HAPA DUNIANI wakati huohuo unafikiri UNASHINDILIA KITU yasemekana ni wakati huohuo nawe UNASHINDILIWA KITU!:-(
>> Friday, November 05, 2010
Katika mambo mengi,...
.... ni MTAZAMO tu usababishao anayefikiria anafanya hastukii kuwa labda ANAFANYWA.:-(
Na katika ung'eng'e kuna wengi,.....
.... wamdakao NEWTON swala hili katika ile ya NEWTON ya ``To every ACTION there is always an equal and opposite REACTION ´´ au katika lugha ya kitaalamu ``Kutendea KIDUDE na majibu ya KITENDWACHO KIDUDE katika KUJIBU MASHAMBULIZI au tu kukabili nyomi ya kitendo cha kisukumizwacho kitu na kisukumiwacho kitu huwa nguvu DROO,´´ ........kitu ambacho katika swala zima kinamna hata LA NIPE NIKUPE kuna ambaye ataliangalia kuwa KIFIKIRIWACHO KINA FANYA katika mtazamo fulani WA WATU WENGINE kuna watakao kuwa na ushahidi KITENDO HICHO HICHO ndicho kinacho toa jibu kuwa HICHO HICHO wakati huohuo NDICHO CHAFANYWA.:-(
Swali:
- SI unajua wakati UNAMUUMIZA mtu kunauwezekano wakati huo NDIO unajiumiza tu MWENYEWE angalau KISAIKOLOJIA?
- Kwani hujawahi kusikia kuna NJEMBA imempiga KIJEBA bonge la NGUMI halafu nalo katika hicho kitendo ikastukiwa imeumia mkono?
Katika kulainisha HOJA hebu swala zima tuliangalie kwa kulifikiria TUMBO la aliyezamia ubwabwa HARUSINI:
Nguvu ya chakula itumikayo KUTUTUMUA aka KUTUNISHA tumbo la mwenye jazba ya ubwabwa wa bure harusini katika CHAKULA KUSHINDILIA tumbo kwa UBWABWA ,.....
..... ni sawsawa na nguvu ya kuta za tumbo kukibana chakula kisije kikatanua tumbo mpaka likachanika KWA TUMBO KUSHINDILIA CHAKULA hasa kama ubwabwa unaliwa kwa SPIDI KALI kabla haujaisha kwenye sinia bila MLAJI KUKUMBUKA kufikiria ni kilo ngapi tayari KIUPROFESA wa UZAMIAJI katika MISOSI kashabwia,.......kitu ambacho kinaweza kustukiwa kwa kushuhudia baadhi ya WAHESHIMIWA kuwahi kwenda msalani kwa kuwa tu tumbo lilijaa sana na katika TUMBO kukabili shughuli umesakizia UTUMBO msosi na utumbo umekubali kuwa afadhali MHESHIMIWA akajisaidie tu haja kubwa yaishe.:-(
Swali:
- SI kuna uwezekano nilicho andika HAPO juu ni UJINGA na eti umeusoma?
Lakini HATA kama ni UJINGA hebu fikiria,....
.... kwa kuwa labda ni kweli ANAYE SHINDILIA wakati huo anashindiliwa ,....
.... na kwahiyo kumbuka kuwa wakati UNAIBA labda unajiibia na ni mtazamo tu ambao haukustui hilo au lile la kuwa ROHO lako linazidi kupwaya KWA UTUPU kwa KILA unavyozidi kujazia ya KILIMWENGU ambayo twajua mtu haendi nayo kaburini roho ikitoka baruti.:-(
Ni wazo tu HILI katika MTIRIRIKO wa MWENDO wa maringo Mheshimiwa NA NI RUKSA KUTOELEWA!:-(
Hebu tuhame na kuendelea kupata kitu FUNK na nani zaidi ya BOOTSY COLLINS awezaye kutekeleza hili kama katika -Ahh The name is Bootsy ,baby/Disco to go
Au tu Bootsy Collins na Snoop dogg waendelee na FUNK katika -Undercova Funk
0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Post a Comment