Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Watu husikiliza na MAISHA yao kwa hiyo uongeleapo HIKI wengine huweza amini unaongelea KILE!

>> Sunday, September 25, 2011

Ndio,...
.....labda WATU husikiliza na MAISHA yao,...
..... kitu kiwezacho fanya aongeacho MTU kieleweke tofautitofauti kutokana tu na ni nani ni msikilizaji na ni mwenye maisha gani!:-(


Swali:
  • Si  ukiongelea SHIDA labda unaelewekaji wake ni  tofauti  kama akusikilizaye ni TAJIRI au MASIKINI, MSOMI au  yule SHULE ni madangacheee?
  • SI unajua yasemekana aliyekulia katika waongeleao MAFUMBO hata ukiongea kitu moja kwa moja atajaribu kufumbua FUMBO?
  • Si yasemekana kuna wasioelewa kuwa sio wote ukiongea hata kwa kunukuu vitabu kanma VITAKATIFU bado sio wote watachukulia huo ndio ukweli kwa kuwa kimaisha yao BIBLIA na KORANI bado ni kitabu tu chenye stori za kutunga na hakina utakatifu waliouzoea wakuliao kwenye MAISHA YA waaminio ?


Ndio,...
......katika sanaa ya KUONGEA uongeleapo HIKI,...
.... yaweza kueleweka unamaanisha KILE!:-(




Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!:-(

Hebu P.Square, Tiwa Savage na May D wabadili vita kwa -Do as I do



Tiwa Savage abaki mwenyewe kwa - Kele Kele love



Au tu tena Bunny Mack azime mshawasha kwa kutuliza na  - Let Me Love You


3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

malkiory matiya 7:48 pm  

Upo sawa Kitururu: Kuna haja ya wasomaji kupambanua hidden and surface meaning ya maandiko.

Na zaidi, hongera kwa ukarabati huu wa nguvu. Kijiwe kimependeza sana.

Unknown 10:51 pm  

Daima ni muhimu tukubali hali ilivyo, halafu tujitahidi kuifanya bora zaidi.

Tusipojikubali kwanza tutahangaika tu hata kukata tamaa hatmaye.

Simon Kitururu 8:37 am  

@Mkuu Malkiory: Asante Mkuu!Ila nasikia siku hizi usipolainisha maandiko husomwi kwakuwa mambo yote video na picha! Ila tatizo ni kwamba hata picha na video zina hidden meaning na kwa kuwa watu wanaona kama ni njia rahisi zaidi ya uwakilishaji kitu,.... kitu hicho huweza kufanya kuna meaning zinapotea. Si umestukia bado hata katika BLOGU zile za picha kwa wabongo ndio huvutia kuliko za maandishi hata yale rahisi.:-(


@Rasta Mcharia:Na mimi naamini hakuna kitu kibaya kama kukata tamaa kwa kuwa huweza kufanya hata yawezekanayo yasiwezekane yani!:-(

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP