Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Kuna MIPAKA utamu ukivuka TAMUTAMU hugeuka sio UTAMU tena, KAMA vile kulivyo na MIPAKA maumivu yakivuka MUUMIAJI huwa hasikii tena MAUMIVU!:-(

>> Friday, December 17, 2010

Swali:

  • Umeshawahi angalau SIKIA  kuwa   mtu akiumia KUPINDUKIA huwa  HASIKII tena MAUMIVU?
  • Na si inasemekana TAMU ikizidi NA KUVUKA MPAKA  inaweza kugeuka CHUNGU?


MPAKA!:-(

Na ukivuka mpaka,...
... LABDA WEYE SASA utakuwa unachezea KWENYE KIDUDE  pembeni ya TUNDU.:-(

Kwa hiyo LABDA ili PAKA aendelee kuitwa PAKA,....
.....inahitajika  PAKA asivuke mipaka na KUWA  KAMA MBWA  mpaka wachunguliao PAKA  kuchanganyikiwa KWA KUONA KIFANANACHO NA PAKA kinafanya maswala kama MBWA  ya  mpaka katika kujamiiana  ili kieleweke  KUNASIANA kitu ambacho  HATA KAMA NI UTUNDU  yaweza kuwa huo   sio UTUNDU utegemewao na utafsirio  KIUMBE  ni  PAKA hata kama hiyo ni FASHENI MPYA ya utundu katika  JAMII YA PAKA kiutundu!:-(



Swali:

  • Si unajua ukivuka mipaka ya MAADILI na SHERIA zifanyazo mtu aitwe MUISLAMU - KIISLAMU wewe sio tena MUISLAMU kama tu ukivuka mipaka ya KIROMANI KATHOLIKI uwezavyo kujikuta wewe siku hizi ni MPENTEKOSTE na labda KIKANISA KATOLIKI unachemsha?




MIPAKA!:-(

Na ukivuka HATA  ya urafiki MIPAKA,.....
....... labda wewe  ni ADUI .:-(


Na ukivuka ya utamu wa MUWA mipaka,...
.....kwa kutaka kuuongezea MUWA utamu  kwa kuumwagia  ASALI huo MUWA na pia kuunyunyizia tena zaidi pilipili na ndimu huo MUWA ,...


....labda kuna uwezekano utafutacho si KUFAIDI  utamu wa MUWA wala MIGAGI au tu  utamu wa muwa weye huujui  NA HAPO NI tukiachilia mbali uwezekano wewe ni kabisaa wa MUWA adui!:-(


Swali:

  • AU?
Ndio,...
....labda kuna MIPAKA utamu ukivuka hugeuka sio UTAMU tena kama tu  vile kulivyo na MIPAKA maumivu yakiivuka MUUMIAJI huwa  hasikii tena MAUMIVU!:-(

Ndio,...
....KIBINADAMU hata UTU una MIPAKA kama  kugawa  KWA KIUTU hutaki kugeuke umalaya  hata kama ni ule  usio na UMIVU!.:-(

Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!:-(
Ijumaa na WIKIENDI NJEMA Mheshimiwa!




Naacha kukuzingua MHESHIMIWA na hebu moja kwa moja  Meiway katika kusawazisha hali ya hewa kijiweni aingizie kitu - Oh Lele!



Au tu mwanamke wa shoka kwangu kwa jina Singing SANDRA arudie-True Colours




Mwanamke wa shoka Singing Sandra aendelee kushusha shule katika-Ghetto Of The Mind



Au tu huyu mwanamke wa shoka SINGING SANDRA arudie tu kufunda wanawake wenzake katika kitu kizito kiujumbe-Women Their Own Worst Enemy




TUKO PAMOJA WAKUU!

9 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Mzee wa Changamoto 7:17 am  

Duh!!!
Kweli "UjingaBusara" huu

Simon Kitururu 7:23 am  

@Mzee wa Changamoto: Kunauwezekana mkubwa tu ikawa HUU ni ujinga mtupu tu Mkuu!:-(

emu-three 7:31 am  

Kuna usemi kuwa `mpupia wingi hugogwa' sijui nimeupata wapi huu usemi lakini maana yake ni kuwa `ukiwa mfano unakula, ukawa unajaza mdomoni kwa wingi, mwisho wake utakabwa koo na hicho unachokula!
Umbile la kibainadamu lina mipaka yake, ndio maana mkuu kwa wale wanaopenda ulabu, ukiwa mlabu sana, utaitwa mlevi, ingawaje hata anayekunywa funda moja kiimani bado ni mlevi!
Hapo ndipo hoja ya kitamu kikizidi hugeuka kuwa sio-utamu tena, bali ...ndio hata uchungu ukizidi sana, labda unaweza ukawa utamu...!
Nini nimegundua hapa, ni kuwa kila jambo lina kipimo chake, vininevyo utavalisha bangili, usije ukaumiza, ...
Ni hayo tu mkuu

EDNA 11:49 am  

No comment weekend njema kwako pia.

Yasinta Ngonyani 12:10 pm  

O-Lele! Ijumaa njema nawe pia!!

Simon Kitururu 1:05 pm  

@M3: Si utani!
@Edna: Nahisi umesha comment!:-( Weekend Njema kwako pia mtu wangu!

@Da Yasinta: Ijumaa njema kwako pia MWANAKWETU!

ADELA KAVISHE 4:08 pm  

mmmmmh inawezekana kwani maisha hayatabiriki

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) 6:14 pm  

Kuna jamaa mmoja mhafidhina hapa nilikuwa namsoma akikandia mashoga alinichekesha sana. Anasema kwamba kamwe maishani mwake hajawahi kuona ng'ombe au punda dume akiparamia dume lenzake ili kungonoka. Iweje leo binadamu - kiumbe pekee mwenye akili anaparamia madume menzake? Kwa maoni ya mhafidhina huyu - huu ni unyama kuliko hata unyama wa punda na ng'ombe!

Ni hilo tu nililokumbuka baada ya kukusoma japo unayozungumzia ni kanuni ya muhimu sana katika maisha.

Simon Kitururu 6:49 pm  

@Adela:Katika kukubaliana nawe usemavyo Maisha hayatabiriki,....

......tatizo WANADAMU moja ya shughuli kubwa waifanyayo duniani HATA ukifuatilia mipango yao, mpaka WASOMEAYO mashuleni ,....nk. ni kujaribu kutabiri MAISHA. :-(

@Mkuu Matondo:
Tushukuru tu kuwa bado nasikia WANYAMA wengine hawajaanza bado kuigilizia matendo ya BINADAMU!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP