Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Hebu tupitie HANDENI kule KWETU!

>> Friday, September 30, 2011
Ndio,...
... twende  HANDENI  KWETU ,....
.....kama iwakilishwavyo na  Kambi Mbwana,..
... hasa kama muda WAKO unaruhusu kwa kubofya kiwanzabanga;.....
.........  HAPA

Read more...

Tupendao TWADANGANYWA kirahisi na MPENZI!

Na yasemekana MPENZI  husikilizwa kirahisi,....
...... hata kama  kisemwacho ni UONGO,...
.... kisa KAPENDA!


Swali:
 • Si adui yasemekana haaminiki  hata katika yasiyoadui kirahisi kisa ni ADUI?Na kwa MPENDWA,....
...... labda tumia nafasi hiyo kutodanganya,...
.... kwa kuwa katika ndege wawili wafao kwa jiwe MOJA wewe waweza UA elfu ,...
... ikiwa ni mpaka ROHO ya akupendaye!:-(

Ni wazo tu hili MKUU!:-(


Blaq Poet aanzishe upya kwa kurudia - Ain't Nuttin' Changed


Blaq Poet aje na N.O.R.E. walime - HateN.O.R.E. wabaki peke yao katika - Nothin'Erick Sermon na Redman wa- React
Pharoahe Monch azime kwa - Simon SaysNdio,...
....tuendelee tu na SIKU Mkuu!

Read more...

DANGANYA watoto kama wewe ni BONGE la MZAZI kiuleaji toto hata ambalo litakuja kuwa KUBWA kititi!

Haitabishwa  kuwa,...
.... yasemekana kuna  ya UKWELI ,...
.... kwa watoto yasemekana yachubua  zaidi ya MAWAZO,...
.... ya kikubwa MAWAZO yakiwekwa UCHI!:-(

Swali:
 • Si uongo ni kitu kibaya?
 • Lakini si kuwaambia ukweli watoto  MAMA katoa wapi mtoto ni MATUSI?
 • Na si labda ulidanganywa katika MAKUZI yako na ndio maana bado kuna MAUONGO kwako bado ni KWELI?KUDANGANYA watoto,...
... yasemekana ni moja ya staili YENYE MAFANIKIO SANA ,...
......katika  KULEA WATOTO vizuri!

Tunakumbushana tu KITU hapa MHESHIMIWA,...
... katika WAZO  hata kama hakuna USAHIHI kichokozi!:-(

Hebu ETTA JAMES aanzishe upya kwa-At lastSijui kwanini ila ngojea arudie,..BB KING, Billy Ocean, Stevie Ray Vaughan ,... na Etta James waendeleze kwa-Midnight Hour
Halafu BB King, Eric Clapton,Buddy Guy,...
......na Jim Vaughn wamalizie tu kwa-Rock Me Baby

Read more...

Katika INJILI si kuna adanganyaye?

Kwa jinsi  MAKANISA yazidivyo kuwa MENGI,...
.... hata tukaneje lazima kuna adanganywaye.:-(

Swali:
 • Kwani unafikiri  kila adaiye anahubiri MUNGU ni mkweli?
 • Ushawahi  kudakwa kona na kushushiwa mahubiri matamu na watu ambao unamashaka  wamekaa kitapeli?

Ndio,...
... leo nilidakwa kona na kupewa bonge la MAHUBIRI na wajanja,...
.... na cha ajabu waliyokuwa wanaongea  yalikuwa yanaleta MAANA kitu kifanyacho mtu ujiulize  ni NANI sahihi  kusikiliza kutoka kwake yaliyo SAHIHI!:-(

Swali:
 • Kwani  si muongo huwa hadanganyi kila wakati?
Ndio,...
.... siku hizi,...
... kama zamani tu,...
.....DINI ni BIASHARA!

Bado natafakari  niliyoshushiwa KIMAHUBIRI,...
.... ambayo yanagusa kama tu nisingekuwa fulu MACHALE!:-(Hebu KIDDUS I ajaribu kupindisha kwa - GRADUATION IN ZION

Au tu J Dilla aendelee kwa-Believe In GodHalafu The Roots wazime kwa - Dear God 2.0


Read more...

Maisha ya Frank HumplickFrank Humplick ni mwanamuziki ambaye pamoja na kuwa alipiga nyimbo zake miaka ya 50 , bado nyimbo zake zinapendwa hadi leo. Wangapi hawaujui wimbo kama Embe dodo imelala mchangani,?

Msome misha yake hapa:Nimepigiwa krosi hii na
John Kitime wa :

Read more...

Vituko vya baadhi ya wanamuziki wetu wakiwa nje ya nchi

Vituko ughaibuni....wanamuziki wetu wakienda ughaibuni wanapoteza bahati  muhimu ambazo hutokea mara moja tu moja, hebu angalia hapa:

--

Nimepigiwa krosi na:
John KITIME wa:

Read more...

KAPINGAZ DADAZ!! NDANI YA MSASANI BEACH CLUB USIKU HUU!

Wadada wa KAPINGAZ Blog ndani ya sherehe ya kumpongeza Dada Rehema kwa kufanya maamuzi mazuri ya kuolewa.
Sherehe hiyo ilifanyika leo usiku katika ukumbi wa Msasani Beach Club.

Mmependezaa!!


Nimetumiwa na Henry Kapinga,...
...... wa KAPINGAZ blog

Read more...

KIINGILISH Pliiz!


Deku mpindo,....
... kama umekaa mkao wa kuchungulia kinafasi/muda....

Nimeidaka ,...

Ijumaa na WIKIENDI njema MHESHIMIWA!

Read more...

Amkabiliye ADUI labda kashastukia ANAWEZA huyo!

Na mkabili ADUI kama UNAWEZA,.....
........ na mzidi akili kama yawezekana!

Swali:
 • Na kwa kutumia AKILI si adui yoyote anakabilika?

Nawatakia kila lakheri,...
.... wote wakabilianao na KITU,...
......hasa ukizingatia  labda ni KILA mtu hapa DUNIANI!

NI hilo tu !

Hebu Zahara aanzishe upya kwa - LoliweCurtis Mayfield aingilie kati tena kwa - PushermanThe Notorious B.I.G. arudie matusi katika - One More Chance
Au tu azime tena kwa -Big Poppa


Read more...

Wakati tamutamu na CHUNGU za ipatikanavyo na kuondoka MIMBA YA JAMBO -kuna wadaio ziko kwenye VITENDO!!

 Kuna waumizwao wengi na MANENO,....
......kisa neno ndio lilizalisha KITENDO  cha hiari! Swali:
 • Kwani ni nani KIVITENDO ambaye  HATASHITAKI UMEKARIBIAKUBAKA  au  kwa kuguswa  atanyegeleshwa?
Na kuna wenye mtazamo huo wa kudharau NENO ,...
... kisa wanadai wanajua tamutamu mpaka za MIMBA zina vitendo,...
....ingawa kwa VITENDO  bado kuna MANENO yalionyegelesha  FUNDI akawa FUNDI kivitendo hata kama  wakati huo neno la MWALIMU lilikuwa  SHENZI!:-(


Swali:
 • Si yasemekana kuna wadaio WAVIVU ni wavivu wa VITENDO kama vite hakuna wazembeao kivivu kwa MANENO hata kama neno lenyewe ni la MUNGU liokoalo au tu lile likemealo maovu  ambalo lategemewa kutoka kwa wadaiwao ni watu wazuri  hata kama si wazuri kikutongozwa?


Ndio,...
.... hapo MWANZo kabla ya KITENDO,...
.... labda kulikuwa na NENO,...
... nalo neno hata kipumbavu ,...
.... yawezekana ndio siri ya MIMBA ya KITENDO!:-(
NI wazo tu hili BINGWA!


  Hebu Daniel Beaty amwage NENO katika - Knock Knock  Shihan arudie NENO katika - Sick and Tired  Black ICE aongelee NENO katika neno kwenye-Bigger Than Mine  Mutabaruka akatizie denge kwa - Dis Poem

  Mutabaruka aongezee dozi kwa - Any which way... FREEDOM
  MUTABARUKA arudie - Whey Mi Belang?
  Au tu ngojea azime tu kwa -DISPEL the LIE


  Read more...

  Siri ya aanzaye KUTOMASATOMASA,..

  >> Thursday, September 29, 2011

  ... labda huyo anajua tayari KITU,...
  ... na katika hicho KITU  anajua kuwa kuna  MBIVU na mbichi kimtekenyo,..
  ... na  KWA HILO labda wala sio siri HUYO anajua mpaka kuna KUTOMASA katika mbinu ya  kujua ni ipi IMEIVA kwa kuwa hiyo itabonyezeka kititi!:-(


  Swali:
  • SI  unajua  AJISIKIAYE ni mwenye tatizo kwa kuwa HANA  sabuni  katika KUFUA huyo anajua tayari  kuna kitu huitwa SABUNI  na HIYO  inawezesha kirahisi kuondoa uchafu kwenye nguo  kama isaidiavyo tu baadhi ya vidume kujichua ili kuondoa maungoni kitu?

  Ndio,...
  .... labda usilolijua ,...
  ....HILO sio tatizo lako !:-(
  Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!


  Hebu BUJU BANTON aingilie kati kwa kudai-Make My Day  Au tu huyuhuyu Buju Banton ajaribu kuzima manyanga kwa - Wanna Be Loved
  Au turudi tu TANZANIA ili NGWAIR afunge breki na kuamishia wazo kwenye -MIKASI  Read more...

  Tatizo la FASHENI ni zamuzamu!

  Na haki ya nani kama sasa hivi wewe ni BABU KUBWA,...
  ....  kuna wadaio KUBALI kuhesabu tu  muda ,...
  ....  kwa kuwa umzarauye na uyazarauyo huweza kuwa ndio kifasheni yana tako KUBWA hata kifasheni za  mbilimbi!:-(

  Swali:
  • Kwani hukumbuki wapendayo watu KIJUUJUU kama lebo ya CHUPI kwa kuwa ni GUCCI  pendo lao ni kijuujuuu?
  • SI unakumbuka kuwa hata  kwa wapendao  TTII KUBWA na TITI DOGO kwa wapendao watu kijuujuu ni zamuzamu na litapendwa lililo kwenye fasheni  hata kama  HOTELI YA MTOTO sio saa sita?

  Ndio,...
  ... kipengele  kitamu sasa hivi KIFASHENI  kwa kuongezewa SUKARI,...
  ... baadaye hichohicho ni  kwa nyanya , kitunguu , chumvi na PILIPILI inaweza kuwa ndio siri ya wajanja walewale KUDAI WANANOGEWA  na ni wale waliokuwa wanakisifia kisukari TU ndio siri ya TAMUKUNOGA ya  hicho KIDUDE!:-(

  Ni wazo tu hili MKUU!:-(


  Hebu Amy Winehouse akatizie denge na kunisemea - You Know I'm No Good
  Sting aingilie kati kwa - FRAGILE  STING ajaribbu kuzima kwa-Englishman In New York
  Au tu Shinehead ndio azime kwa -Jamaican in New York

  Read more...

  Yasemekana MUDA kiboko,....

  ...na  haki ya nani YADAIWA  hata UWAOGOPAO muda ukirihusu,.....
  ... WATAFIKIA unyonge ,..
  ... na wenye NGUVU ndio watakuwa kona kukuombao MSAADA mnyonge!


  Swali:
  • Kwani huna subira?

  Ndio,...
  ..... subiria utaona,...
  ...ujanja hata kwa mjanja YASEMEKANA una TAIMINGI ZAKE na taimingi ZENYEWE sio milele,...
  ... na ndio maana baada ya Rais NYERERE pale TANZANIA ,...
  ....kulikuwa mpaka na MWINYI!:-(

  LABDA ni wazo tu hili MHESHIMIWA!:-(

  Hebu Erykah Badu aanzishe upya kwa-KISS ME  Erykah Badu aaongezee dozi kwa - Didn't Cha Know  Au tu Macy Gray aingilie kati kwa - I Try

  Read more...

  KASEBA na MTAMBO WA GONGO wakumbushwa sheria.
  Mabondia Japhert Kaseba (kushoto) na Maneno Osward (Mtambo wa Gongo)wakitunishiana misuli walipokutana, Dar es salaam leo kukumbushwa sheria mbalimbali zitakazotumika katika mpambano wao utakaofanyika jumamosi hii .
  Katikati ni Katibu, wa Chama cha mchezo wa ngumi kinachosimamia mpambano huo. PST. Anton Lutta
  (Picha na habari  www.superdboxingcoach.blogspot.com)


   (SUPER D)
  DIRECTOR
  www.burudan.blogspot.com
  BURUDANI MWANZO MWISHO
  P.O Box 15493
  DAR ES SALAAM

  Phone no. 0713/0754/0787/0774/ 406938  --

  Super D Boxing Coach
  Photojournalist at Majira, Business Times
          +255774406938
          Po.Box. 15493
  Dar es Salaam Tanzania  Nimetumiwa na :
  RAJABU MHAMILA( SUPER D)

  Read more...

  Labda UNAPENDWA jamani KIJEBA kama tu apendwavyo KIGOLI!

  Na kumbuka tu akikosea  vyanzo vya sifa MTU ,...
  .... anaweza kukonda kwa kufikiria HAPENDWI,.... 
  ... kisa ni mpenda MCHICHA na wakati huo yuko kwa Wazee wa KITIMOTO.:-(

  Swali:
  • Si unajua kila mtu katika apendacho -NI ukorofi  KIKUKOROKOCHOA kabisa kitu fulani kwa mtu fulani MWINGINE ?
  • Na si kama unapendwa na MAMA yako  labda huo ni ushahidi wapendayo apendayo MAMA YAKO wanakupenda pia  na kwa kuwa wao sio MAMA YAKO labda ni ruksa wakupendavyo uchi kiutuuzima?

  Ndio LABDA  unapendwa,...
  ... na kama  hujiamini halafu  unang'anga'ania au tu uko kwa wasiohusudu yako,...
  .... unaweza kuamini pia kuwa YAKO HAYALIPI na HUPENDWI,...
  ... kitu ambacho huweza kuwa ni ``SHAURI ZAKO aisee!´´:-(

  Ni wazo tu hili MHESHIMIWA,...
  .......unayependwa na usiostukia PENDO LAO!:-(

  Hebu Dj Nkoh aanzishe upya kwa kupindisha kwa- Zulu Love Letter  Dj Nkoh ajaribu kuongezea pia ujazo kwa - Kabishi  Au tu Yvonne Chaka Chaka abadili zaidi tena kwa - Thank You Mr DJ  Halafu azime tu kwa -Motherland

  Read more...

  SI kila avaaye chupi kichwani ni KICHAA kwa HATA WALE wafikiriao CHUPI ni mali ya TAKO ,...

  .... kama tu ilivyokuwa si kila avaaye joho la KIPADRE  ni PADRE,...
  .... kwa kuwa kama ilivyo UKICHAA ni utovu wa akili KIKICHWA kwa wafikiriao KICHAA HATUMII AKILI  ambayo  HATA ILE inamsaidiayo kuweka KIFICHA NYETI KICHWANI ,...
  ....labda hata UPADRE uko moyoni na sio kwa JOHO LIKO WAPI  kwa  aliyevaa joho hata  KIASKOFU,...
  ....  wakati huyo BADO,...
  ......hasa kwa kuwa kuna uwezekano JOHO  lake  ,...
  ... ni  KWA KUWA ni kirahisisha kutembea bila CHUPI kiheshima kwake!:-(

  Swali:
  • Si  unajua  UGALI labda ni jina tu na ndio maana unga wa MIHOGO mpaka mahindi  moja ya tengenezo LAO  tofauti kutokana na MALIGHAFI tofauti vyote huitwa UGALI?
  • Unafikiri  UNGA wa MUHOGO na UNGA wa MAHINDI vyote hutengeneza UGALI au tumekosa MAJINA?

  Ndio,...
  ...... kuna tabia yakutoita SEPETO ni SEPETO katika jamii,...
  ... nawa kati SEPETO inaitwa SEPETO  kutoangalia undani wake kama idhaniwavyo kichaa ni KICHAA,...
  .... kitu  kiwezachofanya UMALAYA  na  roho nzuri KIUGAWAJI kuwa ni kitu kilekile KWA MTU  kisa kwa agawiwaye na malaya mwenye roho mbaya,...
  .... bado MALAYA huyo kwa kugawa ana roho nzuri kwa apimaye ROHO NZURI  kwa UGAWAJI wa VIKATALIWAVYO NA WENYENAVYO hata kama  safarihii KIPIMO cha roho nzuri ya yenye kipimo KUGAWIWA  inapimwa kwa  kipimo cha spidi ya kupanuliwa ZAWADI  ile ya LAWALAWA nyama!:-(

  Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!:-(
  Hebu JUDY BOUCHER aanzishe kwa -That Night We Met  Judy Boucher aongezee dozi kwa - Can't Be With You Tonight  Halafu siju kwanini ila turudi KENYA ili ghafla Eric Wainaina tena abadili kwa -Dunia Ina Mambo


  Halafu hapahapa KENYA yule Chizi na Eric Wainaina wazime manyanga kwa - Wacha Waseme

  Read more...

  Wakati RAFIKI akufaaye kwenye STAREHE ili ustarehe kwenye STAREHE , kwa wengine ndiye RAFIKI,...

  ....bado labda KUNA KAUKWELI  kuwa  urafiki ukirahisishwa,...
  ....waweza kukuta AJINYEAYE  mwenye kuhitaji KUCHAMBWA  huyo  hana rafiki hata kwenye MARAFIKI!:-(

  Swali:
  • Si unajua URAFIKI  ni  noma  kwa kuwa  rafiki  ya mtu LABDA  ushahidi NI  kitu  na kitu chenyewe  inaweza kuwa ni kuficha  siri ya kikojozi KWA KUWA NI RAFIKI  kwa wachukiao vikojozi?

  Ndio ,...
  ... haki ya nani tena kuna wasahauo MARAFIKI kwa kuwa ,...
  ... kuna wanaowafikiria ni MARAFIKI ambao vikibumbuluka hao ni fulu kukimbia MTU kiadui au tu ki -SIKUJUI WEYE!:-(

  Ni wazo tu hili hata kama lina KIBIONGO!:-(

  Hebu Harry Kimani aanzishe kwa -Haiya
  Harry Kimani aongezee kinu - Man From the Ghetto  AU Bob Marley na GURU wajaribu kubadili mchezo kwa -John was  Au BOB MARLEY azime tu mkuno kwa-Stiff necked fools

  Read more...

  Katika swala la usichague MSICHANA kwa SURA NZURI wakati kashajiremba KIMSHEBEDUO!.

  >> Wednesday, September 28, 2011

  Ndio ,..
  ... yasemekana kwenye SIKUKUU  labda kila msichana ni MREMBO,...

  .... sababu KUU ni  kwa kuwa KASHAJIREMBA,...
  ......  hasa kwa kuwa yasemekana SURA YAKE  sio uionayo ,...
  .... kwa kuwa SURA yake KIKWELI  iko chini ya VIPODOZI!:-(


  Swali:
  •  Si hapa unajua nimeruka MORANI wa KIMASAI?
  • Si bado nasikia kwa MIDUME lukuki MWANAMKE MZURI ni SURA NZURI  TU ile yenye kushikiliwa na BONGE la KICHWA kwenye  mwili wenye KIFUA chakutosha kimatiti , tako  ujazo wakutosha na  bila kusahau bonge la usafiri kimiguu yenye paja  mwanana- NA wala uzuri  sio TABIA?

  Na siri ya kujua sura halisi ya WAREMBO wa siku hizi ambao ni fulu kujipodoa,...
  ....KUNAWASHAHURIO  mchungulie KIMWANA  asubuhi akiamka tu  wakati bado ananuka mdomo kwa kuwa bado hajaenda maliwatoni kujipodoa hata ndani ya MDOMO !:-(


  Swali:
  • Hivi  si nasikia yasemekana kuna VIMWANA wazuri ambao kujipodoa ndiko kwawafanya waonekane vituko?
  Samahani ni UCHOKOZI tu HUU Mwayego,...
  ... na wala usikonde  kama unajipodoa kwa kuwa ,...
  ... urembo U-jichoni mwa MTU  na kama unafikiria kwa  kujiremba kwa KUNYOA NYUSI za juu na CHINI au  hata kwa KUJICHUBUA unapendeza,...
  .... basi wewe unapendeza KIGOLI  kwa kuwa MAISHA ni YAKO na JICHO ni lako wengine kama akina Simon Kitururu kwa kimbelembele chao wakidai umekaa ki sura FANTA -mwili COCACOLA  yako hayawahusu na WAKUKOME kabisaa na kimbelembele chao! 

  Msuto kidogo kwa akereketwaye na kujiremba kwa mwingine :
  • LOH! Yani watuwengine bwana ,pilipili iko shamba  kibarazani kwa shoga sijui yawawashia nini?

  NIMEACHA taralila hii ILIYOPINDA!


  Moja kwa moja hebu tuangalie mwanadada  KOKO  ,...
  ...akitoa  moja ya siri katika  KUJIPODOA SURA  kwa AKINADADA katika  kusaidiao hata waopoao demu DISCO KISA ANA SURA NZURI ,...
  ...nini KILIFANYA  asubuhi hawana uhakika kuwa  kigoli aliyepo kitandani ni yuleyule aliyeopolewa KLABU usiku  kwa ajili ya dhambi ya chapuchapu ya ZINAA ,....

  ...katika :Foundation Tut/Review: feat Mac Match Master Foundation


  Read more...

  Mficha uchi HAZAI,...

  ... na kwa bahati mbaya tatizo hilo humpata pia MFICHA ujinga ,....
  ...... kwa kufanya kuna  heri  KIUELEWAJI hazitatotolewa kwa HUYO kwa kuwa,...
  ...MJINGA kaficha UJINGA hata kama sio chupini!:-(

  Swali:
  • AU?
  • Na si unajua kuna UHURU ujao na kuweka jambo WAZI? 
  • Ndio  mimi ni mjinga na nafikiri nina dhambi-WEWE je?
  Ndio,...
  ....ukificha GONO  ili mtu mwingine hata kama ndiye DAKITARI asijue,...
  ... unaweza kukatika kidude au harufu ikaumbua kwa kuwa nanihii inamchezo wa kuoza hata kama imefichwa chini ya GWAGURO safi na la bei MBAYA!:-(


  Tunakumbushana  ki-UjingaBUSARA tu hapa   MHESHIMIWA!
  Jumatano NJEMA!

  Hebu Upendo NKONE alete injili kidogo kwa-Usifurahi juu yangu


  Tupitie kiduchu Pakistani na kumbushwa ya ALLAH na SAIN ZAHOOR AHMED katika kibao kizito-Allah Hoo  HALAFU  turudi tu BENIN ili mwanadada RAMOU abadili  MCHEZO MZIMA na kuweka mnuso live kwenye -Wen Vive  Na hapahapa BENIN hebu  Zeynab aingilie na kumalizia hii sesheni kwa kudinya - Aye Le

  Read more...

  WASIMAMIZI WA HAKI ZA WANYAMA MPO WAPI?

  Mganga wa Kienyeji Maarufu kama Dr Manyaunyau.
  Vijana hawa wakiwa Bara barani wakimzungusha huyu Mnyama aina ya Paka, kwa akili zao wakiamini wamemshika mchawi na wameamua kumsulubisha.
   
   
   
  Vitendo hivi vya kikatili kwa wanyama vimekuwa vikiendelea mara kwa mara hasa katika maeneo ambayo yana mrundikano wa makazi ya watu, na hata vingine vikionyeshwa kwenye luninga zetu lakini wahusika wa haki za wanyama wakivitazama tu vikiendelea bila kuvikemea wala kuwachukulia hatua wale wote wanaoshiriki kufanya vitendo hivi.


  Kwa mataifa ya wenzetu ni lazima upate hukumu ya kifungo kwa kufanya vitendo hivi.

  KAPINGAZ Blog inawaomba wahusika waweze kutimiza majukumu yao na ikiwezekana wawachukulie hatua hawa wote wanaoshiriki kufanya vitendo hivi.
   
   
  Nimetumiwa na :
  Henry Kapinga wa KAPINGAZ blog

  Read more...

  Uliza halafu kaa KIMYA usikilize JIBU,...  ... kwa kuwa inasemekana ni wachache sana WAULIZAO,....
  ....hujifunza kitu wakati wao wenyewe wakati huo WANAONGEA!:-(

  Swali:
  • SI inasemekana wakati mtu anaongea ni machache sana WAKATI HUO huwa  anajifunza kutoka kwa wengine?
  • Unafikiri  wakati unaongea yawengine wakuongeleshao unajifunza?
  • Unafikiri wakati unaongea kuna jipya unajifunza?
  • Unafikiri wakati unaongea huwa UNASIKILIZA vizuri?

  Ndio,..
  ... labda kaa kimya,...
  ..... wakati unaSIKILIZA!

  Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!:-(

  Hebu twende Mauritius ili MICHEL LEGRIS aanzishe kwa-Mo Capitaine  Tubaki hapahapa Mauritius ili Michel Legris aongezee dozi kwa-Dalma Dalma  Hapahapa Mauritius , Monaster waachie-Mo Fam Lo Téléfon  Au mhasisi wa muziki wa sega ya kisasa Mauritius huyu Ti Frere aamalizie tu kwa - Papitou  Halafu tupitie tu REUNION ili Toulou wazime kwa-Doudou cherie


  Read more...

  Ya DUNIA: TOTO la KIUME likijisikia ni SICHANA na SICHANA likijisikia ni DUME!

  >> Tuesday, September 27, 2011

  Haya WAZAZI,....
  .... deku...


  Swali:
  • Si nasikia toto la kiume likilegealegea kike BONGo  dawa iaminikayo ni kulichapa VIBOKO, kufinywa kwa sana na bila kusahau adhabu na kudhalilishwa?:-(

  Tuendelee,...

  Hongera zenu wote WAZAZI mliofanikiwa kulea WATOTO kisahihi!
  Ni  angalizo tu hili MUUNGWANA!

  Read more...

  MATESO yakibadilishwa JINA,...

  .... kama tu kurushwa kichurachura kukiitwa ni MAZOEZI,....
  .... kuna wayazoeayo kwa JINA JINGINE!

   Swali:
  • SI MATESO ili yasikiliziwe kimateso inabidi ATESWAYE ayatambue kwanza kuwa afanyiwacho ni KUTESWA? 
  • SI kushinda na NJAA kukiitwa ni KUFUNGA kuna wafarijikao kirahisi kwa kujitakia wenyewe  kutokula ?

  Ndio,...
  .... hata ugumu wa KITU ,...
  .... ukipewa maana tofauti hata kama jina ni lilelile kuna wafarijikao na MAANA ya magumu  kwa kuamini mchango wa hayo kwenye MAANA YA MAISHA yao kitu ambacho huweza kufanya watu wajiingize kwenye MAGUMU hata kwa kupenda wenyewe!

  NI wazo tu hili tena dhaifu  MKUU!

  Hebu KIDUM aanzishe upya kwa-MAPENZI


  Chiddy Bang wabadili kwa - Opposite Of Adults  Chiddy Bang waongezee - Dream Chasin'  Au tu Mad Lion aharibu tena kwa kuihamisha tena kwa - Take it Easy


  Read more...

  MBWANA na MIYAYUSHO watambulisha MPAMBANO WAO.  Bondia Fransic Miyayusho (kushoto) na Mbwana Matumla (kulia) wakitunishiana misuli wakati wa utambulisho wa mpambano wao wa ubingwa wa Mabara (UBO) Dar es Salaam , utakaofanyika mwishoni mwa mezi ujao .

  Katikati ni mratibu, Mohamed Bawazir.
  (SUPER D)
  DIRECTOR
  BURUDANI MWANZO MWISHO
  P.O Box 15493
  DAR ES SALAAM

  Phone no. 0713/0754/0787/0774/ 406938


  --
  Super D Boxing Coach
  Photojournalist at Majira, Business Times
          +255774406938
          Po.Box. 15493
  Dar es Salaam Tanzania


  Nimetumiwa na;...
  ....RAJABU MHAMILA(SUPER D)

  Read more...

  BALOZI WA BRAZIL NCHINI, ASHAURI MBINU ZA KUWEZESHA WANANCHI KUISHI MAISHA BORA

  Mh. Balozi katika picha ya pamoja na Mhariri Mkuu wa habari wa MO BLOG Jennifer Sumi  baada ya mahojiano maalum kuhusiana na ziara ya Waziri Mkuu nchini Brazil

  Balozi Luz akifafanua jambo wakati wa mahojiano na MO BLOG.


  Pichani ni Balozi wa Brazil nchini Mh. Francisco Luz.


  Balozi Luz katika mahojiano na MO BLOG ofisini kwake jijini Dar es Salaam


  Na.Mwandishi wetu

  Balozi wa Brazil nchini Tanzania Bw. Fransisco Luz amesema, Serikali ya Tanzania imebarikiwa kuwa na rasilimali nyingi kwa upana wake ila inahitajika  kufanya kazi ya ziada kuhakikisha inatengeneza  nafasi nyingi za rasilimali watu ambalo ndilo tatizo kubwa linalopelekea nchi kuyumba kiuchumi na wananchi wake wengi kuendelea kuwa maskini.

  Balozi Huyo aliyasema hayo katika mahojiano maalum yaliyofanyika kwenye ofisi za Balozi huyo zilizopo maeneo ya Oysterbay jijini Dar es salaam na Timu ya Moblog, wakati  mwandishi wa habari hii alipotaka kufahamu maandalizi ya ziara ya kikazi ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda , anayetarajiwa kufanya ziara ya siku SITA Nchini BRAZIL kuanzia mwanzoni mwa Mwezi ujao.

  Balozi LUZ alisema, Kutokana na nchi ya Tanzania kuwa na Rasilimali nyingi akitolea mfano GESI ya ASILI,Makaa ya Mawe na Mafuta  ambayo yako katika mchakato wa kutafutwa kupitia  kampuni kutoka nchini Brazil,  katika maeneo ya bahari ya hindi, Tanzania itaweza kufanikiwa kwa  kiwango cha juu katika kukuza  uchumi wake pamoja na kuwawezesha wakulima wadogo wadogo ambao ndiyo wainua uchumi wa nchi.

  Amesema, Nchi nyingi  zilizoendelea  hivi karibuni zmeionyesha nia ya kuja kuwekeza nchini Tanzania  kutokana na ukweli kuwa kuna nafasi nyingi za kufanya hivyo katika maeneo ya Nishati, lakini kinachokwamisha ni suala la NISHATI na Miundo mbinu ambalo limekuwa ndiyo changamoto kubwa katika kuwezesha hilo na limeendelea kukua siku hadi siku.

  Aidha Balozi LUZ akizungumzia nchi yake ya Brazil ambayo awali ilikuwa ikikabiliwa na tatizo la kiuchumi na sasa kuibuka kuwa Taifa linaloibukia kiuchumi pamoja na nchi za BRICS,Alisema kuwa, Awali kila kitu kilikuwa mikononi mwa serikali na hivyo kusababisha mambo mengi kutoenda sawa lakini baadaye wapenda maendeleo walikaa na kuamua kuweka mpango uliwezesha kuwainua watu wa daraja la kati ambao ni wengi kwa kuwapatia msaada wa pesa na kuwasaidia familia maskini .

  Akizungumzia suala la Rasilimali watu, aliishauri Serikali kuanzisha vyuo  AU Kushirikiana na vyuo vikuu vitakavyotoa elimu ya juu katika kuwezesha kutoa  wahitimu wenye sifa za kufanya kazi katika sekta za Nishati akitolea mfano shughuli itakayohitaji wahandisi wengi wa uchimbaji mafuta katika kipindi kijacho.

  Kuhusu Safari ya Mheshimiwa waziri Mkuu,Balozi LUZ amesema, Katika ziara hiyo mheshimiwa waziri anatarajiwa kutembelea maeneo mbalimbali ya kuvutia na yatakayoleta tija kwa nchi ya Tanzania, zikiwemo sekta za kilimo kwasababu kilimo Kwanza ndiyo kipaumbele cha nchi, pia atatembelea maeneo ya mifugo, Miundombinu  pamoja na miradi ya mbalimbali ya maendeleo nchini humo sambamba na kukutana na wafanyabishara wenye nia ya kuwekeza Tanzania na muungano wa vyama mbalimbali.

  Sambamba na hilo balozi huyo wa Brazil amesema, Waziri Mkuu pia katika ziara hiyo  atakutana na Makamu wa Rais wa nchi hiyo, Waziri Mkuu, Waziri wa Mambo ya Nje wa Nchi ya Brazil pamoja na mawaziri wengine.

  Katika ziara hiyo Waziri Mkuu PINDA , ataongozana na msafara wa Viongozi kadhaa kutoka hapa nchini Akiwemo waziri wa Nishati na Madini Bw.William Ngeleja, Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu uwekezaji na uwezeshaji Dr. Mary Nagu pamoja na viongozi wengine wa juu wa serikali .

  Regards,
  --
  Zainul A. Mzige,
  Operation Manager,
  MO BLOG,


  Nimetumiwa na ;...
  ....Zainul A. Mzige wa MO BLOG

  Read more...

  UDHAIFU wa MATUMAINI ya ya KESHO,....

  .... ni  ile HALI ya  kutufanya tusiinjoi ya LEO kwa UKAMILIFU,...
  .....KISA,...
  ....tunatumainia ya KESHO yatakuwa BOMBA zaidi!:-(

  Swali:
  • Si labda ya LEO  yangekuwa matamu vyakutosha kama tusingetarajia TUYATUMAINIYO ya baadaye ya hata KESHO  yatakuwa BOMBA zaidi?
  • SI LEO haijirudii MAISHANI na labda leo  ndio LEO?

  Ndio,...
  ..... labda  MATUMAINI ndiyo YASABABISHAYO mpaka walioelimika vyakutosha DARASA LA SABA  WASIRIDHIKE na kuendelea  mpaka na vyuo ambavyo WATAJIFUNZA wasiyoyahitaji MAISHANI kwa matumaini tu kuwa  WAJUAVYO hayatoshi na siri ya FURAHA ni kuendelea na SHULE ya hata yasiyowafunza kitu MAISHANI!


  Swali:
  • SI nasikia ni mengi tu yafunzwayo MADARASANI huwa hayamsaidii MTU na ni matumani tu yafanyayo watu kibao KUKOKOTOA sana tu MAKALUKULASI wakati  hawatayatumia hata siku moja MAISHAI?

  MATUMAINIIII!

  Ndio,...
  .... MATUMAINI ni KIBOKO,....
  .... na yanamsaada mpaka wa kufanya baadhi wasiwe MALAYA wala MAJAMBAZI ili kukwepa tu dhambi  kwa kutumainia ya MBINGUNI.

  Ni wazo tu hili MUUNGWANA!

  Hebu Jaguar aanzishe upya kwa - Kigeugeu
  Sijui kwanini lakini turudi HAWAII ,...
  .....ili J Boog airudishe palepale kwa - Lets Do It Again  J Boog aungwe mkono na Richie Spice warudie-Got To Be Strong


  Halafu tu tena KIDUM na Lady Jay Dee wazime kwa -Nitafanya


  Read more...

  Asante SUBI!


  Kama umestukia mabadiliko hapa kijiweni,...
  ......kamanda wa mabadiliko ni SUBI wa WAVUTI!

  ASANTE SUBI,...
  .... kwa yote  ujitoleayo DADA!  Habari ndio hiyo!

  Read more...

  Cesaria Evora ang'atuka toka ulimwengu wa muziki !

  Cesaria Evora kazini!  Kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa MOYO.....
  ..... Mwanamama CESARIA EVORA  kutoka Cape VERDE kashauriwa kuacha MUZIKI.

  CESARIA ni moja ya wanamuziki kutoka AFRIKA niwapendao SANA!

  HABARI zaidi kongoli HAPA au HAPA

  PUMZIKA  MAMA na nakutakia MAISHA MAREFU!


  Ngojea mie niendelee kukusikiliza,...
  .... katika Miss Perfumado  Africa Nossa  Besame Mucho  Au tu hebu alete tena na -Angola

  Read more...

  TANESCO WATUMA SHUTUMA NZITO KWA KAMPUNI YA PAN AFRICA.

  >> Monday, September 26, 2011

  Afisa Uhusiano wa TANESCO Badra Masood.
  Leo katika kipindi cha Breakfast kinachorushwa na Redio ya Clouds FM Afisa uhusiano wa TANESCO ameishutumu kampuni ya PAN AFRICA Enegy ndio inayosababisha matatizo haya ya Ugawaji wa umeme uwe haufuati Ratiba.
  Hayo aliyasema baada ya kuona shutuma nyingi zinatumwa kwa TANESCO badala ya kampuni hiyo inayo iuzia Gesi Tanesco kwa ajili ya kuzalishia umeme. Ameyasema haya ili kampuni ya PAN AFRICA nayo iwaeleze wananchi ni kwa nini umeme mgao wake haueleweki. 
  Tanzania kwa kipindi cha zaidi ya miaka mitano imekuwa na matatizo ya umeme yasiyo isha.

  KAPINGAZBlog inampongeza kwa kuonyesha ujasiri, kuamua kutueleza wananchi nani anayetusababisha kupata umeme kwa mgao usioeleweka, pia tunapenda kuwashauri wajitahidi kutafuta vyanzo vingine vya kupata nishati hii muhimu kwa maendeleo ya Taifa.
  Nimetumiwa na Henry Kapinga,...
  .... wa KAPINGAZ blog.

  Read more...

  PIPI tamu , NYAMA tamu,...

  ... na kwa bahati mbaya  na MCHICHA  pia MTAMU!:-(


  Swali:
  • Si umestukia labda liutamu LABDA LIKO kwenye  LIULIMI LAKO lisikialo tamu hata kwa kupapasa KITOVU na lisananishalo pengo kwako ni MWANYA?


  Na CHAI  ni  chungu, ...
  .... PIPI  pia lama MBILIMBI TAMU ni chungu,...
  ......kwa kuwa nasikia hata SUKARI huingia MDUDU!:-(

  Ndio,...
  .... ni wazo tu hili MHESHIMIWA na kutolielewa RUKSA!:-(
  JUMATATU NJEMA MHESHIMIWA!
  Hebu INI KAMOZE aingilie kati nakuanzisha upya kwa-GENERAL


  INI KAMOZE aongezee dozi kwa -Trouble You A Trouble Me

  Ini Kamoze aweke kidangachee ndude- Them Thing Deh  Ini Kamoze huyuhuyu a - Cool It Off  Au INI KAMOZE amalizie tu tena kwa- Here comes the HOT STEPPER


  Read more...

  Wakati tunamendea KINACHOHITAJIKA na kusahau umuhimu wa KILICHOPO!

  KILICHOPO labda  ndio kitiacho nguvu MTU,...
  ... hata ya kufikiria  kile kiaminikacho ndio KIHITAJIKACHO!:-(

  Swali:
  • SI SHILINGI iliyopo labda inamchango mkubwa kuliko ITARAJIWAYO  ambayo hatunauhakika itakujakuwepo?
  • Si kidude cha ZUBEDA labda kinatosha hata kama aliye na ZUBEDA anaamini  ahitajicho  ni kile cha KHADIJA?
  • Na vidhaniwavyo vingi si nasikia ni VYAKUFIKIRIKA kama kilichopo hata kama ni ugali tu kwa maharage  hicho ndio  bonge la NGUNA  kwa rojo?


  Ndio,...
  ..... kilichopo labda ni MUHIMU ZAIDI ya kile kidhaniwacho ndicho chahitajika,...
  ....... kwa kuwa  nguvu ya MAHITAJI labda inamisingi yake ambayo ni muhimu zaidi  hata kama ni kwasababu tu inawezesha mtu  mpaka kufikiria MENGINE  kistaili ya MAHITAJI!:-(

  Ni wazo tu hili NGULI ,...
  .... na wala USIKONDE!:-(

  Hebu Kevin Hart ajaribu kubadili kwa kuongelea - Other peoples personal problems  Capleton aingilie kati na kurudisha bolingo katika - That Day Will Come  I-WAYNE ajaribu tena kukiri - Can't satisfy her  I Wayne aongezee dozi kwa kukiri pia - Need Her In My Arms  Halafu sijui kwanini ila hebu FALLY IPUPA aibadili tena  kwa -CADENAS
  Halafu LOKUA KANZA afunge tu ukurasa kwa - NAKAZONGA


  Read more...

  R.I.P Wangari Muta Maathai !

  (1 April 1940 -26 September 2011)


  Asante kwa yote,...
  .....hasa kwa kutukumbusha,...
  ....... nguvu ya MTU MMOJA katika JAMII!
  Pumzika Mama!


  Hebu tumsikilize kidogo,...

  Halafu,...

  Habari zaidi,...
  ...HUKU au,...
  ......HUKU

  Read more...

  Katika SULUHISHO la kuvunja kioo ili MWANAIDI asijione ``SURAchaUPELE´´ na kujisikia VIBAYA!

  Ndio,...
  .... kunawashaurio kivunjwe KIOO,...
  .... ili siye wenye sura mbaya tujisikie vizuri kwa kutojiona!

  Swali:
  • Si  kujiangalia ndio saa nyingine hukumbusha mtu  ujazo wa pua   kama jipu?

  Ila TATIZO tu ni kwamba,...
  ..... kuvunjika  kwa KIOO kusababishako  MTU  asijione,...
  .... bado hakubadili  SURA ya MTU!:-(


  Swali:
  • Si hata tufanyeje kukwepa kutambua tatizo lipo kwa kutoliangalia huwa hakuondoi tatizo?
  • Na si WASENGE wapo tu BONGO  hata kama jamii inadai  hawapo na matatizo yao yasitambulike ingawa yapo?

  Ndio,..
  ..... moja ya  dalili ya matakwa ya MWANAIDI  kioo kivunjike ,...
  .... labda ni yale ya kumlaumu MESENJA wakati afanyacho ni kuwakilisha tu meseji  ambayo ipo tayari  na wala yeye  mesenja hahusiki  katika mtengenezo wake!:-(

  Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!:-(


  Hebu twende tena Zimbabwe ili Oliver Mtukudzi aanzishe kwa - Neria  Oliver Mtukudzi arudie- Ndakuvara  Oliver Mtukudzi aongezee dozi kwa - Tozeza baba

  Aongezee zaidi tena-Todii  Au tu tena Ringo Madlingozi aingilie tena  kati kwa -Into Yam


  Read more...

  Katika UJEMADARI KIMBOO muongozo LABDA ni HISIA,....


  ..... na KATIKA nanihii labda kweli ni UJEMADARI,...
  .... kama KUINGIZWA  mtu kichwakichwa  kwenye giza asikokujua ni UJEMADARi  ,...
  ..... kama tu  katika UJEMADARI wa VITA ambayo nanihii itabidi ingie gizani kichwakichwa,...
  .... bado ni UJEMADARI labda kwa kuwa MTU kiaina ni kichwa kwa kuingia  waogopako WENGINE kwa kuwa hakijulikani kilichondani huko kwenye GIZA!:-(


  Tahadhari:Inawezekana kile kidude kifananacho JINA ambacho hata mbwa na sungura wanacho -LABDA hakimaanishwi hivyo katika TARALILA HII  iliyopinda kiwazo na KITARALILA HII !:-(

  Ndio,...
  ...JEMADARI ,...
  .....hata KIMALAIKA wa KIHISIA   ,....
  ... tukiacha kugusia asifiwayo YAJULIKANAYO  YALIYOWAZI ,...
  ...labda  kama hakuna afikiriaye  labda hakutakuwa na JEMADARI asifiwaye kwa YALIYOWAZI njenje  ,...
  .........na tutabaki na wenye sifa  zenye UJEMADARI kimboo  wa kuingia kwenye matundu ya giza  bila kutumia macho , pua au hata KUHOJI kiakili JAMBO  kwa kuwa NI HISIA TU  HILO na sio HALIHALISI  kiukweli ndio MUONGOZO kuwa  TAMU !:-(  Swali:
  • Na si SUKARI nasikia ni tamu KIHISIA  hata kama imetiwa SUMU?
  • Si wewe KWA WENGINE  labda ni  jengo tu la mtalimbo KIKIFIKIRIWACHO TU KIHISIA  kisa umevaa MIDABWADA  wakati ukweli ni kuwa wewe ni NGULI  utatuaye kwa UBONGO na sio MTALIMBO ?

  Na kwa kuwa kuna wajisifiao MJENGO kihisia,...
  ....    labda MTU asivimbe KICHWA  kwa kuwa ukweli wawezakuwa   BADO ni kwamba  KIHISIA TU  kuna wasifiwao kama tu WALAANIWAO  kwa ya kweli amabyo MTU akiyafikiria na KUNYAMBULISHA kwa kutumia AKILI  na si HISIA TU kuna  kitu kinaweza kumstua kuwa si kweli  harufu ya WALI ni lazima iwe kuna WALI kwa kuwa INAJULIKANA  kuna mpaka NYOKA wanukiao  KIUBWABWAUBWABWA.:-(  Swali:
  • AU?

  NA  ndio ,...
  ...labda JEMADARI kikuma yupo pia  kwa ya JEMADARI kimboo,..... 
  ....kwa kuwa pamoja na kwamba mambo mengi sio UDHU na hayahitajiki kwenye JENGO  na  hayana uhusiano na UMALAIKA uingiliwao  mtalimbo ingawa yapo ndani ya JENGO,...

  .... kihuswishwi  cha KITU  BORA   labda sio  tu  kiko kwa  NJE  KIONEKANAKO KIRAHISI  kwa kuwa  vingi bora viko NDANI  na  UJEMADARI kikuma ni ile ruksa ya kuruhusu visivyotathiminiwa viingie ndani KUCHOKONOA vyenye MALIGHAFI BORA kitu ambacho kikuma LABDA  ni UJEMADARI!  Swali:

  • Si unajua  kwa ndani  hata ya jipu hakuishi usaha tu peke yake na na labda ni UJEMADARI kuruhusu SINDANO kimtumbuo?
  • Na kwani JENGO kanisani AU msikitini ni lazima WASWAHILINA au WALOKOLE wawe ndani ili  kisala SALA itoke STIRIO?


  Ndio MHESHIMIWA ufikiriaye mpaka neno MBOO au KUMA ni tusi,...,...
  .... labda MATUSI yako ndani ya  ufikiriavyo KIHISIA TU ZAIDI kuliko halihalisi ya TUSI  au utendavyo kuliko hata jengo ambalo ni NENO,...
  ... na KIHISIA kama kimaneno  labda  ya hata ´´KHADIDJA HAJAVAA CHUPI ´´haibadili ukweli  kuwa    kivitendo yaweza kuwa ni kweli ``KHADIDJA hajavaa CHUPI´´  na sio HISIA hiyo .:-(  Swali:
  • Si unajua tusi la ukweli  laweza kuwa bado ni HISIA tu ZA MTU?

  Ndio,...
  ....kwa UNDANI,...
  ...... labda BINADAMU hana undani sana na ndio NDANI kwenye GIZA hata kama sio ndani ya kidude cha MTU  kunawezatisha WATU au ndio  maana kirahisi ana MPAKA dini ambayo anaamini  ni sahihi  kiasi kwamba waaminivyo wengine sio SAHIHI ,..
  ... wakati anajua misingi ya IMANI ni imani na imani  haina ushahidi  kama tu wengine waaminivyo  KIHISIA  ZISIZO NA USHAHIDI ambazo kiana zajenga UJEMADARI wauaminio ambao kwa lugha ya kipicha unaweza kuuoanisha na vitendo vya sehemu za siri vya ujemadari wa kuingia au kuingiliwa kwa ukakamavu bila woga wala kutumia akili  ingawa zaweza samehewa kwa kuwa SEHEMU ZA SIRI HIZO kimboo au kikuma hazina UBONGO.:-(


  NIMEACHA wazo hili nyoko MHESHIMIWA!!:-(


  Hebu IPHY OKOLI aabadili kwa kuanzisha mchezo upya  kwa -Ifeome
  Lil' Kim ajaribu kugusagusa eneo kwa - No Matter What They Say
  Au tu hebu Missy Elliott amalizie tu,...
  ............kwa kusema ukweli kuwa - She's A Bitch  Ndio,...
  ... bado nipo!:-(

  Read more...

  Kuna MATATIZO yapewayo MAJINA mazuri mpaka unaweza usiyaoanishe na TATIZO,.....

  .... lakini  TATIZO labda ni TATIZO tu hata kama kijina  limegeuzwa kuitwa MFADHAIKO wakati kivitendo TATIZO  lionekanalo  kwenye foleni,...
  ....ni  mdada wawatu kachafuliwa na lijidume KAME lililotokwa mbegu kimfadhaiko  KAMA tu  itokeavyo  kwenye DALADALA.

  Swali:
  • Si unakumbuka eti kuna wauguao mfadhaiko  na ugonjwa ukizidi  ni hatari hata hadharani wakiguswa na MDADA?
  • Na si MWIZI hurembeshwa jina na kuitwa FISADI saa zingine kisa  ni MHESHIMIWA?:-(

  Ndio,...
  ..... binadamu  hata TOTO baya la MBWA huweza kulitungia JINA zuri,...
  .... utafikiri   kwa kukipa kitu JINA zuri huondoa makali ya ubaya wa kitu!:-(
  Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!

  Hebu tena Mahotella Queens warudie - Umculo Kawupheli  Simon Mahlathini aingilie kati na kuja na Mahotella Queens katika - Kazet  Au tugewe tu tena -Dikgomo remix

  Read more...

  Watu husikiliza na MAISHA yao kwa hiyo uongeleapo HIKI wengine huweza amini unaongelea KILE!

  >> Sunday, September 25, 2011

  Ndio,...
  .....labda WATU husikiliza na MAISHA yao,...
  ..... kitu kiwezacho fanya aongeacho MTU kieleweke tofautitofauti kutokana tu na ni nani ni msikilizaji na ni mwenye maisha gani!:-(


  Swali:
  • Si  ukiongelea SHIDA labda unaelewekaji wake ni  tofauti  kama akusikilizaye ni TAJIRI au MASIKINI, MSOMI au  yule SHULE ni madangacheee?
  • SI unajua yasemekana aliyekulia katika waongeleao MAFUMBO hata ukiongea kitu moja kwa moja atajaribu kufumbua FUMBO?
  • Si yasemekana kuna wasioelewa kuwa sio wote ukiongea hata kwa kunukuu vitabu kanma VITAKATIFU bado sio wote watachukulia huo ndio ukweli kwa kuwa kimaisha yao BIBLIA na KORANI bado ni kitabu tu chenye stori za kutunga na hakina utakatifu waliouzoea wakuliao kwenye MAISHA YA waaminio ?


  Ndio,...
  ......katika sanaa ya KUONGEA uongeleapo HIKI,...
  .... yaweza kueleweka unamaanisha KILE!:-(
  Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!:-(

  Hebu P.Square, Tiwa Savage na May D wabadili vita kwa -Do as I do  Tiwa Savage abaki mwenyewe kwa - Kele Kele love  Au tu tena Bunny Mack azime mshawasha kwa kutuliza na  - Let Me Love You


  Read more...

  KAPINGAZ Blog SIO MUDA MREFU TUTAKULETEA JEZI ZENYE LOGO YETU KAA MKAO WA KUVAA.


  Mfano wa Jezi itakayokuwa na Logo yetu, karibu sana mdau.

  Jezi hizi zitakuwa zikigawiwa Bure, haziuzwi. Kama utahitaji usisite kuwasiliana nasi mapema kupitia mawasiliano yetu yaliyopo kwenye Blog. Tunashauri ni vema ukatumia Email ili tuweza kuwa na kumbu kumbu nzuri badala ya simu

  HABARI ndio HIYO!

  Nimetumiwa na Henry Kapinga,...

  Read more...

  Katibu wa TA Reading na Mkewe Wameremeta!

  Salam,


  URBAN PULSE CREATIVE Inawaletea picha za tukio la Harusi ya nguvu iliyofanyika Jumamosi Tarehe 25 septemba 2011 Katika ofisi ya Reading Registrar kati ya Katibu wa Tawi la TA Hapa Mjini Reading Amri Dello na Alice Kapya.


  Baada ya Kufunga pingu za maisha tafrija ilifanyika ndani ya Boat na kuzunguka mitaa ya berkshire hadi windsor kwa Queen na kumalizikia katika Mji wa Reading.

  Wadau mbalimbali walikuwepo katika sherehe hii akiwepo Mh Balozi wetu Peter Kallaghe.

  URBAN PULSE inapenda kuwapa hongera sana Maharusi wetu na kuwatakia kila la kheri katika safari yao ndefu walioianza leo.

  MUNGU AWABARIKI,
  Asanteni

  URBAN PULSE CREATIVE

  Bonge la kiss

  Zawadi Maalum kutoka kwa Mzee Abdul Dello

  Boti inayoitwa caversham Princess ikiwasubiri maarusi tayari kwa ajili ya sherehe

  Bwana Harusi akiweka Sahihi kwenye cheti cha ndoa

  Bwana harusi Dello

  Bwana na Bibi Harusi

  Bwana na Bibi Harusi wakiwa wanameremeta

  Dello akimlisha keki mkewe

  Kila Kitu kimekwenda poa na jiko nshavuta sasa tugange yajayo

  Maarusi wakipewa maelekezo kabla ya kuingia kwenye boti

  Mh Balozi akitoa nasaha zake kwa bwana na bibi Harusi

  Mh Balozi Kallaghe Akiwa na MH Balozi Kapya wakibadilishana mawili matatu

  Mh Balozi Kapya na Binti yake wakiingia katika ndani ya Reading Registry Office

  Picha ya Pamoja kutoka kwa pande zote za famailia na wadau waliokuja leo kushuhudia Harusi

  Pozi baada ya Harusi

  Wadau wakijimwaga kwa raha zao

  Wakati wa kulisakata Rumba

  Read more...

  Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


  Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

  Partner

  save mt. Kenya campaign
  In partnership with africapoint.com

  Taswira BANANGENGE

    © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

  Back to TOP