Katika juhudi ya KUKUMBUSHA mtu kuwa matumizi ya KINYEO cha KUKU sio kutaga MAYAI tu ila ni mpaka kunya MAVI ya KUKU!:-(
>> Saturday, November 20, 2010
Binadamu huchagua,...
...na katika kuchagua KWAO wanaweza kuangalia HATA uzuri tu wa MSHAHARA wa MHESHIMIWA,...
...bila kustukia MSHAHARA HUO UTOKEAKO kingine kiwaumizacho ni NINI,...
...au labda kuna uwezekano huo huo MSHAHARA MKUBWA ndio ufanyao MCHAGA kajitahidi ashindwe kuuza viatu vyake VYA brandi ya MCHAGA KAJITAHIDI kwa kuwa WAHESHIMIWA na MISHAHARA yao jinsi inavyoendelea kuwa mikubwa ,...
....ndivyo wazidivyo kuwasaidia zaidi WACHAGA WALIOJITAHIDI Paris na CHINA na wala sio wanakijiji wa MKULANGA ze-BONGO ambao kwa MSHAHARA ukuavyo NDIVYO wazidivyoonekana waporipori na vyao si bomba kama cha KIITALI vitokavyo MILANO .:-(
Na kwa kuchagua,....
....eti kuna hata wachaguao kutokumbuka hata matumizi ZAIDI YA MOJA ya cha MTU kikojoleo ambacho tumizi lake kuu hudhaniwa ni KUKOJOA hasa kama vilivyo tawala mawazo ya WAHESHIMIWA kimwili ni MILANO.:-(
Swali:
- Si unakumbuka pamoja na uzuri wote wa JUA bado JUA linaweza kukuletea pia SARATANI?
- Na siunajua pamoja na uzuri wote wa CHAKULA , chakula ndicho chaweza kukuletea PIA madhara kama KITAMBI , utapiamlo au tu hadi VITA?
Ndio,...
.... labda hata MAISHA mazuri ya MHESHIMIWA,.....
..... kwa MTU kuyastukia HIVYO ndio kisa KUNA mtu maisha yake sio mazuri,....
....kwa kuwa inawezekana MOJA ulionalo kama upande mmoja tu wa shilingi,...... bado ni kweli SHILINGI ina pande mbili.:-(
Swali zaidi kiduchu:
- Huwa ukiona ZURI hufikirii uwezekano kitoacho zuri kinatoa na baya lake pia?
- Si unakumbuka kama umeme uonekanao ni mzuri tu wa NYUKILIA utawalao NCHI ziitwazo zimeendelea huwa unakuja na uchafu utokanao na nguvu hiyo ipendwayo ambao mpaka leo hakuna ajuaye jinsi ya kuudhibiti ?
- Na si unakumbuka pamoja na uzuri wote wa MAGARI bado magari ndio chanzo cha hewa MBAYA mijini na mazingira kuharibika mpaka katika kijiji cha Mkulanga?
Ndio,...
.....tumizi kuu la kinyeo cha KUKU taka usitake ni KUNYA mavi,...
...na wala hata sio kutaga mayai yafanyayo MPENDA Chipsi -MAYAI amfagilie sana KUKU.:-(
Swali nje kidogo ya tundu:
- Si unakumbuka PIA uharisho ni kinyesi cha kawaida tu chenye afya nzuri kwa BATA na kitokeako hutokea pia YAI kubwa kuliko la KUKU?
NIMEACHA na ni wazo tu ambalo RUKSA kutolielewa MHESHIMIWA!
Moja kwa moja Mad COBRA aingie GHAFLA kubadili mshawasha kwa-SHOOT to KILL
Na labda atulize kidogo jazba huyu huyu MAD COBRA kwa -Too MUCH
Au tu MAD COBRA amalizie kwa kulainisha zaidi kabisa kwa-FLEX
0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Post a Comment