Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

KHERI ya MWAKA MPYA kwa waislamu wote!

>> Thursday, November 15, 2012

Nawatakieni AL -HIJRA (1434 H.) Njema!

PAMOJA sana!

Read more...

RAIS anapolia!

>> Saturday, November 10, 2012





Read more...

Na kwa SABABU!

>> Thursday, November 08, 2012

Na SABABU,...
... mara NYINGI,...
...ni za KUJITAFUTIA sababu TU!:-(



Swali:

  • AU?


Ni wazo tu hili NGULI!

Read more...

MWISHO wa dansi hata DANSA mzuri hutoka STEJINI!

Na  hata MLAJI mzuri PILAU ,...
... aking'ang'ania KULA   sana kisa  eti PILAU ni tamu,....
....LABDA atafanikiwa zaidi ya KUVIMBIWA....
....kiusumbufu ambao sio uletao tu CHOO kwa MHESHIMIWA!!!

Swali :

  • AU?


Na hata alaye sana kisa chakula ni KITAMU,...
... kuna kipimo chake tu ambacho atafikia  ambacho TAMUTAMU kunoga hugeuka BUGHUDHA!


Swali:

  • AU?
Ndio,....
....hata kama unajua KUNENGUA kinamnagani,...
... mwisho wa siku KUNENGUA sio starehe,...
... kama tu ulivyo utamu wa UCHI ukizidishiwa kupewa!

Ni hilo tu,...
... na ni WAZO tu hili MHESHIMIWA!

Nipo lakini...:-(






Hebu Dr Dre arudie kukumbusha I have been there..and DONE THAT

   


 Halafu sijui kwanini ila Gregory Isaacs ngojea aje tu TENA  fulu....


 

Read more...

LABDA.....

>> Sunday, November 04, 2012

...kwa asiyepotezaye MUDA sasa hivi,... 
...labda HUYO muda wake WAJA kiwakatiwa BAADAYE  tu!:-( 


 Swali: 

  • Si labda hupotezi MUDA kwa kunisoma KIUJINGA busara zangu ki WAKATI huu TU?:-( 
  •  NA si asiyepoteza MUDA sasa hivi labda WAKATI wake waja  tu akimaliza SWALA ,..... na kula,.... na mambo yake ahisiyo ni MUHIMU ? 



 Na WAKATI tuna poteza MUDA,...
 .....kuna mengi labda ni LABDA tu kwa kuwa MUDA haupotei,...
...LABDA!!:-(


 Na ni wazo tu hili NGULI!
Na nakutakia siku KIBONGE aisee MHESHIMIWA!


Hebu GARNET SILK aingilie kati.....







Ndio,...
...NIPO aisee!:-(










Read more...

Wakati NJEMBA inahangaikia KUJUA ambayo hayatamsaidia KITU !

>> Friday, November 02, 2012

Wakati MTU anahangaikia KUJUA yasiyomsaidia ,...

.... kuna uwezekano,...
...yahangaikiwayo sana ndiyo YASIYO na MSAADA sana kwa MTU!

Swali:

  • AU?
  • SI kuna UWEZEKANO kwa kuangaikia kujua sana BAADHI ya vitu ndio sababu kubwa ya MTU kuruka kujua MENGINE hata ki ni kiainagani kwake ni MSAADA?



  • Na si KUNA UWEZEKANO asilimia KUBWA ya usiyoyahangaikia NDIO yakuwekayo sawa leo hii hata weye bila KUJUA?


Ndio,...
.... LABDA mengi yakuvutiayo kama tu  UTAKAYO SANA  kuyajua,...
.....kama tu yale yapewayo umuhimu kama UZURI wa MAPAJA kwa mpenda mapaja  ambaye  ahitajicho KIMALENGO  ni mtu apate UJAUZITO,...
....labda MICHANGO yake ni DHAIFU kiumuhimu wa ili MALENGO ya mimba yatimilike,...
... na hapa siongelei tu yale malengo ya ili mtu apate mimba ambapo labda paja halihusiki kihivyo kuliko sehemu za siri na viungo vyake vya uzazi ambavyo si makalio wala paja,....
..... au tu KAMA nguo za mtu safi akiwa na BIBLIA au KORANI yake KANISANI au MSKITINI vilivyo DHAIFU kama  roho na ya kiroho HAYAJAANDALIWA kupokea ufunuo wa ya yakiroho ili ya KIROHO yatimilike.

Swali:

  • SI unajua labda kuipa kipaumbele  BIBLIA au KORANI hata kwa MKRISTO au MUISLAMU  bila kuandaa ukunjufu wa MOYO labda ni kujiangaisha kujua ambayo mwisho wa siku hayatamsaidia muungwana katika swala zima la kuweza kuifikia  MBINGUNI kwa kuikodolea macho ?


Ndio,...
.... labda kuna vigezo vitusababishavyo kujikuta kuna mambo twayapa KIPAUMBELE katika kutaka kuyajua,...
... na hapa siongelei tu yale ambayo hayatusaidii KITU kama YALE ya kutaka kujua :

  • Hivi  sijui SIMON KITURURU katukana tena hadharani LEO kimaandishi?
  • Hivi sijui ni kweli MKE wa Mheshimiwa matako yake ni ya fulu Mchina kama NYONYO zilivyo?
  • Hivi sijui Rais Kikwete ananunuliaga wapi chupi?
  • Hivi fulani kala nini?

... au tu yale MENGINE mengi ambayo kwa kweli HAYATUSAIDII zaidi ya kutupotezea MUDA.

Ila swali:


  • Hivi unadhani MTU anaweza kupoteza MUDA kweli?
  • Si asiyepoteza Muda SASA hivi ,huyo atapoteza tu  MUDA BAAADAYE wakati wake ukifika?
  • Kwani unafikiri asiyepoteza MUDA anafanya nini la maana ambalo lamfanya kila MUDA afanyalo LIWE ni la MAANA TU na halipotezi muda wa huyohuyo kufanya jambo jingine MUHIMU zaidi?


Ndio,...
.... labda wakati jamaa linahangaika KUJUA,...
.....lapoteza MUDA wa kulala au hata NGONO ambayo kwa wakati huo ingekuwa na UMUHIMU wake zaidi kuliko KUSOLVU mahesabu ambayo kwa BIASHARA yake ya NGURUKA hayatamsaidia kitu katika KUUJAZA ulimwengu ,...
..au hata  wala haitamtuliza mawazo kipumziko liletwalo na KULALA.:-(

Ni wazo tu hili MHESHIMIWA na ni RUKSA kutolielewa!!
Nakutakia SIKU MWANANA sana tu AISEE!

Hebu Arrested Development warudishe-Everyday People





 Arrested Development waongeze kidogo dozi kwa- Mr. Wendal

 


 Ghafla Mark Morrison aingilie kati kwa - Return of the Mack

 



 Planet Digable wajaribu kuzima kwa-Rebirth Of Slick (Cool Like Dat)

 


Halafu Genuwine ndio azime kwa- PONY

 

Read more...

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP