Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Labda afadhali hakuna VITABU vya jinsi ya kuwa MCHAWI TANZANIA kwa kuwa vingekuwepo ambaye angekuwa MCHAWI mzuri kikukubuhu KATIKA UCHAWI WA KITANZANIA asingekuwa ni MTANZANIA.:-(

>> Wednesday, November 03, 2010

Yani kwa wenzetu hata ukitaka kuwa MCHAWI utakuta wameshakuandikia  pia  mpaka KITABU,.....
... wakati SIE hata kwenye DINI ZETU za kuiga kama za KIKRISTO na KIISLAMU ndani ya TANZANIA,...

....utakuta WENGI WETU tunategemea MAPADRE na MASHEKHE ndio watu somee yaliyopo kwenye hivyo vya DINI ZETU vitabu na pia kututafsiria maana ya vilivyoandikwa kwenye hivyo vitabu ili tuelewe angalau hata jambo kama hivi  MWANAMKE  sehemu yake ni ipi NYUMBANI , kitandani au  tu CHUMBANI.:-(


Swali:
  • Hivi  wachawi wa KIAFRIKA  kwanini wana siri hivyo?
  • Hivi unadhani katika mabloga wa TANZANIA hakuna aliye MCHAWI?


Ndio,...
.... bado inasemekana ukitaka kumficha MTU MWEUSI[Mmarekani mweusi incl. ] kitu,...
... ficha hicho kidude kwenye KITABU.


Ndio,...
.... nami nasema ukitaka MAHALI PAZURI pa kuficha pesa ili MWIZI wa PESA  wa KITANZANIA asizistukie wakati kaingia nyumbani mwako kukuibia MAPESA kitu,....
..... zifiche kwenye vitabu.:-(

Hebu cheki tena huyu MCHAWI akikueleza jinsi ya kujifunza aina ya uchawi aufuatao yeye.....


Au tumcheki KIGOLI huyu naye....




Ndio,....
..... najua mpo wasomaji VITABU wengi tu  WATANZANIA,....
.... ila swala hili bado ni  gumu sana  kwa wengi kitu ambacho ukilinganisha na WENZETU  si chakujivunia.:-(


Swali:
  • Hudhani kuwa labda ni KWELI wachawi wa KIAFRIKA hawaandiki vitabu kwa kuogopa watakao jua zaidi UCHAWI kwa kuwa ndio wasomaji wa vitabu watakuwa sio WAAFRIKA?


NAWAZA TU kwa sauti KINGUNGE na wala GHAFLA usibanwe chupi!:-(


Hebu tubadili hali ya hewa kwa kurudi Ivory coast ili MEIWAY adinye tu -DJ Tassouman



Meiway aingizie pia-Ma folie




Au tu MEIWAY amalizie tu na - Emeraude

3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Ney 11:53 am  

ha ha aaaaaaaa, imebidi nicheke tu maana unayowaza ni kweli kabisa, Lakini najiuliza kwanini wachawi wengi ni masikini? kwani hawawezi kujichawia wakawa na mafanikio? au wakajichawia wakapata elimu ya darasani kwa njia ya uchawi? Au uchawi ni kwaajili tu ya kuwafanya wengine wawe wanateseka kwa njia moja au nyingine? mmh

emu-three 12:31 pm  

Mhhh, na jana nilikua tangazo linasema `njia ya kupata utajiri, njia ya kurudisha nyota ya utajiri, na jinsi ya kumpata mpenzi...'
Sasa wameanza kuweka matangazo, manake wateja hakuna!
Mimi najiuliza kama mtu anaweza kusafiri kwa ungo usiku kwanini asiiboreshe hii ikatuondolea adha ya usafiri, au ni kwa vile nasikia wanasafiri wakiwa kama walivyozaliwa. Sio mbaya, mnachukua ungo mmoja,kila mmoja anaangalia sehemu nyingine, hakuna kuangaliana!

Simon Kitururu 1:48 am  

@Da Ney: Ndio hapooo!
@M3: Nilikuwa najaribu kuimajini wasafiri hao kwenye ungo ambao wanaogopa kuangaliana.:-)

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP