Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Kwa kuwa kunauwezekano MWIZI hajisikii ni MWIZI wakati anaiba!:-(

>> Tuesday, March 02, 2010



Kwa bahati mbaya,...
.... UWEZO WA KUNYA hauhakikishii MNYAJI kuwa wakati anakunya ANAJISIKIA anakunya:-(


Kabla sijaanza,....




Swali:

  • Unafikiri  umjuaye kuwa ni MALAYA huwa ni kweli anajisikia MALAYA wakati anafanya umalaya?



Ndio,...
.... kuna uwezekano MJINGA hajisikii anafanya ujinga ,...
.... ndio maana LABDA ufanyikaji wa YAKIJINGA kwa kawaida  ni rahisi.:-(


Ndio,....
.....YAFANYIKAYO Iringa,...
... labda ni yaleyale ya DAR-es SALAAM  kama  hayaoanishwi na IRINGA kwa kuwa KIMPUMU au tu KONYAGI ileweshayo  ni ileile ,...

...na kama UKILEWA HUFANYA UJINGA  waweza kurudia ujinga uleule uliofanya SUMBAWANGA  ukiwa KIBAHA kirahisi.

Swali:
  • Si unajua KUUA MTU ni rahisi kwa baadhi ya watu kama wafikiriacho WAKATI WANAUA MTU  sio KUUA ila ni kwamba wanampiga tu  MWIZI?


Ndio,....
.....kuna uwezekano unachofanya sasa hivi  unakifanikisha kwa kuwa hujisikii na KUONANISHA wewe ULIVYO na WEWE  UFANYACHO,...

... ndio maana kirahisi unaweza kuwa  mahiri katika KAZI YAKO  ya UZIBUA CHOO wakati unajisikia  VYEMA TU kuwa wewe ni  bonge la MKURUGENZI hasa kwa kuwa choo usafishacho ni cha IKULU nasio cha STENDI na jina la cheo chako ni AFISA USAFI.:-(




NI WAZO TU HILI Mheshimiwa na nimeliacha!

AU?


Hebu DOROTHY MASUKA abadili hali ya hewa kwa kitu- IMALI YAMI




DOROTHY MASUKA aendeleze kwa ndude-Kwa Nhingirikiri





Au hebu tu DOROTHY MASUKA arudie pia ndude- TEYA TEYA

3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

o'Wambura Ng'wanambiti! 6:27 pm  

Lakini kweli mkubwa!

Mija Shija Sayi 7:29 pm  

Nimekubali Simon.

Simon Kitururu 2:35 pm  

@Kadinali Ng'wanambiti + Dada Mija: Si utani!:-(

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP