Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Jibu kwa DA MIJA lenye kucheza karibu na DINI na IMANI za watu kwa hiyo CHEZA kwa stepu usimkanyage MWENZIO!

>> Monday, December 27, 2010

 [Tahadhari: Nachoandika ni kutokana na tafsiri yangu BINAFSI ya mambo kama Simon Kitururu na mie sio Mwanahistoria wala Aliyesomea DINI ingawa kila siku mambo haya mawili nayaingia kichwakichwa kivyanguvyangu kutokana na VIANZO vyovyote vya TAARIFA  nibahatikavyo kuvipata kwa hiyo KUKOSOA mtazamo wangu RUKSA- na  bila kusahau MLENGWA hasa wa hii taralila ni Da MIJA!:-( ]




Nafasi ya kiboxi cha maoni kwenye Blogu ya Da MIJA haikunitosha,....


....kuingia kichwakichwa swala  HILI lililoanzishwa na Da Mija kutuonyesha PICHA ya ZIZI au MAHALI alipozaliwa YESU kama lionekanavyo siku hizi baada ya Miaka Elfu kadhaa ....

Hebu tupadeku.....


Na chachandu ya kuongelea swala nilijuavyo mimi kama SIMON KITURURU ililetwa na  Swali la Da MIJA:
  • Swali langu ni kwamba kwa nini tunakataa hiyo siyo sehemu alipozaliwa Yesu? ni kwa vile Yesu alizaliwa zamani sana na kumbukumbu ya mahali hapo haiwezi kutunzwa au? na kama hiyo ndio sababu mbona Kaaba kule Mecca inasemekana ilijengwa kwanza na Abrahamu ambaye aliishi miaka mingi tu kabla ya Kristo?


JIBU langu kwa kifupi kwa swali hilo hapo juu kwa wale wapenda NJIA YA MKATO ni :
  •  Si wote wakataao hapo ndipo alipozaliwa Yesu ndio maana kuna watu wanapata ulaji hapo kwa kuwa kuna MTUZ kibao zinaamini ni hapo ndipo palikuwa MATENITE WODI.

  • Kwa tupingao kuwa swala hilo lina utata wengi wetu ni baada tu ya kufuatilia HISTORIA ya BIBLIA na pia ya eneo lenyewe kitu kifanyacho kama mimi niamini hapo ukweli wa swala hilo misingi yake ni IMANI na sio KWELI kama kweli ya FACTS aka data nyomi ziwezazo kuhakikiwa.:-(

  • Na kuhusu KAABA bado ni vile vile kama utafuatilia HISTORIA yake  utastukia sio watu wote wanaafiki unalo- SUGGEST kuwa  kila mtu anaamini hivyo  kuwa palijengwa na ABRAHAMU, ingawa asilimia ya wengi wakubalianao na wewe ni WAISLAMU ambapo tutarudi tena katika swala la DINI na imani ambavyo AAMINIYE huo utakuwa ni KWELI TUPU hata kama asiyeamini atakuwa na vigezo vyake. Na kunawatakao kusahihisha kidogo ambao ni WAISLAMU  kwa kusema :

Abrahamu na Ishmael kwa KIISLAMU  walirudia tu  tena KUJENGA katika misingi ya zamani  kwa kuwa  mtu wa kwanza kuijenga KAABA alikuwa ADAM ,na  kuna wengi  waaminio HAPA DUNIANI kuwa  hapo ndipo kulikuwa na jengo la kwanza DUNIANI.

Hebu tudeku KAABA  katika mchoro kabla sijaendeleza kulima N'GWE kitaralila:

KAABA



1 - Black Stone on the south-west corner.

2 - Entry door, on the East wall 2.13 metres above ground level. It is accessed using a set of portable steps.

3 - Rainwater spout made of gold. This was added in the rebuilding of 1627 after rain the previous year caused three of the four walls to collapse.

4 - Gutter, also added in 1627 to protect the foundation from groundwater.

5 - Hatim, a low wall originally part of the Kaaba. Pilgrims do not walk in the area between this wall and the Kaaba. Some believe this area contains the graves of Hagar and Ishmael.

6 - Al-Multazam, the part of the wall between the Black Stone and the entry door.

7 - Post of Abraham. Abraham is said to have stood on this stone during the construction of the upper parts of the Kaaba, raising Ishmael on his shoulders for the uppermost parts.

8 - Corner of the Black Stone (South-East).

9 - Corner of Yemen (South-West). Pilgrims traditionally acknowledge a large vertical stone that forms this corner.

10 - Corner of Syria (North-West).

11 - Corner of Iraq (North-East).

12 - Kiswa, the embroidered covering, replaced annually.

13 - Marble stripe marking the beginning and end of each circumperambulation.

14 - Post of Gabriel






Kabla sijaendelea cheki  zaidi  BAADHI ya Hoja kama hizi zilizotangulia HAPA kwa DAMIJA :

Anonymous said...

  • Sista huu uongo usiuvalie njuga na wewe utaonekana mwanamke wa fimbo sio shoka tena! ni uongo mtakatifu waliotudanganya miaka tele na bado wajinga wanaendelea na upuuzi huu mpaka kwa watoto wao??!! jamani hebu tutoke huko, tuwaachie wazungu na fantacy zao, waafrika tuna yetu tulioyadharau, tumebaki kupokea kila kitu... WAKE UP


Blogger nyahbingi worrior. said...

  • we nani kakwambia?au ndio vitabu vinavosema?kwa habari kama hii naamini vizazi havitokaa kamwe kujuwa ukweli kuhusu 25/dec/...



SIMON KITURURU said...

  • Binadamu kweli kiboko! Wamegundua Yesu alikuwa ana sura gani ingawa kwa mamia ya miaka inajulikana hakukua hata na mchoro wa sura ya YESU,...
.... na eti siku hizi wanajua mpaka ni zizigani alikozaliwa Yesu ingawa ukisoma BIBLIA utajua ZIZINI alipozaliwa YESU hapawezi kuwa katika hali ambayo kiujengaji ingedumu kiasi hicho ukizingatia kwa mtazamo wa sasa palikuwa ni kakijiji fulani tu!

Anyway,...

X-mas njema!




OOOOOKAY!One two one two Microphone check:

NAANZA  kuvamia stage zaidi kidogo KIKIFUPI :

Nianze kwa kusema IMANI ni kitu chaajabu sana na NDIO MAANA  ni kwa imani pekee ndio mpaka waaminio Ng'ombe huamini ni kweli Ng'ombe anamchango wake baada ya kifo hata kama wasio na imani hiyo kutoona uhusiano wowote wa Ng'ombe na nguvu za KIUNGU.

Kwa hiyo kabla sijaendelea;...
.....Ningependa kurudia busara za WAUNGWANA wapenda DINI kuwa kama unaamini na unataka kutunza imani yako``Don't  let a little KNOWLEDGE wreck your FAITH, kwa kuwa ni FAITH na SIO KNOWLEDGE iaminiwayo KUOKOA MTU hasa kwa kuwa kwa KUJUA unaweza kirahisi kuona katika yote ya imani ni UJINGA na ni FAITH aka IMANI ifanyayo uamini hata KISICHOLETA maana.

And as they say wale waponyaji KIMOSESI KULOLA : ``Imani yako ndio ITAKAYO kuponya hata gono na ukiwa vuguvugu labda mambo yatakuwa madangachee kinoma``.:-(



Niendelee kwa kukumbusha;...
.....Moja ya tatizo la KANISA na WANAHISTORIA,...
....kihistoria ilikuwa ni msuguano wa WANAKANISA kuamini BIBLIA ni kitabu chenye historia sahihi ya ulimwengu na WANAHISTORIA ambao walikuwa wanabunbulua ukweli kuwa Mengi kihistoria yaliyoandikwa kwenye BIBLIA hata ukifuatilia yajulikanayo kuhusu MISRI kutoka kwenye MAPIRAMIDI na maandishi mengine HAYA machi aka HAYAFANANI  na ukweli wa FACTS ,......
.....kitu kihakikishiacho wanahistoria kuwa BIBLIA sio kitabu cha HISTORIA kama WAAMINIO BIBLIA wapendavyo kukinukuu kihistoria. 


Na nagusia hili kabla SIJACHOKONOA zaidi swala,...
....kwa sababu hili pia HUJITOKEZA kwenye dini nyingine za hapa ULIMWENGUNI za waumini kutaka sana kitabu cha miongozo ya IMANI kiwe ndio jicho la kila kitu KIHISTORIA pia jambo ambalo huleta msuguano hasa ukizingatia KNOWLEDGE and FAITH mara lukuki havishabihiani na mambo mengi katika dini umuhimu wake uko tu KIIMANI na ukiuchokonoa KIHISTORIA matokeo yake moja ya mfano wake ni vita vya WAYAHUDI na WAARABU visivyoisha.:-(

Nanirudi kwenye hoja KWA KURUDIA  kuwa;.....

......tukiachana na ya UKRISTO na kwenda mpaka ya UISLAMU mengi misingi yake iko kwenye IMANI na ukifuatilia utastukia kukuta sentensi nyingi zisemazo``INASEMEKANA ´´ kwa kuwa ni stori ambazo ni inasemekana na wakati zinapata umaarufu hakuna aliyekuwepo kushuhudia - kwahiyo ndio maana kwenye KAABA katika ile POST of Abraham mara karibu zote sentensi itumikayo ni ``INASEMEKANA hapa ndipo ABRAHAM alisimama wakati KAABA inajengwa sehemu ya juu huku amembeba Ishmael MABEGANI.  

Note neno :``INASEMEKANA´´



Nianze kuiingia hoja kutoka ANGLE nyingine:....
.....Ukifuatilia HISTORIA ya mji wa Makkat Al Mukarramah aka MECCA na mpaka  KAABA lenyewe ,....
......utakutana na mambo kibao ambayo VYANZO tofauti vya habari vitakueleza kitu kingine.

Kwa mfano ;..


Kuna vyanzo vya habari vidaivyo jiwe BLACK STONE liliwekwa na Nabii Mohammad na kuna vidaivyo ni Abraham na Ishamael waliloliweka.
Kuna waaminio kati ya Hatim na KAABA ndiko waliko zikwa Haggar na Ishmael ingawa kuna wakataao hilo.
Na kuna wadaio Makkah a.k.a BAKKAH a.k.a  Makkat Al Mukarramah au tu MECCA ,....
....ulikuwa MJI muhimu  katika BIASHARA kama kazi za Ptolemy zidaivyo mji huo wakati unaitwa Macoraba kitu ambacho wanahistoria na ARCHAEOLOGY kwa ujumla inapinga kwa kuwa kipindi kinukuliwacho hakuna hata andishi au vinyangarakata vyovyote viashiriavyo uwepo wa MECCA ingawa FALME kibao za eneo hilo na miji mingine katika eneo iko kwenye recodi za kihistoria .


Kwa hiyo ukimsoma Wensinck katika Encyclopedia of Islam, halafu ukaja kusoma ya IMOTI adaiye kuwa kipindi hicho kulikuwa na Kaaba nyingi ila hii iliyobaki leo ndio pekee iliyokuwa ya JIWE na kusababisha iwe ya kiania yake , ukaenda kwa Patricia Crone katika Makkan Trade and the Rise of Islam,.......mpaka ukaja kwa akina Karen Armstrong katika Islam: A Short History, ukaenda kwenye majibu ya Dr. Amaal Muhammad Al-Roubi kwenye kitabu cha -A Response to Patrica Crone's book,......
....HADITH , na mpaka ukaja kumaliza na KITABU KITAKATIFU cha KORANI ,....
....unaweza kujikuta kama LAINI KIIMANI umeshaitia uvuguvugu IMANI yako kama tu WATUMIAO akili baada ya KANISA kuruhusu waumini kujisomea wenyewe BIBLIA wapaparikavyo na MADHEHEBU mbalimbali kisa kuna kitu tu KUHUSU MUNGU wanadhani wanajua.:-(







Kuna watakaodai lakini kuwa ,....
....uhakika tu ni kwamba KAABA ni ya zamani zaidi ya dini ya KIISLAMU na kabla ya UISLAMU wapagani washaabudu sana hapo na HUBAL akiwa ni moja wa miungu MAARUFU wasemekanao waliwahi kuwepo hapo ingawa pia kuna wadaio kuwa mpaka sanamu la Yesu na Maria vilishawahi kuwepo hapo kama MASANAMU tu mengine ambayo inadaiwa kunakipindi yalifikia 360 hapo yote yakiabudiwa.




NIKIRUDI kwenye SWALI lako Damija :

Naongea yote haya na LABDA HATA KUTOKA NJE YA ULICHOULIZA yote ikiwa ni kujaribu tu kusema kuwa ;...
.....sio KWELI watu wote wanakubaliana na MECCA na KAABA kama swali lako ninavyoonyesha KUEGEMEA au tu KUSAJESTI.

Na ni rahisi sana kuhakiki hilo kwa kusoma vitabu tofauti tofauti vya historia ya UISLAM au tu hata kwa ku -GOOGLE hili swala kwa kuwa kirahisi TU  hata kwa kulisoma  pasipo aminika sana kama kwenye WIKIPEDIA na utakuta pamoja na udhaifu wake kama CHANZO CHA HABARI ZA UHAKIKA lakini utastukia kitu kimoja ambacho hakipingiki KIRAHISI  kuwa,....

... hata kuhusu KAABA na MECCA kama tu PICHA uliyotuletea ya padaiwapo alizaliwa YESU,... ....ukiutafuta utata kuhusu UKWELI wake utaupata KWA KUWA UTATA UPO,...
...na kwa hiyo labda tuachie IMANI kuongoza katika hili SWALA  kwa kuwa ni WENYE imani tu ndio watakuwa na asilimia MIA ya KUAMINI vinenwavyo ni FACT.:-(




NACHOJARIBU KUSEMA pia  ni kwamba:


Na kama ilivyo wasio WAISLAMU wengi waaminivyo kuwa kwa kuwa WAISLAMU katika kuswali huelekea KAABA basi hawatofautishi kitendo hicho na cha WAKANISA la KIROMA cha kupigia magoti sanamu ya MARIA ambavyo vyote kwao ni MAKOSA hata kama kwa WAISLAMU KAABA haiko mbele yao kama sanamu ya MAMA Maria ilivyo kwa  WAKATOLIKI,....
..... kitu KIJITOKEZACHO TU TENA  tena ni jinsi WAHUSIKA WATAFSIRIVYO,...
....na tafsiri za watu KIIMANI ni HATARI kitu  ambacho ukicheza nacho kuna maeneo unaweza hata KUKOLIMBWA kwa kuongea wazi wazi mitazamo ambayo huweza kugeuza IMANI za watu kuonekana ni ZA Kibulicheka tu.:-(

Na moja ya DINI ambayo WENGI huogopa kujiingiza waziwazi kuongelea mambo yake ni ya KIISLAMU kwa kuwa  ni moja ya DINI ambayo waumini wake hawataki mchezo na TAFSIRI za ajabu ajabu ya wakiaminicho kitu kifanyacho hata kati ya WAISLAMU na WAISLAMU  ukiwa MSHIA ujihami na WASUNNI na ukiwa MU- AHAMADIYYA ufuataye mafunzo na TAFSIRI za KORANI za Mīrzā Ghulām Aḥmad,...
...wajikuta unakwepa WASUNNI na WASHIA kwa kuwa wote wanaweza kukukolimba,....
.....kitu kichangiacho pia kuzuia kusikia kwa wengi  tafsiri tofauti tofauti watu wazitoazo kwenye KORANI kwa kuwa  kuna hofu kama tu ilivyokuwa kwenye UKRISTO zamani ambapo kama unajua kitu kama vile DUNIA HAIKO kama MEZA inabidi ULE TU KOBISI kwa kuwa ukitamka PAPA na TIMU yake wange KUKOLIMBA.:-(





Na tukiachana nahilo ;...
....nukuu muhimu kuhusu SWALA ZIMA hili nashauri soma mwenyewe: Korani.


Au jaribu pia kucheki watu kama :

Hafiz Ghulam Sarwar's -Muhammad The Holy Prophet

Wensinck, A. J; Ka`ba- Encyclopaedia of Islam

Diane Morgan 's Essential Islam: A Comprehensive Guide to Belief and Practice



Na kwa kuwa siku hizi  Google IPO, basi jaribu pia kutafiti mwenyewe VITABU na SITES unazofikiria zina aminika zaidi hasa ukizingatia:

  1. 1. Chunguza mwandishi ni nani na hakuna hila za kisiri katika aandikacho.
  2. 2.Zingatia kuwa WENGI waandikao wanaweza wakawa wameathiriwa tayari MTAZAMO -nanafikiri unatambua kuwa ni kawaida KITABU alicho andika MSABATO kuhusu kanisa la KIROMA kwa kawaida huwa tofauti na ALICHOANDIKA Padre wa kanisa la Roma kuhusu Kanisa la Roman Katholiki kuhusu swala hilo hilo.
  3.  3.Na wategemeao WIKIPEDIA kunukuu wakumbuke katika WIKIPEDIA hujui ni nani kaandika na anania gani katika hili kuwa ni moja ya UDHAIFU wa kuitegemea kama kweli tupu ingwa inaweza kukupa mwanga kidogo hasa kukupa pia majina kadhaa ya VYANZO vya waliotafiti HABARI hii ukawatafuta na kuwanukuuu moja kwa moja katika mkao wa nani unapenda kuamiani asemacho ndicho kiko karibu zaidi na ukweli.


Na narudia :

SWALA HILI ni la KIIMANI zaidi na umuhimu wa UKWELI utategemea zaidiIMANI YA MTU kwa hiyo cheza nalo KIUANGALIFU la sivyo unawezajikuta umekuwa MPAGANI hivihivi!:-(


Kumbuka inasemekana katika IMANI:
.....A little knowledge is a dangerous thing ,...
...DON'T LET A LITTLE knowledge wreck YOUR FAITH kwa kuwa kunauwezekano- YOU are JUSTIFIED by FAITH alone!:-(


Na kama HITIMISHO:...
....DaMIJA kuhusu swali lako BILA kutaka kuchezea sana  zaidi IMANI za watu kwa kuongea sana mpaka nikwaze zaidi mtu NALIACHIA hapa:-(



Tubadili swala kwa kwenda BRAZIL kukutana na Carlinhos Brown arudie-Ashansu



Carlinhos Brown aendelee na -Zanza


Au tu Carlinhos Brown amalizie na - A Namorada

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Anonymous 2:45 pm  

DINI(IMANI), FALSAFA NA HISTORIA! LAZIMA UTAKWAMA TU MZEE!!! KAZI KWAKO!!! NILISOMA SOMA KIDOGO MAONI YAKO LAKINI NIKAONA NI USHUZI MTUPU!

Simon Kitururu 2:55 pm  

@Anony:

Si utani!Kukwama kupo na Ushuzi mtupu upo tu na kwa bahati mbaya hata kwa wajionao yao sioushuzi MTUPU hasa ikiwa nao ni BINADAMU!


Na ukiingilia kama NILIVYOINGILIA maswala ya IMANI za watu nahisi si kitu cha ajabu kwa mtu aonaye kwa mtazamo mwingine kuona hata IMANI za wengine ni USHUZI mtupu!

Asante kwa kunikumbusha lakini hilo Mkuu!

Kumbuka pia niandikacho hapa moja ya eneo ligusalo ni Ushuzi mtupu kwa kawaida kwa MTU fulani!

Vipi lakini Za siku?
Nyumbani hawajambo lakini?

Tuko Pamoja lakini na ingekuwa bomba kweli unge andika BUSARA kidogo wenye ushuzi mtupu tufaidike nasi kidoago.

AU?

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP