Showing posts with label Uchokozi. Show all posts
Showing posts with label Uchokozi. Show all posts
Halafu KATIKA YOTE ....kunatubanwao na UCHI aiseee!!
>> Monday, July 16, 2012
Na uchi wa KIMAISHA,...
.... unaweza kuwa ni TUMBO aisee!
Swali :
- SI mdomo na kinyeo KIMAISHA ...labda mambo mengineyo ...KIMAISHA ...kuna vipengele visakiziwavyo tuuu huko nanihii?
Ndio,....
...kuna wabanwao hata na KAZI pia,..
... wakati kujipendekeza kwao kwenye mikazi yenyewe labda ni MSHAHARA tu,...
... ingawa MSHAHARA wenyewe wala sio UCHI kivile kwa mpenda UCHI ,...
... hata wakati kimaisha wako UCHI aisee!:-(Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!
JUMATATU njema NGULI aisee!
Ndio ,...
....I can feel it coming IN THE AIR TONIGHT
GREGORY ISAACS asaidie,...
....nilalamikiye ya kuhusu weye kuwa-SAD TO KNOW
....nilalamikiye ya kuhusu weye kuwa-SAD TO KNOW
Halafu STEEL PULSE warudishe ghafla udini,....
..... kwa ku-rudia -Chant A Psalm
Halafu,...
...NIPO aisee!
Read more...
CHAKULA chalika hata ndani ya CHUMBA cha CHOO cha STENDI!
>> Friday, July 13, 2012
Kinyaa ni LAKSHARI kwa mwenye NJAA,...
..... na ukiumwa vizuri NJAA ,...
... popote ni mahali pakulia MAAKULI!Swali:
- Na si unakumbuka MAHALI popote ni KITANDA ukichoka vizuri?
- Na si NGURUWE hustukiwa UHARAMU wake kama kuna kingine kichaguo kiwezacho KUGIDWA?
Ndio,...
... kama UNACHAGUA,...
... hujabanwa vizuri na KIBANO bado.
Ni wazo tu hili NGULI!
Hebu MSAFIRI ZAWOSE aingilie kati kwa-Mkungwe
CAROLINA eeeh!
>> Wednesday, July 11, 2012
Basi BWANA hebu tu AWILO LONGOMBA ndiye atekenye kidude...:-(
Au aongezee pini-COUPE BIBAMBA
Yes I am still OLD school....
I still spin LPs.. ... and YES,....
those are in my SITTING room
....
YEAH!
STORI fupi kabla kila kukicha TANZANIA hakujawa na MIKOA mingine MIPYA lukuki ... kama siku HIZI !
.....kabla MIKOA haijaongezeka TANZANIA BARA ......
....Waheshimiwa wakijadiliana CHOBISI!
Mheshimiwa wa kwanza:
- Si ZANZIBAR inataka kujitenga eeh?
- Basi ngojea tuongezee MIKOA Tanzania BARA ili Wabara wajisikie Njombe haikuwa IRINGA, na ARUSHA ni kubwa vilevile ... na kwa wengine wale tutunge KATAVI na.... ili hata ZANZIBAR ikijitenga kipande kimoja cha MKOA wa MOROGORO tukiite ZANZIBAR.
Waheshimiwa wote kwa pamoja kikaoni:
- Bonge la AIDIA aisee.. ila turefushe kikao .. si unajua tena MARUPURUPU tena?
Halafu waheshimiwa wote kwa pamoja karibu na mwisho wa KIKAo :
- Eee Bwana si wajanja kweli aisee!
Mwisho wa STORI ya KIZUSHi kitungo dhaifu!!
Hebu turudishe WAGHAIBU ,...
....ambao haki ya nani ELIMU ZAO ,...
... ndio tuzisifiazo wenyewewenyewe kama KIPIMO nani MSOMI zaidi....
.
... tustukie tu KIMAGHARIBI ya PERFECT Day ki -LOU REED
Lou REED huyuhuyu aongezee tena - Walk on the Wild Side
Au tugewe tu ALLAH HOO kimashariki na
-Nusrat Fateh Ali Khan
NDIO ni UCHOKOZI tu HUU aisee MHESHIMIWA NGULI!
Read more...
SAUTI yako unavyojisikia MWENYEWE labda sivyo isikikavyo na watu WENGINE aisee MUUNGWANA!
>> Thursday, July 05, 2012
Ndio,...
... kama unabisha kuwa ujisikiavyo ukiongea ndivyo usikikavyo JIREKODI,...
... halafu SIKILIZA!Swali:
- Si kunauwezekano pia mpaka UJIONAVYO ulivyo BOMBA labda ni katika MACHO yako tu kama tu ujidharauvyo wakati kuna mtu ANAUMIA roho jinsi akutamanivyo isivyo vya kichini ya kitovu tu?
- Na si labda hufanani hata na picha zako uzipendazo?
Ndio,..
... ni uchokozi tu huu!
Hebu Trombone SHORTY arudie-SOmething Beautiful
Trombone SHORTY arudie -Where Y'at
2PAC akumbushie kuna-SHORTY wanna be a THUG
Halafu BOB MARLEY azime tu tena kwa -Time will tell
Read more...
Lebo:
Mmmmh,
Mtonesho,
Uchokozi,
UjingaBUSARA
Moja ya almasi ithaminiwayo sana na Malkia wa Uingereza !
>> Thursday, June 28, 2012
WAKATI kuna UHAKIKA kuna zawadi nyingine zimetoka TANZANIA,....
..... LABDA angalia tu baadhi ya ALMASI za wamaskini WATANZANIA ziendako.......
... msisitizo UKIWA ni pale tu MKANADA zawadi yake ni kutoka TANZANIA....
.... wakati simaanishi kuwa MKANADA zawadi zake lazima zitoke KANADA.
Swali:
- Si Tanzania ni NCHI masikini?
Just SAYIN'!:-(
Read more...
Lebo:
Krosi KIAINA,
Mtonesho,
Uchokozi,
UjingaBUSARA
Kuhusu UONGOUONGO wa WAKUBWA hata kama sio kikubwa huwa KUNA adanganyikae PIA kitoto!:-(
>> Monday, June 11, 2012
Na ukipendacho kiupendavyo hata kama kikweli ni UONGO NANILII ki NANIHII,...
... labda AJULIAYE hata kwa bahati MBAYA,...
..... hunogesha UONGO kikweli kabisa na sio KINANILII,...
.... au hata KINANIHII!!:-(
Swali:
- Si Unajua WAONGO wengine wanakudanganya vizuri kwa kuwa LABDA wana SURA nzuri za KIUONGO?
Ndio,...
... labda kuna usio wastukia wakikudanganya,...
...kisa SURA...
.... na wala hata sio ile SURA ya sehemu za chini KINANILII au KINANIHII!:-(
Ni wazo tu MHESHIMIWA!
Nakutakia Ijumatatu PANAAAA ,njema na yenye SHIBE!
Hebu Coumba Sidibe avalishe bangili kwa-Nale Na
Hebu The Ousmane Kouyate Band warudie- Kounady
Halafu kabla Tshala MUANA hajakatizia denge kwa ...
Au tu Tshala Muana arudie-Koumba
Apenyeze-Kalume
Halafu huyuhuyu Tshala Muana azime kwa-DEZO DEZO
Lebo:
Mmmmh,
Uchokozi,
UjingaBUSARA
Kuhusu KINA cha KISHIMO ambacho HATA KAMA hakiko UCHI!
>> Wednesday, June 06, 2012
Kina cha kitu hata kama sio KISHIMO cha MTU,...
.... KWA KIPIMO labda huwa mtu UNAJIJAZIA TU mwenyewe!:-(
Swali:
- AU
Na ujazo wa kina ,...
... kama tu kurefusha kilicho tuna kisicho KITU,...
..labda ni kipimo chako tu AISEEE!:-(
Ni wazo tu hili ,...
....na wala halijaambatanisha tusi MHESHIMIWA!
....na wala halijaambatanisha tusi MHESHIMIWA!
Hebu Warren G a-Regulate
Warren G aongezee-ya This DJ
Au azime in-SO MANY WAYS
Read more...
GHAFLA!- Na kwa ghafla unaweza kubanwa hata na haja ISIYO kubwa kwa WENGINE!
>> Thursday, May 31, 2012
Ila GHAFLA,....
.... labda wala sio GHAFLA,....
...... kwa kuwa yasemekana kila kitu hapa DUNIANI huchukuwa MUDA,...
.... na inategemea tu na uharaka wa KIPIMO cha MTU kuhusiana na KITU uwezeshao kugeuza SEKUNDE igeuke MWAKA.Swali:
- Si ghafla tu KIJANA anaweza kujikuta MZEE na anahangaika UZEENI kisa hakustukia UGHAFLA wa UZEE ukaribiavyo- kitu kilicho chelewesha KUJIANDAA?
Ndio,...
....labda inategemea tu na jinsi ulipavyo SWALA umakini,...
.... na kama humakini,...
.... kila kitu chaweza kuwa MITOKO YAKE ni ya kighafla tu,...
.... na hapa wala siongelei MTOKO kishahawa , kibaruti orgazimu ,ughafla wa KUHARIBU URAFIKI, Ughafla wa KUJIMIMINIA dhambi,ughafla wa kuingia ofisini na KUJIFUNZA UFISADI , ufuska kiduchu wa GHAFLA mtu akihisi haonwi......
... au tu HATA jinsi gani ghafla UTAKAVYOSAHAU hii topiki,...
..... baada ya KUNISOMA!:-(Swali:
- Kwani si umeshawahi kubanwa hata na HAJA ghafla halafu baada ya kujisitiri ghafla UKASAHAU ulivyobanwa kabla ya FARAGHA?
Ndio,...
.....labda kitu ``GHAFLA´´,...
...... hutegemea tu na spidi yako katika SWALA.:-(
Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!
Nakutakia SIKU NJEMA!
Hebu Billy Ocean aingilie kati,...
... na kuongelea jinsi PENZI lilivyo leta maana GHAFLA katika kitu-SUDDENLY
Lebo:
Mmmh,
Uchokozi,
UjingaBUSARA
Leo katika UCHOKOZI: Gen. Colin Powell na WAPENZI wa JINSIA MOJA wakitaka KUOANA!
>> Tuesday, May 29, 2012
Lebo:
Uchokozi
KATIKA urafiki wa MWANAUME na MWANAMKE-labda UMPENDAYE mkwepe ili abakie kuwa ``JUST a FRIEND!!
>> Sunday, May 20, 2012
Kuna wadaio,....
.....URAFIKI usiowakinafiki kati ya MWANAUME na MWANAMKE,...
.... huwezekana tu kama RAFIKIYO hakuvutiii.:-(Swali:
- Si umestukia nimerahisisha hoja?
- Na kwani si ni UNAFIKI kama kuna ajenda za siri katika udaiwao kuwa ni URAFIKI wakati kwako LENGO ni zaidi ya u ``JUST a friend´´?
Ndio,...
..... labda udhaniaye ni RAFIKI TU,...
.... . uhusiano wenu umejengwa KINAFIKI kwa kuwa hakuambii tu kuwa atakacho ni zaidi ya URAFIKI tu wakuchekeana na kusikilizishana UDAKU!:-(
Wadeku hawa....
Ni uchokozi tu huu MKUU!
Nakutakia siku NJEMA! Read more...
Lebo:
Uchokozi
KATIKA yahusuyo UCHI mzuri!
>> Friday, May 18, 2012
Na kuna YAVALISHWAYO nguo MAISHANI,...
.... ingawa bado yasemekana MAISHANI yale ya KIKWELI ni yale yaliyoko UCHI,...
.... hata kwa ALIYEVAAA!:-(Swali:
- AU?
- Na si YALE mazuri hata yakikaa UCHI huwa yana mchezo wa KUPENDEZA?
Ndio,...
... labda ni kweli UCHI mbaya hufichwa na mwenye UCHI,...
.... hata FARAGHANI!:-(
Na ni wazo tu hili MHESHIMIWA!:-(
Hebu J. Martins aingilie kati tena kwa -OYOYO
Halafu Fally IPUPA aingilie ya J. Martins halafu kwa pamoja wazime kwa -JUPKA
Lebo:
Mmmmh,
Uchokozi,
UjingaBUSARA
ILI UBENJUE KISIASA labda kihitajikacho ni kidude KIBENJUKACHO hata bila SIASA!:-(
>> Wednesday, February 08, 2012
Na ili uwe MSOMI hata KISIASA,...
.... labda yahitajika kihitajikacho hasa KUSOMWA hata na wasio WANASIASA ,....
.... na labda ndio maana siku HIZI unajua WASOMI WENGI na USOMI wao MADUDU na hata chamuhimu kwako KIKISIMI KISIASA hawajui labda waongeacho ni siasa na WANANCHI watakacho ni kutibu ni KLOROKWINI na tatizo ni MALARIA na wala sio SIASA!:-(Swali:
- AU?
Na kihitajiwacho KUBENJULIWA ,...
... unajua KIPO aisseee!:-(
Swali:
- Unabisha?
Na KIBENJULIWACHO kipo aisee,....
... hata kama ni KIMAWAZO tu aisee MHESHIMIWA na kiuheshimiwa siku hizi ni mpaka MHESHIMIWA awe ni yule JAMII inamtambua kama yeye ni MHESHIMIWA hata KIDINI na wala huyo BINGWA kwa kuwa ni SHEKHE au ASKOFU basi hana jina katika heshima za JAMII zimtambuazo kama MWANASIASA kisa yeye ni ukiondoa DINI ana GOVI lenye UTOKO!:-(
Swali:
- SI labda CHA KIKWELI hata kile KISICHO BENJULIWA bado kipo na ni kweli ni CHA KIKWELI ingawa VYA UKWELI kwa WENGINE ni vile viishivyo MAWAZONI tu na havipigiki punyeto mMMmmmmkikweli kisa vyaishi tu kwa ambao vyakikweli vuko sebuleni huyo hata ki- MAWAZONI yake yako CHOONI hasa kutokana na WAHESHIMIWA yao YAKIHESHIMIWA ni NINI?
Ndio,...
.... labda KIWAZWACHO,...
.... kwa baadhi wawezao hata kuwa ni wengi KULIKO AMBAO NI WACHACHE TU -tu hata kwenye wingi wa mavuzi pale ambako UNAAMINI kihitajikacho ni KIKISIMI,....... kiwazwacho ni MUHIMU ZAIDI hata kama sio kama umfikiavyo MUNGU wa WACHAWI afanikishaye kwa WACHAWI wanafanikiwa kuliko wewe katika yako ufikiriayo ni yapendwayo hata na PADRI poa hata kama ni yule mwenye nyege za waumini wake kisiri na kashawapa watoto wa watu MIMBA ambaye kisifa kakaa kisifa za KIMUNGUMUNGU wa asiye wa IBURAHIMU,...
...KWA KUWA umuhimu LABDA kitafsiri ni tofauti kwa baadhi ya WATU,...
....ili UBENJUE labda unabenjua tu kwa MAWAZO na wala hata sio kwa kushikilia tonge KIKUFINYANGA kwa kuwa kuna watu kimawazo tu hilo ni TENDO na ndio maana labda twajua TANZANIA ni nchi TAJIRI hata KIMAWAZO TU ingawa wajanja ambao fulu ufunguo IKULU na maeneo ambako POCHI lako ndio HULOANISHA kiharage kisiasa za BONGO wasio na pesa wanazidi kutoonekana.:-(
Swali:
- Hivi ushawahi kustukia katika ufikiriayo ni ya BAADHI labda kwa mwingine WENGI hicho hicho ni kingi na cha WENGI?
Ndio,...
... ili UBENJUE ,...
... labda BENJUA kivyako kwakuwa cha siri ufikiriayo ni yako MOJA ,...
... labda ni siri kweli yako moja ila kihitajikacho ili ujisikie VIZURI ki vile ambavyo unajisikia ukijamba huru wakati uko choooni,...
... ni labda hata ambayo hutaki KUYABENJUA angalau ujisikie huru kuyaongelea kwa nini hutaki KUYABENJUA hadharani.Ni wazo tu hili na kutolielewa RUKSA!:-(
Hebu tubadilishiwe kimuanzisho mpya kwa bezi gitaa katika kukumbushwa kiFANKYbezigitaaa aisee -THE name is BOOTSY baby
Hebu Bootsy Collins ajaribu kulainisha kwa katika kigitaa ...Bass Solo
Bootsy Collins aongezee SPESI BEZI na kama unaelewa FANKI MUZIKI na pia jinsi ya kupiga bezi gitaa utaelewa ni kwaniii...
Snoop Dogg ajaribu kulainisha zaidi tena umwagia maji kwa ya NGULI huyuhuyu Bootsy Collins katika mpanuo-Undercover BROTHER
Snoop Dogg, George Clinton na Bootsy Collins warudi kiaina ....
Au tu hebu SNOOP dogg DOGGY azime akiwa tena na The Dogg Pound & The Dramatics katika kidude- Doggy Dogg World
Au tu Black STREET , Dr DRe na QUEEN Pen waweke nukta tena kwa- No Diggity
Read more...
Lebo:
Mmmmh,
Uchokozi,
UjingaBUSARA
Kwa kuwa labda PROFESA wa KUKUPENDA KIMAPENZI kwako UNGEPENDELEA asiwe MALAYA!
Ndio,....
.... yasemekana AKUPENDAYE ,....
... moja ya sifa zake kwa wengi ni UCHOYO,...
.... hasa kama anyimwaye sio WEYE !
Swali:
- Si unajua lakini UCHOYO ni sifa mbaya KIAINA?
- Na ugawaji si KIAINA kunawadaio ni ushahidi wa ROHO nzuri ya MTU apendaye WATU ingawa bado kuna watafsirio wagawaji kuwa ni MALAYA kutokana tu na wagawacho kitu?
Ndio,...
....TAFSIRI balaa,...
... kwa kuwa zaweza kugeuza MGAWAJI kwa ROHO NZURI TU kutafsirika kama MALAYA,...
... na MCHOYO kuwa ni MTU mwenye tabia MWANANA kwako hasa kama kiaina AGAWACHO ni kipenzi chako na uchoyo wake kwa wengine kuhusiana na hicho KIDUDE ndio kichocheo cha upendacho kukitafsiri kama TABIA NZURI!:-(
- AU?
- Hufikiri labda Profesa wa KUGAWA penzi - PHD yake huhitaji awe MALAYA kiaina kistaili za kugawa?
Ndio,...
.... KIMPENZI,...
.....labda wala UJUZI SANA hauhitajiki kwa kuwa USHAPENDA na ukitekenywa hata kidogo kama akudongolosaye unampenda unaweza ukastukia UNACHEKELEA kwa sana TU hata kama ni kwa KUJICHEKELESHA kwa kuwa wala haichekeshi sana.Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!:-(
The Mighty Sparrow aanzishe tena UPYA kwa- Good Morning Mr Walker
Lloyd D Stiff ajaribu kubadili kwa - Bum bum fatty
Lord Kitchener aingilie kati tena kwa - Drink Ah Rum
Mighty Sparrow arudi kidogo na kuongelea kidude katika- Saltfish
Halafu sijui kwanini Lord Kitchner azime tena kwa-Sugar BUM BUM
Lebo:
Uchokozi,
UjingaBUSARA
Hata kama SURUALI ni ileile,...
>> Tuesday, February 07, 2012
... MFUKO wa MBELE,...
.... ni tofauti na MFUKO wa NYUMA.
Swali:
- Kwani hata mtu abishe bado ukweli uko palepale MBELE ni tofauti na NYUMA?
Ingawa labda,....
... ukigeuka,...
..... kulikowahi kuwa nyuma,....
.... ndiko MBELE kisafari hata kama safari yenyewe ni ya KURUDI nyuma.
Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!
Hebu tukatizie GHANA tena ili Nana Boroo na Mugeez warudie- Bebia Soso
Hapahapa GHANA ngojea tu tena Nana Boroo arudie- Ahayede
Au tu hebu WINSTON SOSO azime kwa-I don't MIND
Read more...
Lebo:
Uchokozi,
UjingaBUSARA
NYANI kwa kutumia KIOO au tu KAMERA ya SIMU siku hizi -LABDA huona KUNDULE aisee!:-(
>> Saturday, February 04, 2012
Ndio,....
.... labda msemo wa NYANI haoni KUNDULE,...
.... sio kweli kwa asilimia MIA!
Swali:
- Kwani unafikiri ni kweli kila udhanialo NANILII halistukii KISA anaonyeshadalili za kutolijali kama WEWE ULIJALIVYO maana yake ni kweli huyo NANILII wako HALISTUKII hilo li kitu?
Ndio,...
.... nyani wa sikuhizi hata kwa VIDEo na KAMERA za kwenye simu zao,...
.... labda vizuri tu huona yao makundungu,....
.... ila wanakomalia kujibaraguza kuwa hawastukii kwa kuwa hata KIFISADI inalipa bado!:-(
Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!
Hebu KWANZA UNIT waturudishe Dar-es Salaam kwa -MSAFIRI
Halafu sijui kwanini hebu turudi SENEGAL ili Daara-J warudie- Allah
Read more...
Lebo:
Uchokozi,
UjingaBUSARA
Somo MOJA kutoka ZIMBABWE!
Kila MTU anaweza kuwa MILIONEA,...
.... ingawa pamoja na UMILIONEA WAKE,....
..... MKATE na VITUMBUA bado vikawa GHALI na havinunuliki!:-(
Swali:
- Ushawahi kusikiliza MABABU hapa TANZANIA wakakuambia jinsi gani SHILINGI tano ya TANZANIA ilikuwa inatosha kimshahara ?
Ndio,...
..... labda UCHUMI ni kichaa,....
.... kwa kuwa waweza kukujaza MANOTI na kuondoa makali ya UTHAMANI wa hayo ma- NGAWIRA PESA!Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!
Jumamosi NJEMA MDAU!
Hebu Kenyan Boys Choir waingilie kati kwa kudinya- Jambo Bwana
Halafu tena Mighty Sparrow ajaribu kuzima kwa -Jean & Dinah-The Lizard-Melda-Drunk & Disorderly (Medley)
Halafu The Roots ndio wazime kwa-Next Movement na Pussy Galore
Read more...
Lebo:
Uchokozi,
UjingaBUSARA
Unafikiri WATANZANIA bado ni WABONGO miaka yote hii baada ya UHURU na BONGO zenyewe hazijafanya tuwazidi angalau KENYA angalau KIUCHUMI?
>> Friday, February 03, 2012
BONGOOOOO!
Na ukisikia tu jina hilo maarufu kwa WATANZANIA,...
.... wawezafikiri ni kweli UBONGO ni misingi katika kila wafanyalo WABONGO ni kistaili ya kutumia sana UBONGOSwali la KICHOKOZI:
- Na kama tunatumia BONGO sana sie WABONGO,....
......mbona BONGO zenyewe hata katika kuchagua VIONGOZI wetu kuna watakaodai na kutoa ushahidi labda BONGO hazifanyi kazi?
Ni wazo tu hili!
Hebu tena Jaziel Brothers warudie-Ngeke Ndiphinde
Au tu hebu Oliver Mtukudzi na Thomas Mapfumo warudie-Muchatuta
Lebo:
Uchokozi,
UjingaBUSARA
Subscribe to:
Posts (Atom)



