Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Kama unasikia nachosikia na KUONA NACHOONA!

>> Wednesday, March 31, 2010

Waweza kustukia SIKU HIZI ,....

....Wanasiasa wanachukuliwa kama VICHEKESHO na WACHEKESHAJI wanachukuliwa siriasi!:-(

Kama unaona nachoona na KUSIKIA NACHO SIKIA siku hizi,....
...... unaweza kudhani MWISHO WA DUNIA umefika mpaka usome HISTORIA na kustukia dhambi nyingi zistukiwazo ZILISHA ANDIKWA KUWA ZINAFANYIKA tokea kabla ya  enzi za kina YESU na kuna waliodai dunia imefikia mwisho enzi hizohizo wakiwa tu vilevile siriasi.:-(

Swali:
 • Unafikiri akina FARAO wa MISRI nao hawakuwa na kitu wakiitacho SIKU HIZI?Kuna uwezekano IDADI YA WATU imekuwa sana siku hizi,...
... na ukichanganya KITU HICHO na TEKINOLOJIA ZA HABARI zisababishavyo mpaka UDAKU KUPATIKANA kirahisi ,....
... labda kuna tunayoyasikia  TU zaidi SIKU HIZI ingawa yalikuwepo tu hapa DUNIANI toka enzi za madanga chee.:-(

Swali watu wenye imani fulani :
 • Unadhani baada ya ADAMU na EVA kufanya dhambi ya kula tunda , dhambi yao iliyofuata ilikuwa ni nini?
 • Ushawahi kusikia msemo hakuna jipa chini ya anga na kama KITU hakijafanywa na MTU basi kimefanywa na angalau mjusi?

Ndio,....
.... kama unasikia nachosikia na KUONA NACHOONA,...

..... labda kibadilikacho hapa duniani ni staili tu  LAKINI MAMBO NI YALEYALE,...
....kama tu  salamu kubadilika  KUTOKA ``Mambo dukinaa! ´´ kwenda  ``Mambo POA!´´ na  salamu YA KISASA kuwezakwenda mpaka kuwa  ``Mambo Kukojolea dodoki!´´ - lakini zote zikimaanisha JIBU la  salamu HIYO HIYO ya tokea enzi ya kuwa ``Mwenzetu hujambo lakini!´´.:-(Ndio,....
.... kama unasikia na kuona nachoona,...
..... labda HATA udaku  ni uleule kibadilishwacho ni MAHALI  lugha tu  itumikavyo  au itumikayo.:-(

Na haki ya nani  labda mambo ni kama SURUALI ,...
...iwe ni PEKOSI , kodrai  au hata JEANS ya nailoni lakini vyote ni suruali  na kupendeza  au kutishwa na jinsi suruali imbinyavyo tako mtu HUKO KUKO  tu machoni mwa mtazamaji na LABDA hakuna WATAZAMAJI wawili WAONAO na kuoanisha suruali na muonekano wa tako sawasawa.:-(


NI WAZO tu la GHAFLA MHESHIMIWA na wala usikonde kama unauwezo wa kula BAGIA !:-(


Namuachia SADIKI aendelee katika-Do You Hear What I Hear


Au tu Rick James abadili zaidi kwa ndude -Cold Blooded

Read more...

Yakisikilizwa MALALAMIKO YA MPENDA KULA asiyependa kupika wala kuosha VYOMBO,....

>> Tuesday, March 30, 2010

.... yaweza KUSAHAULIKA kuna watu WASIOPENDA KULA pia DUNIANI.:-(

Na akisikilizwa KIDUME mpenda WANAWAKE,.....
.... kwa muda fulani UNAWEZA kusahau kuna wasenge pia DUNIANI.:-(


Swali:
 • SI unakumbuka katika kiwanja cha MPIRA WAMIGUU unaweza kusahau uwezekano wa kuwepo washabiki wa NETIBOLI hapo?Ndio,...
.... kwa kuwa WATU WENGI wanaelekea upande wa kulia USIJE TU KUSAHAU kuwa kuna AMBAO kwa makusudi yao kabisaa wanaelekea KUSHOTO ndio maana wakati una sikiliza stori za waenda MSIKITINI au KANISANI usisahau kuna waendeao UCHAWI PIA duniani.:-(

Ndio ,....
... labda APENDAYE kula ndio anaweza stukia matatizo ya KUPIKA na kuosha vyombo na KIRUKA NJIA aliye chacha ndiye atakuwa anastukia matatizo ya gesti za migombani LAKINI na wachawi yawezekana pia wana matatizo yao tu kitu ambacho ni MCHAWI tu atastukia ni hali ya hewa gani kupaa kwa ungo ni shwari zaidi DUNIANI.:-(

Ndio,...
... labda wakati unasikia MALALAMIKO ya hili kumbuka uwezekano wa kuwa kuna MATATIZO YALALAMIKIWAYO ya lile lisilo kuhusu pia hapahapa DUNIANI.:-(

Ni wazo tu hili MHESHIMIWA na wala usikonde!:-(

Hebu Ray Barretto na Mongo Santamaria katika kubadili hali ya hewa kijiweni warudie - Congo Bongo

Au tu na Kofi Olomide arudie-Sylvie


Read more...

KUWAZA!

Kama ingewezekana kuchagua nini KISIWAZWE,....
...ningewazia chakula na kuruka kufikiria mpaka  kama NI KWELI hakuna  mavi yenye ulemavu .Kama ingewezekana kuchagua nini KISIWAZWE,..........ningechagua  kuwaza ya busara na kukwepa kuwaza kuwa moja ya alichonacho MWEREVU ni  upumbavu.


Ningechaguliwa cha kuwaza,....
.....labda NI KWELI  ningekuwa  muda wote ni mpumbavu.

Lakini KWA  kuwaza upumbavu,....
.....kuna astukiaye  WEREVU wa watu  JINSI  ulivyotokana na upumbavu.


Na napenda neno ``PUMBAVU´´,....
..... kwa kusababishia KUNIIKUMBUSHA kustukia wale werevu.

NA ni wewe MWENYE busara na werevu ,....
....hasa kwa kuwa tu WEWE na sio MIMI  katika yangu ya kipumbavu.


Swali:

 • Ushawahi kustukia  kuwa upumbavu  unavyowasaidia  wengine  hasa kama  kwa werevu wako imesababisha  unashindwa kufanya  kitu kipumbavu?

 • Mpumbavu afanyaye kitu na MWEREVU ajizuiaye kufanya kitu unafikiri ni nani mchango wake UTASTUKIWA zaidi na  jamii?
 • Unafikiri MPUMBAVU kwa kawaida  anajistukia?


NI WAZO TU HILI MHESHIMIWA!


Hebu The Roots wabadili zaidi kwa ndude- Proceed


Au tu The Roots warudie kitu - The SeedAu tu A Tribe called quest watulize kwa - Oh my god


Read more...

MIPAKA iwekwayo na UHESHIMIWA!

Kwa kuwa jamii ndio inaweka MIPAKA ya nini kisemwe,....
..... WAHESHIMIWA ndio wafao kisabuni kwa kuwa KIHESHIMA kiwakeracho wamejifunza kuwa huwa hakisemwi hadharani.:-(

Ili kisichozoeleka kisemwe,...
....yawezekana WAHESHIMIWA wajuaji inabidi waangalie upya ni nini HAKISEMWI ambacho KINAFANYIKA kwa kuwa tu jamii imeamua kiheshima hicho kitu kisiongelewe HADHARANI.:-(


Swali:
 • Si unajua kuna aliyepata mimba au UKIMWI kwa kuwa tu WAHESHIMIWA hawaongelei ngono kwa kuwa HAWATAKI KUDAKWA wakiongelea waaminicho sio tpiki ya kiheshima hadharani?

 • Hujawahi kuuonea wivu UHURU wa mtu apendaye kukusimulia ufikiriavyo ni vitu vya FARAGHA ambavyo wewe unavionea aibu mkiwa hadharani?


MIPAKA iwekwayo na HESHIMA,....
....kwa bahati mbaya inategemea mtu na mtu na ukiheshimucho kwa mtu mwingine wala HAKINA HESHIMA.:-(


Ndio ,...
.... kuna viheshimiwavyo kama tu TISHU CHOONI ambavyo hata TISHU IHESHIMIWEJE bado tumizi lake lisaidialo kuongezea heshima ya mtu hubakia ileile ya baada ya shughuli nzito TISHU ndio itakayogeuzwa kichambio.:-(

Swali:
 • Si unafahamu TISHU nayo inaheshima zake za kimakokoneo?Hebu Erykah Badu abadili kwa kitu- Window Seat


Erykah Badu arudie ndude - Didn't Cha KnowAu tu Outkast na Slick Rick walete tena ndude- Da Art Of Storytellin

Read more...

HISTORIA ya uchaguzi wa MCHUMBA TANZANIA iwezavyo kusaidia CCM Tanzania.

>> Monday, March 29, 2010KIHISTORIA WATANZANIA walichaguliwa MCHUMBA !
Swali:
 • Unauhakika historia ya kujichagulia MCHUMBA  ina muda gani katika familia yenu?


NI HILO TU wazo dhaifu MHESHIMIWA!!


Hebu Loray Misik wasaidie ndude - Gede
Au tu THE DON JOSE PACHANGA wanusishe sikio  - SESTETO LA PLATA

Read more...

Kama UMESHAWAHI kuosha uchi,...
...kumbuka labda hicho KITU kimesha kupa uprofesa wa kuosha kitu chochote KILE.:-(
Swali:
 • AU?

 • Si unakumbuka CHOO KINUKACHO ni matunda ya kazi  za uchi hata zifanywazo kiheshima na MHESHIMIWA?
Ndio,...
... sikubishii HASA kama umeshawahi kufikiria WAKATI  ukipenga MAKAMASI ushikacho ni MAKAMASI.:-(
NAACHA MUELEKEO wa wazo nisije kugusia kugusia BURE mpaka nyanya za kachumbari uzipendazo zipendavyo kucheza na mbolea ilio oza kuliko kucheza na wewe.:-(

NI HILO tu na haki ya nani wazo hili la TARALILA halijafanyiwa utafiti wa kina  na limeruka vyoo vinukiavyo vizuri bila kunyunyiziwa manukato .:-(

JUMATATU NJEMA MHESHIMIWA!
Hebu tubadili kwa kwenda YEMEN kuwasikiliza wanawake washabikiao kuoongezea shughuli kwa watoto katika ndude-The right to marry as a child


Au hebu Marijani Raajab na Fresh Jumbe waangushe ndude - MasudiNdio,...
... aliyeandika taralila yenye neno lisilo LAKIHESHIMA kwa baadhi ya waheshimiwa ni huyuhuyu mimi kama HUYU MIMI aonekanavyo kwenye picha zifuatazo akijitafutia matatizo na halafu  akinunia MATATIZO baada yakustukia alivyojiongezea.:-(

Photobucket
PhotobucketPhotobucketPhotobucketPhotobucketPhotobucketPhotobucket

Read more...

Uhusiano wa UKE na UUME WA PANZI usipochanganywa na UHUSIANO wa PANZI MWANAUME na MREMBO panzi JIKE!:-(

>> Sunday, March 28, 2010

TUKIMGEUZA PANZI KUWA  nzige au  tu BIN -adamu MKUBWA,...
 ..... labda kuna BINADAMU anaweza kukumbushwa kwa HII TARALILA  kuwa  MWANAMKE na MWANAUME sio  UBINADAMU kwakuwa  pia kuna MBWA  MVULANA ingawa labda ni BINADAMU ambao  inabidi waoshe UANAUME au UANAUKE kwa kuwa wanamchezo kuwa wasipojiswafi watanuka zaidi ya KIKWAPA.:-(

SWALI banangenge:
 • Unauhakika UKE ungekuwa rafiki ya UUME kama PANZI asinge ugeuza kuwa ni MATUMIZI?


 • Unafikiri CHAKULA kinaupenda MDOMO WA PANZI hata kabla ya kugundua hata kisichokuwa nia ya panzi ni kugeuza CHAKULA CHA PANZI mavi?
 • Ushawahi kufikiria kuuangalia UKE WA PANZI kwa kuwa hata PANZI DUME havai chupi?

NI WAZO tu lililopinda MHESHIMIWA na kama umenisoma mpaka hapa SHAURI YAKO miye simo!:-(


JUMAPILI NJEMA MHESHIMIWA !Ngojea Teddy Pendergrass adai - It Don't Hurt NowAu tu The Isley Brothers warudie - ContagiousDUH Makassy MASIKIONI ananilazimisha niachie pia TENA  ndude-Mambo BADO

Read more...

FARAGHA!

>> Saturday, March 27, 2010

[Tahadhari  : Wazo limepinda!:-(]


Tatizo la FARAGHA,...
... ni kwamba hurahisisha mpaka  LILE TATIZO ULIJUALO LINAMKERA MHESHIMIWA liwekwe pembeni kwa kuwa kuna FARAGHA na kufanya lile tatizo ambalo hujui mtu analo likawa ndilo LINAPEWA KIPAUMBELE ambalo ni la MHESHIMIWA kujiangalia  uchi kila nafasi ikitokea kutokana na kukwazika kwake ambako HADHARANI hakujulikani,...

...kuwa  MHESHIMIWA anajihisi ana uchi wenye sura mbaya kitu ambacho  ndicho kimpacho MOTISHA NA nguvu ya kukivulia gwaguro ilia KUJICHUNGULIA  kuliko ILE MOTISHA YA KUDAI HAKI YA MNYONGE  Mheshimiwa AJULIKANAYO KUITETEA  kwenye hutuba zake zisizo kuwa  faragha.:-(LAKINI  uzuri wa FARAGHA,...
...ni kwamba  inaweza kukufanya UTULIE na kufikiri VIZURI jinsi ya kutatua MATATIZO YAKO na hata  YA DUNIA  kwa kuwa haubughuziwi  na WAKUDA hapo KWENYE faragha.:-(

Swali:
 • Kwani unabisha kuwa kuna watu FARAGHA ZAO huzitumia zaidi kufanya vitu vyenye undugu na KUNUSA chupi zao ili kujihakikishia ni kweli mkojo wao ukivunda haunuki vibaya sana  kuliko WAFIKIRIAVYO watajiinuaje KIMAISHA wakati  maisha mazuri yanapendelea MAFISADI?

 • Unauhakika aamuaye kuloga mtu huwa anawazia hilo FARAGHANI au katika kijiwe cha wachawi?
 • Unauhakika FARAGHA yako huwa unaitumia kufanya vya faragha au unaitumia ZAIDI kuwaza maswala yenye undugu zaidi na kitu kama  kati ya KITUMBUA na MAANDAZI nini ni TAMU TAMU KAMA SUKARI zaidi?

FARAGHAAAA!
NI kweli mawazo YA MTU  yasingekuwa  YA FARAGHA labda tungestukia MHESHIMIWA sasa hivi umuaminiye kwa ufundi wa kusali,....

...SASA HIVI   anafikiria kikojoleo na baada ya hapo wazo HILO ,...

....kitakacho hitimisha siku ni lile WAZO lake la kila siku la kufikiria UBWABWA na wala sio jinsi gani Tanzania itapata umeme wa kuaminika  au wataunyimaje UKIMWI usinenepe kama ifikiriwavyo na wamheshimuo MHESHIMIWA wafikiriavyo ndivyo MHESHIMIWA anafikiria.:-(

HILI NI WAZO TU na halijafanyiwa utafiti wa kina  kwa hiyo  kifaraja unaweza kulitukania ZAIDI ya SHENZI.:-(

Hebu Matonya abadili kwa kuongelea-Spair Tairi


Diamond alainishe zaidi kwa ndude-Kamwambie
Hebu Isley Brothers waje live na kitu -Between the SheetsAu nimuachie tu na Notorious B.I.G a sample Between the sheets na kuifanya kitu kiitwacho  -Big Poppa

Read more...

Moja ya WAZO LA MWANAMME kuhusu haki za MWANAMKE zikifikia kucheza karibu na mwanaume kunyimwa FARAJA za kike!

wali:

 • Umewahi kunyimwa wakati unataka?

Haki ya kutaka  na inayoeleweka,...
....KIBONGE  cha mpinzani wake ni KUWA  mtu mwingine NAYE anaweza kutoa madai hayohayo   kuwa  HAKI  YAKE ni kukunyima.:-(

Na kwa bahati mbaya MWENYE haki anaeleweka,....
... asipoelewa ni kwanini katika HAKI YAKE YA KUTAKA   kuwe na mtu mwingine mwenye haki pia ya KUNYIMA.:-(


Na haki NISHAI,....
.... ndio maana wakati kuna ateteaye matumizi ya kikojoleo na bado haja fikiria kuwa KINYEO NACHO NI TAKWA kuna adaie haki ya matumizi ya kinyeo ambayo hataki yawe kisheria katika kifungu cha kimlazimishacho kisheria hicho kipengele kwa wakitakacho katika burudani au mahusiano  KUKINYIMA.


Swali:
 • Unauhakika wakati unanyimwa unamfikiria akunyimaye ni kwanini ananyima  saa nyingine kinukacho kipengele?

 Na HAKI  nishai,....
....ndio maana kuna wateteao DINI watakuambia mpaka ni upotofu wa maadili  kwa jinsi HAKI ZA WATU ZIDAIWAZO KUKUBALIWA SIKUHIZI KUWA WANAPOINTI  zinavyotukania maadili ya dini kwa jinsi wafuasi wajaribuvyo kuzielewa dini zenye maelfu ya MIAKA kwa taratibu za uelewaji wa IMANI wa isemekanavyo ni kileo.:-(Na haki NISHAI,...
.... kwa kuwa haki za wengine zisipofanana na ZAKO wewe zaweza KUKUUMIZA NANIHIII na  na kukupa nyege hata ile ya  kilio.:-(


Swali la marudio :

 • Umewahi kunyimwa HAKI YAKO wakati unataka?


Kikubwa cha KUJIFUNZA ni kwamba ,...
.....baadaye BAADA YA KUNYIMWA unaweza kugundua ndio ilikuwa BONGE LA BAHATI NA MSAADA  KWAKO,....


... uliosaidia HUKUGAWIWA UKIMWI kwa kuwa ulinyimwa na ndio sababu baadaye ukafaidi tamu zaidi  MBIVU zile.:-(Swali:
 • Umeshawahi SIKIA mtu aliyelalamikia kukosa USAFIRI anavyosifia BAHATI YAKE baada ya kusikia GARI LILILOMNYIMA LIFTI limeata ajali na wasafiri wote wame ZE DEDI a.k.a wamekufa na KUFARIKI?

Labda KIKUBWA CHAKUJIFUNZA ni kwamba,...
.....ucheleweshwaji wa HAKI za mtu waweza kuwa na fundisho angalau la nini hasa ni haki kwa ANYIMWAYE.

Si utani,...
... HAKI ZA WANAWAKE zicheleweshwavyo  LABDA kuna kizazi cha VITUKUU zitafikia kusifia hilo kama sababu wanawake wamezidi NGUVU na UBABE  WA NANIHII kuliko wanaume .

Swali:
 • Umeshafanikiwa wewe binafsi kumnyima MWANAMKE haki yake ?
 • Unafikiri mwanamke hajawahi kukunyima haki yako wewe KIDUME?
 • Umewahi kunyimwa?
 • Haki ni nini?
DUH!

Nimeacha na NI  WAZO TU HILI MHESHIMIWA na NI  ruksa kulibishia!

Hebu Macka B na Dada Kofi wajiunge na makundi ya watu waliozoea kusifia kwa ndude  - Proud Of Mandela


Hebu tupumzishwe kwa MANDELA ikisemekana akishabikia watu weupe wauawe


Au hebu Baby Cham na Carl Thomas wabadili mkao kwa ndude- Oh No

Asante WADAU wote tuliokutana juzi fulani ya hivi karibuni ambao baadhi ni hawa katika picha zangu...


Photobucket


PhotobucketPhotobucket
Photobucket

Photobucket

Photobucket
Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket
Photobucket
Photobucket
Photobucket
Photobucket
Photobucket
PhotobucketPhotobucket

Read more...

Tukiangalia uwezekano wa kwamba labda KUNUNA NAKO kunaambukiza!:-(

>> Thursday, March 25, 2010


Tukiachana na kununa na kumuangalia MCHUMBA MWENYE SURA MBAYA  TULIYEMPENDA KWA TABIA wakati KANUNA  anavyotufanya TUJISIKIE ,...


... labda twaweza MPAKA kustukia ,...
.... kama una-HUZUNI jaribu kujichanganya na wenye FURAHA ili uambukizwe  ANGALAU kuchekelea HATA  kanyau bila sababu.:-(

Swali:
 • SI unajua  FURAHA nayo huambukiza na ndiyo isababishayo HUWA UNASHUHUDIA  hata baadhi ya uwajuao kwa busara nao wakichekelea pia ujinga kisa wako katika mazingira ambayo komedi babu kubwa ni MTU kajamba?

 • Umefanikiwa kununa leo?
Ndio,....
..... kama unafuraha unaweza kuambukizwa KUNUNA kisa kila LIMTU likuzungukalo limenuna utafikiri kama limebanwa HAJA-kubwa   halafu aliyeko chooni anachelewa kutoka  na kuachia wengine nao starehe.ya  kupunguza  uzito MSALANI..:-(


NI HILO TU MKUU na ni wazo tu!

SIKU NJEMA Mheshimiwa!

Au hebu tumsikilize mgomvi Winnie Mandela
Au tu wa mahaba  SHAKILA arudie tu  ndude -Moyo unalia macho yanacheka

Read more...

Tufikirie tu UTAMU wa wimbo mzuri wenye MANENO MABAYA!

>> Wednesday, March 24, 2010

Utamu wa wimbo una mambo yake,...
... ndio maana ukichunguza utakuta MPAKA kuna mtu anapenda wimbo FULANI  kwa kisa tu unaneno TAKO.:-(


Na avutiwavyo mtu na wimbo kila mtu staili yake,....
....na kuna wadaio WIMBO MZURI sio mirindimo wala maneno na ni jinsi uwakumbushavyo KITU au MTU na hata wakikuimbia huo wimbo hawafikirii maneno yanasema NINI na yana MAANA GANI na haiwaingii akilini labda huo wimbo ni matusi KWAKO.:-(


Swali:

 • Kwani kwako  wataka kusema wimbo mzuri  ni ule uuelewao maneno yake tu?

Ndio,...
... kuna ambao uzuri wa wimbo ni VIDEO yake.


Swali zaidi kidogo:
 • Huwa unafikiria LAKINI  ni kwanini unaupenda wimbo fulani?
 • SI unajua ni  kawaida  maeneo fulani  kusikia nyimbo za KANISANI kwenye baa na kuna wajipozao baada ya kuzini kwa kusikiliza nyimbo mpya za dini?


Ndio,...
.... labda unavyosikiliza wimbo  unachosikia ni VIPENGELE  VYA MAISHA katika MAISHA YAKO VIGUSANISHWAVYO na wimbo  na wala huusikilizi  wimbo kama idhaniwavyo kwa MIRINDIMO YAKE na MANENO YAKE   kitu ambacho chaweza kuwa KIMESHASABABISHA umewahi  kuukatikia kiuno wimbo wa msibani badala ya kuufanya ukusaidie kutoa BONGE LA mchozi.:-(


NIMEACHA WAZO MHESHIMIWA!

Hebu JOE ARROYO alete - YAMULEMAO


Hebu na Tshala Muana alete pia ndude-Sikila

Read more...

Mazoezi ya KUSIKILIZA usichotaka KUKISIKIA!

Jizoeshe kukumbuka ,...
....kwa kawaida kunatofauti kati ya WEWE na kisemwacho kuhusu WEWE hasa kwa kuwa hakuna akujuaye kama unavyojijua WEWE.:-(Jizoeshe kukumbuka,....
...kuwa kukwepa kusikia USICHOPENDA KUKISIKIA hakibadili kuwa kinaendelea kusemwa USICHOTAKA KUKISIKIA - na kwa kuwa hata sasa hivi kinavyosemwa hakikuathiri LABDA hakina ATHARI SANA KWAKO KISEMWACHO  hata kama sasa hivi ungekisikia kwa masikio yako MWENYEWE kwa kuwa hata sasa hivi KINASEMWA na  labda asiyekisikia tu ni  WEWE.:-(


Swali:
 • Si unajua labda sasa hivi kuna anayekuwaza vibaya na kukusema  vilevile ingawa wala hilo halikuathiri?


Tatizo lijitokezalo ukisikia USICHOTAKA KUKISIKIA ni  kwamba SASA UMEKISIKIA ,...
... lakini mambo  yako vilevile kama tu kabla hujasikia KWA AJIAMINIYE  kwa kuwa ni KWELI HUWA UNASEMWA hata kama KWA  uwezo wa binadamu  mdogo BINADAMU HUATHIRIKA pale tu agunduapo  ANASEMWA.:-(


Kumbuka kama  umefanikiwa mpaka KUSIKIA,...
.... kibaya kuhusu WEWE ambacho mpaka umekisikia labda HICHO  hakina nguvu ya kukuua  ndio maana mpaka UMEKISIKIA  WAKATI UKO HAI na kupata muda wa kukionea aibu au kukiruhusu kukuumiza tu moyo kisa eti umekisikia  KIKISEMWA .:-(


Swali:
 • Hufikiri kwenda KANISANI au MSIKITINI ni moja ya mazoezi ya waumini  ya kusikiliza WASICHOPENDA kusikia kuwa  kuna DHAMBI WAKATAZWAZO bado wao  wanazisiki tamu?
 • Huwa unafanya masoezi ya kuzoea kukosolewa au unafarijika na kumnunia au kumtukania uchi unayemsikia anakukosoa?
Ndio,....
.... inauma hasa usiyemtegemea kuwa NAYE anakusema vibaya  kwa kuwa ni NDUGU au RAFIKI YAKO,...
....ukimsikia kwa sauti yake anakuteta  au tu anatukania matege yako wakati ulifikiri anafikiri unabonge la usafiri.:-(

Ndio,....
...... yawezekana moja ya SIRI YA USHINDI KATIKA MAISHA YAKO ni  kukabili usiyopenda KUSIKIA hata YASIYOKUHUSU WEWE KAMA MTU kwa mfano ya JINSI IDAIWAVYO KUWA  tu  Michael Jackson alidai Tanzania YAKO  inanuka kwa  kuwa labda kuumia tu roho hakutakusaidia kitu UKIFIKIRI.:-(


Swali:
 • Si unajua hutaathirika hata ukisikia likitajwa jina la kitendo wazazi wako walifanya mpaka ukazaliwa ingawa hupendi hilo KUSIKIA?


NAACHIA  HAPA zoezi  la kukuzoezesha kusoma maneno usiyotaka kuyasikia!.:-(

Twende kidogo Kenya tukajifunze ya kutoa mimbaAu tu Fally Ipupa abadili zaidi kwa ndude-Ko ko ko

Read more...

UANDUNJE wa kujifunza kutoka katika matatizo WALIYOPITIA watu wengine!

>> Tuesday, March 23, 2010

Inasemekana ,...
...ni muhimu kujifunza  kutoka kwa waliofanya HICHO KITU kabla yako.:-(


Ndio inasemekana,...
....unaweza kutopoteza MUDA kwa  kuingilia BIASHARA ya chipsi mayai  kwenye eneo kama UTAJIFUNZA kwa waliotangulia kuuza CHIPSI MAYAI kwenye eneo na kujua kuwa  wateja hakuna na wapitao hapo huwa wana ulizia UGALI na sio CHIPSI MAYAI ambayo ndiyo biashara unaelekezea mtaji wako.:-(Na inasemekana;...
....utatatua tatizo la KUTUNZA MUDA kwa kutegemea  kujifunza kutoka katika MATATIZO YA WENGINE na kuepuka kufanya matatizo kama ya hao wengine yawepia ni YAKO.

Swali:
 • SI umesikia kuwa INASEMEKANA kuna msaada UNAOTOSHA FUNDISHO kwa  kujifunza kuwa ukishika moto utaungua kutoka katika stori za wengine waliowahi kuungua kwa kushika moto kuliko weye mwenyewe kugusa moto ukaungua?

CHAKUKUMBUKA tu ni kwamba,...
....aliyetangulia kufanya  KITU anaweza kuwa alikuwa MFUPI  KULIKO WEWE na stori zake za ugumu wa kufikia KIDUDE unaweza ukawa uliongezewa ugumu kwa kuwa STORI YAKE KATIKA UGUMU ilijumlisha na KURUKIARUKIA KITU KUTOKANA NA UFUPI WAKE iliafikie KIDUDE kitu ambacho hakitakuathiri wewe ambaye NI MREFU VYAKUTOSHA na huhitaji kuhangaika  na mihitaji ya msaada wa kigoda ili kujiongezea kimo UFIKIE kidude.:-(Swali:
 • Si unakumbuka WEWE sio YULE kwa hiyo ingawa ngoma ya SINDIMBA ni ileile yawezekana kukata kiuno KWAKO  ni rahisi zaidi kuliko YULE kwa kuwa wewe una kiuno kama NYIGU na ujazo wa MAKALI YAKO unatosha zaidi  NAKUIFANYA SHUGHULI YA  kuitingishia ngoma MAKALIO kwako kuwa rahisi zaidi kuliko  wengine wenye kiono kama kabati na makalio chapati ?


Ndio,....
.... kuna stori  za waliofanya UTAKACHO KUFANYA ambazo zaweza kukutisha kwa kuwa umeambiwa ni jinsi gani zilivyo washinda watu,....


.... lakini kumbuka labda walioshindwa SHUGHULI walishindwa kwa kuwa hawakuwa na kitu ulichonacho ambacho ni MTAJI WA PESA na wewe ukiingilia shughuli waliyoshindwa unachohitaji ZAIDI ni mtaji tofauti wa KUTUMIA AKILI ambao nao unao na SHUGHULI ZILIZOWASHINDA WENGINE ukiziingia kivyako mambo yatakuwa mswano.

Swali:

 • Hujastukia kujifunza kutoka kwa wengine NDIO MOJA YA SABABU  watu wengi huhofu kujaribu wenyewe hata wawiwezavyo?
 • Unauhakika hakuna CHA MANUFAA ujifunzacho kizuri kwa kuungua mwenyewe NA MOTO ili kujua maumivu ya MOTO badala ya kuogopa moto kwa kusikiliza stori za wengine za makali ya moto?

Kwa kifupi ,...
... labda kunakitu ulichojifunza kwa KUSIKILIZA STORI NA UZOEFU WA WENGINE,...
... ambazo ulihitaji kujaribu mwenyewe ili kujikwamua katika tatizo lakoLA SASA hata LILE la kuogopa KUTONGOZA MTU kwa kuwa anasifa za kunyima watu KUTOKANA NA STORI ZA WALIOJARIBU WENGINE ,....
....kwa kuwa labda KWA STAILI yako na kwa kuwa WEWE sio WALE ungekaribishwa katika ufalme na utukufu wa ukitakacho hasa ambao uko kwa UMUOGOPAYE kumtongoza.:-(


Kwa kifupi,...
....kwa kuwa CHIPSI MAYAI yasemekana haziuziki katika eneo yawezekana ni kwakuwa sio WEWE uziuzaye,...
... na ungeanzisha biashara ya CHIPSI mayai wewe na KWA UKARIMU WAKO ,usafi wa mgahawa wako, BONGE LA BATASAMU LAKO, na jinsi tu uwafanyavyo wateja wanajisikia wako nyumbani  , ungeweza kufanya mpaka  WAPENDA NGUNA aka UGALI  waanze kuja kula chipsi mayai mahali ambapo wengine wanadai hakuna wateja.:-(

Swali:
 • Umeshawahi kustukia KUJIFUNZA KUTOKA KWA WATU WENGINE haina maana ndio ujaribu KUWAIGA HAO MTUZ WENGINE?


Ndio,....
.....kujifunza katika MATATIZO YALIYO WAKUTA WENGINE,....
... labda isiwe ni KUJITISHA TU kuwa  kwa kuwa wengine walipata matatizo basi na MTU MWINGINE atakutana na MATATIZO hasa ukizingatia labda wengine waliona NI TATIZO kwa kuwa ilibidi waonge mwili wakati KWA MWINGINE ASITAYE KWA KUTISHIKA NA STORI ZA WENGINE  tayari ni MALAYA kwa hiyo hilo la kuhonga mwili ili atatue tatizo la kupanda  cheo wala si TATIZO kwake.:-(

Ndio,...
... matatizo uyasikiayo YALIYOWAPATA  wengine ,...
...yana UANDUNJE  hasa kama HUYASTADI katika kunyambulisha yatakuathiri vipi hasa kwa kuwa WEWE sio WATU WENGINE na  staili na rasilimali zako za kuanzia AKILI mpaka ujiandaavyo tu kwa kuwa na kondomu  au tu polishi ya viatu kabla viatu havijachafuka yawezavyokutofautisha TATIZO LILELILE  kwako kutofautiana na hilohilo tatizo KWAKE.:-(


NIMEACHA na ni wazo tu hili MHESHIMIWA!

Hebu twende Beira Msumbiji Djaaka wapoze mchecheto


Tubakie hapahapa Msumbiji Djaaka warudie ndude-DjogoroAu tu James Brown na Lenny Kravitz wabadili tu tena kwa ndude-Papa's got a brand new bag

Read more...

UHUSIANO wa UNACHO WAZA na WEWE!

>> Monday, March 22, 2010

Anachokiwaza MTU   kingekuwa ndicho pekee kitambulishacho UTU wa mtu ,...
... labda  wengine tusingeitwa WATU na WEWE.Na ukisoma HISTORIA utastukia , HITLER aliamini mpaka WARUSI kuwa sio watu vizuri, WAJAPANI waliamini WACHINA SIO WATU, na bila kusahau AFRIKA KUSINI kuna waliohubiri mpaka makanisani kuwa WATU WEUSI sio WATU,....
.... na ukiwaza waweza kustukia ni jinsi gani misingi ya MAWAZO HAYO yawezavyo kuota mizizi ambayo chimbuko lake ni imani kuwa MIMI kwakuwa sifanani nawe basi sina uhusiano na  WEWE.Unachowaza ,...
... labda sicho WEWE.

Lakini unachowaza,....
..... kinaweza kuwa  kinachangia  ulivyo WEWE.:-(Swali:
 • AU?

Kwa bahati mbaya NACHO -kuwaza,....
..... pamoja na yote nijuayo yana kuhusu wewe bado nikiwazacho sio WEWE.

Labda akiwazacho mtu wakati anawaza,...
... HICHO NI WAZO tu hata kama ndicho kifanyacho ufikirie unayekabiliana naye ni sio jini au MALAIKA  na ni MTU kama WEWE.:-(

Swali:

 • Unafikiri katika tafsiri yako ya ni nini ni   MTU ni asilimia ngapi inachukuliwa na ANACHOKIWAZA katika  kukutambulisha kwako kuwa yeye ni MTU?
 • Unauhakika kionekanacho kama mtu hakitoshi kuitwa  MTU?


UKIWAZA,...
... unaweza kuanza kuamini kuna watu uwajuao ambao wala SI WATU kwa kuwa labda wawazavyo na NGEDERE  wawazavyo ni sawa.:-(

UKIWAZA,...
... waweza mpaka kuamini kuna BATA wanafikiria kama KUKU kama kipimo ni mwendo wao wakuvuka barabara wakati wanalikimbia gari lako kwa spidi sawa.:-(

Swali:
 • Unauhakika unachowaza sio kikufanyacho  WEWE ni wewe au unafikiria ni sura lako zuri ndilo linauzito zaidi kuwa wewe ni WEWE?
 • Unafikiri SURA LAKO halinamchango fulani katika UNAVYOWAZA ?
 • Unauhakika sura yako haichangii unavyowazia MAHARAGE?

NIMEACHA na hili NI WAZO TU!


Hebu USTADHI Zakir Hussein atupigie-Tabla solo

Au tu turudi Msumbiji Mariza abadili kwa ndude-Barco Negro
Mariza alete pia - Oh gente da minha terra


Au tuamie tena Cape Verde ili LURA amwage kitu-Na ri NA

Read more...

Leo JUMATATU kama siku ya kufikiria KAMA ulidanganya vizuri JUMAPILI uliyoipita!

Labda waongo wazuri LEO,...
....ni wakumbukao walidanganya nini siku za JANA zilizopita.

Na labda mwenye AKILI ambaye anadanganya mtu LEO,...
....katika kusaidia kufanya uongo wake udumu vizuri anatakiwa kukumbuka ADANGANYACHO LEO na baada ya kumaliza kudanganya ADANGANYACHO LEO kuKIkumbuka ALICHODANGANYA LEO SIKU ZIJAZO  kama anataka uongo huo WA LEO ubakie na sura ileile na asiugeuze kuwa NI UKWELI siku zijazo kwa BAADA YA KUDANGANYA   kuchukulia alichodanganya KAMA NI kitu kilichopita.Swali:
 • Unakumbuka mwaka jana muda kama huu ulijidanganya nini ambacho kinaathiri kitu maishani mwako ambacho kimaisha KAMA HUJIKUMBUSHI KUWA hicho ULIJIDANGANYA hutaweza kukipita?

 • Kwani hujui KUDANGANYA vizuri kudumuko ni kazi ya WENYE akili wakumbukao kuoanisha uongo wao wa leo na ULE wa siku zilizopita?
 • Unakumbuka labda leo kunakitu umedanganya  na unakichukulia kitendo hicho kama kitu kilichopita?
Ndio,...
... labda KUSEMA KWELI  hurahisisha mambo kama nia na madhumuni ya MTU ni kujulikana MKWELI,...
... na kama UNADANGANYA lakini ukiwa na lengo lilelile la kuonekana MKWELI  wahitaji kutumia akili vizuri LABDA ZAIDI YA MSEMA KWELI  na pia jaribu kutosahau  uhusiano wa ya leo na ULIYODANGANYA yaliyopita.:-(


NIMEACHA !
Kumbuka hili ni wazo tu MHESHIMIWA ambaye angalau katika KUTONGOZA hudanganya mtu!:-(

Hebu kwa kuwa leo ni JUMATATU tujikumbushe JUMAPILI kwa kuwasikiliza Maroon 5 wakiongelea-SUNDAY MORNING

Read more...

STORI YA KAWAIDA inaweza kusaidia MTU kuisikia ikiongelea USENGE kama msomaji au ASIKILIZAYE STORI anafikiria USENGE.:-(

>> Saturday, March 20, 2010Katika stori ya kawaida ya MTU,...

... mtu anaweza kusahaulika katika SHUKURANI kama msikilizaji ni yule  aaminiye ashukuriwa ye ni MUNGU KWA YOTE hata kama ni mtu ambaye ndiye akumbushaye ya MUNGU .:-(Swali:
 • Unafikiri wakati unashida ya chumvi JIRANI akikusaidia chumvi naye hastahili SHUKURANI kwa kuwa unaamini awezeshaye yote ni MUNGU?
 • Si unajua stori ya matatizo kwa atafutaye na afikiriaye MASHUJAA anaweza kuwa anasikia  stori za kishujaa tu katika ZE HADITHI?Ndio,...
... stori ya KAWAIDA YA UHANGAIKALO NALO,...
... unaweza kuigeuza kuwa ni YA MATATIZO ingawa uhangaikalo nalo na JINSI UHANGAIKAVYO NALO wengine huita HILO ni ``MAISHA TU`´hasa  kama unaangalia uhangaikalo nalo kwa LENSI ya matatizo na sio kwa lensi  YA MAISHA ambayo  moja ya jinsi ya kusaidia jipu lipone NI KULIBINYA JIPU.:-(

NI WAZO TU HILI MHESHIMIWA!

Hebu turudi MALI   ili Mama Toumani KONE arudie ndude - NiemogoAu tu turudi Tanzania Omar KOPA arudie ndude nzito iitwayo-UNYAGOAu tu Omar Kopa aongee busara zilizo tafutiwa mpaka siku kwa WABONGO -Kitchen Party

Read more...

UNAFIKIRI NI MARA NGAPI mtu aongeaye na wewe huwa ANAONGEA NA WEWE yakuhusuyo wewe na sio uliyompa nafasi tu KUYAONGEA ingawa alikuwa nayo kichwani kabla ya kukutana na WEWE?

Kuna waongeleao WALI ukiwapa nafasi ya kuongelea WALI ,...
... wakati wakifikiriacho kabla ya wewe KUSAIDIA UWEZEKANO WA WALI KUONGELEWA  kilikuwa ni UGALI.:-(


Swali:

 • Unabisha?Aongeacho mtu kuhusu WEWE kinawezekana hakikuhusu wewe na kinatokana tu na UZOEFU WA YASIYO KUHUSU YA AONGEAYE hasa ukizingatia hakuna amjuaye mtu mwingine vizuri UKIFIKIRIA  ingawa ni rahisi  hata kudhania kwa kuwa mtu ni ndugu yako basi kuna kitu anajua katika wako UBINADAMU.:-(Swali:
 • Lakini wewe unajijua?
 • Unauhakika unawajua vizuri hata wazazi wako hasa ukifikiria hujui kwa uhakika walikutengeneza chumbani  au  migombani wakati wanatoka kwenye msiba wa jirani?
 • Lakini si unajua kwa kutojiamini na kujijua kwako kunaweza kuwa ndiko kusaidiako KUAMINI KWAKO kuwa labda kuna mtu mwingine zaidi yako ndiye anaye KUJUA zaidi?


Ndio,...
.... baadhi ya tafsiri ya MATATIZO MENGINE YA MTU hutokea kwa kuwa MTU HUYO MHESHIMIWA kajifunza na kufudhu kutegemea WATU WENGINE WANAFIKIRIA NINI KUHUSU YEYE mpaka wanafikia kuamini hata kitu kidogo ambacho wanakijua kwa kujiangalia kwenye KIOO kinategemea watu wengine waseme uzuri wa MIDOMO YAO KAMA BIRIKA ni mizuri namna gani au tu ni watu wazuri vipi kwa kuwa hawakosi kwenda msikitini.:-(


NIMEACHA!

Hebu tubadili kwa SANCHEZ kurudi ndude- FRENZYAu Tanto Metro and Devonte warudie kitu-Gal say Wooee
Tanto Metro na Devonte warudie-Everyone Falls in Love

Read more...

Siku mtu akionjwa WAKATI kashadakwa na ugonjwa wa kichaa uitwao MAPENZI!


Penda,....
..... na waweza kujikuta unashabikia vijulikanavyo na wanao kujua kuwa huwa vinakutia KINYAA.:-(

Penda,....
.....na waweza kujikuta aibu zinakuisha na kukusababisha uonekawaida na kudhani ni moja ya kuonyeshwa penzi kuombwa kitengeneza watoto sehemu ambazo zilitengwa katika majengo ili bila BUGUDHA watu wajifungie na KUNYA.


Penda,...
.....na waweza kujikuta kwa mara ya kwanza KWA SAUTI UNABISHANA na wazazi wako ambao busara zao ulikuwa unazitegemea kama ndio misingi ya maamuzi yako ya hata ni kwanini wewe INJINIA SIKU HIZI wakati ungekuwa MPISHI  MENYE FURAHA kama ungejisikiliza wewe mwenyewe kama ujisikilizavyo WEWE BINAFSI  NA KUWA NA UHAKIKA NA BUSARA ZAKO KATIKA MAAMUZI YAKO kama  hasa UJIAMINIVYO NA MAAMUZI YAKO katika kutiii ni muda gani ILIUSIJINYEE inabidi uende chooni KUNYA.:-(


Swali:

 • Unafikiri kama ungekuwa mtiifu kwa unaloliamini ni KWELI ,- kama ulivyokuwa MTIIFU KUHUSU YAKUHUSUYO WEWE BINAFSI kuwa iliusijikojolee ni muda gani inabidi uende kukojoa,... -unafikiri ni mangapi katika maisha yako yangefanana na wewe au picha yako ya dunia utakavyo iwe?
Ndio,...
... kuna uwezekano ukiongea na mgonjwa wa MAPENZI busara zako hazina maana kwa kuwa zinatetea kitu KWA KUTUMIA AKILI ZAIDI YA HISIA wakati uongeaye naye anatumia HISIA ZAIDI YA KUJADILI SWALA KIAKILI kitu ambacho labda ni aina ya UKICHAA.:-(


Na kwa bahati mbaya naweza kusema pia; `` NDIO´´,...
....UKICHAA uletwao na PENZI huweza kusababisha CHUNGU KIDOGO kuonekana tamu SANA  na kwa hilo labda MAPENZI ni aina tu ya UKICHAA.:-(

NIMEACHA!

Kumbuka NI WAZO TU HILI Mheshimiwa na unaruhusiwa kulitukania!:-(

Hebu Ray Parker Jr abadili kwa kuwatetea wanaume katika ndude- I don't think MAN should sleep ALONE.
Au tu ASWAD warudie -Gotta find a wayAu tu ASWAD waendelee tu na ndude- I need UR LOVE

Read more...

Kwanini ?: -(

>> Friday, March 19, 2010


[Tahadhari: Katika wazo LILILOPINDA KWA WAVIVU WAKUFIKIRIA bado taralila ina neno CHUPI.:-(].......WAKATI  kuna  MPENDA KEKI alazimikaye  KUGIDA MIHOGO wakati  wengine  kwa hiari yao  WENYEWE hawaonji wagawiwazo KEKI  kwakuwa wanasubiria MIHOGO,...
....yaweza kumtungishia  MTU MIMBA ya swali;...
....``KWANINI?´´:-(


Swali:
 • AU?

Ndio ,...
...KWANINI ,...
....ni SWALI la kawaida la  mtu!:-(
Swali:

 • Unabisha?KWANINI katika taralila yaweza kuwa  ,...
....katika chupi YA KITABIA  ivaliwayo siku ya MTU kupania kumuonjesha MCHUMBA  utupu kwa mara ya kwanza  ,...
...chupi HUWA imepaniwa iwe SAFI ZAIDI ya siku ambayo MCHUMBA HATA ANGALAU  kwa mbali hatapewa nafasi ya kukodolea uwezekano wa ``MPENZI hajavaa KIFICHA NYETI ´´  kistaarabu ,... na labda NDIYO kiashiriacho  kuwa MSTAARABU HUTAKIWI KUJUA kunasiku  mtoto mzuri  UMJUAYE KWA USAFI  labda chupi yake sio safi sana kama KIBANGA ALIYEMPIGA MKOLONI ,...

.... NA inaweza HILO  kuwa ndilo  SWALI  la MTU!:-(

NA kwanini,......
....msibani AU HARUSINI  kuna wahisio PILAU HUNUKIA  vizuri zaidi kuliko KWA MAMA NTILIE YULEYULE ambaye  ndiye aliyekuwa na TENDA MSIBANI na PIA ZILE HARUSI KADHAA ULIZO HUDHURIA  ambazo ilibidi tu uende kwa kuwa hukuchangia  pesa hata za kujionyesha tu KWA WAPAPARIKIAO WAJIONYESHAO  kuwa wanapesa kweli kifisadi ,....
...na LABDA  hilo pia NDILO ni SWALI  la mtu!:-(
Kwanini,...
...HATA ambaye kwa kawaida ndiye MWENYE NYEGE  YA DINI  AAMINIZO ZINAPELEKA WASIO WAJANJA DUNIANI  kule MBINGUNI wakati  KUMBE  sio kila wakati HUYO NDIYE anajiamini kama ATAMKIAVYO WASIOJIAMINI  hasa wakati atulizavyo manyanga ILI MEZA  itulie,...
....halafu ikitulia ndio mnastukia kumbe YEYE  NDIYE  yule  mtu wa MIZOGA wakati anaokoa SIKU  katika juhudi zake za wa ngono YA ufisadi,....


....ndio  laweza kugeuka kuwa ndilo  GUMU KINAMNA swali la MTU.:-(

Swali:
 • Kwa WATANZANIA unafikiri ni kwanini Mheshimiwa KIKWETE na sio Mheshimiwa PROFESA SARUNGI au Mheshimiwa RASHIDI KWAWAWA ndiye aliye tangulia kuwa MHESHIMIWA RAIS  WA TANZANIA kabla ya Waziri mkuu  MORINGE SOKOINE ?

 • Unauhakika kwanini YESU hakuwa MWANAMKE?

 • Umeshawahi kujiuliza NI KWANINI SIO kila lifanyikalo LIKUHUSULO HUWA UNAKUMBUKA kujiuliza KWANINI?


Ndio,...
....LABDA ni kweli  ,....
....KWANINI ni KIBONGE LA SWALI  ndio maana SIO rahisi KUJIULIZA
ni kwanini  inasemekana kuna  MWINGINE  aliyevulia mtu chupi mara moja tu  na akapata KITU CHENYE THAMANI YA UWAZIRI wakati kuna aliyevulia chupi  ZAIDI YA WATU WANNE NA NUSU  na kutopata  angalau  BILAURI MOJA ya UJI WA MUHOGO wa asubuhi moja.:-(


Ndio,...
...labda kuna sababu ,....
....KWANINI ,...
....ni SWALI la mtu.:-(
Swali:

 • KWANINI?
 • Tukiachana na UjingaBUSARA wa hiki KIJIWE huwa  LAKINI unakumbuka kujiuliza KWANINI mara kwa mara MAISHANI?

DUH !
NIMEACHA WAZO MHESHIMIWA lakini ni wazo tu HILI MKUU !:-(

IJUMAA na WIKIENDI NJEMA MHESHIMIWA!

Hebu Hugh MASEKELA abadili tu kwa kutukumbusha SOUTH AFRICA katika JAZZ katika ndude- Strawberry

Tubaki tu Afrika Jimmy Dludlu aendelee TENA kujaribu kulainisha wajanja kwa ndude -Tote
Au tuhame tu na tupate ndude -Casanova kutoka katika unajisi wa   shughuli wa - Levert

Read more...

kWA bahati mbaya MUDA hauponyi MAUMIVU!:-(

>> Thursday, March 18, 2010

Ndio,...
....kunauwezekano UFANYACHO NDANI YA MUDA baada ya kuonja UTAMU ndicho KIKUPONESHACHO kumbukumbu ZA jinsi  ulivyowahi kuusikilizia UTAMU.:-(

Ndio,...
....kuna wasemao kwa ung'eng'e ``TIME HEALS´´ a.k.a ``MUDA UNAPONYA´´ ingawa mimi ningependa kukualika ukae mkao wa kufikiria uwezekano wa kuwa - ``IT IS WHAT YOU DO within that TIME  that DOES THE TRICK´´ a.k.a  kwa lugha ya wajanja-``NI UFANYACHO baada ya KUUMIZWA au KUSIKILIZISHWA UTAMU ndicho kinaweza kukusahaulisha na KUPONYA uyakumbukavyo MAUMIVU  au  tu ule wa lawalawa UTAMU´´.:-(
Swali:


 • Kwani ni kweli  ulifikiria maumivu na WIVU wa mwenye MPENZI aliyestukia MPENZI wake aliyekuwa anafikiri ni wake peke yake tu  anagawia na wengine UJANJA huwa yanaponeshwa na MUDA TU bila kwa hilo lijamaa aka HILO lililostukia linadokolewa penzi na wajanja kujishughulisha na kitulizo kingine ambacho labda ni KWA kujisomea KORANI na kumsikiliza mchungaji wa PENTEKOSTE?

 • Unafikiri ni MUDA TU na sio na michango ya vitu hovyo kama vile WALI , mikate na VIAZI  ambao vitakusaidia kusahau UTAMU wa UGALI NA MAHARAGE   hapo baadaye ukiamua kujisahaulisha tamu yake kwa kuwa inakukumbusha sana MBWA wako mpenzi alipozirahi na kufariki dunia?Ndio,...
... labda MUDA haukuponyeshi  UKUMBUKAVYO utamu wa MAKANDE YALIYO CHACHA kama ndani ya muda baada ya kula PURE a.k.a MAKANDE yaliyochacha hautashughulika na kitakacho KURUDISHIA kumbukumbu ya UTAMU HALISI wa yale matamu MAKANDE.:-(Ndio,...
....ukifikiria LABDA utastukia  ni KWELI kuna kitu umefanya katika muda  na sio MUDA TU ndicho kilichofanya hukumbuki vizuri ulivyotishika na DHAMBI baada ya kufanikiwa kwa mara ya kwanza kuifanya MAKUSUDI ndio sababu LABDA siku hizi unarudia HIYO dhambi makusudi KIRAHISI bila kujisikia vibaya sana.:-(


Ndio,...
....MATUMIZI ya MUDA na labda WALA sio muda ndicho kisababishacho kuna aina ya UTAMU huisahau na kunaaina ya MAUMIVU labda unailenga makusudi ili kujikumbusha jambo FULANI ingawa bila kufikiria ndio maana kuna MPENZI husahau maringo yake.:-(NI WAZO TU HILI MHESHIMIWA na haki ya nani tena NIMELIACHA!

Hebu tubadili kwa kwenda kiduchu  BRAZIL  Sergio Mendes atuletee tena kitu-Magalenha
Au tu Sergio Mendes na The Black Eyed Peas warudie ndude-Mas Que Nada


Basi bwana , tubaki tu na Black eyed Peas ya enzi ZILE katika kitu kitukumbushacho wikiendi bado haijafika kiitwacho-Weekends

Read more...

BABA n'takusemelea kwa MAMA! OooooHO!

>> Wednesday, March 17, 2010

[Tahadhari: Wazo linatapatapa katika TARALILA HII!]


NIA ya kumsemelea MTU kwa mtu,....
..... inaweza kutoa SIRI ya MTU WA TATU  ASEMELEAYE MTU ya anawafikiriaje hao watu wawili ajitahidio kuwaunganisha kwa MSEMELEO.:-(


Kuna wadaio PIA kuwa ukisemelea mtu,...
.... nia yako ni kutaka tu UKWELI ujulikane na  SIO KINGINE,...
...na ikitokea kama unayemsemelea AKIPATA KIBANO basi hiyo huwa ni BONASI  tu kama kwenye CHIPSI dume ilivyo KACHUMBARI ,....

....NA NI BONASI tu PIA  kama  UTAPATA FARAJA SANA TU  hasa ikitokea ukashuhudia matunda yale YAKUSEMELEA KWAKO - yale  ya KUGOMBEZWA kwa MTU, kubinywa KWAKE makende, KUFINYWA au tu KUDHALILIKA kukifanikishwa kutokana na wako MSEMELEO.ILA kwa bahati mbaya ukiangalia tabia za watu,...
.... utastukia KWA KAWAIDA afikiriwaye ni MNYONGE ndio HUSEMELEWA kwa MBABE ili ikiwezekana ishuhudiwe akigawiwa MKONG'OTO au angalau KUGOMBEZWA kidogo baada ya MSEMELEO.:-(

Swali:
 • Unafikiri KIINI cha KUWASHWA kwa mtu mpaka ASEMELEE KITU kwa MTU huwa ni kweli ni NIA UKWELI UWE WAZI  watu tumjue anyaye pembeni ya choo na KUFUTIA UTAJIRI kwenye ukuta wa choo ni nani au nia ni KUJIFAJIRI kwa MSEMELEAJI kwa KITENDO CHA KUSEMELEA?
 • Unakumbuka mara ya mwisho uliposemelea MTU?

 • Unafikiri kwa kawaida Tanzania , BABA akisemelewa kwa MAMA ina -nguvu?


NABADILI kidogo;....

Ndio,....
..... kunauwezekano hata ukiisemelea SERIKALI YA TANZANIA  kwa WANANCHI,...
..... wananchi hushindwa kufanya kitu  ingawa ndio wenye NGUVU na matokeo yake wengi twashuhudia  WASEMELEAO  WANANCHI kwa SERIKALI  kwa kuwa wanajua  SERIKALI ina polisi  na MAGEREZA-  bila kusahau vyombo vya habari ivitawalavyo ambavyo vyaweza kustua watu NCHI NZIMA  wasiona HATA NA mpango na WEWE  kuwa umekaa uchi bila kificha nyeti  UDHALILIKE kwenye jamii na kwa ALIYEKUSEMELEA.


NARUDI PALEPALE;.....


Ingawa kirahisi katika JAMII ya KITANZANIA inaweza kuaminika ``MAMA ntakusemelea kwa BABA´´ inanguvu zaidi ya ``BABA ntakusemelea kwa MAMA´´,...
.... ukweli wenyewe waweza kuwa  uko kinyume kwa kuwa labda MAMA ndio mwenye nafasi nzuri ya kumuadhibu BABA kama  adhabu aamuayo kuitumia NI ITUMIAYO AKILI ZAIDI na sio ile ioanishwayo na MIGUVU ya MISULI na PESA za BABA.:-(


Swali:

 • Si unakumbuka achangiaye kuonekana MWANAMKE ni dhaifu inawezekana ni MIMI na WEWE hasa weye mwenyewe MWANAMKE?

 • SI imekuwa kawaida kwa MWANANCHI kusemelewa kwa vyombo vya mabavu vya SERIKALI mpaka inasahauliwa ni WANANCHI HAOHAO WAOGOPAO SERIKALI  ndio bila wao hakuna SERIKALI hata hiyo isiyowajali yaweza kujitutumua kwa MAGUVU?

 • Unauhakika lakini BABA mwenye MIGUVU na MAMA wakianzisha vita baada ya wewe kumsemelea BABA kwa MAMA hawezi kudedi MDINGI ambaye kazoea kupikiwa na MAMA MWENYA AKILI  na kutarajia MINOFU YOTE MIKUBWAMIKUBWA ya BATA apewa yeye kwenye ZE MLO ambao watoto huambulia mchuzi na  mabakimabaki ya chembechembe za mnofu wa BATA kabla BABA hajarudi usiku KALEWA?
Ndio,...
NIA ya kumsemelea MTU,....
..... inaweza ikawa ni kujisikia vizuri tu kwa ASEMELEAYE hasa kama anachokisemelea hakimuhusu ASEMELEAYE kuwa UNANANILIHIII   ambacho   hata KISIPONANILIWA hata afanyeje HATA KINANILII  YEYE .:-(

Ndio,....
.... sibishi kuna ASEMELEAYE mtu,....
.... kwa nia ya kusawazisha kosa ili UNAYENANILII usijezoea tabia MBAYA ambayo itasababisha UNANILIWE hapo baadaye.:-(


NIMEACHA wazo MHESHIMIWA na kumbuka hili ni wazo tu ambalo ni  RUKSA kutolielewa!:-(
BWANA na BIBI wasifiwe!


Tupoze basi kwa kumsikiliza tena Mheshimiwa IDD AMIN
Tuendelee kidogo na Mheshimiwa Idd AMIN


Na tumsikilize kidogo tena Mheshimiwa  KIBAKISasa twende kwenye KIPELE nikilengacho bila utani-Where Will We Find Tomorrow's Leaders?

Read more...

UBINADAMU DHAIFU uletavyo mapungufu mpaka katika kile KITU watu HUNUNUA!:-(

>> Tuesday, March 16, 2010

[Tahadhari: Taralila hii KUNAUWEZEKANO  ina wazo lililopinda!:-(]
BINADAMU katika anunuayo:....


....katika CHAKULA,...
....LABDA katika MAPUNGUFU hununua msosi akifikiria UTAMU badala ya VIRUTUBISHO VYA MWILI ambavyo kwa BINADMU ndivyo muhimu kiafya na UZIMA.:-(


Katika WACHUMBA ,....
.... labda hununua hata kwa mizawadi LIMTU ZIMA na MITABIA YAKE MIBOVU wakati labda wahitajicho katika mtu ni SEHEMU ZAKE TU BAADHI au tu zile za siri , - kitu kisababisha BINADAMU huendelea  kujikuta CHUMBANI  yuko na Limtu LIZIMA.:-(


Katika fulani  DINI,....
....kwa sadaka na MWENENDO labda MTUZ hujinunulia STAILI YA MAISHA  kama IHESHIMIWAVYO NA BINADAMU badala ya kustukia havinunuliki VIKUZA IMANI vile vilainishavyo woga wa  MUNGU MWEMA lakini ACHOMAYE VIUMBE alivyoviumba KATIKA wabadaye UZIMA.:-(


Swali:
 • Unafikiri KIBINADAMU ni rahisi kununua samaki bila shombo yake?
 • Kwa BINADAMU unafikiri kuna anunuacho ambacho hakina makapi hasa ukifikiria hata katika chakula kitamu KILIWACHO ni asilimia ngapi huja na kile ambacho BAADAYE binadamu hukiita  mavi?


Ndio,...
....LABDA katika UDHAIFU WA KIBINADAMU huwezi kununua SAMAKI bila MIBA yake.:-(


Na NDIO,...
....labda kila BINADAMU anunuacho lazima kiwe KIKUBWA zaidi ya ahitajicho na akinunua GARI basi amenunua na matatizo  YA GARI LAKE  na akinunua CHAKULA kitamu basi HICHO  lazima kije  na uzito utakaogeuka mavi yake. .:-(

Swali:
 • AU?

Ndio,...
...labda katika kila kitu anunuacho BINADAMU ni KIKUBWA kuliko MAHITAJI YAKE,....
....na labda hata chupi inunuliwayo NA KIGOLI imezidi UKUBWA kama inaziba tako zima KAMA nia ya asili ya UTUMISHI WA CHUPI ili kuwa ni ili izibe matundu mawili tu YA SIRI ya KIGOLI yaliyo mbele na  SEHEMUSEHEMU ZILE  fulani katika ramani YA  YALE  makalio YAKE.:-(

Swali:

 • AU?

Ndio ,....
...labda hata uendeayo SHULE ili ujisikie UMEELIMIKA yamezidi UKUBWA kuliko MAHITAJI YAKO ndio kisa  katika MIA ya uyasomayo darasani  labda ni moja KATIKA HAYO  ambalo UKIKAA VIBAYA  utakiona cha mtema kuni  kikweli  MAISHANI NA KUKIKUMBUKA  UKIJUTIA kwa kuwa DARASANI hukuelewa hicho MAANA YAKE .:-(.

NI WAZO TU HILI MHESHIMIWA !:-(


Au tu tumpate Ex Plantashun mwingine a.k.a 2FACE IDIBIA akija na Wyclef Jean katika ndude- Proud to be AFRICANAu tubaki tu hapahapa Nigeria Ex Plantashun Boiz  2FACE IDIBIA aje na R.Kelly waweke twist katika wimbo wa ya MAD COBRA katika -FLEX


Au tu MAD COBRA mwenyewe arudie classic -FLEX

Read more...

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP