Leo siku ya UHURU tukiangalia JINSI YA KUPOTEZA uhuru wa TANZANIA ukifananishwa na upotevu wa UHURU WA MTOTO wa kuendelea KUJINYEA HADHARANI baada ya KUACHISHWA kuvaa NEPI!:-(
>> Thursday, December 09, 2010
Mwanzoni MTOTO huwa huru KUJINYEA ,...
.... na wazazi mpaka WATU tu wengine kuona ni kawaida hata kama choo kimekaaa kimharisho HARISHO.:-(Lakini toto likikua na KUACHISHWA NEPI bado likiendelea mpaka hadharani kujinyea,....
.....ni tatizo na IKIBIDI kuna watakalo lipiga hata KONZI kulikumbusha kuwa baada ya kuachishwa nepi mpaka kuanza kujifunza kuvaa mwenyewe KAPTULA huo ni mwanzo wa kuanza kupoteza uhuru wako wa kujinyea na hata kukaa uchi HADHARANI hata kama bado kwa jamii si HATARISHO!:-(
Watu wengi hutafakari UHURU wa TANZANNIA kwa mkao wa kudhania labda kuna ufinyu wa UHURU TANZANIA kwa hiyo nia na madhumuni ya kuangaika naye iwe ni kujiongezea UHURU hata kama hapa siongelei UHURU ule wa kujinyea,....
......ila MIE BINAFSI naanza kuwa na wasiwasi kuwa LABDA TANZANIA imepitiliza KATIKA SWALA la uhuru kama MTOTO ambaye sasa anavaa suruali na anatakiwa awe HIGH SCHOOL lakini anan'gan'gania uhuru wa kuendelea kujinyea HADHARANI .:-(
Swali:
- Si inawezekana SWALA zima la UHURU linakosewa jinsi ya kuangaliwa na visivyotakiwa KUWA HURU Tanzania ndio vinapewa nafasi ya kuendelea kuwa huru HATA KIMUANGALIO TU kitu ambacho kinafanya matokeo yake yawe ni UFISADI, umasikini, ujinga mpaka umalaya kwa mbaali ingawa kuna UKIMWI kuendelea kwa uhuru kushamiri Tanzania?
- Kwani wewe ukifikiria UHURU wa Tanzania unafikiria uhuru gani ukizingatia Tanzania iitwayo huru hata BAJETI yake wafadhili wakikataa kuichangia Tanzania haina kibezi cha kuwalazimisha waichangie ili WAHESHIMIWA waendelee kununuliana magari ya FAHARI?
Naamini Tanzania MPAKA miaka arobaini na tisa ya udaiwao ni UHURU,...
...kila siku inatafuta kujiongezea UHURU wa kutafuta sababu za KWANINI bado ni NCHI MASIKINI ya kutupwa na sio kutatua kimkao wa kwa hali na mali kuondoa UMASIKINI.:-(
Inatafuta kuendeleza sababu ni kwanini MAMBO yalivyokuwa mkweche bado tu ni kosa la WAKOLONI tu.
Tanzania na WATANZANIA tunatafuta njia za kuendeleza uhuru wa kulaumu WENGINE na sio sisi wenyewe hata katika maswala kama KUFANYA KAZI kwa BIDII ambayo tuhusikao ni sisi wenyewe.:-(
Tunalalamikia mpaka ELIMU wakati kwa uhuru hata ELIMU za jadi zilizotufunza jinsi ya kuishi na WATU kufanya kazi kwa bidii kama jambo linaloweza kukufanya angalau upate demu kijijini na huyo DEMU akafundwa kama ulivyofundwa ili mitoto yenu iwe na tabia nzuri eti nazo tumeua.:-(
Na eti katika KIBANO hicho kilalamikiwacho leo TANZANIA ,...
....kinamna HARUSI za KIFAHARI tunazing'ang'anina wakati tunaimba jinsi maisha yalivyo na kibano kwa UHURU tu.:-(
Na ukifikiria haya ,...
....ukiwa unamchezo wa kuwa na MAWAZO yaliyopinda kama Simon Kitururu,...
...unaweza kujikuta ghafla unafikiriaTANZANNIA kama MTOTO aliyekua ang'ang'aniaye kuendelea kujinyea NA KUNYONYA kwa UHURU hadharani halafu anataka achukuliwe kakua ,.......KWAHIYO kwa uhuru BIA anywe na mke aozeshwe pia.:-(
Mie SIMON KITURURU naendelea KUWAZA TU hapa MKUU ikiwa leo ni siku ya kumbukumbu labda ya USIO UHURU -TANZANIA!:-(
Tubadili tu na Art Blakey & the Jazz Messengers: Bobby Timmons, Wayne Shorter, Lee Morgan wadinye-Moanin'
Au tupitie Senegal DAARA J warudie ndude-Allah!
Au tujikumbushe tu tena kuwa TANZANIA ni bomba la kisura mnono ingawa labda SIKU HIZI twakumbushwa tu ZAIDI kuwa pamoja na yote YA UREMBO WAKE HUYU KISURA -ni vipengele vya kuwa anakwenda haja ndogo na kubanwa haja kubwa zaidi ya istailivyo - mpaka mahali tusipostahili kukumbushwa YA KINYESI hayo katika ....
2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Mungu ibariki Tanzania.
@Edna: Kweli tunahitaji mibaraka maana Mmmmh!:-(
Post a Comment