Leo katika wa wanawake uchokozi: Eti WANAWAKE waliosoma sana huogopwa na NJEMBAZ!:-(
>> Thursday, December 16, 2010
Nimesikia kuna wanaume LUKUKI,...
....moja ya kitu kifanyacho waamue MTOTO MZURI hafai kuoa,...
... ni kiwango chake kikubwa cha SHULE yake.:-(Ndio,...
...inasemekana wanawake walioenda shule sana NI WASUMBUFU hasa kwa kujifanya MACHINOO aka wanajifanya wanajua KILA KITU kitu kifanyacho kisa KIGOLI ana PHD ya KEMIA mwanaume anaweza akajikuta anabishiwa na kufanywa mjinga katika kuongelea hata JIOGRAFIA ya tako kama tu abishiwavyo ile JIOGRAFIA ya nchi.:-(Ndio,...
...inasemekana WANAWAKE walioenda sana SHULE ndio wabishi zaidi KUITWA CHUMBANI hata katika maswala ya kutoa CHAKULA CHA USIKU ghafla kisiri kabla watoto hawajalala na KWA BAHATI MBAYA sio kwa kama ufikiriacho ni MAADILI ndio kizuizi kwa kuwa WATOTO HAWAJALALA - ila ni kwa kuwa tu wanadai MWANAUME hawezi kuwageuza KIFAA cha STAREHE a.k.a kiburudisho murua wakati wao wasomi na baada ya siku ndefu kazini HAWATAKI BUGHUDHA kwa kuwa wameshafanya kazi ofisini zile muhimu sana za kujenga nchi!.:-(
Ndio,...
...inasemekana wanawake wasomi sana MATAKWA YA MUME huwa hayana kipaumbele kama matakwa ya OFISI au tu nchi!:-(Swali la kizushi:
- Kama ni kweli kwanini WANAUME wasikwepe WANAWAKE wa namna hii ikiwa wale waliofundwa kuhudumia MWANAMUME kwanza au wale wategemeao tu kila kitu kuletewa na BABA WATOTO wapo na wanaadabu HATA KAMA HAWAJAENDA SHULE na wakitekenywa tu wanakubali hata kama kwa kutoandaliwa vizuri itauma na michubuko SEHEMU SEHEMU inaweza ikatokea?
Na inasemekana JAMII ya siku hizi iliyoenda shule,...
....inasahau kitu kwa kutotetea SHULE za MAADILI ya zamani yaliyofunzwa na shule za elimu DUNIA ya WATU waliojua mazingira na maadili yafaayo WATANZANIA ,.....kwa kuwa tu eti WATU katika JAMII WANAKWENDA shule hizi za kisasa zilizoletwa na MKOLONI siku hizi,....
.....ambazo pamoja na mazuri yote ziletazo ila bado HURUKA kitu ambacho WATANZANIA wenyewe walitakiwa wakiboreshe kutoka katika elimu za jadi ambacho kilikuwa NA MAZURI YAKE ambayo misingi yake inge neemeshwa yangetatua matatizo YANAYOENDELEA kujitokeza au tu KUIKUMBA JAMII kisa jamii inaiga yote kutoka nje SIKU HIZI kutoka katika elimu za NJE au tu mambo ya jamii za NJE na KUJARIBU kuacha hata yale mazuri YA JADI kisa yanaonekana ni ya JADI zaidi kwa hiyo ni ya KISHAMBA ambayo LABDA ni ya MSINGI kwa JAMII ya KITANZANIA na yangeboreshwa na sio KUACHWA KABISA yangesaidia sana tu MWANAMUME na MWANAMKE wa KITANZANIA sebuleni , chooni ,..... mpaka CHUMBANI katika MAISHA yazidiyo kupoteza MAADILI na yageuzayo mtu awe na tabia kama za MBWA malaya.:-(
Swali zaidi la uchokozi:
- Kwani nani hapendi URAHISI WA MAMBO katika DUNIA HII yenye maisha magumu halafu ,HALAFU twafa?
Ndio,...
....nasikia WANAWAKE waliosoma sana ,...
...kuna NJEMBA zinawakimbia,...
...na nasikia kuwa LABDA sababu zao labda ni za MSINGI kinamna.:-(
...na nasikia kuwa LABDA sababu zao labda ni za MSINGI kinamna.:-(
Ndio,....
.....kunawezekana kuna kikubwa WAKIKOSACHO hawa njembaz,...
...kwa kukimbia WATOTO WAZURI wasomi wajuao kuongea mpaka YESYES NO mai milk is stending,.......kitu kifanyacho JAMII nzima kupungukiwa na kitu.:-(
Na ni ndio,...
....hili NI WAZO tu la KICHOKOZI TU mwaya NA wala usikonde MWANAKWETU na kuanza kunisuta bure NIKALIA!:-(
Tubadili wazo basi kwa kuwapata De la Soul katika mdinyo-BABY PHAT
Au tu De la SOUL na CHAKA KHAN warudie-ALL GOOD
Au tu badili tu kabisaaa na kurudisha AFRO BEAT uwanjani kwa FELA KUTI akirudia-Lets Start
3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Ni vigumu kwa mafahari wawili kuishi zizi moja!
Si utani Mkuu Malkiory!
Kaazi kwelikweli:-(
Post a Comment