Mambo MENGI ni RAHISI mpaka uyatafute undani KIDOOOGO!:-(
>> Friday, November 05, 2010
Ndio,...
... kuanzia SHULE, Imani mpaka MAHUSIANO YA MTU na MTU,...
....kwa juujuuu HAYAKUNISHI SANA KICHWA,....
.... ila ukianza tu kuingia ndani zaidi na kuanza kutafakari ,KUYACHIMBUA na kujiuliza mpaka katika UKRISTO ya MUNGU BABA, Mungu mwana na ROHO MTAKATIFU ni MUNGU MMOJA,........ kama tu uanzapo kustukia MPENZI WAKO si kila siku anajisikia KUKUCHEKEA kama ilivyokuwa wakati MAHUSIANO YENU ni YA JUUJUU tu na yenye lengo KUU MOJA nalo ni kusikilizia tu UTAMU au
kama tu jinsi uendeleavyo kustukia MPENZI alivyo na ngozi mbaya ASIPOJIPODOA baada ya kuliingia ndani zaidi penzi kwa YA MPENZI mliyekuwa hamuishi pamoja na sasa hamkutanii migombani kwa kuwa penzi limepamba moto na kwa kuliingia undani zaidi sasa MNAISHI PAMOJA,........HAPO NDIPO utastukia jinsi URAHISI huwa na tabia ya kugeuka na kuwa UGUMU na unaochanganya kisa UMEINGIA tu kichwakichwa kitu wake UNDANI:-(
Swali:
- SI unajua kwa undani labda ADUI yako ni rafiki yako na ukimchunguza kwa undani ufikiriaye ni RAFIKI YAKO unaweza kuta kuwa kumbe huyo ndiye BOMBA YA ADUI yako?:-(
- SI unakumbuka kwa kumfikiria BINADAMU kwa undani ni kweli karibu kila BINADAMU ukutananaye anatembe na kinyesi mwilini hata kabla bado hajabanwa haja kubwa?
.... kuna watu na BUSARA zao watakuambia,....
.... hata MKE au MME wako achilia mbali LIMPENZI TU lako kama mnataka muishi bila kukwazika ,...
... LABDA usichunguze sana wake UNDANI kwa kuwa unaweza kustukia mpaka kitu ambacho ndio hasaa hukipendi MAISHANI mwako ,....... na hapa siongelei kuwa utastukia moja ya undani wa ni kwanini LIMTU lako likiwa na mafua huchukuwa muda kutoka BAFUNI ni kwa kuwa huwa linatumia muda wa bafuni kulamba kwa uhuru MAKAMASI ambacho ndicho uchukiacho sana zaidi kuliko mtoto mkubwa mgonjwa umuhudumiaye AJINYEAVYO.:-(
Swali kidogo zaidi:
- SI inasemekana ukichunguza sana CHAKULA cha HOTELINI kiundani unaweza kuugua tu kwa kuwa waweza mpaka kustukia anayekatakata KACHUMBARI huwa hanawi vizuri mikono baada ya kujisaidia NAMBA MBILI?
NI wazo tu hili Mheshimiwa!:-(
Hebu SAM COOKE arudishe busara na USTAARABU hapa kijiweni kwa kuachia ngoma-You send me
Sam Cooke aendelee na-Only Sixteen
Au tu Otis Redding aingilie kati tu na -Sitting on the dock of the bay
Au tu Otis Redding amalizie tu na-Pain in my heart na I can't turn you loose.
0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Post a Comment