Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

MAHARAGE ni yaleyale YA JANA lakini si kila siku yana UTAMU ULEULE wa jana.:-(

>> Wednesday, March 10, 2010

UTAMU wa kitu ni tafsiri tu  ya UBONGO,....
......ulavyo maharage yaleyale si lazima unasikia UTAMU uleule.:-(

Na utamu wa MAHARAGE yaleyale waweza kuathiriwa na hali ya ULIMI wenye vionjo vipelekavyo umbea kuwa umekula tena maharage kwenye UBONGO,...

.... kwa hiyo labda KUNA SIKU  usipounga maharage na UKIUNGA maharage HAKUNA TOFAUTI YA UTAMU na utamu uusikiliziao huwa  ni MAZOEA TU  yaleyale kuwa kwa kuwa maharage yana rangi ILEILE basi utamu wa matako yake ni uleule .:-(


Swali:
  • Si unakumbuka utamu wa hata PENZI  lilelile NI  KEMIKALI  mwilini zitafsiriwazo na UBONGO na laweza sababisha penzi la juzi na jana la mpenzi huyohuyo kutofautiana makali ya usikiliziavyo ya chachandu ya penzi?

  • Kwani HUSTUKII kama leo umekula chakula kile kile ulicho kula jana kunatofauti ya utamu?


Utamu ni michezo ya UBONGO,...
..... kama una njaa ya kutosha  ,....
...LABDA huo sio wakati wa kuamua UNAUHAKIKA na UTAMU wa kitu  kwa kuwa MKAO wa  UBONGO WAKO WAKATI UNA NJAA waweza kusababisha nyama ya KUNGURU  kiutamu KWAKO  ifanane na ya KUKU.:-(


Swali:

  • Unabisha?

Kwa bahati mbaya ,....
....WAKATI UNASIKIA TAMU ,...
.....ukichunguza aina ya utamu nyuma yake KUNA SABABU.:-(

NI WAZO TU HILI MKUU!



Hebu tudeku porojo kuhusu UBONGO



Au HEBU tu GEORGE CLINTON na THE P FUNK ALLSTARS warudie- Atomic DOG



Au HEBU tu turudi tena ALGERIA ili CHEB KHALED alainishe kidogo kwa-DIDI

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP