Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Kuhusu UCHAGUZI wa VIONGOZI uliopita HIVI KARIBUNI Tanzania!

>> Wednesday, November 17, 2010

Ukiniuliza MIMI,...
....bado nitadai TATIZO haliko zaidi katika nani ANAYEONGOZA,....
.... bali liko kwenye mfumo mzima wa SERIKALI na TAASISI ZAKE kitu kiwezacho kufanya ,....
.... hata KIONGOZI awe mzuri vipi,....
.... kwa mtaji wa mfumo wenyewe KIUONGOZAJI ulivyo shaghala bagala,....
.... utekelezaji wa MASWALA ya TAIFA kwa manufaa ya WATU wake  bado utakuwa HAFIFU na uliodhoofu.:-(


Ndio,...
.... naamini mengi hata ambayo YANAFANIKIWA sasa hivi katika uendeshaji wa TANZANIA ,....

.... umeegemea katika UBAHATISHAJI TU zaidi ya UHAKIKA.:-(


Na KAMA HATA nini KIFANYIKE kwa kiasi kikubwa bado ni cha KUBAHATISHWA ,...
.... jinsi gani utekelezwaji utafanyika ndio HASWA waweza kukuta ndio CHABAHATISHWABAHATISHWA tu kwa kuwa KWA KIASI kikubwa hakuna mwenye UHAKIKA.:-(

Sasa jiulize:....
....kama nini kifanyike ukiwasikiliza VIONGOZI wetu utastukia hawana uhakika, sasa jiulize ni nini hasa kitatekelezwa ndani ya mfumo ambao hauna UHAKIKA.:-(

Ndio,...
... naamini KUBAHATISHA ni kwingi sana zaidi ya UFANYAJI MAMBO kwa uhakika  wa maswala katika NCHI niipendayo ya TANZANIA,.....
.....ukiniuliza leo hii ndio ntakavyodai.:-(




NA HILI ni wazo langu tu MHESHIMIWA na  ni RUKSA kulibishia.:-(
NI HILO TU Mkuu!

3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

malkiory 6:20 pm  

Fikiria Zakia Meghji pamoja na kukumbwa na matumizi mabaya ya ofisi, leo hii anakuwa mbunge mteule kupitia mgongo wa rais mwenyewe. Kichekesho!

Anonymous 10:39 pm  

Naunga mkono hoja yako bro! Ila taratibu muamko unakuja. Nategemea mabadiliko makubwa 2015.

Simon Kitururu 12:44 pm  

@Mkuu Malkiory: Si ndio hapo!:-(
@Anony:Kweli kabisa Anony.!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP