Binadamu HAJAUMBWA kupigana KILA VITA!:-(
>> Tuesday, December 28, 2010
Kwa hiyo,....
......CHAGUA vita yako,...
...chagua cha muhimu kwako,...
...kwakuwa MWANADAMU hategemewi kukabili yote!
Swali:
- Si inasemekana MAISHA YA BINADAMU ni mafupi na hakuna aliyewahi KUISHI aliyemaliza kila kitu ?
Na inasemekana,.....
.... kama MTU anajitahidi sana na bado haelewi SWALA,....
....labda HILO SWALA sio lake na ni la WENGINE hilo KUELEWA!:-(
Swali tena:
- Si inasemekana kila mtu kuna ambayo kwake ni MARAHISI kwa hiyo isifikiriwe ni kwa kila mtu UMALAYA ni mgumu?
Na labda fanya UWEZAYO ,...
...na usiyoweza waachie wawezao,....
....huku kikubwa KIKIWA ni kujifunza kuridhika na yale katika JITIHADA ndiyo yaliwezekana kama nia ni FURAHA maishani.:-(NI wazo tu hili MHESHIMIWA!
Hebu Billy Ocean arudie-SUDDENLY
Na IMAGINATION wakumbushie tu-Just an Illusion
2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Maneno ya hekima. Kama binadamu tungelielewa hili, pengine migogoro ingepungua na tungekwepa kupigana hata vita visivyoshindika.
Wamarekani kama wangelitambua hili pengine wangefikiria mara mbilimbili kabla ya kujitosa vitani Afghanistan pamoja na kwamba walionywa na Warusi na wanahistoria kwamba Waafghanistan kihistoria wana tabia ya kutoshindika! Wamarekani hawakusikiliza na matokeo yake tunayaona.
Yapo mambo mengi katika maisha ambayo tunayaparamia tukidhani kwamba tunaweza kupambana nayo na baadaye tunaishia kugundua kwamba tulikosea na kwamba tumejiletea maumivu ya bure. Wanafalsafa wa kale wa Kigriki hasa Epictetus na Epicurus waliwahi kuligusia jambo hili walipokuwa wakijadili mada ya kifo. Unaweza kuyasoma mawazo yao kwa kifupi hapa:
http://matondo.blogspot.com/2009/01/tuzungumzie-kifo_28.html
Asante Mtakatifu kwa kutukumbusha kuhusu hili.
@Mkuu MMN:Nakubali kabisa uliyosema na Asante kwa LINK.
Post a Comment