Ikizimwa TAA sina AIBU,....
>> Tuesday, September 20, 2011
.... gizani naogopa GIZA!
Jua likiwaka naungua na sipendi joto,...
.... na MVUA ikinyesha sipendi MATOPE.
Njaa ikiniuma nanywea kwa kukosa nguvu,...
.... nikishiba nazembea nakusikia usingizi kwaajili ya SHIBE.
Swali:
- Si umestukia chochote kile BINADAMU anaweza kukilalamikia ?
- Nachochote kile KIBINADAMU huweza kukosolewa?
NI hilo tu!
JUMANNE NJEMA MKUU!
Hebu Bamboo na Archapello waongelee - Tabia Mbaya
Au tu Bamboo amalizie kwa - Mama Africa
4 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Ni bonge la ujumbe...Ahsante sana uwe na siku/jumanne njema nawe pia
baadhi yetu kulalamika jadi,hakuna kizuri kwetu.huyo ndiyo binaadamu wa ajabu.umetukumbusha ujumbe kabambe. na wewe juma nne njema.kaka S
Binaadamu hatuna jema kaka, Ahsante kwa ujumbe mzuri.
@Wote : Asanteni wote kwa kutoacha kunitembelea! Tuko Pamoja!
Post a Comment