MAISHANI kama kingeonjwa PIA kirahisi kila KIDUDE kinukacho VIBAYA,....
>> Saturday, December 25, 2010
.... labda WENGI wangegundua HARUFU na utamu labda havina uhusiano wa karibu KIHIVYO.:-(
Swali:
- Si inawezekana mtoto wa PWANI azimiaye PILAU anaweza asihusishe harufu ya MATOKE na utamu wa MATOKE azimiayo MHAYA?
Na kunusa,...
.....ndio moja ya siri KWANINI kuna virukwavyo VITAMU ,...
....ingawa PIA kuna vijulikanavyo tu ni kwa kuwa vimeoshwa ndio maana wakati vinaonjwa havinuki na wanusao,...
.... ambao wamezoea kuoanisha HARUFU na utamu,....
...huku wakijua HARUFU sio UTAMU!:-(
Swali:
- Si inakumbukwa EMBE halinukii kama NDIZI ingawa labda vyote ni vitamu?
Ndio,...
....kama alivyo SENENE na harufu zake mtamu,...
.....kuna waaminio kiutamu zaidi ni KUMBIKUMBI hasa wakati anakaangwa kifanyacho harufu yake pia iwe moja ya UTAMU!:-(
NAACHA wazo!
Na hebu tubadili wazo na kukumbushwa UTUMWA na Burning Spear katika -Slavery days
5 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
nanukuu "MAISHANI kama kingeonjwa PIA kirahisi kila KIDUDE kinukacho VIBAYA,...." mwisho wa kunukuu nimekipenda kicha cha habari lakini sina uhakika ni kitu gani hicho kinukacho..LOL. Heri ya krismasi Mtakatifu:-)
DUH!
@Yasinta: Kidude kinukacho chaweza kuwa kitu chochote!
Si nasemekana Duniani karibu kila kitu kina harufu yake na ni Mtu tu mwenyewe unaye weza kuamua hicho kitu KINANUKIA au KINANUKA kutokana na umahiri wa PUA yako?
@Serina: DUH!
"labda WENGI wangegundua HARUFU na utamu labda havina uhusiano wa karibu KIHIVYO.:-("
Kama tunda la Doriani (Dorian fruit) - harufu mbayaaaa ila taste yake kitu kingine...they say, try it before you die :-)
@Candy1: Ndio hapooo!Watu huoanisha sana utamu na harufu wakati inajulikana kunavinukiavyo vizuri vikipakwa kwenye kikwapa kama DEODORANT ingawa haina manaa kwa kunukia vizuri ndio vilambwe!:-(
Post a Comment