Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Nyolinyoli

>> Monday, April 30, 2007


Ushawahi kumnyolisha mtu?
Halafu ushastukia nyolinyoli nyingi watu wanyolishazo ni zawadi walizopewa na wala hawakununua wenyewe.
Si unakumbuka ile pipi ulionyolisha watu?
Duh !Muda unanipiga chenga kuendeleza Nyolinyoli talk..


Lakini tuendelee na Steel Pulse!

Read more...

Kuhusu Raisi Kitururu-:-)Duh!- IDI amINi!

>> Sunday, April 29, 2007

Samahani nakubaliana na Ndesanjo kwa hili!
Ndesanjo eeh!
Samahani, lakini ,!:-)
Niachie namba yako ya simu chobisi basi!
WENGINE.........................!
Ngojea Ndesanjo aseme kuhusu Idi Amini.......
ndesanjo has left a new comment on your post "Generali Idd Amini Dada akiongea, duh!":

Ingawa simuoni kama kiongozi wa kuigwa, Idd Amin Dada namvulia kofia. Huyu ni bwana ambaye kusoma na kuandika kulimpa tabu. Ila aliweza kutumia mbinu mbalimbali kuwahadaa Waingereza na baadaye Obote hadi akaja kuwa rais. Alikuwa na ndoto, akaifanyia kazi, akawa rais wa nchi akiwa hajui kiingereza au kiswahili sawasawa. Akiwa ni mbumbumbu. Kumbe umbumbu wa darasani sio kikwazo kwako kutimiza ndoto uliyonayo.

Waandishi waliowahi kumhoji wanasema kuwa maswali mengi makali waliyokuwa wamepanga kumuuliza au shutuma walizokuwa wamepanga kumpa zinatokomea wanapokaa naye chumba kimoja kumhoji. Wanasema alikuwa na uwezo mkubwa sana wa kukufanya umwamini na kumhoji kirafiki.

Kuna mambo mengi alikuwa akifanya unajiuliza mbinu hizi alijifunzia wapi? Wakati viongozi wengi husoma vitabu na kuwa na washauri waliomaliza madarasa yote ili kupata mbinu za kutawala, Amin alikuwa akianzisha mbinu hizo mwenyewe bila kujifunza toka vitabuni.

Alikuwa na mbinu moja ya ajabu na kinyama aliyoitumia kwa watu aliokuwa ameamua wauawe. Kama mtu huyo ana jina au nafasi kubwa nchini, basi Amin alikuwa anaweza kumkaribisha ikulu ale chakula cha jioni na kunywa mvinyo. Wanapiga picha ambazo zinatolewa magazetini zikimuonyesha Amin na huyo mtu wakicheka kwa furaha na urafiki wa hali ya juu. Kisha baada ya siku tatu, idadi ya siku tunazoambiwa yesu alikufa, unasikia huyu jamaa katoweka. Baadaye unasikia amepatikana akiwa ameuawa baada ya kuteswa.

Urais katika mfumo wa kisiasa kama wa Uganda enzi za Amin sio kazi rahisi. Kuongoza nchi ya kidemokrasia ni kazi rahisi sana. Ila kuongoza nchi ya kidikteta, kujenga utamaduni wa ukimya na woga kwa wananchi wote, kuchunguza nani maadui zao na kuwaondoa duniani...aliwezaje kunyamazisha nchi nzima? Hofu. Alijua kuwa silaha kubwa kabisa dhidi ya mwanadamu ni hofu. Alijua binadamu wanapenda sana uhai. Binadamu wanaongopa, mara nyingi, jambo lolote ambalo linaweza kuhatarisha maisha yao. Amin alijua ukweli huu na akautimia ipasavyo.

Tuache hayo, hivi kuna mtu mwenye uhakika kuhusu Amin kuivamia Tanzania? Je ni kweli aliivamia Tanzania kisha sisi tukajibu au habari ya uvamizi huu ilizushwa kama propaganda ya kuhalalisha vita vya kumtoa madarakani kutokana na kuonekana kuwa tishio la usalama Afrika Mashariki?


Sasa mnambishia Ndesanjo?
Mimi nimekubali.
Namuacha huyu MuHaiti aishiye Ndesanjo na Mtanzania wajibanzako

Read more...

Kuhusu Kinyeo!

>> Saturday, April 28, 2007


Kastarehe kakutumia kinyeo!
Ni kakitu ambako hakajaanza leo.
Hata ukibishia mamboleo!
Kikalio bado chaficha mbolea.
Samahani kwa sababu lazima utumie kinyeo!
Namuacha Ben Harper akiwa na The Blind Boys of Alabama

Read more...

Kuhusu Kikojoleo!


Msalani kuna starehe yake!
Ila unajua yatokeayo msalani ni siri .
Lakini hizi siri , Duh!



Wikimwisho yako bomba eeeh?


Nisikufiche sisahau pale chobisi ya homu na mengineyo.......
Lakini umetumia kikojoleo chako leo?
Samahani!
Najua sisi kama wabongo hata kama kikojoleo kiko mawazoni hatutakiwi kukiongeleaaaaa.................!


Lakini..........!


Sasa Ngoja niache Kassav......

Read more...

Ule Muungano!.

>> Friday, April 27, 2007

Mzee Mtanzania ananiambiakua tuchangie kumsaidia huyu Mzee Muungano wa Tanzania na Zanzibar.Lakini mimi sina data nyingi za hili swala.
Lakini.......
Najua Zanzibar na Tanganyika zitakuwa poa tu zikiwa pamoja au zikiwa sebule tofauti.

Au?

Duh Aliko eeh!








Wewe Mzanzibari, utanitenga Tanganyika na Zanzibar zikienda chochoro tofauti?










Aliko eeh!Jana shoo ilikua poa!

















Nilirekodi yale maswala lakini haikufikia kwaliti ile tuitakayo na itakwayo!
Sasa!
HALAFU UNAJUA KUNAWATU HAWAJUI KAZI ZAKO KAMA MSANII?
Lakini nawapa muda tu!
Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Aliko na Tompura the sound engineer aka Bass Guitarist

Ngoja niwaache Israel Vibration watukumbushe sisi walalamikaji....Naamini sisi wote tutaimba wimbo mmoja tuwe pamoja au la hasha!...
Ee Bwana ee?
Nimependa kuandika hili neno lahasha!:-)


Mzee Ogola eeh?!
Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Tupo pamoja!
Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket






Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Mkuu wa Kikao! Asante!Lakini ulikuwepo kijiografia tu!:-)

Lakini wale mapacha wabongo ambao mpaka leo sijui nani Kurwa nani doto.
Nistueni basi nani doto halafu kura nitamjua...
Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Mmoja halafu....
Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Mwingine..
Sasa kabla sijaendelea...


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Mimi na Tony Flash!
Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Tony Flash
Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Mimi na Prince.Prince anahitaji kura yako kuwini OurVision Contest Next week.
Mtanzania Halisi eeeeeeh!
Yule Mzeee Muungano wa Tanzania na Zanzibar anaumwa! Halafu matibabuyake bado sijayastukia!

Ngojea nikuache na Zuku.....akuzingue Jocellyne Labylle na Cheela akiwa na Jacob wa Kassav na rapa wa Kifaranza aitwaye Passi wakikupa Laisser Parler Les Gens

Read more...

Leo ni Siku Ya Malaria!

>> Wednesday, April 25, 2007


Huwa natishika sana kuiita siku moja kuwa ni ya kaugonjwa fulani.
Lakini kusema ukweli huu ugonjwa unatumaliza. Inasadikika watu milioni moja huondoka kutoka kijiwe hiki cha dunia, kila mwaka kwa ugonjwa huu.

Chakutisha nikwamba unazidi kuwa sugu kila siku!
Na kingine ni kwamba wataalamu hawachoki kutuhakikishia kuwa ugonjwa huu unakabilika!

Kinachotushinda nchi masikini ni pamoja na umaskini wetu .
Eti fedha ya hawa matajiri za kukabilia huu ugonjwa, ambayo baadhi ipo, bado ina masharti.Ukiwa hununui vyandarua ambavyo wanakubaliananavyo, madawa ambayo wanakubaliana nayo au hata kama huna mfumo wa kudhibiti ugonjwa huu wakubalianao nao , hupata hizi fedha.

Lakini.....!
Wenzetu nao walikua na ugonjwa huu!Lakini wao wakatumia DDT na madawa mengine ya sumu kuumaliza.Sisi lakini haturuhusiwi kutumia dawa hizi , kwasababu wanasema kuwa zinaharibu mazingira.
Siwabishii hilo!....

Siwabishii kuwa hazi haribu mazingira,...
lakini najiuliza kuwa kwanini wao mambo huyahalalisha na yanakua mabaya tu pale wengine wanapotaka kufanya kama wao?

Umestukia pia hata katika viwanda , nguvu za nyukilia, nk; kwao ni sawa lakini ukigusa mwingine Umoja wa Mataifa unaanza kukuwekea vikao kuwa mkorofi?

Labda ni kweli kuwa wao walitangulia mapema wakastukia madhara ndio maana hawataki na sisi kurudia makosa.
Lakini!....
Mbona wao wanajinoma? Sisi je?

Nakubali kuwa nia ya mbu jike ni kujitafutia damu ili kupata lishe bora kwa ajili ya taifa lake la kesho na sio kuwa mbeba malaria. Hivyo kama akikosekana mtu mwenye vijibaba vya Malaria basi akikuonja hana madhara.
Sasa kuhakikisha kuwa hakuna mtu mwenye vijibaba vya Malaria maeneo, hapo ndio kasheshe!Wenzetu kwakutumia sumu wakaweza.

Unakumbuka kuwa sehemu kama Florida , Marekani ni sehemu zenye mbu kuliko sehemu nyingi duniani?

Hivi kwa wale washabiki wautunzaji wa mazingira:...........
Hivi kunasiku kutakua na mradi wakutunza Mbu wasipotee duniani?

Duh!
Inasikitisha sana kuwa mapka kuna statistics zijulikanazo, zidaizo kuna mtoto anakufa na Malaria kila dakika tatu Afrika.

Tujaribu kufanya kila tuwezalo wajameni , kusaidia kufuta hili.Hata ikiwa ni kufukia vidimbwi uani kwetu au kutotunza lilekopo lakwendea msalani lisilotumika pale nje ya choo.
Basi ngoja niondoke zangu!
Lakini nakuacha na Amadou na Mariamwakikupa kile kibao Senegal Fast Food

Read more...

Chakula cha Mawazo

Wewe kama Mtu mweusi unazifikiriaje picha kama hizi?


Picha hii nimeipata kutoka katika blogu niipendayo ya Saharan Vibe.










Tukiachana na watu weusi....
Hawa weupe je?

Read more...

Kautamu kakukuna kidonda!

>> Tuesday, April 24, 2007


Maswala ya utamu ukiondoa yale mistukio yake tumezaliwa nayo, yote mengine umejifunza tu.
Au unafikiri ni nani alikuambia bia ni tamu?
AU unafikiri nyonyo ya mama ukipewa leo utaizimia utamu wake?


Nisikutishe .......!
Sina uhakika kuwa unaweza usizimie utamu wa ziwa la mama leo hii.
Kwasababu.......

Maswala ya utamu yanauhusiano pia na mazoea yako katika kushabikia kautamu.

Utamu kwa wengine huupata kwa kukuna kidonda.
Au unabisha?
Halafu usiusahau ule utamu unaoupata hasa kwa sababu ni kasiri kako kuhusu kautamu hako.

Lakini...
CHAI TAMU HATA BILA SUKARI!

Sasa ni kweli baada ya kuonjeswa sukari , hutaki hesabu za.....
Chai bila sukari =?
Hatakama hatupendi, jibu ni :Chai
Au unafikiri....
Kachumbari bila nyanya= na nini?
Ushastukia wengine hawazimii ugali wa muhogo ukunogeao?
Duh!
Naacha basi , tuendeleze siku.

Mpate Linton Kwesi Johnsonakikuambia Want fi goh Rave

Read more...

Ukitaka kupigana!

Kwa kawaida ya binadamu huchagua kugombana na yule aaminiyo anamuweza kumpiga.
Ukiona njemba , mara nyingi ni rahisi kughairisha ugomvi.
Hii imetusababishi dunia ambayo njemba kunaanga anajinoma kweli.

Lakini.......
Baadhi hata kama sio manjemba, wakistukia mnyonge hawakawiii kumuonea.

Duh!
Lakini ushawahi kustukia mpaka watoto wadogo wengine wakikustukia mnyonge wanakuonea pia?

Inasikitisha wanyonge kwa wanyonge huchaguana wenyewe kwa wenyewe wakishindwa kukabili njemba mbabe.

Lakini......

Kama wewe ushawahikushuhudia mtoto mdogo akitaka kumzidi dada au kaka yake katika kudai haki yake kutoka kwa mama, anaweza kushinda si hata kwa kutumia mabavu asiyokuwa nayo, huwa anatumia ile silaha yake ya kulia. Akishalia basi unaanza kuona mama anaanza kufikiria labda mtoto apewe tu yale maziwa au ule mdoli.

Sasa....
Mtoto aliliapo kitu mara nyingi hupata haki yake.
Lakini jinsi anavyokua staili hiyo yakudai haki huishiwa nguvu.Toto kubwa likilia linaweza hata likapigwa konzi anga nyingine.

Najiuliza tu sisi nchi masikini ,tulio halalisha misaada ni haki yetu, staili yetu ya kuomba misaada kwa haki inakipingamizi kizingatiacho umri wa nchi?

Samahani!
Niko mawazoni tu....Usistuke sana.Haya tuendeleze.....!
Pata Steel Pulse

Read more...

Ushawahi kuiba Peremende?

>> Sunday, April 22, 2007

Peremende tamu
Ukiilamba lazima upate utamu
Inakudaka hata ukijua hakuna yake umuhimu


Duh!
Unajua nilikuwa najaribu kuandika shairi!
Lakini labda nikuache na wadau ambao hawakunitenga wikimwisho hiii.....
Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Mzee wa Nairobi

Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Mzee wa Kameruni

Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Heidi , asante kwa kuwakilisha Darfu!Alafu saamahani kwa kutofikiria unaongea Kiswahili


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Tommy


Lakini ... ngojea Jamiroquai aseme....


Sasa aaaaaaaaaa..........
Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Mzee Aliko. Lakini Mzee hujui tu jinsi gani wewe muhimu kwangu!
Lakini tuache hilo.....
Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Mkuu wa Kikao na Al Tunes


Lakiniiiiiiiiii........!

Tukiendelea....
Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Marina
Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Vera
Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Sophie.Kwa wasiomjua, anaimba kama malaika..............
Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Dj Amara na mimi....
Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Aiyekoto na....
Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
New York, Dar-es- Salaam na Morogoro
Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Lakini unajua huyu mwanamke alishaniibia mpaka simu jana!
Ila timu yangu ilikuwa kubwa tu ndio maana nikatoka mzima.
Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Ni huyu tena.
Unajua si kila mtu aonekanaye freshi maanayake hana issues. Basi ndio huyu aliye nipa aidia ya kutunga shairi- Usha wahi iba Peremende.Ingawa nimeshindwa kulimalizia:-)
Lakini tuache hilo!
Nakuacha na Sanchez...

Jumapili njema!Lakini ukinipitia hapa niachie ile meseji.AU?

Read more...

Ukiwa Uchochoroni!

>> Friday, April 20, 2007

Najua unakumbuka ukiwa uchochoroni nini kinatokeaaaaaa!
Duh!
Unaweza kubakwa.
Unaweza kubaka.
Lakini unaweza ukafanikisha mambo fulani fulani bila washikaji kustukia.
Umekumbuka eeeh?
Duh!
Nisikutishe kile kitu siri yako, hatukustukia !
Usiwe na shaka!
Lakini kabla sija sema sana......Magic System wako mawazoni.....

Duh!Lakini nimewakumbuka washikaji niliokuwa nao wiki jana.....
Sasaaaaaaaa.....
Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Mzee Ogola!
Labda ngojea aseme....

Kuhusu hiyo video hapo juu sisemi!Usiniulize!
Tuendelee......
Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Mzee Allen na Mimi



Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Mzee Allen na Martin


Mzee Allen ,Mimi na Martin











Au ngojea kidogo....


Okeiii nimestukia hicho!Ngojea nikutulize kidogo na Cheb Bilal hapa...


Basi tuendelee....



Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Mzee Johan




Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Mimi na Dj Ezza


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Mheshimiwa Bonanza aka Cool Brother.
Kumbuka ni mimi tu naruhusiwa kumuita hivyo:-)
Asante kwa yote Bro!


Tukirudi Uchochoroni.....




Nisikufiche kuwa mara nyingi ni mimi muoga.
Lakini kwanini ni wewe unachagua kuogopa?

Ushastukia hakuna ajuaye unasilaha gani ndani ya koti?
Unajua hatujui nguvu za ile karate yako na u Bruce Lee wako ?

Samahani!
Lakini............najua....!


Ushawahi kuwa gizani, uchochoroni halafu ikawa ni wewe unaogopa.
Lakini najua ushawahi kwenda kujisaidia kichakani bila kujiuliza kuwa kuna nyoka wala sisimizi.Nakukubalia kuwa kichakani si uchochoroni.

Lakini.....?
Halafu ushajua kwenda haja hata kama ni muhimu kuna kastarehe kake?

AU UNABISHA?

Duh!


Sasa.......
Unafikiri kama wote tuko gizani, uchochoroni kwanini ni wewe unayeogopa?
Kwani unafikiri jambazi yeye anauhakika kwamba wewe.....
Duh!
Ngoja niache!Nisikuzingue!Kama huelewi nasema nini usiniulize:-)!

Ijumaa njema!

Nakuacha na TEEYAH akikupa couper decaler

Read more...

Msenge aongeleapo maswala ya Uke!

>> Thursday, April 19, 2007


Ilipotokea ile filamu ya Darwin's Nightmare, watu wengi walilalamika jinsi gani mtu kutoka sehemu nyingine kutengeneza filamu kama hii kuhusu Tanzania.Hata mimi kama binadamu ambaye sipendi kudhalilishwa ilinigusa kinamna, ila ikaanza kunifanya nijiulize sana maswali kibao.
Moja ya maswali yalikuwa....

  • Hivi kipofu kwa kua haoni , hawezi kuusimulia uzuri wa vionekanavyo?
  • Je, msenge hawezi kuwana kauli zenye kina kuhusu mahusiano ya mawanamke na mwanamume?
  • Hivi mtoto hawezi kuona jambo wakubwa waliotealo makengeza?
  • .............nk


Basi ngojea nikupe trailer ya Darwin kama umeisahau.......



Basi bwana.......!
Katika kujiuliza sana haya maswala nikaona kuwa mara nyingi sisi wabishi tu. Kipofu na aonaye wote tunamapungufu. Naamini kuwa tutake tusitake mara nyingine kipofu ndio aonaye kuliko mwenye macho. Inategemea tu nini mnalenga.Ingawa pia jambo hili si rahisi kufananisha, lakini mara nyingine mwenyeji huzoea jambo, muonekano , hata harufu ambazo ni mgeni huweza kustukia au kuona ni tatizo.
Unaweza kubisha lakini!Sikukatalii!
Lakini kabla sijaendelea ngoje nimuache Steve Wonder, miongoni mwa vipofu wawezao kukusimulia uzuri na upendezaji wakitu kuliko wengi sisi tuonao......


Sasa ...!
Swali:
Baada ya ile filamu ya Darwin's Nightmare unafikiri nini kimebdilika kuhusu swala aliloliongelea?Au ndo lishapita tena?


Haya basi nikipata muda nitaendelea kuongelea swala hili. Lakini nachotaka kukuambia ni kwamba usishangae Msenge akakufundisha maswala ya uke. Au unafikiri msagaji kwasababu ni msagaji hajui maswala ya uume?
Hebu nikuache na George Michael , msenge ambaye jicho lake kwenye baadhi ya lirics zake zaonyesha anaweza akafundisha maswala kadhaa ya jinsi ya kumuangalia msichana.....

Read more...

Maswala ya maandamano na kupandisha Mori

Kudai haki ni haki ya kila mtu, hivyo naamini kuandamana katika kudai haki ni haki ya kila mtu.Kupandisha mori ni ubinadamu, hivyo sidhani kuwa ni jambo lakushangaza kuona wadau wamechachamaa.

Sanaa ya kupandisha mori, mkwala na kugombania swala nahisi linakaujuzi ambako watu hukapuuzia.Ukicheki taarifa za habari zinazogusia maswala ya waandamanaji hukawii kujionea jinsi wadau walivyofuzu katika sanaa ya kuwakilisha ujumbe. Hukawii kuona kundi likiimba , kuzomea au hata kutumia silaha ndogo ndogo kama mawe kuwalenga wababe wenye bunduki.

Kinachonidaka kinamna ni saikolojia ijifichayo nyuma ya mtupa jiwe.
Nachojiuliza ni, ni nini wanafikiria wabebao bunduki hasa pale wakubalianapo kihoja na madai ya waandamaji waliopo mbele yao.


Kinachonizingua ni jinsi nchi mbalimbali zikabilivyo waandamanaji.
Bongo hukawii kupigwa virungu au hata risasi ukiandamana na kukutana na askari walio tumwa kukutawanya.

Lakini kuna kitu kingine ambacho mara nyingi huwa nakiona kwa wadaio haki,ni swala la mori kuchanganyika na lugha ambayo unaweza kushangaa mara nyingi. Unaweza ukastukia wanaodai haki za kuleta amani wakawa wanaimba au kupayuka maneno yaashiriayo mauaji na hata yakiukayo maadili ya haki wadaiyo.

Hebu cheki maandamano ya katuni hapa.....


Nadhani hapo juu hukawii kuona jinsi gani mchoraji mmoja wa Tanzania awezavyo kugeuza watu wadaio amani kuamua kuwa Watanzania wote ni kitoweo halali.


Sasa...
Ndio najua maswala ya kurahisisha majibu ya swala ni rahisi kwa binadamu hasa kwa maneno.Hivyo nakiri kutojua sana nini huendelea ndani ya kichwa cha binadamu akiamua, sasa basi, liwalo naliwe!
Lakini vilevile utasemaje ukisikia kuwa Wamasai huwa wanaweza kukupa dawa ya kupandisha mori ukitaka kukasirika kisawasawa?

Lakini tukiacha utani kuna baadhi ya Mori wapandishazo watu mimi naona zinapitiliza.Eti utasikia kuwa katika maandamano yakupinga mashindano ya U-miss huko India baadhi ya waandamanaji wakajichoma moto!Duh!Yani kabisa mtu kajimwagia mafuta ya taa au petroli halafu kajitia kibiriti kupinga mashindano ya U-miss!
Lakini ndiyo hivyo tena hataki tamaduni zao zichafuliwe na haya matamaduni machafu.Sasa haya matamaduni machafu mara nyingine kuyapiga vita yanataka jicho lionalo kote. Je, televisheni haichangii zaidi kuharibu tamaduni ikiwamo pia swala la mitazamo ya uzuri na matendo ya watu?Sasa ukijichoma kupinga u-miss ukaacha kujichoma mbele ya kituo cha televisheni ......Du ngojea niache hili swala

Lakini hebu cheki wenzetu wa Northen Ireland wafanyavyo maswala.....

Hawa jamaa walifikia hadi kupiga mawe watoto wa chekechea kisa wamekosea njia. Haya maswala ya Orange Order
ya wa protestanti ukichanganya na ya wakatoliki basi huwa kasheshe.


Nachoshindwa kuelewa ni jinsi nchi mbalimbali ziwathaminivyo watu wake kitofauti.
Naamini pia jinsi serikali iwakabilivyo waandamanaji na wafungwa ni jinsi ionyeshavyo ithaminivyo utu wa watu wake.

Eti...
Mkimbizi Afrika msosi apewao ni tofauti kabisa na mkimbizi Kosovo.Wakosovo bajeti yake kubwa.Hapa labda tutasema kuwa ni kwasababu wao kwa wao wanapendeleana.

Sasa...
Muandamanaji Dar kirahisi anaweza kupigwa virungu au hata risasi na Mtanzania mwenzake hata kama anakimbia tayari. Halafu unaweza kusikia Ujerumani wamewatawanya waandamanaji kwa kutumia maji.
Duh!
Nakubali kila mtu anatumia uwezo alionao kushughulikia swala akabiliano nalo.

Swali:
Hivi lile swala la kumkabili mtoto kwa kumchapa Tanzania linanguvu sawa na lakumnyima kutazama TV pale sehemu sehemu?


Kabla sijaliacha swala la kukabiliana......
Kali ni ile niliyoikuta Scandinavia ambapo wafungwa huwa wanalikizo, halafu hukawii kukuta kuwa unafanyanaye kazi sehemu na ukonaye bar ila yeye ni mfungwa kwasababu anarudi jioni jela.Halafu eti anateseka na kuapa kuacha kale katabia kaliko mfunga.

Ushastukia lakini kuwa mara nyingi kumtesa binadamu ni rahisi kuliko watu wengi wafikirivyo na wafanyavyo?


Tukirudi kwenye maandamano hebu wacheki kidogo Wa-South Afrika hapa...

Halafu kama ulivyosikia, eti kundi hilo lililokuwa na mchanganyiko wa weusi na weupe lilikuwa linashiriki nyimbo za kuapa kuua weupe.Duh!

Swali la pembeni:
Ushawahi kupiga mkwala mtu wakati unajua akicharuka utakimbia?

Mimi nisikufiche nishawahi kufanya hivyo halafu nikachelewa kukimbia, basi wachanibwengwe!
Lakini tudai haki zetu!Lakini pia tukumbuke wakati tunadai tunasema nini na mara nyingine tujiulize kuwa hivi ni kweli hii haki ni yetu?Hebu mcheki fisi akistukia kuwa yuko na washkaji wakutosha amfanyiavyo Simba....

Usiwaonee huruma mara nyingi ni simba waporao fisi kitoweo.

Samahani usizinguke sana!Alhamisi njema!

Lakini tukumbuke mpandisha mori na mpandishiwa mara nyingi ni damu moja.. Au ngoja nimuachie Junior Reid

Read more...

Karibu tena Chifu Nyerere!

>> Tuesday, April 17, 2007

Samahani nilikuwa na maanisha Chifu Mandla Mandela!

Nakubali kuwa Afrika Kusini si Tanzania. Na nakubali ukiwauliza watu wengi wanaweza kusema kuwa lilikuwa wazo zuri kuufuta uchifu Tanzania. Mtu anaweza kudai kuwa uchifu ulikuwa unagawa watu na maeneo katika hali ambayo ingehatarisha utaifa wa Tanzania.

Sasa hivi baada ya miaka siku kadhaa, nafikiri si vigumu kugundua tofauti ya Dar es Salaam na Mtwara. Nafikiri si siri kuwa ukubwa wa kipenyo kati ya tajiri na masikini unakua kila siku.

Ndioo..!

Naamini labda ukabila ulikatwa nguvu baada ya kuua uchifu,
Labda tulivyounganishwa chini ya kiongozi mmoja lilikuwa jambo zuri.
Sasa unafikiri tuko chini ya kiongozi mmoja nchini Tanzania?
Kama ni kiongozi mmoja , je mbona matabaka ambayo tulikuwa tumetafutia dawa kwa kuwa chini ya kiongozi mmoja yanakua?

Hivi unafikiri Kikwete ni kiongozi wa matajiri au masikini?
Utashangaa uchifu ukirudi Tanzania kama Ulivyorudi kwa mjukuu wa Nelson Mandela?

Usitishike, nawaza tu!

Read more...

NAHISI KUNA KAKICHAA KIDOOOOOGO!

>> Friday, April 13, 2007

Pale....

  • Binadamu waendapo kupigana vita huku wakidai ni kwaajili ya kutunza na kuendeleza amani
-eti hata vita ya Iraki ni ya kuleta amani Asia katikati.
  • Wamagharibi watembeapo nusu uchi wakati wa kiangazi, lakini kuacheka waishio sehemu zenye kiangazi siku zote kwa kutembea nusu uchi
  • Waafrika waendapo makanisani zaidi ya hata wale wamagharibi waliowaletea Ukristo
  • Wairaki wapiganapo wao kwa wao kisa nani Mshia nani Msunni ,badala ya kumgombania Mmarekani na wenzake ambao wanawashutumu kwa kuvamia nchi.
  • Tukubalianapo uzuri U machoni mwa mtazamaji lakini hatuachi kuwaambia watu nani mzuri na nani mbaya.
-Kama uzuri umachoni , vipofu wanastukiaje maswala?
  • Miziki iitwayo ya asili- Afrika izidipo kupigwa kwa vyombo vya kizungu.
  • Mwanamume ajengapo uhusiano na matiti mpaka karibia kumshinda mtoto
  • Mwanamume ajengapo uhusiano wa macho yake na matako ya mwanamke
  • Katika dunia ya sayansi na tekinolojia zirahisishazo kazi kukuta wanawake wenye uhusiano wakaribu na misuli mikubwa ya wanamume.
  • Wanamume kwenye dunia ya sasa, ya sayansi na tekinolojia, waaminipo kuwa wanawake hawawezi kitu kwakuwa hawana nguvu za misuli kama wanamume.
  • .......................................nakadhalika kadhaaa mbili
Au?
Duh!Sijui kwanini Barry White yuko kichwani bado.
Ngoja basi nimuache na kibao Can't Get Enough Of Your Love Babe

Read more...

AFANDE BIKIRA!

Bikira mtoto mzuri
Mwanasesere bei ghali
Bikira kijana shwari
Kijiweni ye dalali
Ua hariri
Msibani ye wali
Ishara isiyo hatari
Mtoni atuna ka-jabali
Japo hazina kwa kukariri
Jihadhari kwenda Mbali
Bado ni kaukweli.....
Hajui kuendesha gari

Na:Simon Kitururu

Nakuacha na Miriam Makeba akikupa kibao Kilimanjaro.

Read more...

Uganda Histori Yajirudia/Wolfowitz naye adakwa


Mtu usipoangalia unaweza kuacha kufuatilia habari za dunia.Halafu si mchezo , ukizoea kuangali habari hukawii kudumaa kinamna. Kila siku utasikia huyu kafa wale wamelipuliwa , wale wanakufa njaa, mafuriko nk.Inasikitisha kuwa habari muhimu zimekuwa ni zile zenye maswala mabaya mabaya tu.Halafu naamini akili inazoe kuwa hizi ndio habari.

Ukitaka kujua kuwa hii tabia ya kwamba habari mbaya ndio habari nzuri imewaingia watu kisawasawa, tembelea blogu au tovuti zenye habari nzuri za watu au kitu. Hapo utakuta watoa maoni wanaanza kutoa maoni mabaya kuhusu huyo mtu au hicho kitu.Hivyo kuna watu tayari wasipopewa habari mbaya , wakichangia watatoa maoni mabaya.

Lakini kama kawaida hakuna haja ya kulichukulia hili swala kijuujuu. Labda mimi na wewe ni kweli hatudakwi tukizubalia habari mbaya.

Au?
Lakini umesikia Uganda Waasia wanabwengwa kisa mmoja wao mfanyabiashara ya sukari alitaka kukata msitu wa Mabira kwa ajili ya shamba? Inasemekana kulikuwa na watu kibao waliokuwa wanadai Waasia warudi kwao. Na hisi hii inanikumbusha Idi Amini.

Duh!La hasha!
Inanikumbusha Mchungaji Mtikila enzi zake alipoanzisha kampeni yake yakuwaita wahindi Magabachori.


Nilishuhudia mawe kadhaa yakiandama magari ya Wahindi na biashara zao Bongo.

Na umesikia Mzee Wolfowitz, raisi wa benki ya dunia ambaye anasifika kupiga vita rushwa katika benki hiyo, kadakwa akimpa uchochoro wakufikia juu kwenye mshahara mzuri mpenzi wake?

Duh!
Ngoja nifikirie habari nzuri ya kuandika!
Bingo!
Ni bomba sana kuwa mimi na wewe ni wazima!
Ijumaa njema!

Read more...

Mwanadada akikuuliza kama kavaa ulimbwende!

>> Thursday, April 12, 2007

Mwanadada:Eti nimependeza?
Mzee Mzima:Ndio umependeza!
Mwanadada:Mbona umejibu hata bila kuniangalia?
Mzee Mzima: Wewe hupendeza kila siku, unajua wewe mzuri sana.
Mwanadada:........=pointi tupu
Mzee Mzima:........=kubunia na kujing'ata

Ushastukia unaweza ukawa umedanganya mara kadhaa ukipigwa maswali ya namna hii?
Halafu usisahau zile tarehe maalumu za kusherehekea nanihiii.

Duh!
Akinadada kwanini mwatuweka konani namna hii?
Mpaka kesho haka kamchezo kamahusiano kananizingua kweli.
Lakini asanteni akinadada kwa yote!
Nawaacha na kibao hiki The Secret Garden ikipigwa na Quincy Jones, Al b sure, Barry white, na Debarge kinikumbushacho .......

Read more...

UTAIFA mtamu , lakini ukizidi.........


Bendera twazipepea sana! Nchi zetu twajivunia!

Hiki kitu Utaifa mara nyingi huchukuliwa kuwa ni kizuri. Na sipingi uzuri wake. Nachojiuliza ni , ni nini nafasi ya Utaifa wa mataifa yetu ya Afrika ambayo bado yanasumbuliwa na Ukabila, Udini nk au kifupi yanautaifa unaoendelea kujengwa?
Napenda kusema hivi kwa sababu mimi binafsi naamini kuwa Utaifa wa nchi kama Tanzania haujakamilika. Bado utasikia kuna Uzanzibar na Utanzania bara. Bado utasikia maswala kibao ya ukabila yakiwa msitari wa mbele.Ni kweli wakati wa kushangilia michezo tunapeperusha bendera zetu.Na siku hizi tumeongeza kuvaa bendera zetu ingawa bado nafikiri tunavaa zaidi bendera ya Marekani na Uingereza zaidi.

Tukiachana na hilo......

Utaifa ni hali mojawapo yakujibagua. Hii ni kusema mimi si wewe.Mara nyingi hasa ni kusema mimi ni zaidi ya wewe. Hii mimi si wewe inatumiwa sana hata na vikundi vya UNAZI na UNEONAZI katika kubagua waaminiwao kuwa si Wataifa wa taifa husika.Utaifa huu uliwanyemelea na kutaka kuwatenga hata akina Nyerere, Generali Ulimwengu nk.

Lakini....

  • Wakati tunadhamiria kuunganisha Afrika, je, tuachane na kung'ang'ania Utaifa?
  • Je, tung'ang'aniapo Utaifa tuuuche ukabila uondoke kabisa?
  • Je, katika ulimwengu huu wa utandawazi udaiwao kuwa dunia imekuwa kijiji, umuhimu wa Utaifa unamaana ilele?

SIJUI!
lakini....
Inasemekana mapinduzi ya viwanda tutayaruka Afrika na kuingia huku chobisi. Je , hii inamaana si lazima tupitiengazi zote za Utaifa kabla ya kuunganisha bara la Afrika.

Sijui!

Lakini nachojua ni kwamba chochote kikizidi huzaa madhara yake.
Wewe unafikiriaje swala hili?
Alhamisi njema!
Mpate Gil Scott Heron

Read more...

Maswala Ya kulamba Makamasi!

>> Wednesday, April 11, 2007


Mambo ya aibu na uchafu ni baadhi tu ya mambo yatawalayo mitazamo ya jamii .Ni jambo ambalo hutusababishia muelekeo wa matendo yetu na hata muonekano wetu.Inawezekana kabisa lile bugaluu na panki tulilonalo ni juhudi tu ya kujibanza kwenye jamii.
Lakini kuna maswala ya uchafu na aibu ambayo kwa mara nyingine watu huyaepuka hadharani tu . Ukiwaweka sehemu wakahisi hawaonekani basi mambo hutafsiriwa vingine.
Mimi si muhukumu mtu, nachojaribu kuuliza ni:
Je, ushawahi kujamba hadharani, watu wakasikia?.
Basi labda ulijikausha ukafikiri watu hawakukustukia.Lakini vilevile ukajua watazungumzia hilo baadaye.
Nafikiri hukufa kwa hilo. Naamini kuna mambo ni ya kibinadamu tu , huweza kutokea, lakini maisha yanaendelea hata baada ya kijambo tarumbeta. Lakini hebu mcheki Silvio Berlusconi akilamba kamasi kabla sijaendelea...

Sasa, ushawahi lamba makamasi kisirisiri?
Duh!Nimesahau kuwa wewe msafi. Lakini sinasikia unalamba na kunyonya sehemu-viungo vya kutolea haja ndogo , na mara kadhaa umefikiria kulamba sehemu ile nyingine.

Samahani tena!

Unajua nimechanganya watu!Nisamehe!
Lakini katika maswala ya uchafu watu wengi husahau chombo cha mabusu, yani mdomo yasadikika unavijemedari vihusianavyo na uchafu kuliko hata sehemu za haja ....

Duh!
Ushastukia kuwa mara nyingine common sense inatuchezea akili katika mahusiano yetu na uchafu?


Hivi ni tendo gani chafu kuliko yote ushalifanya?

  • Ushawahi kushika mavi kwa kutaka kuyaangalia kwa karibu?
  • Ushawahi kujikojolea?
Kwa wakubwa:
  • Wanaume: unakumbuka mara ya kwanza uliposhuhudia yale majimaji yenye mbegu ?
  • Wanawake: Je unakumbuka , hasa kama utu uzima ulikukuta ukiwa hujajianda na mashabiki wawapo?


Twaweza kukubaliana kuwa tutake tusitakake kila siku tunachukua hatua kadhaa maishani.Kama tukohai matendo yatatendeka tutake au tutusitake.

Nisikufiche kuwa wengi wetu hupendelea matendo yetu yenye kutuletea sifa nzuri ndio yaonekane kwa watu. Matendo ambayo twahisi yatatuaibisha twayakwepa kwa kila njia.

Lakini..

Sisi kama binadamu lazima ubinadamu utatokea katika matendo yetu. Kuna mambo yatuleteayo sifa kwenye anga moja lakini yanatujengea maadui katika kambi nyingine.
Nachojiuliza ni jinsi tulivyoweza kutawaliwa na hulka hii ya kuonaaibu iwapo kunamapungufu katika matendo yetu. Inashangaza hata tuwezavyo kukwepa watu ambao twahisi hawatuletei sifa nzuri.
Nachojaribu kusema ni ni kwamba, sisi kama binadamu tutaendelea kufanya matendo kama binadamu. Tutajaribu kuwa malaika. Na ni vizuri kujaribu kuwa malaika. Lakini mapungufu tunayo.

Je umuhimu wa usafi tuuabuduo leo hii si zao la kuwepo kwa uchafu?
Hivi tunavyo jaribu sana kuwa wasafi ni kweli hatuutaki uchafu?Je , kuupiga vita uchafu si ni moja yashughuli tu ituwekayobize sisi kama binadamu?
Usitishike , nawaza tu!Ukweli ni kwamba baadhi ya mambo yapo tu hata tusipokumbushana. Lakini je ni vibaya kukumbushana? Sijui.Tuendelee kuupigavita uchafu. Lakini ushastukia kuna vile vimambo ni afadhali tu vifanyike kisirisiri ingawa hata ingawa tunajua vilivyotafsiriwa kuwa vinatia aibu mara nyingi ni mtazamo tu.
AU?
Namrudia Nina Simone akikuimbia Four Women

Read more...

Leo , Jana imepita.

>> Monday, April 09, 2007


Kuna mambo ambayo tunajitahidi sana kuyapinga kama binadamu. Lakini kuna mambo hayapingiki kama sisi ni binadamu. Au niseme.....


Lakini kuna kitu nashangaa baadhi ya watu wananitumia barua pepe kuwa niache kuweka. Mojawapo ni picha zangu na za rafiki zangu. Napenda kusema ni ukweli rafiki zangu kibao picha zao hazija tokea hapa. Na walio tokea ni rafiki zangu kibao pia ambao sijilaumu kwanini ni rafiki zangu ambao ukweli wananisaidia kujisikia naishi kisawasawa. Ee bwana eeh! Kama unajua maana ya blogu, basi niache nifanye nacho takakufanya na nachofanya.
Duh!
Tuishi basi!
Kwa wale wanaodai nimezidisha labda niongezee na picha za leoleo. Lakini kwani ni nini nimezidisha? Kama tunapata choo basi siye mabigwa.AU?
Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Au labda...



Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Samahani lakini kwa kukataa kuacha kuweka mambo yangu au picha zangu.
Au msikilize Buju Banton akisema Destiny

Read more...

KUMTONGOZA MGONJWA!

>> Sunday, April 08, 2007

Ukiwa mgojwa huna ujanja.Dakitari akisema hunabudi kutii.Ubishe unalakubisha?
Kweli usipoangalia unaweza kuamini kuwa mnyonge hana janja ya kusema hapana.

Duh!Au niseme.....


KUMTONGOZA MGONJWA!

Mgonjwa si mali
Hana kauli hata pale penye wali
Na sina hata kaushauri
Mambo yote ajua dakitari
Yasemwa kauli zake si hatari
Japo twajua hata kwa siri
Si zote siku ye kachumbari

Lakini samahani!
Nsikuweke mashakani
Masharti kufuata kijiweni,
so ndo maji wapata kisimani?
Mwamini jiamini
Je ni kweli huna jinsi?
Jiamini muamini
Je umelikwepa jinamizi?

Mwamini usimuamini
Jaribu pata yako firigisi
Na: Simon Kitururu
Nakuacha na Manu Dibango basi akupe Afrika.....

Read more...

Jamani kaka mimi sitaki!Ntakusemelea kwa mama weee!

>> Friday, April 06, 2007

Kuna mambo ambayo tamaduni nyingi zimekataa. Mojawapo ni hii ya ndugu kuingiliana kimwili au ku.........

Duh! Bado sielewi ni kitu gani kinafanya baadhi ya watu kumtamani dada au kaka yake kimapenzi. Lakini hiki kitu kipo.Wengine wanadai katika familia zinazolindwa sana. Nikimaanisha wazazi wakali, basi kuna baadhi inabidi wafanye kale kamchezo mumo kwa mumo.

Cha ajabu nasikia haka kamchezo ka kupata nyama ya hamu mumo kwa mumo si kuvunja sheria katika nchi nyingi. Halafu unajua tena enzi hizi za demokrasia wadau wa Ujerumani wanapigania haki ya kula mapochopocho ndani kwa ndani.
Wasikilize basi dada na kaka hawa wakipigania haki yao ya mapenzi ya mumo kwa mumo...

Duh!Jamani haka kakitu mapenzi ni kagumu , lakini kweli ni kagumu mpaka hakapatikani nyumba ya jirani?
Tupendane lakini.........!

Read more...

Ushawahi kutungiwa jina halafu likashika?


Kuna watu wakikikutungia jina au hata wakitunga neno linashika. Kuna wengine hata wajaribu nini jina halishiki na wala kale kaneno watakako kukafanya maarufu watu wanakaacha kushoto.

Katika baadhi ya watu jina lao kama halishiki kama lilivyo basi watu hawachezi mbali na jina lake.Tukianzia na Amerigo Vespucci. Huyu jamaa kutokana na vyanzo vya habari vingi tu, ndio inasemekana aligundua Marekani na sio Christopher Columbus kama isemekanavyo.
Inasemekana misafara ya kadhaa Mzee Chris alikuwa anaishia katika visiwa kadhaa kama West Indies nakadhalika. Lakini haya yote inategemea na vyanzo vya habari tofauti kuegemea sehemu tofauti.
Tukirudi kwa Amerigo, huyu ndio inasemekana alichangia sana uchorwaji wa ramani ya marekani. Kwa kushirikiana na mchora ramani waenzi hizo maarufu aitwaye Martin Waldseemüller
Huyu mchora ramani alipomaliza kuchora ramani ya dunia bara la Marekani akaliita America kwa kuhusisha bara hilo na stori za Amerigo na mtazamo wa Amerigo aliompa.
Katika historia utakuta kunakipindi wachora ramani walitaka kubadili jina hilo kutokana na mashabiki wa Christopher Columbus kumpiga vita Amerigo kuwa muongo. Lakini wapi jina likan'gan'gania mpaka leo. Sitaki kuingia ndani katika swala hili la Christopher Columbus na Amerigo nani mkweli au muongo. Lakini nafikiri wote tutakubali kuwa wadau wa Christopher Columbus wamefanikiwa kumuekajina lake masikioni mwetu kuliko wadau wa Amerigo. Kuhusu kwanini likaitwa america na sio amerigo, kuna stori nyingi. Lakini iliyo shika ni kwamba mabara yote yalikuwa yanachukuliwa katika majina ya Kike. Africa, Europe....nk yote ni majina ya kike enzi hizo.
Lakini....

Lakini poa tu ukimuita mtoto wako wakiume Africa. Sikuizi yote zembwela , ngoma ya ukae.

Afrika , hili jina kasheshe. Wengine wanadai hawa jamaa waitwao Afri kutoka Tunisia, kuwa wamechangia.
Wengine wanadai limetokana na neno Aprica la kilatini nimaanishalo sehemu yenye jua.
Wengine wamedai kuwa linatokana na neno la kigiriki Aphrike limaanishalo bila baridi.

Lakini unajuatena hakuna haja hapa yakuingia sana. Nachotakakusema kuna kamjamaafulani sina uhakika nani lakini nahisi ni kajamaa ka bara jingi kakasema na jina liwe Afrika. Na likawa.

Lakini....

  • Ziwa Victoria tumeenda mbele sendema kurudi nyuma sendema. Lakini pamoja na kujua jina lake la kweli, Watanzani wengi bado twaliita Victoria.
  • Dar-es-Salamu-Duh !Hivi Mzizima lilikuwa naubaya gani?
  • Na kadhalika kadhaa. Najua unajua majina kadhaa tuyatumiayo au
Usitishike.Labda jina ni jina tu. Au?
Mimi mwenyewe nimefanikiwa kuitwa majina mengi. Nayameshika.Lakini chaajabu vikundi tofauti vyaniita jina tofauti. Hakuna noma lakini.
Nimejaribu kutungia watu majina na yameshika. Lakini nawaonea wivu walio tungia mpaka barazima jina na lika shika.

Duh!Kumbe wivu mbaya eeh?
Lakini si kweli kuwa kila wivu ni mbaya. Ukifanya vitu poa nivihusuduvyo sitakuloga napata nguvu tu ya kujaribu zaidi.

Sasa Baadaye basi!
Ngoja nikuache na Sina Makosa na Soukous Stars

Read more...

Binadamu kwa madoido!We acha tu!

Napenda kukiri kuwa kuna watu wafanyavyo vitu vyao huwa hawanichoshi hata siku moja kuwa sikiliza au kuwaangalia. Lakini mara nyingi nashindwa kuacha kuzinguliwa na jinsi binadamu wanavyotengeneza vikorombezo mbalimbali vya aina mbalimbali kwa ajili tu ya kutaka kuwadaka binadamu wenzao kimawazo hata ki..... nakadhalika.

ukiangalia matambiko mbalimbali binadamu amfanyiayo Mungu wake hutaacha kuzinguka na madoido aonyeshayo. Wengine watalia huku wamenyosha mikono juu wengine watainama, wengine watalala juu ya misumari, ilimradi tu kumuonyesha Muumba au mauunguzaji jinsi gani wanamaanisha.
Duh!
Halafu hili swala la Mwenyezi Mungu watu wengi wanamuona kivyao!Halafu kila mmoja hakawi kuhisi mwenzie kapotea.Hapo ndio kasheshe.

Kinachoniacha hoi kingine ni jinsi binadamu akitaka kuonyesha madoido jinsi wachaguavyo mavazi yaendayo na madoido. Basi wengine watachagua kanzu, wengine vibwaya na vibuju , makofia makubwa kwa madogo na kadhalika kadhaa.

Ukweli ni kwamba hili swala la madoido nadhani mara nyingi tukubaliane tu halina mpango , lakini linaleta viutamu na vituko vyake ambavyo labda ni muhimu kwa sababu tumeamua tu kua ni muhimu .

Swali:
Hivi duniani binadamu anajali vitu muhimu?
Muhimu yako unaikumbuka?

Sasa....
Kwasababu tuko katika kipindi cha pasaka kwa wakrito na wakristu ngoja tuangali madoido katika kanisa la Holy Sepulchre


Hapa naona utaona jinsi madoido ya wanakanisa. Cha ajabu ni kwamba ingawa hapa ni miongoni mwa vipengele vya ardhi wakristo wavioanishavyo sana na yesu , huwa wanabwangana hapa kuhusu nani anamiliki kishkaji sehemu. Sasa hapo ndio madoido yanapo nishinda . Maana mpaka watu wanabwangana katika sehemu waziitazo takatifu. Duh!
Lakini wengine wanaonyimwa kuonyeshwa madoido yao hapo wameamua kuhamia huku kwa Garden Tomb


Lakini achana na madoido ya dini zihusianishwazo na Mungu. Turudi katika uchawi.Wachawi kwa madoido huta waweza. Ila wachawi wakizungu huwa wananiacha hoi na madoido yao pia . Maana hawakawii kukuuzia DVD ujifunze nawe.

Swali:
Hivi kwanini wachawi wa Kiafrika wasirisiri sana?

Hebu wajifunze kwa hawa hapa chini.....


Sasa kama kunamchawi yeyote atakaye tufanyebiashara yakuuleta uchawi huu karne hii tuwasiliane basi:-)


Lakini ushastukia wajanja wengi haswa hawa wanadini , wanasiasa, waigizaji na nasikia hata wachawi, ni wabunifu sana wa matumizi ya sauti. Wanajua jinsi ya kukutisha, kukufanya uwaamini, na hata.......
Lakini wote mimi nawaamini kwa kuigiza.

Duh!Kabla sijaendelea ngoja nikuache na vuduMaana hii ya wadominika imeanza kuuzwa. Ya Benin na kwingineko sijasikia bado.


Sasa Tanzania vipi? Madoido ya nguvu za giza kuexport lini?Maana nasikia kuna wajanja wanatengeneza radi na kadhalika.Naamini zao la radi pekee linaweza kukomboa wengi hapa duniani kwa jinsi tesivyopendana,

Ee Bwana eeh !Kama msherehekeaji basi Pasaka njema!

Read more...

Roho ya Kwanini!

Sijui kwanini
Nani na nani ana nini
haiepuki mimi na ninyi
Ya washawasha maini

Matajiri kwa masikini
roho ngumu kama nini

Lakini kwanini?

Ni nini kiini?

Wataka yote maini

Tugaiane kwa makini
Yatutosha wote hiyo nini
Sasa, nini?
Na:Simon Kitururu

--



Read more...

Generali Idd Amini Dada akiongea, duh!

>> Wednesday, April 04, 2007

Kama ukipata muda angalia hii kitu. Mimi sisemi....
Read more...

Kuna watu nasikia wanajua kila kitu

>> Sunday, April 01, 2007

Maisha ni shule.Kila siku tunajifunza. Lakini kuna watu nasikia wanasema wanajua hata kama hawajui. Sasaaaa.....

ee bwana ye Luambo alikuwa anaongea hapo.
Nisikutishe !sikuelewa anasema nini.

Lakini kujua ni kitu kigumu. Nafikiri unafikiri unajua.
Lakini kuna kitu kama...ngojea niseme basi....





Sawa basi ngojea niache kusema. Msikilize basi Ninjaman

Read more...

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP