LABDA kunahaja ya kuongelea UDINI Tanzania hasa kama ni kweli UDINI unaogopwa TANZANIA!:-(
>> Tuesday, November 30, 2010
Kwa kukwepa MADA za UDINI Tanzania,....
..... kunaweza kukawa kunachelewesha tu TATIZO ingawa hakuliondoi au KULITATUA tatizo la UDINI Tanzania.:-(
Swali:
- Si kuna uwezekano kwa KUTOONGELEA tatizo haimaanishi ndio unatatua TATIZO kwa kuwa tu umefunga bakuli lako na UCHEMI kitu?
Ndio,....
.... kuna tabia ya KUOGOPA kuongelea mambo TANZANIA kwa kuhofia ukiongelea vibaya TUKIACHILIA DINI ,....
....labda hata CCM kuna kibano utapata au tu kulipandisha JAZBA tatizo ambalo INADHANIWA usingelichokonoa lisingejitokeza.:-(
Ila kwa bahati MBAYA,....
.... inawezekana kwa kukwepa TOPIKI ndio kwanza unachangia UKUBWA wa tatizo ,.....
....na wala wakati huo HUTATUI tatizo.:-(
NI WAZO TU HILI!
Hebu Fally Ipupa na Krys wabadili tu wazo kwa-Droit chemin
Au tu P Square warudie tu- Ifunanya
Au tu Bracket na P Square wamalizie tu na -NO TIME
2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Mtakatifu;
Umegusa penyewe hasa. Siku za hivi karibuni kila mtu amekuwa akipiga kelele kuhusu kushamiri kwa udini lakini hakuna anayesema huo udini uko wapi na kama umeshamiri, kipi kifanyike.
Kulikuwa na hoja kule Jamii Forums kipindi fulani kuhusu suala hili na nilichong'amua ni kwamba pengine katika awamu fulani za uongozi, wenye mfumo wamekuwa wakipendelea watu wa dini moja (kama yao) katika kutoa vyeo na nafasi muhimu za uongozi. Na inasemekana kwamba hali ilipofikia sasa siyo nzuri. Lakini kama ulivyosema hapo juu, hakuna anayesema wazi huo udini uko wapi na kipi kifanyike. Juzi juzi hapa tumesikia kwamba makanisa yamechomwa kule Zanzibar....
Mtu mmoja aliniambia kwamba pia hali siyo nzuri kule UDOM kwa tatizo hili, na kama wewe siyo muumini wa dini moja hivi basi usidriki hata kuomba kazi huko kwani hutaipata na hata ukiipata hutafika popote!
Ujinga wa kuachia tatizo likitokota bila kuchukua hatua ni hatari. Kama kweli udini umeshamiri basi yawezekana tukawa tunacheza na moto. Hoja nzuri Mtakatifu!
@Mkuu Matondo: Yani basi tu !Kinachosikitisha ni kwamba inaonesha kuwa sisi WATANZANIA na amani zetu tumeshindwa hata kuwa na ujasiri na busara la kukabili TATIZO .:-(
Post a Comment