Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Kwa kuwa KUMBUKUMBU ni fupi!:-(

>> Wednesday, December 22, 2010

WAKATI tunakaribia mwisho wa mwaka,....
.... ukifuatilia yaliyotokea MWAKA mzima,....
.... waweza kukuta kuna waliosahau yaliyotokea HAITI waliokuwa wameguswa na YALIYO wakumba waliokumbwa na tetemeko la ARDHi Wahaiti,....
....kuna wapendao kutunza MAZINGIRA waliosahau mafuta yaliyomwagwa na BP Marekani,....
... na mpaka kuna waliosahau jina la MBUNGE waliompigia kura juzijuzi kwa kuwa ni CCM  na KWA HIYO hatishi kama wapinzani TANZANIA,....
...kama tu kuna waliosahau kuna siku waliamua KUACHA pombe baada ya kustukia pombe si chai baada ya maji kuzidi unga MWAKA HUU.:-(

CHAKUJIULIZA:

  • NI nini unafikiri umeshakisahau ambacho kuna kipindi kilikukera sana MWAKA huu mpaka utashangaa ukikumbushwa hicho kitu kwa kuwa LAKUSHANGAZA  ni kwamba  umeshakisahau na kilitokea mwaka huu huu?

Naamini KUSAHAU kuna umuhimu wake,....
....kwa kuwa ndicho MOJA ya kitu kifanyacho huoni WATU wengi WAKILIA MITAANI,....
...kwa kuwa kama BINADAMU angekuwa hasahau makali ya yale MACHUNGU kama ya misibani au tu kudharaulika,......
..... labda DUNIANI asilimia ya watu wote ungekuwa ukiishuhudia IKITOA mchozi mitaani.:-(

Swali:
  • AU?
  • Si unajua labda kunamtu TANZANIA kashasahau Dr Remmy Ongala amefariki?

Na ndio,.....
....pamoja ya kwamba kuna umuhimu wa kusahau,.....
..... busara za kukumbuka nazo huhitajika kama nia ni kuepuka kurudia MAKOSA kwa kuwa funzo lililopatikana kwa KUCHEMSHA bado lakumbukwa.




Naendelea kuwaza!:-(






Hebu twende South Africa  Guffy alete - Vuka Ma O Lele



Makapkap warudie -Bum Jive



Au tu Professor , Oskido na Dj tira kutoka Durban ,South Africa nao waachie tu tena - Jezebel

3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

emu-three 10:47 am  

Wanasema kama binadamu asingepewa kusahau wanawake wasingekubali kubeba mimba tena, kwa kukumbuka yale machungu ya uzazi, lakini mmmh, raha ya masaa machache inasahaulisha kila kitu!
Ni miujiza ya mungu, kweli naiita miujiza, kwani ni juzi tu, au unaona kama jana, watu walikuwa wakirukaruka na kupiga mawe kwenye mabati wengine wakichoma matiari ya magari , eti twashangilia mwaka mpya, mwaka huo ndio huo unayoyoma, na umri nao huo unayoyoma, jana ulikuwa ukiitwa mtoto, ikaja kijana leo unaitwa Mzee.
Mkuu wewe upo wapi kijana, au mzee, ingawaje sasa hivi ukifika maofisini mameneja wengi ni vijana, lakini wanaitwa `wazee' kwahiyo usiogopwe kuitwa `mzee' kwa kuchelea kukosa vimwana, lakini yupo nani vile wanayemtangaza kila siku anavizia watoto wa shule kwasababu ni mzee. Mbona huyu meneja nanihi sote twamuita mzee,lakini kila sikuu na dogodogo hatumlaumu, au kwa vile tafsiri ya Mzee imeingiliwa@!
Ni hayo tu mkuu

Yasinta Ngonyani 1:53 pm  

MMM! umenena hilo la kuzaa si mchezo lakini kweli unajua hata mimi nilisahau..LOL Najaribu kukumbuka ni lini mara ya mwisho nimekwenda kanisani..mmmhh! ngoja niache nisije nikakumbuka....

Simon Kitururu 3:34 pm  

@M3:Kweli nasikia kuna WADADA waapao kuto nanihii tena kutokana na uchungu wa kujifungua ingawa sina uhakika ni kuanzia siku ya ngapi hamu ya mchezo na ujasiri wakurudia mchezo hurudia pale pale.:-(

@Yasinta:Si nasikia KANISA kama watu wangefuata aliyofundisha YESU basi sio nyumba kwa kuwa hata mwili wako waweza kutafsiriwa kutoka katika mafundisho ya BIBLIA kuwa ni hekalu la BWANA?

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP