Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

UZURI wa HADITHI NZURI kwa TAKO MOJA ikiwa ni kwa kuwa ina stori MBAYA kwa TAKO FULANI jingine!:-(

>> Tuesday, March 16, 2010

Misingi ya  uzuri wa HADITHI NZURI  kwa WATU hutofautiana,.....

... na kuna WENGI  ili wanogewe na HADITHI basi HADITHI hiyo inahitaji kuwa na PANDE MBILI na moja ni ile yenye  kuhakikisha USICHOKIPENDA au USIYEMPENDA stori HIYO inampa sifa MBAYA.:-(


Swali:

  • Si unakumbuka hata stori ya KIBANGA ampiga MKOLONI kwa waipendayo  wengi  ni kwa kuwa inapande mbili ile ya``KIBANGA´´ na ile ya ``MKOLONI´´ ,- na waipendayo hiyo stori hasa wamshangiliao ``KIBANGA`` ni kwa kuwa wanajua stori ina habari mbaya kwa ``MKOLONI´´?

  • Si unakumbuka MOJA YA MISINGI ya stori za SUNGURA MJANJA na MWEREVU   ili ziwe tamu huhitaji kumfanya FISI aonekane ZEZETA na anatabia mbaya?

Ndio,...
.... HADITHI NZURI za MUNGU hasa kwa wenye dhambi,...
.... zinaweza kuwa ni TAMU tu kwa washabiki wa MUNGU kwa kuwa kwa kawaida  katika hadithi hizo  MUNGU hushinda na UPANDE WA PILI  WA HIZO HADITHI  huwa  zina stori zimpazo SHETANI sifa MBAYA.


Swali:
  • AU?


Ndio,...
... kuna watu hata katika STORI IKUHUSUYO wewe na MTU MWINGINE ,....
..... ili STORI IWE TAMU watanogewa kama katika stori hiyo WEWE UNACHEMSHA, unapewa kibano au tu UNA SURA MBAYA kuliko huyo MWINGINE  mwenye pua  kama JIPU zuri.:-(

Swali:
  • Unafikiri kwa watu wengine ILI stori nzuri ya WAAFRIKA IFANE  haihitaji kumgeuza adui YULE MWINGINE,  yule MZUNGU, Mhindi  au MUARABU?
  • Si unajua ni kwanini kuna MA-HATERS duniani  na  ni kwanini  inabidi stori NZURI ili iwanogee inabidi wachukue hatua mkononi na  kusababisha stori nzuri ya CHUPI YAKO  WAIHARIBU TU MAKUSUDI na kuitia UBAYA kwa madai unaipenda KWA KUWA mbele kidogo kwa chini imetoboka YOTE NI  ili KUKUNUNISHA TU ujisikie VIBAYA?
Ndio,...
....stori nzuri ya TAKO HILI zuri,...
....labda imejengeka katika misingi ya kuwa apendaye stori hiyo ya tako,...
...NI KWA KUWA inamsaidia kujiaminishia TAKO LILE jingine  asilolipenda ni BAYA.:-(


NIMEACHA!

Hebu twende NIGERIA tukutane na ex-Plantashun Boiz  FAZE aongeleekuvunjika kwa kundi katika- Faze Alone


Au tubaki tu Nigeria FAZE aongee na mmoja wa ex-Plantashun Boiz 2FACE IDIBIA katika-
Letter to my Brother

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP