Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Naye muadimaya leo ni : JEAN -François CHAMPOLLION!

>> Sunday, December 19, 2010

Jean-François Champollion, by Léon Cogniet


Jean-François Champollion (23 December 1790 – 4 March 1832)  kazi yake MCHANGO wake ndio unafanya leo hiii tunajua MENGI  kuhusu MAFARAO wa MISRI,...
.... kwa kuwa ndiye aliyechangia kustukia maandishi na michoro ya zamani ya WAMISRI inamaana gani.

Kwa kifupi ndiye aliyestukia lugha  ya MAFARAO wa MISRI baada ya miaka  MAELFU ya watu kutojua   michoro na maandishi  ya kwenye MAPIRAMIDI yanamaana gani.

Kinachonizingua zaidi  pia ni HISTORIA yake,...
....hasa ukizingatia inasemekana kwa kuwa WAZAZI wake walikuwa ni MASIKINI,...
....hakupelekwa shule na kuandika na kusoma alifundishiwa nyumbani na KAKA yake.

Lakini  pamoja na kupata mizinguo ya kwenda shule kutokana na umasikini alipofikisha miaka 20 alikuwa ameshamasta lugha ya KILATINI, Kigiriki, Kiyahudi, Kiamharic, Sanskrit, Avestan, Pahlavi, Kiarabu, Kisiria, Chaldean, Kipersia , Ge'ez na pia lugha yake ya Kifaransa kwa kuwa Nguli alikuwa Mfaransa.

 Na ni udadisi wake kwenye lugha ya COPTIC ya MISRI ndiyo iliyosababisha apewe kazi ya kujaribu kuelewa maandishi yaliyokuwepo kwenye JIWE la ROSSETTA aka ROSETTA STONE na kama wadaivyo  wabongao ung'eng'e -the rest is HISTORY.



Ni historia yake hii ya kujisomea mwenyewe KATIKA mazingira  magumu ambayo huwezi kutegemea MTU anawezakufanikiwa UKIZINGATIA sikuhizi ni mpaka UENDE angalau CHUO KIKUU  ndio uaminike UNAJUA KITU  KISOMI inayonifanya nimuadimaye leo.

Kumbuka kipindi anabumbulua MAFARAO walikuwa wanaongea nini ilikuwa ni KIPINDI kanisa la KIROMA aka KATOLIKI linapiga vita  kitu hicho kwa kuhofia mtu ukijua WAMISRI hao walikuwa wanaongea nini ataua nguvu ya BIBLIA hasa kwa kuwa kipindi hicho BIBLIA ilikuwa inachukuliwa kama kitabu chenye historia ya kweli KIHISTORIA .

Na ilikuwa inaaminika GHARIKA la enzi za NOAH lilifuta kila kitu hapa duniani isipo kuwa FAMILIA YA NOAH na vilivyokuwepo kwenye SAFINA YA NOAH kwa hiyo KANISA liliogopa ikijulikana kuwa kama MAPIRAMIDI na vinyangarakata vingine vilivyopo MISRI aka EGYPT vikionyesha kuwa ni vya zamani kuliko miaka iliyo kadiriwa  kutoka kwenye BIBLIA kuwa ndio MUNGU alileta GHARIKA na kuuijaza DUNIA maji na kufutilia mbali kila kitu kasoro NOAH na familia yake pamoja  na wanyama mpaka KUNGUNI na CHAWA  wawili wawili NOAH alio wachagua kuingia kwenye SAFINA,...
.... watu watabumbulua kuwa BIBLIA sio ukweli mtupu kihistoria na kufikiria KANISA la KIKATOLIKI  ni  mizinguo mitupu.:-( 

Na  inasemekana KUTOKANA  NA HILO  kuna mambo ni mpaka HUYU jamaa alikufa ndio wakastukia kwenye maandishi yake kwa kuwa aliogopa kusema WAZI  kwa kumuogopa PAPA wa kanisa la ROMA ambaye kipindi hicho ukicheza na DOKTRINI za KANISA la KIKATOLIKI alikuwa anauwezo wa KUKUKOLIMBA.:-(

Kama nimekupandisha nyege ya kumjua zaidi huyu nguli MGOOGLE tu !

Swali:
  • AU?

Au mpate kilaini  zaidi kama unaamini baadhi ya mambo kwenye WIKIPEDIA ni kweli hapa


NI HILO TU MHESHIMIWA!
Jumapili NJEMA Kijeba!

Tubadili mkao hapa kijiweni kwa msaada wa Lord Kitchener akiongelea-De Doctor Daughter



Lord Kitchner arudie-Kaka ROACH


Au turudi tu New Orleans tukakutane na Aaron Neville ili  atukalishe kijumapilijumapili kwa mdinyo-Ave Maria

1 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

emu-three 1:15 pm  

Mkuu umenipa vitu adimu vya watu kama hawa, lugha zote alikuwa akiziongea na kuzifahamu. Leo hii tunajua lugha tatu kwa shida, kilugha, kiswahili na kiingereza...mmh wengine Kifaransa!
Nashukuru mkuu, nimejifunza kitu kwa huyu jamaa, soma hata kama sio darasani soma, na hifadhi, wasipopenda hawa wa leo, kesho kwa rejea zako watazipenda tu!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP