Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

MTU na KITU kichezacho karibu na AJISIKIAVYO VIZURI!

>> Friday, March 05, 2010



Aina yako ya KUJISIKIA VIZURI,....
......  kama vile tu  ilivyo uchaguavyo ni nini TAMU yawezekana staili zake UMEJIFUNZA tu.



Swali:
  • Si unakumbuka KUJISIKIA VIZURI baada ya kuangalia MPIRA wa miguu unahitaji UJIFUNZE  kwanza ujue MPIRA WA MIGUU ndio nini na utamu wa BIA kuna walioona chungu kwanza kabla ya kufudhu KIFUNDISHO  na kugeuza utamu uleule wa KILAJI  kuwa ni MTAMU?



.....KUJISIKIA VIZURI  ,...

..... ni bonge la sayansi  NA USIPOANGALIA inawezekana UMESHAJIFUNZA  NA KUKOMALIA kutaka UPATE KITU  au MTU ndio ujisikie vizuri kuwa ni kweli UNAISHI na hauko hai tu.





Swali:
  • Unauhakika KUJISIKIA KWAKO VIZURI hakutegemei upate kitu hata chakijinga kama vile PETE?



Na ukichunguza waweza kugundua kabla ya kutaka uwe na KITU kama GARI  zuri , CHUPI NZURI , baiskeli ngangari au tu NYUMBA NZURI ili UJISIKIE VIZURI,.... 

... ulianza kufanya mazoezi ya KUTAKA VITU  ili UJISIKIE VIZURI  kuanzia ULIPOZALIWA tu kwa kustukia ili UJISIKIE VIZURI ulihitaji KITU NYONYO la MAMA, halafu ukaelekea kwenye KULILIA kitu  PEREMENDE ili UJISIKIE VIZURI , mpaka ukahamishia kuhitaji kitu - RABA MTONI aka LA KUCHUMPA ,  yote IKIWA  ni katika kuendelea kuhitaji KITU katika shughuli nzima ya kujaribu kila siku KUPATA KITU  ili ujisikie vizuri  na hatimaye KUJISIKIA KWAKO VIZURI  kunaweza kuwa SASA HIVI  kunahitaji kilazima KITU  FULANI tu ili angalau UJISIKIE  VIZURI kiduchu tu.:-(


Swali:
  • AU?


Kama unabisha,....
...jiangalie tu KUMOYO hali halisi  kama ILIVYO  ,....
.....waweza kugundua KUJISIKIA  KWAKO VIZURI labda kunahitaji  GARI ZURI leo ingawa HATA  kwa hilo  umejifunza GARI ni nini KWANZA hasa  kwa kuwa KWENU  sio  maporini ambako bomba la HAIWEY ni UCHOCHORO,....

... na KUJISIKIA  KWAKO VIZURI kwa kuwa una bonge la  NYUMBA nzuri HUKO KWENU  kumetokana na jinsi gani  KABILA LENU siku hizi HAMHAMIHAMI  kutafuta mihogo a.k.a MSOSI kila wiki kichaka cha pori la jirani  nyingine , AU TU hamuhitaji tena kuhamahama ili kutafuta PAKUCHUNGIA MBUZI  wa MAHARI  na WALE  ng'ombe zenu wa KISUSIO ambao ndio KITU ambacho kilikuwa kinawaletea KUJISIKIA VIZURI kabla yakugundua nyumba yenye choo cha ndani.:-(




Swali:
  • Unadhani hakuna kaukweli katika hilo na nimezidisha CHUMVI kwenye  porojo?






Ndio ,...
.... ni kawaida kwa baadhi ya watu kuoanisha VITU na jinsi wajisikiavyo VIZURI, kitu kisababishacho watu kutafuta msaada mpaka wa kujinunulia vitu MURUA kama :

  • Raba la Kuchumpa
  • Kitabu cha Juma na Rosa chenye bonge la jalada
  • Bonge la CHUPI
  • Isiyoya miti NYUMBA
  • BAISKELI
  • TOROLI na bonge la BELESHI jipya
  • Bonge la Kibajaji
  • GARI MOSHI kwa kuwa BENZI halikutoshi tena siku hizi
  • nk. kadhaa wa kadhaa...

....NA WAPO pia  wahitajio WATU WENGINE au tu DINI  katika harakati zao za KUJARIBU kufanikisha KUJISIKIA KWAO VIZURI.



MIYE naamini kila MTU kivyake katika  kusaka KUJISIKIA VIZURI ,...

...na LABDA vyote vinamsaada ikiwa tu UNAJIJUA UDHAIFU wako na katika KUVIBANJUA VIKUNAVYO UDHAIFU WAKO  huumizi kwa makusudi watu WENGINE,....

... kwa kuwa WAJUA swala la KUJISIKIA VIZURI lilivyo NYOKO  wanaojijua wanajua kuwa kuna watibuo TATIZO hilohilo lao BAA kwa kitu CHA BAA  ambalo kwa mwingine dawa yake KATIKA KUCHOKONOA ni lazima  SWALA aliendee KANISANI au  MSIKITINI.





Swali:

  • Si unajua kuna watu kibao aka BWELELE  ambao WAKO kwenye dini zao kwa sababu ya kutibu swala hili tu la KUJISIKIA VIZURI  na wala huwa hawawazii  kuogopa JEHANAMU kama wewe ndio kisa HASA  wako MSIKITINI au KANISANI?


Ni kweli ,....
...ili kujisikia vizuri kuna watu WANAJIKATA a.k.a JICHINJA maeneo damu itoke wafarijike na KUJISIKIA VIZURI.

Lakini pia ,..
...UHAKIKA wa utambuaji wako wa  UJISIKIAVYO VIZURI waweza kukuokoa KUNUNULIA SWALA GARI  wakati kikunacho UJISIKIAVYO VIZURI ni BAISKELI na BWANA  wa nje akunaye na kujazia majibu ya UDADISI wako wa nje ya ndoa KUNANI ambacho chamfanya MMEO asiache kuonja nje.:-(

Kumbuka tu,....
..... ni uungwana lakini kama wakati unajitafutia KUJISIKIA VIZURI basi cheza kwa stepu ,....
...USIKANYAGE WENZIO.


Swali katokori:
  • Unajiasikia VIZURI lakini leo au unahitaji kitu kikune MSHAWASHA?
  • Umewahi kufikiria ni nini siri  ya KUJISIKIA KWAKO vizuri?


NIMEACHA wazo hili nyoko MHESHIMIWA na jaribu tu kukumbuka HILI ni wazo tu MKUU!
IJUMAA na WIKIENDI NJEMA!


Tupoze tu kwa kupata tena SINDIMBA kidogo kutoka kwa FIRST LADY, sasa tutafanyaje.:-(



Au tu DIANA ROSS na MICHAEL JACKSON warudie ndude-Upside down

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Sisulu 5:50 pm  

hay uwe na heri mkuu

Simon Kitururu 11:36 pm  

Asante MKUU Tandasi!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP