Kama huogopi katika kufanya UKIFANYIAVYO KITU kidude,....
>> Monday, November 01, 2010
.... katika ufanyacho wewe sio SHUJAA!:-(
Na kwa aogopaye hata MENDE,....
.... akifanikiwa hata kuua mende waliokuwa kwenye droo ahifadhiyo chupi zake AZIONEAZO AIBU zilizotoboka,...
.... alicho kifanya ni USHUJAA kwa kuwa ni kitu ambacho si rahisi kwake kumpa kibano MENDE,....
.... ingawa pia ingekuwa ni ushujaa pia kwake kuomba msaada kwa mtu mwignine aje kuua huyo mende lakini kwa KUTOA MSAADA hivyo ajue siri ya MHESHIMIWA aioneayo aibu ya kuwa chupi zake zimetoboka.:-(Swali:
- Muungwana si unakumbuka sifa mojawapo ya BINADAMU ni kuogopa?
Ndio,....
.... kama unakutana na MTU ambaye haogopi kitu chochote,....
...labda kumbuka kujihami kwa kuwa hapo unakabiliana na MTU ambaye moja ya sifa ya UBINADAMU hana.:-(
Na kumbuka,....
... kila mtu anaweza kuonekana ni SHUJAA jichoni mwa mtu MWINGINE ,....
.... ukizingatia kuwa HOFU zetu ni tofauti tofauti ndio maana kuna umdhaniaye ni mwoga kwa kuwa umeona akikimbia MENDE lakini ukimjua undani waweza shangaa asiyoyaogopa kama vile JEHANAMU uiogopayo,Kula nyoka, BUNDUKI uiogopayo kwa kuwa yeye ni JAMBAZI au tu jisi asivyoogopa uogopavyo kama vile zile sehemu za siri kubwa za akumendeaye udhihofuzo ki- muziki munene.:-(
Swali:
- Si unajua kuna mashujaa mchana ambao eti usiku wanaogopa GIZA?
- Na si unajua kuna mashujaa usiku tu na hapa siongelei mashoga zako wale usiojua ni wachawi?
Ndio,...
.... kama HUOGOPI,...
.....ufanyacho,...
....wewe umepoteza chansi ya kuwa SHUJAA katika hilo kwa kuwa UPIGAPO JAMBAZI Mbata kwako ni sawa tu na ufinyangavyo tonge la UGALI kwa mboga ya Msele.:-(
Ndio,...
.... kwa kuwa hatukujui na sisi tuogopacho ni kugombea UBUNGE wa Kariakoo,...
... wewe kwa kugombea hapo twaweza kuamini ni SHUJAA ingawa kwako ufanyacho ni kama tu wengine wafanyacho bila woga baada ya kumaliza kiheshima haja kubwa.:-(Samahani NI WAZO tu HILI MHESHIMIWA na nimeliacha na kulitemea mate POO!
Hebu tujifunze jinsi ya kujifunza UCHAWI -How to Learn White Magic AU kwa kuleta ustaarabu tumuachie huyu Freddie Mercury aliyezaliwa Zanzibar ingawa nasikia Wazanzibari hawamhusudu kwa kuwa kabla hajadedi alijulikana KWA KUPENDA WANAUME WENZAKE na kutiwa kinyaa na sehemu za siri za kike akija na bendi yake ya QUEEN katika ndude-Another one Bites the dust
Au tu Killer waingilie kati na kurudia-All I want
0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Post a Comment