Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Kama KUKOSEA ni UBINADAMU,....

>> Friday, December 31, 2010

..... KUSAMEHE ni zaidi ya UBINADAMU,...
..... na ndio maana  ni moja  ya SHUGHULI ihusianishwayo na kazi  mpaka afanyazo MUNGU.

Swali:

  • Si inakumbuka MUNGU huwa hahusianishwi na KUKOSEA?
  • Hivi kwanini bado kuna wadaio KUMZIMIA Mungu lakini wagumu kumuigilizia MUNGU  katika ya KIMUNGU zaidi yale ya  KUSAMEHE  na kung'ang'ania yale yasemekanayo pia ni ya KIMUNGU ya kutoa ADHABU tu  kama Mungu  ?

Ndio,....
....pamoja na yote ambayo hufanya kwa mtu KUSAMEHE kuwe kugumu,....
.....BADO yajulikana  kusamehe kwa mtu ni bonge la TIBA kwake.:-(


Swali:
  • Kwani unafikiri ni ALIYESAMEHEWA TU ndiye anufaikaye na kitendo cha KUSAMEHE?


Ndio ,....
....katika kusamehe kuna wafikiriao  ni VYEMA kusamehe aliyeomba MSAMAHA TU  kwa  kuonyesha kastukia alipokosea,....

....ingawa pia kuna WADAIO  wenye busara zaidi husamehe hata wasioomba MSAMAHA kwa kuwa labda hata hawajastukia WALIPOKUKOSEA hasa kwa kuwa KIBINADAMU hawastukii kila kitu  WAKIGUSACHO kikugusacho ambacho kwako ni MAKOSA,....

.....kwa hiyo,....



....wasamehe tu  akina SIMON KITURURU,  Babu Seya,  Limpenzi lako, NDUGU LAKO, Rais KIWETE ,jamaa tu lililokusonya bila sababu wakati unanunua nyanya na bamia  KIGENGENI huku ukimtamani muuza genge kimahaba, .....

......kama tu labda walivyosamehewa akina Mheshimiwa Rais IDI AMIN,  Winnie Mandela na Rais Mandela, Mheshimiwa CHENGE  na ......,.....,.......,.......


........hata kama  BADO hawajisikii kukuomba msamaha,....:-(

...MIYE nawaza tu hapa MHESHIMIWA jamani!:-(




Mimi Simon Kitururu naomba MSAMAHA kwa yote lakini MDAU  hasa  kama kunamaeneo nimekukwaza KIZEMBE!!:-(




Tubadili wazo  kwa kumsikiliza CHUCK BROWN...



Chuck Brown aturudishe enzi hizo kwa-Bustin' Loose



Au tu CHUCK Brown arudie-The Party Roll

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP