tofauti kama ni a ni kuangaliwa na mpenzi ,....
.....kitu kigeuzacho wafanyayo mtaani KAMA CHUMBANI katika MWENDO na vitendo kuweza kukwalifai kama MAIGIZO tu .lwa kuwa kihalihalisi CHOONI kusiko na washuhudiao mambo huwa tofauti.:-(
Swali:
Unafikiri umzimiaye kwa mwendo na sauti OFISINI ana mwendo uleule na sauti ileile nyororo katika choo cha ofisi aliko pekee?
Nawaza tu kwa SAUTI Mheshimiwana wala usikonde!:-(
Hebu Tabu LEY arudie- SARAH
Jacob Desvarieux aingilie kati na-Mwen malad aw
Au tu naye Papa Wemba amalizie tu tena kwa kinu-Oldies are goodies
... na KATIKA kiona nyeti labda macho yanasingiziwa kwa kuwa hata yakichungulia HAYAELEWI kile UBONGO unafanya mtu akiona ATAJUA.:-(
Na mwili wa mtu ni UDONGO,...
..... na hata nyama za mwili labda zasingiziwa na kuna mpaka KABURI la MTU laweza kutoa ushahidi wa hilo kwa WASIOJUA.:-(
Na labda HATA matatizo ya LADHA yako kwenye ulimi na sio wote MDOMO,....
.... na labda wala sio TUMBO lenye tatizo na chakula chenye ladha iliyochacha NA mwenye njaa na asiye na chaguo la CHAKULA anaweza hilo KUJUA.:-(
Na mtu akinywa hata sumu LABDA kiuacho sio tumbo ,....
....sumu ilikonyonyewa KUINGIA KWENYE MZUNGUKO WA DAMU kama kizimikacho KUDUNDA ni moyo na ubongo ufanyao aliye hai AKIFA iwe kuwa MAREHEMU aliwahi TU kitu KUJUA.:-(
Swali:
SI kwa wenye macho husahau ni UBONGO uonao na MACHO bila ubongo hakutakuwa na sababu ya kujitahidi kumchungulia aliyevaa sketi fupi na kakaa vibaya kwa kuwa hakuna KILICHOKUNJA SURA huko chini kitakacho tambuliwa kama kuna macho NA UBONGO utambuao konokono katikati ya vyura hakuna ?
Na si kificha nyeti hugeuka tu kwa baadhi kutambulika kama CHUPI kama UBONGO ndivyo hivyo unatambua?
Ndio,...
... kificha NYETI ni UBONGO,....
....na siri nyeti ni UBONGO uwatunziao WANAOJUA.:-(
NI WAZO tu hili MHESHIMIWA!:-(
Siku njema BASI Mkuu!
Hebu Boyz II Men waingilie kati shughuli kwa - Doin' Just Fine
Brian McKnight asawazishe kwa - Back At One
Au tu turudi Kameruni RICHARD BONA abadili tu kwa -Eyando
Kuna uwezekano BINADAMU hana kipimo cha uhakika kithibitishacho kuwa,...
....haiwezekani kwa MTU kupenda vyakula viwili vya aina tofauti tofauti kwa usawa,...
.... kitu kifanyacho WATU waamini kama wewe ni MPENZI wa UTANDU SANA hauwezi kuupenda na UKOKO hivyo hivyo sawasawa kama idaiwavyo kama mtu anapenda sana UGALI hawezi kuupenda wali hivyohivyo kwa kipimo cha UPENDO sawa,....
... kitu kifanyacho watu waamini kuwa kama unampenda sana ASHURA kwa kuwa ana bonge la sura lenye MWANYA kama mfereji wa maji machafu na DIMPOZ kama kama mashimo ya choo cha shule ya msingi ya jirani ihitajiyo msaada wa DANIDA ili choo kimalizike,...
.........
......basi huwezi kumpenda hivyo hivyo KWA MAPENZI SAWASAWA kimwana ASHA ambaye umpendeacho ni TABIA na kiuno chake kama NYIGU mjamzito na MAKALIO YAKE aka SANGARA WAMO kama masufuria makubwa ya kupikia ubwabwa MSIBANI.:-(
Swali:
Kwani unauhakika UPENDO unapimika mpaka uamini aina tofautitofauti za mapenzi yako KUMI kwenye mzani wa MAPENZI sio ngoma DROO?
SI ni kawaida hata kwa MPENDA magari kununua magari ya aina tofautitofauti kwa kuwa MAPENZI hutosha kupenda zaidi ya PICK UP truck?
Ndio,...
....LABDA mapenzi ya MTU yanauwezo wa KUKUMBATIA upendo wa AINA NYINGI kiaina nyingi,...
.... ndio maana MTU MMOJA amepewa uwezo wa kupenda watu wengi wenye TABIA za aina nyingi TOFAUTITOFAUTI ,...
.... na hapa siongelei uwezekano wa kuwa mtu anaweza kumpenda MAMA YAKE sawa tu kiujazo na ampendavyo SHEKHE wake amfundishaye DINI na kumfanya ajisikie kuwa AHERA hata enda ,...
.....hata kama katika hilo KUNA wadhaniao kuna tofauti KIUPENDO.:-(
Swali:
Si nasikia kuna wadaio wanamapenzi tofauti kwa MAMA na kwa BABA waliowazaa kitu ambacho labda kungekuwa na mzani upimao tani za upendo labda ingegundulika hilo si sahihi kwa kuwa Mapenzi kwa MAMA hata kama ni tofauti bado = kwa mapenzi ya mwana kwa BABA?
Na samahani,...
.....labda kwa kuwa UMEPENDWA,....
.....weye unakuza uwezekano tu wa atakaye kuja KUPENDWA mwingine asiwe na LIPUA kama lako aka asifanane na WEYE kwa kuwa ni kweli DUNIA IMEJAA wengi wazuri na ukiacha wale wafananafananao na WEYE KIUZURI MWANANA ,...
... wapo pia wengi tu aka CHUNGU MZIMA wenye sura na tabia tofauti halafu kwa bahati mbaya eti na kwa hilo nao WANAVUTIA na kupendeka tu.:-(
Swali:
Ukifuatilia uliowapenda tokea SHULE ya vidudu hustukiii labda umpendaye siku hizi ndiyo yule mwenye BONGE la pua?
Ndio,...
... UPENDO ni KIBOKO,....
...na ndio maana kuna walitumiao PENZI kama kiboko kuwachapia wenzio na chamoto wanakiona!:-(
Naendelea KUWAZA!:-(
Hebu tumuachie Myahudi Barbra Streisand aimbe kuhusu wasichoamini WAYAHUDI katika-Silent night
....labda haihitaji msaada wakiitwacho KUTUMIA NGUVU!:-(
Na siri ya UDHAIFU ya kweli,.....
.... labda aijuaye ni aonekanaye katika suluhisho akitumia NGUVU.:-(
Na ni kweli,...
...kama MTU anatumia NGUVU kuna kitu katika yeye hata kama ni HOJA TU hakina nguvu.:-(
NGUVU!
Kama kijambo tu mwilini ,...
...nguvu kila MTU anayo:-(
Na UBONGO ukipewa nafasi ya kukokotoa na kutambua mambo AKILINI;...
.... labda mengi ya watu YENYE NGUVU YATASTUKIWA na ya watumiao MISULI kwa kutatua kwa kiitwacho ndio matumizi ya nguvu UKIZINGATIA labda wameamrishwa na KIONGOZI wao ASIYE NA MIJISULI ndo utafahamu kama ni kweli KIITWACHO NGUVU ni wao wanacho KAMA VILE moja ya miongoni mwa WAJIVUNIAYO katika waliyonayo.:-(
NGUVU!
Siri ya nguvu ya MTU yaweza kuwa ni jinsi tu atikisavyo tako,....
.... kama mwendo wa maringo huo UTIKISAO kalio ndio siri ya UDHAIFU wa achunwaye buzi kwa kuwa ndicho kifanyacho awe mnyonge kwa mtikisa tako na YOTE bila ubishi akubali!
Swali:
Si inajulikana ASILIMIA KUBWA ya wenye nguvu sana duniani kwa WENGI hata mpaka JUU YAKO ni WALE ambao hawajawahi kutumia kitafsiriwacho kwa lugha ya kawaida kama ni nguvu zihitajizo angalau msuli JUU YAKO?
Naendelea KUWAZA.....:-(
Hebu tujifunze matumizi ya BIBLIA kwa kumsikiliza Joshua Evans katika -How the Bible Led Me to Islam
Hebu tutishane kidogo kwa-OBAMA Worships SATAN
Au tu ngojea Snoop DOGGnaDr Dre wabadili tu mkao hapa kijiweni na kutuliza mshawasha KIBUSARA ZAIDI kwa ujumbe mzito kwa walengwa kuwa -Let me ride/Still Dre
Hivi unafikiri hakuna uwezekano WATANZANIA kuna kitu hawajakichukia vizuri kama CHUKI zao bado hazifanyi kivitendo yadaiwayo kwa maneno yanachukiwa KUTATULIWA badala ya kuwa ndio kwanza yananeemeka?
Kwani unauhakika ASILIMIA MIA hakuna uzuri wa kuchukia hata MTU kama mapendo yako ndio yangemtia matatizoni ?
Ndio,...
.... labda kila KITU kina UZURI WAKE PIA ikiwemo mpaka CHUKI.:-(
Ndio,...
.....labda hata SHETANI ana UZURI WAKE kama ndiye akufanyaye ujipendekeze kwa MUNGU ili usiingie mkenge na kuvaa ihubiriwayo ya wenye DHAMBI uaminio ni ichukiwayo na MUNGU WAKO hata kama huamini MUNGU WAKO ana CHUKI!:-(
SAMAHANI naendelea KUWAZA......:-(
Hebu SHA SHA JONES arudie-Blow my MIND
Au tu BAHA MEN waingilie kati shughuli kwa -WHO let the dogs out?