Kama hustukii MARINGO ya INZI!
>> Monday, November 22, 2010
Inawezekana INZI huringia mpaka BINADAMU,...
.... kama ukikumbuka,...
.... yeyote astukiaye KINACHORINGA ana VIGEZO VYAKE vimstuavyo kuwa,...
... mwendo wa Bi ASHURA wa kutikisa tako ni wa maringo na wala sio KILEMA.:-(
Swali:
- Si unakumbuka kuna baadhi ya mwendo wa MARINGO umfanyao BRAZAMENI anayedundadunda kama usipostukia ni maringo unaweza kuwa na UHAKIKA KIJEBA ni KILEMA?
Na ukifikiria MARINGO,....
......utastukia,.....
...CHOCHOTE KIRINGACHO kina vigezo vyake vilivyo KISAIDIA kuchagua staili ya KURINGA kwakuwa na WALENGWA AKILINI yote IKIWA NI katika kuhakikisha inalenga KWA UFANISI kitakao kuwaringia na hasa kijuacho wanaweza kusikilizia mwendo wa maringo kama sio sauti ya maringo hata kama kipima joto la maringo sio WARINGIWAO kutokwa kama chura anayejifungua MIMACHO.:-(
Na chochote kikuringiacho kikikosea KULENGA ustukiavyo kuwa ni MARINGO,...
.... waweza ukawa unaringiwa na USISTUKIE maringo yenyewe ,...
...kama LABDA usivyostukia maringo ya INZI, bata malaya au tu MBWA ambaye labda kwa MARINGO ndiye LEO akurembuliaye macho.:-(
Swali:
- SI umestukia tukiachana na MARINGO, vigezo hata vya uzuri vikikosea MLENGWA viwezavyo kusababisha mwendo wa maringo wa MDADA mwenye tako kubwa kutia kichefuchefu hasa WASIO WAAFRIKA kama vile WAZUNGU ambao wengi wao hawakunwi na uzuri wa tako kubwa ACHILIA MBALI TAKO KUBWA HALAFU LINATIKISWA, wakati kuna BROTHERS aka MNUBIZ aka WAAFRIKA WENGI FULANI kwa mwendo huohuo Mdada mringaji mwenye wowowo la kigomvi URINGAJI WAKE unacheza kwenye mita bendi ZAO na udenda unawatoka kama ishara ujumbe wa MARINGO wahusika umewafikia?
- Unauhakika wakati huringi hakuna ambaye MITA BENDI ZAKE zinamstua unamaringo?
....kama KUKU hastukii maringo ya BATA,...
.... labda si ushahidi kuwa BATA hamringii KUKU angalau kwa kigezo yeye anaweza kuharisha huku anaendelea na shughuli zake tu za mwendo wa maringo hata bila kusimama kidogo .:-(
Ni wazo tu hili!
Jumatatu Njema MHESHIMIWA na nakutakia angalau upate vyema vitakavyokusaidia UPATE choo MKUU!
Niko kwenye JAZZ mood,...
...hebu John Coltrane & Duke Ellington wadinye - In a sentimental mood
Duke Ellington aturudishe kati kwa lawalawa -Sophisticated Lady
Au tu twende tena mwaka 1943 ili Duke Ellington arudie -It don't mean a thing
2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Kaazi kwelikweli (maringo):-)
@Yasinta: Si utani!
Post a Comment