Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Katika KUFIKIRIA nia ya KITAKACHO kuonwa hata katika kipengele cha MTANUKO wa uchi!:-(

>> Monday, November 08, 2010

[Tahadhari kama wewe ni MHESHIMIWA : Lugha KATIKA TARALILA HII  inacheza KOMBOLELA!]


Kunawatanuao KITU,...
.... na ukifikiria katika watanuacho wanatakakuona nini cha ZAIDI waweza mpaka kugundua ni kwanini kuna walalao huku wamefumba MACHO lakini wanataka kuwe na taa inayowaka ingawa  wahitajicho katika kulala kwa kuwa hawahitaji kuona kitu ni GIZA.:-(



Na kama  nia ni utamu wa kitu,...
..... labda kuna vitu hata kama KITUMBUA  na MAANDAZI ambavyo havihitaji uvione vizuri ili kufaidi kwa kuwa labda utamu wake  kutokana na vinavyonukia tu ni tosha kusaidia mtu kuvifaidi vilevile kukiwa na MWANGA au tu GIZA.:-(

Swali:

  • Si unajua pia kuwa BINADAMU wengi  wakati wamelala WAKIPENDACHO ambacho ni KITAMU ZAIDI ni USINGIZI  kuliko wa mwingine uchi?
  • SI unakumbuka SURA YA EMBE  ni asilimia ndogo sana ya utamu wa EMBE hata kwenye mwanga?


Ndio,...
....kuna mengi ni mazuri tu GIZANI,...
..... na hata uzuri wa URAIS WA NYERERE kwa WATANZANIA kama tu UBAYA WAKE labda wala  hauhitaji kuwe na MWANGA ili  atafutaye KUMLAUMU aone kitu cha KULAUMU.:-(

Ndio,...
... na katika kuuchunguza hata uchi wa NYANI,....
...labda makunyanzi uyaonayo YALIYONUNA VIBAYA  kwa kumulika na tochi ndio asili ya utamu  wenyewe,....
.... ingawa kwa kumulika na kustukia makunyanzi wala HUONI hicho kitu UTAMU  kwa kuwa  kionekanacho saa nyingine  ni kama tu kwa asiyetaka kuona akiona  GIZA.:-(

Swali:
  • Si kuna waonao giza?
  • Unafikiri kwenye MWANGA huwa unaona nini kama  kujikwaa huwepo tu  kwa watu hata kwenye MWANGA?

NI wazo tu hili MHESHIMIWA!:-(

Hebu Peter Tosh aingilie na -No Sympathy




AU tu Peter Tosh arudie-Why MUST I cry



Au tu pia  Peter Tosh ajaribu kumalizia tu na-In my SONG



Au tu sasa Peter Tosh amalizie tu kabisa na ndude - The Poor Man Feel It

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP