Swala la MKIA kutikisa MBWA na sio MBWA KUTIKISA mkia!:-(
>> Friday, November 19, 2010
Ndio,...
....mengi ya KIBINADAMU ni ya KIBINADAMU,...
...na BINADAMU akijaribu kujifanya MALAIKA,....
.... ni sawa na YA MKIA kujaribu kutikisa MBWA na sio MBWA kutikisa MKIA!:-(
Swali:
- Si unakumbuka MWEZI ni mwezi , DUNIA ni dunia na JUA ni JUA na labda ya DUNIA si ya MWEZI?
Swali zaidi kiduchu:
- Unafikiri lakini KILA ya MWEZI , dunia inayaweza ukizingatia kuwa labda si kila ya SISIMIZI mende anayaweza?
Ndio,...
....kujaribu TUSIYOYAWEZA ni RUKSA,....
....hata kujaribu kumuelewa MUNGU kwa akili za kibinadamu ambazo zinaupungufu mpaka zinatafuta cha zaidi ya KIBINADAMU kama tu vile BINADAMU waitacho ni MUNGU ni RUKSA,....
...lakini BADO tukumbuke ukweli uko palepale ,.......ni MBWA ndiye atakayetikisa MKIA na sio MKIA utakao tikisa MBWA na kwa mkia wa MBWA kujaribu kutikisa MBWA ni majaribio tu ambayo jibu la majaribio hayo liko wazi!:-(
NI wazo tu hili Mkuu!
Hebu tubadili kwa kupata busara za MCHUNGAJI kuhusu kama wewe una LIMKE lako halafu umejichanganya kwenye Facebook..
Au tupate hekima nyingine za Wazee....
0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Post a Comment