Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

MTANDAO MPYA WA UNIVERSITIES CONNECTS (SOCIAL NETWORK) KWA AJILI YA WANAVYUO,WANAFUNZI NA WADAU KWA PAMOJA.

>> Wednesday, September 21, 2011

Salam,

Shikamoo wakubwa na vijana wenzetu mambo vipi? kwanza kabisa tunapenda kuwashukuru Mabloga wote popote Duniani kwa kuendelea kutusaidia kwa kiasi kikubwa sana kutufikishia ujumbe wetu pale tunapo omba kusaidiwa, Baada ya shukrani hizo za kipekee kabisa, Pia tunapenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru wale wanavyuo,watumishi wa vyuo na wadau wote ambao wameendelea kuipa sapoti kubwa website ya MATUKIO NA WANAVYUO. Ili kuendeleza kuwaunganisha wanavyuo wote Tanzania na kuwakutanisha na wanavyuo wengine ambao ni watanzania lakini wanasoma nje ya nchi tumeamua sasa kuwaletea njia mbadala ambayo itawaunganisha kirahisi kabisa nayo ni Socilal network.


Hivyo basi kwa heshima na taadhima tunapenda kuwatambulisha kwenu kiunganishi kipya kabisa ambacho kinakwenda kwa jina la UNIVERSITIES CONNECTS . Na Jina la tovuti ni www.tzuniversitiesconnects.tk

Katika website hii maalum kabisa wanavyuo na wanafunzi mbalimbali pamoja na wadau wataweza kukutana humo, kubadirishana mawazo ya kisomi zaidi na kufahamiana zaidi ikiwa ni pamoja na kupata mawazo mapya, pia wataweza kupata marafiki wapya na kama haitoshi kuna Visual Discussion Room ambapo wataweza weka Mada mbali mbali na kuijadili moja kwa moja, na zaidi ya yote utapata nafasi ya kuchati muda wowote.Pia kwa kuzingatia kuwa wanafunzi wengi wanatumia Mobile phones, basi kupitia Mtandao huu utaweza pia kutumia simu yako ya mkononi kuendelea kuwasiliana. Ni matumaini yetu ya kwamba mtandao huu wa kipekee na mpya kabisa utaenda kukuunganisha wewe na mwenzako... Tunaomba ukipata taarifa hii umwambie na mwenzako pia ajiunge ni Bure kabisa. Tunatanguliza Shukrani zetu asanteni sana.

Sisi,
Matukio na wanavyuo Crew
twanavyuo@live.com

ILI KUJIUNGA MOJA KWA MOJA BOFYA HAPA CHINI

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP