Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Elimu kwa kawaida inakuongezea IDADI ya unayojua BILA uhakika wa kukuongezea BUSARA!

>> Monday, December 13, 2010

KWA hiyo  labda ,.....
.....kwa kujua sana tukichukulia kujua ni KUELIMIKA,....

.....hakufanyi MTU ajuaye kuwa pia na BUSARA.:-(


Swali:
  • Kwani hujawahi kukutana na ambao KWA USHAHIDI WA  VYETI wameelimika sana na KWA kujua ndio basi tena- ila wana BUSARA kama za  nguruwe za kunyea wanapolia na kulala?
  •  Si unajua kunauwezekano INZI ni miongoni mwa WADUDU wanaojua sana na WENYE busara sana tu KIINZI labda kuliko BINADAMU wanaojua walivyo na BUSARA kibinadamu?

Ndio,....
...KATIKA MAISHA ,...
.....ni wengi wenye ELIMU  ya umuhimu na UJUZI  wa matumizi ya KONDOMU aka  soksi,....
...ingawa KIVITENDO hawana busara za kutumia KONDOMU katika mpekecho wa YA BINADAMU yenye mpaka GONO.:-(

Swali:
  • Au?

NI HILO TU na ni wazo tu HILI Mheshimiwa!:-(
Jumatatu NJEMA!


Tubadili tu na FERRE GOLA katika kitu -MABOKO PAMBA



Au tu Ferre Gola amalizie na - 100 Kilo

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

emu-three 12:52 pm  

Swali kwani kusoma ndio kuelimika? Unaweza ukasoma madarasa kibao ukakariri yote yakina nanihii, lakini metendo yako yakawa aheri hata ya wale waliobakia nyumbani wakichunga ngombe!
Ndio alyesoma si sawa na asieyesoma, kwani kwa kusoma unaongeza kujua...lakini kuna kusoma na kukariri...na usijue ulichokariri kina maana gani?

Simon Kitururu 1:17 pm  

Kuna mtu aliyenishinda kwa hoja akidai hata akaririye , kwa kukariri atajua kitu zaidi ya asiyejaribu hata kukariri.

Na ukimpa kazi ya kufundisha watu WAKARIRI ,...
... anaweza kuwa ndiye MWALIMU mzuri kwa kuwa yake yote ni ya kukariri.


Na niliambiwa pia asilimia kubwa ya WALIMU wanaweza kukupasisha mtihani kwa majibu ya ulivyokariri KITABU sentensi mpaka sentensi , nukta mpaka nukta, namba ya ukurasa mpaka namba ya ukurasa,....
... kuliko ukijibu swali kwa jinsi tu ulivyomuelewa VIZURI na kiusahihi mwandishi wa kitabu ,...
.... kwa kuwa inadaiwa kama si somo lenye fomula kama HISABATI kitabu kama BIBLIA waelewaji wawili vizuri bila kukariri wanaweza kuzalisha dini mbili zipinganazo huku wote wakinukuu ujuaji walio utoa kwenye kitabu hichohicho BIBLIA.:-(

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP