KWA KUWA utamu wa KEKI labda bado ni SUKARI tu!
>> Wednesday, November 17, 2010
Na haki ya nani tena,....
..... kuna uwezekano kabisa pia UMSIKIAYE anasifia UGALI ,...
..... apendacho sio UGALI bali ni hiyo tu MBOGA tamu iliyo pembeni ya UGALI.:-(
Swali:
- Si unajua SIRI ya utamu wa MAKANDE kwa MHESHIMIWA Bibi KISEBENGO yaweza kuwa ni CHUMVI na NAZI vikisaidiwa na kiungo kikubwa zaidi katika UTAMU aka KUJINOMA kwa MTU akidapo MSOSI ambacho ni JINSI GANI tu huyo MHESHIMIWA Bi KISEBENGO ana njaa KIASI GANI?
- Kwani unataka kusema NYANYA inamchango sawa na vitu vingine katika KACHUMBARI wakati isifiwayo ni KACHUMBARI kijumlajumla tu?
Ndio,...
.... labda ni NJAA siri ya mtutumuko wa UTAMU wa chakula ,....
.... na kama unaumwa njaa vizuri hata UJI wa mtoto ulioanza kuchacha ambao HUJAWAHI KUUNYEMELEA JIKONI kama unyemeleavyo nyama za kuchoma za wageni ambazo unawasiwasi hazitatosha na watu wa nyumbani wazigide ,...
... unaweza kuuona ni MTAMU.:-(
Ndio,...
...labda ni kweli kuwa WATU huzidishia sifa hata vitu visivyohusika hata katika KUSIFIA MTU,....
..... kwa kuwa labda UTAMU wa mtu wala sio umbile lake LOTE kama akusikilizishacho nacho utamu wala sio hilo LIUMBILE LOTE la huyo MAINANIHII wako,....
.....ukizingatia LABDA kazi yote ya KUKUFANYA UONE TAMU hufanywa na kipengele tu kidogo cha huyo KIBONGE ambaye labda ni nguo tu zamfanya mrembo.:-(
Swali:- Si labda ni kweli watu wanaruka michango ya vitu vidogo vidogo kwa kuwa JAMII yahusudu MAKUBWA bila kuchunguza umuhimu wa madogo katika UKUBWA wa makubwa hayo?
Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!
Hebu Mzee Yusuf arudie-ALAMBA
1 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Hii kali! Hadi maimamu wanaserubuka.
Post a Comment