Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Mazoezi ya KUSIKILIZA usichotaka KUKISIKIA!

>> Wednesday, March 24, 2010

Jizoeshe kukumbuka ,...
....kwa kawaida kunatofauti kati ya WEWE na kisemwacho kuhusu WEWE hasa kwa kuwa hakuna akujuaye kama unavyojijua WEWE.:-(



Jizoeshe kukumbuka,....
...kuwa kukwepa kusikia USICHOPENDA KUKISIKIA hakibadili kuwa kinaendelea kusemwa USICHOTAKA KUKISIKIA - na kwa kuwa hata sasa hivi kinavyosemwa hakikuathiri LABDA hakina ATHARI SANA KWAKO KISEMWACHO  hata kama sasa hivi ungekisikia kwa masikio yako MWENYEWE kwa kuwa hata sasa hivi KINASEMWA na  labda asiyekisikia tu ni  WEWE.:-(


Swali:
  • Si unajua labda sasa hivi kuna anayekuwaza vibaya na kukusema  vilevile ingawa wala hilo halikuathiri?


Tatizo lijitokezalo ukisikia USICHOTAKA KUKISIKIA ni  kwamba SASA UMEKISIKIA ,...
... lakini mambo  yako vilevile kama tu kabla hujasikia KWA AJIAMINIYE  kwa kuwa ni KWELI HUWA UNASEMWA hata kama KWA  uwezo wa binadamu  mdogo BINADAMU HUATHIRIKA pale tu agunduapo  ANASEMWA.:-(


Kumbuka kama  umefanikiwa mpaka KUSIKIA,...
.... kibaya kuhusu WEWE ambacho mpaka umekisikia labda HICHO  hakina nguvu ya kukuua  ndio maana mpaka UMEKISIKIA  WAKATI UKO HAI na kupata muda wa kukionea aibu au kukiruhusu kukuumiza tu moyo kisa eti umekisikia  KIKISEMWA .:-(


Swali:
  • Hufikiri kwenda KANISANI au MSIKITINI ni moja ya mazoezi ya waumini  ya kusikiliza WASICHOPENDA kusikia kuwa  kuna DHAMBI WAKATAZWAZO bado wao  wanazisiki tamu?
  • Huwa unafanya masoezi ya kuzoea kukosolewa au unafarijika na kumnunia au kumtukania uchi unayemsikia anakukosoa?
Ndio,....
.... inauma hasa usiyemtegemea kuwa NAYE anakusema vibaya  kwa kuwa ni NDUGU au RAFIKI YAKO,...
....ukimsikia kwa sauti yake anakuteta  au tu anatukania matege yako wakati ulifikiri anafikiri unabonge la usafiri.:-(

Ndio,....
...... yawezekana moja ya SIRI YA USHINDI KATIKA MAISHA YAKO ni  kukabili usiyopenda KUSIKIA hata YASIYOKUHUSU WEWE KAMA MTU kwa mfano ya JINSI IDAIWAVYO KUWA  tu  Michael Jackson alidai Tanzania YAKO  inanuka kwa  kuwa labda kuumia tu roho hakutakusaidia kitu UKIFIKIRI.:-(


Swali:
  • Si unajua hutaathirika hata ukisikia likitajwa jina la kitendo wazazi wako walifanya mpaka ukazaliwa ingawa hupendi hilo KUSIKIA?


NAACHIA  HAPA zoezi  la kukuzoezesha kusoma maneno usiyotaka kuyasikia!.:-(

Twende kidogo Kenya tukajifunze ya kutoa mimba



Au tu Fally Ipupa abadili zaidi kwa ndude-Ko ko ko

1 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

chib 11:16 am  

:-0

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP