Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

KIMWANA kavaa NGUO na kwa nje KAPENDEZA,...

>> Wednesday, September 21, 2011

.....tena kavaa mpaka HERENI  na  BANGILI kapendeza,...

Na yaonekana KIMWANA  hata chini ya nguo zionekanazo KAPENDEZA,...
.....kama dalili zaonyeshwa na SIDILIA ilindayo mtuno wa titi usio bahiri na mpaka kifichanyeti cha mauamaua  chake ambavyo vyote VYAMPENDEZA!


Lakini KIMWANA kama  tu MIDUME kilicho muhimu ambacho ni ROHO labda HAJAPENDEZA,...
.....kwa kuwa KIMWANA kama tu VIMWANA wengine kitabia  za uchafu ni kama MIDUME ambayo roho zao chafu  kama shimo la choo cha stendi na huko sio KUPENDEZA.

Swali:
  • Si  kuna wasahauo kuwa WANAWAKE na WANAUME wote ni BINADAMU  na wote  kama BINADAMU labda wanauwezo wenye kipimo sawa kuwa wachafu KIROHO?
  • Kwani unafikiri  WANAUME wanawazidi WANAWAKE  kwa roho MBAYA?

Ndio,...
... na labda KIDUME kama KIMWANA,...
... kama kuna USAWA katika yao UPIMIKAO tayari,...
..... yaweza kuwa ni ule tayari ujulikanao  ambao  huweza kuwaweka sawa kiuchafu wa ROHO,...
.... ingawa labda ni MUNGU tu  ambaye ndiye JAJI na ajuaye vizuri nani kwa ndani ya roho  KAPENDEZA.:-(


Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!


Hebu KIDUM na SANA warudie-Mulika MWIZI



Bizman asifie - Mademu wa Bongo



K-lyinn na J Mo wakumbushie - Nikipata Wangu



Juliana K na Bushoke watulize mshawasha na kumalizia kwa-Usiende Mbali


2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 2:12 pm  

mulika mwizi ...Kila mtu wa mapenzi hata mwizi wa mapenzi...oh nilikuwa naimba nao nikajikuta naandika hapa:-)

Simon Kitururu 8:43 pm  

@Yasinta: :-)

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP