Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

NIKIKUANGALIA wakati UNA-SHAbikia, CHEkelea au ukiLIA, TIMU yako IKISHINDA!

>> Wednesday, April 30, 2008

Ukiwa na TABIA ya kumtazama binadamu, utastukia kuwa huhitaji televisheni wala kucheza bao ili ujiliwaze.

Binadamu hakosi jipya la kukustaajabisha, kama unatabia au jicho la kumchunguza.

Na....
.....ukijenga tabia ya kumtazama sana binadamu , iko siku utastukia kuwa, kama ni kubwa zima halafu halitumii kinyoleo, linaweza likawa lina nywele nywele zinakua kuanzia mashavuni kama ni janaUME, au linakua manyoya mpaka maeneo ambayo kama halijavaa kificha nyeti, linaweza kuwa na kipilipili mpaka maKWAPAni. (Na cha ajabu ni kwamba ,inaweza ikawa ngumu kwako au kwangu kufumbua fumbo la umuhimu na madhumuni ya kwanini manyoya na nywelenywele hizi nyingine humuota huyu binadamu maeneo fulani fulani bila ya faida iliyouchi ).


Binadamu kwa jina la ushabiki anaweza kulia, kupiga mtu au hata kujiua ,timu yake ikishindwa.

Binadamu hata kama ni mchezaji na achukiaye tabia za kisenge, unaweza ukakuta kampiga busu, akamkatikia kiuno na kumkumbatia mwenziye mwenye sehemu za haja ndogo zilizo fanana na zake ,KISA, amefunga goli, bila kukumbuka kuwa tabia hizo hizo alizofanya kwa kufurahia na aina ya mtu aliyemfanyia vitendo hivyo, ukijumlisha ,ndizo tabia za kisagaji ambazo yeye na jamii yake kama ungeondoa mpira na kuweka muziki wa bluzi , basi angepigwa mawe mtu na wapambe kwa kosa la USHOGA.

Inawezekana UMUANGALIAVYO mtu , unaOAnisha mahali alipo na nini kinafanyika,ili kuwa na uhakika na kitendo kuwa; ingawa anaguna, haiwezekani akawa anajisaidia haja kubwa sebuleni.
Si agunaye chooni hata kama kajikwaa huko msalani , atashukiwa tu anaguna kwa sababu anakwenda starehe kubwa?

Labda ni ka-ubinadamu kakupenda ushindani na kushinda, kamsababishiako binadamu afurahie timu yake ikishinda na ahudhunike akishindwa.
Lakini si kufurahia kushinda na kuhudhunikia kushindwa , vyote ni vitu vya muda mfupi tu?

Au labda ni kaudhaifu ka-kibinadamu kakutojua mwisho wa mchezo matokeo yatakuwaje, kamleteako binadamu tamu tamu ya kufuatilia mchezo mpaka mwisho.
Lakini si wengine huwa na uhakika wakushinda au kushindwa katikati ya mchezo au kabla mchezo kuisha?

Labda ni ka-utamu wa kushinda au uchungu wa kushindwa , kasababishako unaendelea kuwa mshabiki wa timu fulani.
Swali:

 • Unajua ushabiki , inawezekana ni aina ya ugonjwa wa akili kama lilivyo penzi?
 • Ushastukia mshabiki , nukta kadhaa baada ya kushinda au kushindwa anaweza kufanya ambacho hawezi kukiri waziwazi amewahifanya maishani?
 • Ugonjwa wa akili ni nini?

SAMAHANI nawaza tu!
Si unakumbuka hiki ni kijiwe cha Simon kitururu-MAWAZONI?
Siku njema!

Tulia na Acoustic Blues vibes kutoka kwa Eric BIBB akikupa GOOD Stuff

Au turudi tu kwenye Zouk Love ikija katika wimbo La Zouk Horay kama iletwavyo na Kaysha na kuwa remixed na DJ DUKA(samahani video inaweza kumkwaza mtu fulani au kuwa inamdhalilisha mtu fulani kwa mtazamo wa mtu fulani.Kama mtoto au mkwazika kirahisi, usiangalie .SAMAHANI!:-()

Read more...

UKINUKUU BIBLIA, KORANI au kamaSUTRA kwa MTU asiyeamini MUNGU!

Binadamu hupenda kunukuu watu, vitabu, matukio, ..... katika kujazia uzito au hata kuhalalisha kitendo au mtazamo wa mlolomo wao.


Binadamu , kirahisi, husahau wengine hawafikirii wala kuamini ukweli wao ni ukweli hata kama unaitwa sayansi wakati wanamnukuu Einstein kuwa E=mc2

Swali:

 • Unakumbuka kuna ambao E=mc2 ni= na ALbaMU mpya ya Mariah Carey na hakuna uhusiano wowote na Fizikia(Phisics)?
Nachojaribu kunong'ona ni:
....Unaponukuu mwingine asichoamini , unaweza ukawa unajipotezea muda.

Ukijikumbusha nukuu za mtoto.....
.....LImwanaMKE LAKO au LIBWANA LAKO ufikirialo kuwa ni zuri na lina roho nzuri, na ni tamutamu kama lawalawa nyama, linaweza kumliza mtoto mdogo akalia kama vile kaumwa na manyigu , kutokana na kumuogopesha MTOTO, kwa sababu kwa nukuu za mtoto, huliona hilo LImTU LAKO kuwa lina sura kama Nundu na meno kama Ngiri.


Ni rahisi kusahau kuwa kuna vitu vingi mtu umejifunza kuviogopa na hukuzaliwa unaviogopa, kitu ambacho mwenzio anaweza akawa bado hajajifunza kuviogopa na haogopi kama wewe.


Sasaaaa......

....ukimtishia asiyeamini MUNGU, maswala ya MUNGU , anaweza akamtukania Mungu wako , halafu ukajikuta umempiga ngwala, mtama au hata kuMKOLIMBA , kabla hauja MSaddam Hussein.

Lakini naamini kuwa....
......baada ya UBONGO WAKO kuamini kitu, tafsiri na wapi unanukuu viushahidi vyako au vikupovyavyo roho kuwa uko upande sahihi, HUATHIRIKA.

Inawezekana umeathiriwa na ELIMU.
Si ndio maana unanukuu vinavyotoka vitabuni ?

Inawezekana umeathiriwa na dini.
Si ndio maana karibu kila jambo utanukuu VITABU vya DINI ,mapenzi au hasira za MUNGU?

Inawezekana umeaathirika na utamaduni fulani.
Si ndio maana kuna mahali unanukuu mpaka wacheza Sindimba matiti nje, pale AIRPORT wakati Raisi wa nchi fulani ya Kiafrika kawasili,kuwa wako uchi na wafanyacho si utamaduni ASILI wa KIAFRIKA, iLA, unaamini pamba itokayo India inatengeneza nguo halisi za Kiafrika?

DUH!

Sehemu unanukuu, inaweza ikawa ni kama ujumbe uupatao kwa kuangalia sanamu.
Sentensi uitoayo kwenye sanamu ,inaweza kutowakilisha kwa mwingine ilichowasilisha kwako.

Swali:
 • Sanamu ni nini?
 • Sanamu huwakilisha nini kwako?
 • Unajua inawezekana kila mtu ANAABUDU sanamu?
 • Mwalimu asimamaye mbele yako darasani, na kuondoka bila wewe kujifunza au kuelewa kitu , hawezi tafsirika kama sanamu liwakilishalo kitu tu chenye jina MWALIMU?
Kuna atakayesema sanamu huwa alifanyi kitu, linawakilisha tu kaujumbe kawakilishwako na sanamu.


Lakini...
...wako watakao kumbuka, sanamu linaweza kukuangukia na kukuvunja nanihii!

Naacha basi kukuzingua!
Usitishike Nawaza tu hapa!

Karibu tena MAWAZONI lakini!

Pata basi TAP DANCE kutoka kwa Savion Glover

Au....

Mcheki tu Maraya Keri katika wimbo Touch my Body kutoka albamu E=mc2

Read more...

MATANGAZO ya WADAU kiduchu!

1.Filamu zinazowania tuzo ya Vinara wa Filamu Tanzania zatajwa!

Filamu zilizoingizwa na watengenezaji wa filamu nchini kuwania tuzo za Vinara wa Filamu Tanzania 2007/2008 2007/2008 (Vinara Film Awards), zimetajwa.

Katika taarifa kutoka mratibu wa One Game Promotion inayoaandaa tuzo hizo, Khadija Khalili, iliyotumwa kwenye vyombo vya habari zaidi ya filamu sabini zinawania tuzo hizo.

Taarifa hiyo ilizitaja filamu hizo kuwa ni Crying Silently (Kilio Moyoni), Kolelo, Mwanahiti, Zawadi ya Fisadi, Oloboni na Layoni, Mmera (Jando) na Nyamaume.

Nyingine ni Sumu ya Moyo, Segito, A Point of no Return I, A Point of no Return II, Dar to Lagos, Cross my Sin na Penina.

Pia zimo Habari Kubwa, Fake Pastor, Chite Ukae, Surprise, Stranger, Fungu la Kukosa, Sea Man, Mzee wa Chabo, Donda Ndugu, I Love You, Miss Bongo I, Miss Bongo II, Revenge, Behind the Scene, na My Wife.

Taarifa hiyo ilizitaja nyingine kuwa ni My Sisters I, My Sisters II, Machozi ya Nyamoma, Silent Killer, My Wife, Greena, Kiapo cha Damu, Valentine, Mwana Pango, Utata, Yolanda, Picnic, Uwanja wa Dhambi, Misukosuko II, Copy, Lugha Gongana, Mtoto wa Mjini, Nyuma ya Pazia, Macho Mekundu, Tanzia, Welcome Back, Karibu Paradiso, Swahiba, The Game of Love I, The Game of Love II na The Game of Love III.

Nyingine ni Mahabati, Security, Itunyama, The Body Guard, Agano la Urithi, Ndani ya Gereza, Simu ya Kifo, My Heart, Malipo ya Kisasi I, Malipo ya Kisasi II, Mpasuko wa Moyo I, Mpasuko wa Moyo II, Kisasi na Diversion of Love.

Taarifa hiyo ilieleza kuwa, majaji watakutana wiki ijayo kuanza kuziangalia tuzo hizo.

Taarifa hiyo ilisema kuwa filamu zinazowania tuzo hizo ni zile zilizokamilika kutengenezwa Januari 2007 mpaka Machi 31, 2008.

Filamu zinazowania tuzo za Vinara

Vipengele vinavyoangaliwa na majaji katika filamu hizo ni Filamu Bora ya Mwaka, Muigizaji Bora wa Mwaka wa Kiume, Muigizaji Bora wa Mwaka wa Kike, Muigizaji Bora Chipukizi wa Mwaka wa Kiume, Muigizaji Bora Chipukizi wa Mwaka wa Kike, Muongozaji Sinema Bora wa Mwaka, Mchekeshaji Bora wa Mwaka, Mwandishi Bora wa Filamu na Mtunzi Bora wa Filamu.

Vingine ni Filamu Bora ya Kutisha, Muigizaji Mwandamizi Bora wa kike (supporting actor), Muigizaji Bora Mwandamizi wa Kike, Adui Bora kwenye Filamu, Wimbo Bora wa Mwaka (Sound Track), Mhariri Bora wa Filamu ambao wote watapata tuzo na zawadi.

Pia itatolewa tuzo ya heshima kwa wale waliotoa mchango wao kukuza sanaa nchini.

Tuzo hizo zinazotarajiwa kutolewa mwishoni mwa mwezi Mei zimedhaminiwa na bia ya Ndovu Special Malt, Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) na Global Publishers.


2.Kwa habari za ujerumani na historia yake tafadhali tembelea

Habari,
Ule wakati tulio usubiria sasa umefika, Website ya pekee itakayo jishughulisha
ktk kuutangaza muziki wa Tanzania ipo jikoni na ina karibia kuiva.

Unataka kusikiliza muziki wa nyumbani? Basi watembelee wajuzi wa fani hii
kupitia www.mkmusicgalaxy.com kwa miziki mipya na ya kizamani uburudike roho
yako.

4.Ushasikia.......
FotoBaraza?


--------------Mwisho wa MATANGAZO---------------------------------------

Kama una muda kidogo, jifunze WAPAGANI wanafikiria nini kutoka kwa MWANABAOLOJIA Richard Dawkins aliyezaliwa NAIROBI , KENYA

Read more...

Kama MWALIMU NYERERE angeanzisha dini kwa WATANZANIA halafu akawa HAYATi!

>> Sunday, April 27, 2008

Naogopa dini!

Dini kiboko!
Inaweza kukusababisha ukashinda njaa kwa ahadi ;utafaidi mbinguni, lakini bila kuwa na uhakika utafaidi nini AHERA , halafu ukashinda njaa.

Dini kiboko!
Inaweza kukusaidia kusamehe jamaa alivyo kunanihii.
Inaweza kukufanya uende vitani kuua kwa chuki ILI kuhakikisha kuwa MUNGU wa UPENDO na AMANI hadharauliwi.

Dini Kiboko!
Ukichacha unaweza ukaokoka ili kubana matumizi halafu ukajikuta umeokoka kikweli.
Hebu tu ANGA lie.... jinsi VOODOOO a.k.a VUDU ikimuingia MWenyEuke mdogo a.k.a.BINTI... ..


Kama wewe MTANZANIA halafu unaangalia mapungufu, utakuwa na uhakika kuwa hata wajifanyao wanafuata nyayo za NYERERE, wanaangalia TV.

Kama wewe unaangalia MAPUNGUFU,Mwalimu Julias KAMBARAGE angeanzisha dini halafu MWENYEZI ALLAH akamchukua, naamini, ungeweza ukajifunza kwanini fikira zake za MUUNGANO wa TANGANYIKA na ZANZIBAR mpaka leo tunajadili kwa kutumia hesabu kama TANZANIA =TANGANYIKA-ZANZIBAR au TANZANIA = TANGANYIKA+ZANZIBAR

Swali:

 • Hivi unakumbuka UJAMAA ni NINI?
Ukiwa MTANZANIA na unakumbuka MwALIMU KAMBARAGE aliyofanikisha, unaweza hata kukumbuka kuwa hujui jirani yako kabila gani na uliwahi kumuomba chumvi , maji, au kumchekea kwa KISWAHILI.

SWALI:
 • Kama kiswahili ni bomba, mbona ukiwa na pesa unataka kumpeleka mwanaTOTO shule ya INGRISH mediumu.
 • Hivi bado kama shule ni bomba walimu wa KIiNGRISH va INDI au wanatoka Uganda eeh?
DUH!
Hebu turudi kwenye ZE Mwalimu Nyerere akianzisha dini au kwenye dini tu....

Twende KENYA kupata DINI fulani kiduchuuu,...
Usije ukawa unaogopa MUNGIKI tu kati ya dini kadhaa milioni fulani lakini!
Kwani dini yako haija KUTISHA kumtamani au kutamani?


Naogopa DINI!

DINI inaweza ikafanya uogope tu au uogope kitu fulani wenzio wafanyacho ingawa kisiri unatamani MWENZIO alivyo BINYA au KUtomasa NYANYA fulani.

Dini nyingine unaweza kutubu lakini!:-)
AU?

Now I am depressed!:-(

Nataka kuanzisha dini lakini!

Hebu tuwasikilize WAKRISTO fulani walioKUWA na uhakika OPRAH WINFEY kaanzisha dini....

DUH!
Naogopa DINI ingawa nikianzisha moja ya dini fulani, unaweza kujikuta unaifuata kutokana na kwamba kuna KILAJI, mboga ya mchicha na NYAMA ya PaKA kwenye jumba la IBADA!:-(

USITISHIKE!
NAWAZA TU!

Hebu tumsikilize tu MANU DIBANGO atukumbushe kengele za kanisa fulani katika wimbo NEW BELL
(Hard Pulsation)

Read more...

USHUJAA wa KUKOPA!

>> Friday, April 25, 2008

Kukopa ni kazi ngumu, kwa sababu mkopo unakuja na kukutengenezea kasifa wengine wawezako kukaweka ndani ya sentensi kama:JAMAA kwa kukopa hata SERIKALI za AFRIKA hazioni ndani.

Kama si mzoefu, kijasho kitakutoka wakati unafanya maandalizi ya kukopa.

Ukizoea kukopa , unaweza kukopa kisirisiri pia au hata unaweza kukopa sehemu za siri za mwenzio.

Lakini....
....kukopa na staili yako ya kukopa , inategemea tu na ulivyoathirika kisaikolojia fulani.

Swali:

 • Hivi unakumbuka serikali ya Marekani a.k.a USA ndio miongoni mwa serikali zinazodaiwa mikopo sana duniani?
 • Unakumbuka inasemekana sasa hivi MAREKANI haiwezi kumkoromea CHINA kwa vitendo kutokana na CHINA kuwa ndio nchi inayoongoza kwa kukopesha Marekani?

Staili yako ya kukopa , hutegemea sana kuathirika kwako kisaikolojia bado kuna kuhakikishia kuwa wewe unacho au huna.

Staili ya fundi viatu nje ya duka kumkopa mwenye duka, inaweza ikawa ya upole na unyenyekevu kuliko staili ya huyo mwenye duka kumkopa fundi viatu nje ya duka lake , ingawa wote wamechacha.

Swali:
 • Unajua unabadilika sauti wakati unakopa?
 • Unajua unabadilika mwendo ukisha katashauri kumfuata umtongoze na lolote liwe a.k.a mwendo wa kumsogelea unayetaka kumkopa?

Lakini...
..inawezekana mkopaji aliye shujaa si yule aliyezoea kukopa.

Kukopa ni kitendo unaweza kukipamba kwa kusema umeazima.
Naweza kukubishia ukisema kuwa hujawahi kukopa halafu ukashindwa kunibishia ingawa kijiweni wewe ndiye usiokosa chumvi watu wakihitaji chai.

DUH!
NAACHA!

Baadaye , kesho , kesho kutwa au siku nyingine Mwenyezi Mungu akipenda iwe hivyo!
Si inasemekana hata nikifa ni mapenzi ya MUNGU?

Nakasikiliza kawimbo haka , kaitwako- To the Ceiling kalikopigwa na ISAAC BLACKMAN. Anza nako WIKIENDI ukipenda.

Read more...

NAKUPENDA!Si nilikupigia SIMU?

Ukimya unatafsiri nyingi.
Kirahisi tu , unaweza kutafsiri ukimya wa mtu kutokana na nini ulishaanza kumfikiria utakaye jibu kutoka kwake.

Unaweza mpaka kupata jibu kutoka kwa uliye jaribu kuwasiliana naye bila mafanikio, kuwa jamaa ananikwepa au ananidharau.

Wajanja husema ukiwasiliana na jamaa atakusikia au hata kukusoma.

Lakini....
...ukisikia au kusoma cha mtu, inawezekana hajawasilisha au ujumbe wake kuhusu jiko , wewe ukaelewa anazungumzia choo kichafu ambacho kina funza funza fulani WANONO.

Lakini....
...funza funza wanono watutiao kinyaa, kichefuchefu au hata hamu ya kutapika, wanaweza wakawa ni watoto wapendwa jichoni kwa mama yao NZI.

DUH!

Ningependa kuchukua nafasi hii kuomba msamaha kwa wote ambao nimeshindwa kuwasiliana nao.Najua ni watu kibao ambao wamekata tamaa nami kutokana na ka-ukimya fulani.

 • Samahani kama sijakupigia simu wala kupokea simu!
 • Samahani sijakujibu ile barua, e-mail wala labda sikugeuka uliponipigia ule mluzi!
Tuko Pamoja na WIKIENDI NJEMA!

Lakini..
.. kabla sijaondoka kabisa kwenye topiki ya kuwasiliana fulani,
nimefurahi kufanikiwa kukutana uso kwa uso na blogger wa Kitanzania ambaye tulikuwa tunajuana mtandaoni bila kuwahi kuonana uso kwa uso a.k.a EDO NDAKI

Pata baadhi ya picha zangu nilizozidaka baada ya kukutana na EDO NDAKI , pamoja na WADAU wengine.
Photobucket
Kwa wasio jua , huyu ndiyo Mzee EDO NDAKI:
Photobucket
Hapa nilijibanza naye.
Photobucket

Photobucket
MKUU wa Kikao a.k.a RAYMOND alikuwepo.

Tulia na HEAVY D akikuambia NUTTIN but LOVE

Read more...

Kuna WATU wakoKimYa lakini wameona na kusikia! UKIWAPA upenyo ,WATAKUULIZA kama USHAWAHI kuugua Ugonjwa wa akili.

Kuna topiki fulani watu hukwepa kuongelea kutokana na topiki ilivyokaa kushoto.

Ukimpa mtu nafasi au kianzio cha sentensi kuhusu topiki asiyo kuwa na uhakika inakuathiri vipi ingawa akilini mwake anaona inauhusiano sana na jambo la kutia aibu , atakuuliza .

Ukimpa nafasi au kumchekea mara baada ya kumpa tabasamu wakati anahamu na wewe, anaweza kupata nguvu ya kukutongoza.


Cha ajabu ni kwamba , asicho kuuliza uso kwa uso anaweza kuwa kasha jadili na wadau wengine mara mia kadhaa na kufikia kwenye uhakika kuwa lile gari lako umelikopa.

Kuteta, umbea au hata kumuongelea mtu kama hayuko kijiweni, ni BOMBA la SANAA kwa atakaye urahisi wa kuhakikishia ubongo wake alichosikia kwenye redio za mbao ni kweli.

Umbea na kutetana ni dalili kwamba unamuda zaidi katika maisha yako ambao huutumii kujishughulikia au kufanikisha yanayo kuhusu wewe binafsi.

Umbeya , kuteta, uzushi au hata kutungia watu vistori visivyo vya ukweli ni bomba la kazi nzuri kama una hobi ya UMBEA.
Si unaona mpaka PEREZ HILTON kawa milionea kwa kuongea umbea na uzushi?


Si umeona Tanzania kuna magazeti mangapi yanayokiri ni ya UDAKU?
Watu hupenda kuwa na taarifa zako ambazo wanahisi hutaki zijulikane.

Swali:

 • Unahisi ni kwanini humuulizi , wakati unataka kujua kama kweli ana mke mdogo pale mtaa fulani au kama bado ana kaudhaifu ka-mapenzi yake ya watoto wa sekondari ya KIFUNGIRO, kama usikiavyo?
 • Unafikiri ni kwa nini huulizi ingawa unataka kujua?
Lakini.....:
...Ukiuliza aliye ulizwa anaweza kuhisi unajua tayari ,kitu ambacho kinaweza kufanya aanze kukukwepa.
....Ukiuliza maana yake umekiri kuwa hujui.
....Ukiuliza inaweza ukawa umetoa mwaliko wa kutaka kudanganywa.

INAWEZEKANA hujauliza kwa sababu hujapewa nafasi, kianzio cha topiki au kuchekewa, USIKONDE!

Unakumbuka lakini jinsi gani mazingira, topiki iliyokuwa hewani ....vilivyochangia ujisikie huru kuulizia au kutongoza?

Unajua mara nyingi ni wewe , mimi au yule tutengenezao mazingira ya kurahisisha mpaka kutukanwa?

DUH!
Inawezekana nimeshakutengenezea mazingira ambayo utataka kuniulizia ambacho nitakwepa kujibu!:-(

Inaruhusiwa kutojibu ingawa kwa mimi kutojibu unaweza kuondoka ukifikiria ni kweli mimi bado bikira.

NAACHA basi!

Nakutakia kila la KHERI katika maisha haya ambayo yanasababisha tutake kujua mpaka visivyo tusaidia kama vile :hivi yule msichana kavaa chupi au kaptura chini ya lile gwaguro.

Tulia na Mu-Itali (ambaye usipomuona unaweza kufikiri mweusi) kwa jina la Alberto D'Ascola A.k.a. AlBorosie


Au pata ujumbe wewe kama MTU MWEUSI kutoka kwa MORGAN HERITAGE wakimkumbusha MTU mweusi hali halisi ya MTU MWEUSI,
katika songi, FALLIN RACE

Read more...

SAMAHANI! Nawakimbia tena wadau wa BLOGU HII kidogo!:-(

>> Tuesday, April 22, 2008

Samahani wadau wa blogu hii!
Nimebanwa kidogo, kwa hiyo , saundi haitoki stirio....

Lakini nafikiri kuanzia Ijumaa hii , pilau inaweza kunukia tena hapa kijiweni kama kawaida.
Au ngojea niseme.....


SASAA endelea kidogo tu na Lagbaja ambaye ndio baada ya FELA Kuti, katika AFRO BEAT, ananisaidia katika SUKUMA TWENDE wiki hiii, angalau katika wimbo FEYIN E.......akisisitiza utabasamu au kucheka hata kama nanihii ngumu:-(




DUH!
Au unaweza kujifunza kucheka au kutabasamu kitu kutoka kwa mchekaji huyu...

Read more...

NAMKUMBUKA MPENZI KINUKA MKOJO!

Hakuna kitu kamili duniani!:-(

Inategemea na engo au kona umuangaliayo au umchunguliayo kipenzi , kama hutaki kugundua huwa anajamba kama wewe na kijambo kingine kinachembechembe.

DUH!

Kinuka mkojo hanuki mwili mzima.
Kuna maeneo kinuka mkojo ananukia kitunguu swaumu.

AU?

Kwa mpenzi Salome!
Nakuonyesha penzi kwa kukununulia mkorogo wakati sipendi wajichubuao.

Kwa mpenzi Zubeda!
Nakuonyesha penzi kwa kukununulia manukato, wakati napata ashki kwa mnuko wako wa kikwapa.

Kwa mpenzi Tanzania nchi ya amani mpaka inafungwa katika MPIRA wa MIGUU na RWANDA na BURUNDI katika kipindi nchi hizo ziko vitani.
Nakupenda kwa kama kawaida ya Watanzania, nazungumzia penzi la bila vitendo vya kuzuia wafisadi hata kama najua siri zao kwa sababu :SI TUNA AMANI?
Kwa mpenzi Tanzania, nchi yenye Mlima Kilimanjaro , lakini watalii watakao kuuona mlima Kilimanjaro bado wanajisikia vizuri wakija kutokea Kenya na wakishuka mlimani, wanarudi Kenya kwa sababu wanauhakika zaidi ndani ya Kenya.

Bado nakupenda kwa dhati ingawa najua sisi wengi Watanzania hatukiri kuwa Makaka na Madada zetu Wakenya, kunakitu wamefudhu au kwa sababu fulani fulani wanafanikiwa kitu ambacho tunaweza kujifunza kutoka kwao kiridhishao wageni a.k.a. watalii.

Usitishike, kila mtu kuna kitu anaweza kujifunza kutoka kwa mwingine!
Ujanja ni kukiri kuna kitu mwenzio anakijua zaidi yako.

AU?

Swali:

 • Kupenda ni nini?
 • Nikisema nakupenda unaridhika kwa sababu umesikia nimesema nakupenda?
 • Kwa mpendwa, je, nikuache kwa sababu wewe ni kinuka mkojo ingawa unanikojolesha?
Kwa mpenzi fulani!
Najua wengi hulalamika, kusema, na nahisi labda hata mimi hufanya hivyo ilikujisikia vizuri kwa sababu sitendi!:-(
Mawazoni , sisi Watanzania nahisi tumelewa kusikia kuwa tuna amani kiasi kwamba kinuka mkojo nahisi hatukinusi.
AU?

DUH!
Naacha wazo hili, nisije nikajifunga bure halafu ukapata cha kunidaka.
Msikilize tu Mmoja wa wanamziki wa AFRO BEAT niwapendao KUBWA kuliko, Lagbaja akikupa kitu ROCK ME GENTLE

Read more...

CHUPI, BAISKELI, BIRINGANYA, ......Majina ya sehemu ZA SIRI,Harage MOJA au PIA neno lisilo BISKUTI.

Naheshimu neno!

Toto la binadamu likizaliwa, baadhi ya maneno ya kwanza kujifunza ,ni neno baba au mama linatamkwaje.

Jitu zima likishakua , baadhi ya maneno ya kwanza kujifunza katika lugha fulani mpya, ni matusi, kutukana au kama halina aibu kama mimi, litajifunza kwanza mpaka majina ya sehemu za siri kwa Kichina.

Lakini....
....inasemekana kuna maneno, kubwa zima halitakiwi lisikike limesema kama linataka kuonekana lina busara au kama linataka kuheshimika.

MANENO ni kitu cha ajabu sana!

Unaweza ukajikuta umeyatumia kumwambia mtu kitu , ingawa unauhakika kumng'ong'a kungefikisha ujumbe!
SI unajua maneno mengine jamii imeamua kuwa ni matusi?


Lakini....
... ukitukana sehemu sehemu fulani , kuna ambao wataamini wewe ni mtoto wa mjini.

Kuonekana mtoto wa mjini ni dawa ya kisaikolojia ya muda kwa mtoto wa mjini, kuhalalisha njia zozote za kufanikisha yale watoto wamjini wafikiriayo ni bomba na ni ujanja bila kuona aibu ingawa inaaibisha.

Ufundi wako wa kutumia neno kutukana, ni moja ya kipimo cha jinsi gani unakumbuka maneno uliyojifunza ukubwani.

Kama wewe ni kubwa zima kama mimi na unakumbuka matusi, basi akili yako inafanya kazi vizuri kukumbuka hata jinsi ya neno liwezalo kutumika kuomba msamaha au hata kuhakikisha lugha yako si chafu kama yangu katika uwasilishaji wako wa ujumbe .


Najua kama wewe unatoka Afrika ya mashariki na lugha yako ni Kiyao , Kikwere au hata Kijita kama mimi, unajua kutukana kwa kingereza.......

......Lakini.....
... ushawahi kumtukana mtu kwa kumkonyeza?

Tokea enzi za mababu, lugha inabadilika, na huzaliwa maneno mapya karibu katika lugha zote duniani karibu kila siku.

Maneno na tafsiri ya maneno ni dalili ya jinsi ilivyokuwa vigumu kwa binadamu kutumia neno kufikisha ujumbe au kujaribu kufikisha kauli.

DUH!
Ningependa kutumia neno kufikisha ujumbe hapa leo!
Lakini mbona hata nikitumia neno sieleweki?

Ningependa kutumia neno kuelimisha hapa leo!
Lakini mbona walioelimika bado hubakia na kutokuelimika kwa kibinadamu kama hatuoni elimu yao kutatua siri ya nini muhimu kwa binadamu?

Swali:

 • Unakumbuka jinsi wanaojua au pia wanasiasa wetu ambao wengine tunawaita MUHESHIMIWA Raisi, watumiavyo neno kuwatusi wananchi kwa kuwaahidi neno ambalo hubakia kuwa ni neno tu bila vitendo?
 • Unakumbuka neno ulilotumia kudanganya kakitu ambako kamesababisha uwe na amani rohoni leo hii kutokana na watu kukaaamini kaneno na kuacha kufuatilia kwa vitendo unafanya nini?
 • Unakumbuka kuwa utamu wa neno, ni uwezo wake wakutumika kudanganya au kusema ukweli?
 • Uongo mwingine si huitwa fiksheni au porojo na huchukii ukisimuliwa?
DUH!

Naheshimu neno na maneno, lakini kumbuka vitendo inasemekana ndio huongea kwa sauti kubwa kama unataka kumpa mimba au kupewa mimba ambayo matunda yake , ndugu jamaa na maadui wataweza kupotezea muda kwa kunyoshea kidole.

Vitendo vingine hata ukiviona , unaweza kujifanya hujaona ili usitamke neno.

Hebu tumuangalie mbwa akifanya kitendo...(samahani kama utatafsiri kitendo cha mbwa huyu kwa neno matusi au PUNYETO!SAMAHANI lakini kwa FIKIRA zako POTOFU au NZURI!)

DUH!

Siku hizi inasemekana wajanja hutumia neno hata kwenye nyimbo, neno ambalo mwingine ataita ni matusi na kudhalilisha mtu au watu hasa wa jinsia fulani.

SWALI:
 • Umestukia kila kizazi hutumia neno kusema kizazi kipya kimepotea kutokana na matumizi na tafsiri ya neno?
 • Umestukia ni miziki ya aina fulani tu ndio ina asilimia kubwa ya wasanii watumiao neno ambalo laweza kutafsiriwa kama tusi?
 • Kwanini?
NAACHA BASI!

NAWAZA TU USIKONDE!

AU?

Msikilize RAY J akikuimbia huuu wimbo ,(samahani ,hatumii lugha nzuri kwa watu fulani!Sishauri usikilize maneno katika wimbo kama wewe ukosensitivu na neno liwezalo kuwa tusi au wewe ni mtoto. Sikiliza kama kwa kawaida wewe si mfuatiliaji wa nyimbo zinasema nini.)...............

Read more...

SIKO KWENYE MUDI YA KUONGELEA TOPIKI fulani.

Unaweza kuongelea jambo kwa kutoongea.

Lakini....
..... nahisi unajua kuwa kwa siku nzima , ni mambo mengi yapitayo kichwani ambayo binadamu wewe na mimi tunachagua kutoongelea au hali halisi inatukosesha bahati ya kumnong'oneza yule fulani.

Lakini...
...binadamu achaguayo kuongelea au ajikutayo kaongelea , inaweza kuwa ni kwa sababu kuna kitu haongelei.

Swali:

 • Unajua unaweza ukawa unanisoma na kuelewa nisichoongelea?
 • Hujawahi kutishika na kile kilichokupitia mawazoni ambacho hujawahi kukiongelea na hautakiongelea?
DUH!

Ambacho unakipenda na ungependa kumuuliza nanihii, wakati mwingine ni vigumu kukiomba kwa sababu hakiongelewi.

Ambacho kwa kawaida hakiongelewi ,ukikiongelea, jamii na wewe mwenyewe hutumia kajicho fulani kukuangalia na kujiangalia kama tafsiri au jibu lake ni chachu au ni: umelizwa kibuyu na chumvi hupati.

DUH, samahani kidogo!
(``Unajua kama umefika mpaka mstari huu, inawezekana unaendelea kusoma nisichoongelea?´´)

Tuendeleee....

Labda...
...kile kitu ufikiriacho naongelea, unaweza kushindwa kuniuliza au kuuliza kwa sababu hakiongelewi!:-(

DUH!

Swali:
 • Unafikiri ni kwanini uliongea ulichoongea leo na kwanini kuna kakitu hujawahi kuongelea ingawa kanakupitia MUKICHWA?
 • Huongelei kipengele kwasababu hujawahi kutukana eeh?
 • Hivi wakati mwingine ukitukana ,huwa unatumia maneno uyatumiayo katika maongezi?



SAMAHANI lakini kwa KUKUZINGUA kama umezinguka kiduchu kwa nisichoongelea , ambacho ungesikia , ungekibatiza kuwa si au ni kitu muhimu!

HIVI kwa mwenye akili, inawezekana akagundua umuhimu wa kuongea ujinga?


NAACHA basi!
Tulia na BOB Marley akikukumbusha maswala ya maisha kama vile UGUMU wa KUBADILIKA ndani ya wimbo STIFF NECKED FOOLS

Au turudi tu BONGO nakukutana na big 4 the GZ ft NgwearBIG 4 the GZ wakiwa na NGWAIR wakikusimulia maswala ambayo yako katika maisha na ambayo kwa watu fulani huweza kuita ni muhimu na ukashindwa kuwabishia kama vile maswala haya wayaimbayo ya PATI FULANI

Read more...

NANI kawaambia WATANZANIA kuwa WANAISHI ndani YA nyumba YA KIOO?

>> Friday, April 18, 2008

Kama unaishi ndani ya nyumba ya kioo, usirushe mawe.

Inasemekana TANZANIA hakuna arushaye jiwe kutokana na kuogopa kuvunja kioo.


Topiki INAENDELEA.............

Nimebanwa kidogo.........

Tutaonana tena JUMANNE ijayo hapa kijiweni, kama sijafa au kama naweza na inawezekana.....!

WIKIENDI NJEMA!

WAZIRI wa UTAmaduni wa Brazil- Gilberto Gil na TribeCalledQuest walitawala wiki yangu hii , masikioni.

Endelea nao kidogo kama unakaudhaifu na mimi kiduchu:-)

AU?

Tuanze na Gil akikupa Aquele Abraço na BACK in BAHIA




Halafu Akikupa TIME WILLTELL...



Malizia na TRIBE CALLED QUEST wakikuambia JAZZ(we've GOT)



KATAARIFA kaduchu:

J
UMANNE imefika....
Lakini ashki ya topiki hii imenitoka kidogo.:-(
Nitaendelea nayo siku nyingine.

Read more...

NDOTO nzuri, INAWEZA kumchafulia SHUKA mvulana!

>> Thursday, April 17, 2008

Nami hushiriki katika kushawishi watu waote vitu vikubwa na kuvifanyiakazi vitimie.

Lakini....
.....Ndoto zangu zote zingetimia, ningekuwa bilionea , halafu ningeshakufa miaka kadhaa kabla sijabalehe , kwa sababu ndoto nyingine huitwa majinamizi au kwa kiswahili kingine kigumu, huitwa NDOTO MBAYA:

Watu hutukania kulala, ingawa kwa mwaka inawezekana ukawa umetumia miezi sita kulala.
Waliozubaa katika kugombania ubwabwa wa maisha, huambiwa au kutukaniwa kuwa wana ubongo uliolala.

Kulala bomba, kama hupati majinamizi!

Ukilala vizuri , ni rahisi kufanikisha majambo kutokana na utulivu wa akili yako na uwezo wako wakukabili jambo baadaye kama utafanikiwa kuamka. Kulala , si kuna watu wanadai ni nusu ya kifo?

Lakini...
..... nahisi wengine tunalala vizuri au vibaya na kupitiliza kulala mpaka yale maamuzi mazuri tunachelewa kuanza kuyafanyiakazi .

Nafikiri wengine tunalala zaidi , ndio maana ndugu , jamaa na hausigeli wa nyumba ya jirani, wanajiuliza:

 • Mbona hatuoni jamaa afanyalo?
 • Mbona hatuoni hata baiskeli ya swala au ile mashine ya kukoboa pale sehemu sehemu?

Lakini.....

Martin Luther King Jr alisimulia ndoto yake na pia alitabiri kuwa atafariki kabla ya kuona ndoto yake ikitimilika.

Lakini....
...... ndoto yake inatimilika!
Si unaona mpaka Barrack Obama anagombea Urais katika nchi ambayo watu weusi walikuwa wananunuliwa kama KIFUNGU cha EMBENG'ONG'O miaka michache iliyopita?

Nisikufiche sijui sana maswala ya kulala wala ya NDOTO!

Si unajua tena wakati nimelala huwa nakua nimelala, na sifanyii kauchunguzi spidi ya udenda utokavyo mdomoni wakati nimelala ni kilomita ngapi kwa saa kabla haujagonga mto.

Lakini nasikia......
...inasemekana, ukilala kikawaida, unatumia angalau masaa mawili kila siku kuota.

Kumbuka pia , inasemekana kuwa ukilala , kwa wanaume sehemu za uume huweza kusimama na wenyeuke kinukta huweza kuvimba kiaina pia!

DUH!
Nakiri kuacha kuongelea swala nisilolielewa vizuri!

Nacho jua tu ni kwamba!

Ndoto hutimia hata kama ndoto nyingine zitatimia dakika kadhaa tu baada ya mimi na wewe kufa, kufariki au hata kukata roho.

Kama sisi si wachoyo.....
 • Tutimize tu, zile ndoto za kupanda miti ambayo tunauhakika itachukua miaka mia kukua, lakini ikikua itakuwa msaada kwa kizazi kijacho.

 • Tusisite tu ,kufanyia kazi zile ndoto za kupigania haki ya masikini kusikilizwa na serikali yao na matakwa yao kufanyiwa kazi mpaka umasikini uwe ni jina limaanishalo:umasikini ni ile hali ya mtu kujilimbikizia maswala asiyoyahitaji.

 • Tusisite kujaribu kufanyia kazi ile ndoto binafsi ya kuwa na maisha uyatakayo binafsi hata kama ni vigumu kueleweka jichoni mwa ndugu , jamaa, jamii au hata mchumba.

Swali:
 • Unakumbuka uliota nini jana?
 • Hivi masikini na matajiri huota ndoto tofauti?
 • Wanawake na wanaume je?

Ni kweli si ndoto zote nazikumbuka kama nikumbukavyo msosi baadaye kidogo baada ya kuamka..

DUH!

Naacha!
Inawezekana naota tu!
Si unajua tena?

AU?

NAKUTAKIA kila la kheri katika kufanyia kazi ndoto zako!
SIKU NJEMA!
Tulia na WAZIRI wa UTAMADUNI wa BRAZIL , Gilberto GIL
akija na kibao Imagine


Au Mpate tu katika kibao Aquele Abraço


Read more...

WANAWAKE huoga TOFAUTI kwa sababu wana MAtiti. AU?

Wanawake na wanaume ndio binadamu awaonao kila siku ya MUNGU ibadilikayo.
Binadamu anaweza akajisahau kuwa kuna maeneo yamuathiriyo binadamu mwenye uume na mwenye uke ambayo hayajabadilika sana kimawazo hata ki.....ndani ya asilimia kubwa ya idadi ya binadamu waishio katika duniani hii ibadilikayo.


NI RAHISI kusahau kuwa , bado katika dunia hii , haki za wanawake na watoto hazina kipaumbele sana machoni mwa wanaume na hata wanawake pia. Watoto sitawazungumzia sana hapa sana leo hii, ingawa naamini kuna wanawake ambao wamefikia kuamini kuwa wanaume wafikiriavyo na watakavyo, ndivyo watakiwavyo kufanya, kufanyiwa au hata kuonekana.

Wanaume wametawala maeneo mengi hapa duniani mpaka unaweza kusahau kwa nini bado ni watoto wakiume wanaopendelewa kielimu na kikuwezeshwa kujitegemea kuliko watoto wadada.

Watu husahau kuwa katika dunia hii, asilimia kubwa ya watu wako katika nchi masikini na asilimia kubwa ya watu bado wanaamini mafanikio katika watoto wa kiume na si katika watoto wa kike.

DONDOO:(Pamoja na wachina kusifiwa wana akili sana, NAFIKIRI unakumbuka wamefanikiwa kupendelea watoto wa kiume, na kuwa na watoto wa kiume mpaka wanaanza kuishiwa wanawake wa kuoa au kumimbisha hivi sasa.)

Sasaa......

Dunia inabadilika kila siku, na binadamu inabidi abadilike kukabiliana na mabadiliko kama anataka kuhakikisha kizazi chake kuendelea kuwepo hapa duniani.

Ushirikiano wa mwanakaka na mwanadada katika kufanikisha mridhiko wa maisha haya mafupi binadamu aishiyo, unahitajika sana, hasa kama nia ni kujaribu kuishi haya maisha kwa mafanikio na furaha.

Mafanikio ya binadamu hapa duniani , hutafsiriwa na mtu mwenyewe kutokana na jinsi alivyo athiriwa kimawazo na mambo mengi yamzungukayo tokea azaliwe , kuanzia aonje chuchu, apate au akose elimu , mpaka mara yake ya mwisho kupumua.
SAMAHANI KIDOGO........!

Swali:

 • Hivi maisha ya mafanikio ni lazima yawe ya furaha?
 • Hivi kujua kutokanako na elimu hakusababishi kumkosesha tu raha binadamu ambaye asingejua , asingetaka?
 • Unataka kujua una UKIMWI?
 • Hivi unataka mto wa kike au wakiume ukimimbisha au ukimimbishwa leo usiku?
DUH!

Cha ajabu ni KWAMBA, mafanikio ya binadamu JAMIII iyazungumziayo, ni mafanikio YATAFSIRIWAYO na jamiii kuwa NI MAFANIKIO .

JAMII itasifia na hata vitabu kuandika kuhusu yale JAMII itambuayo kuwa ni MAFANIKIO hata kama HAYO mafanikio huweza kuwa si MAFANIKIO kwa muhusika binafsi..

Swali:
 • Unafikiri maisha ya Rais NELSON MANDELA, ya kuachika mara mbili na watoto kukua bila baba, kwa mtazamo wa jamii ni mafanikio?
 • Unafikiri maisha ya MANDELA ya kutaka haki kwa kila mtu bila kuipendelea familia yake binafsi, JAMII kwa ujumla inatambua kuwa ni MAFANIKIO?

DUH!

WAKATI UNAMCHUNGULIA BINADAMU AKIOGA, kuna maeneo unayatolea macho kutokana kuvutiwa kwako wewe binafsi au kwa sababu yalikaa tu karibu na tundu la mchungulio.

Nakiri kuwa lazima utagundua zile tofauti uzionazo mbele yako na labda wakati huo huo , hautakuwa unafikiria au kujali binadamu umchunguliaye anawaza nini tofauti na wewe zaidi ya kugundua nini alicho nacho kilicho tofauti na wewe.

Kwa wanawake na wavulana , karibu kila mtu anakakitu kake ukitokea tu ,kanamsitua kuwa huyu jamaa mvuto wake divisheni ziro: lakini kwanini wengine wanampasisha mtihani?

Kwa wanaume pale kijiweni, kuna atakaye kuambia kuwa yeye ni mtu wa matako, macho , miguu , nywele au hata yule ambaye atasifiwa kwa busara zake na jamii, kwa sababu anasema anapenda tabia ya yule ampendaye kuliko yale macho ya gololi na mashavu ya kumimina.


Nahisi kwa wanawake pia unaweza kusikia kuwa anampenda jamaa kwa sababu anabomba la matege, ana macho kama bundi au hata kwa sababu ana kifua kama simba: si umecheki siksi paki zile?

Swali:
 • Unafanya nini kusaidia kuleta usawa wa haki za wanawake na wanaume?
 • Umejichubua kwa sababu unafikiri wanaume wanapenda au unakubali kuchunwa buzi kwa sababu wanawake kazi yao ni kupendeza na kukupikia chakula kabla ya kukupa kifuko cha dhambarau ukitoka kazini / kabla ya kulala?

DUH!

 • Naelewa mafanikio yako yanaweza yakawa ni kujinyima hapa duniani kwa sababu unafikiri utafaidi mbinguni ukishafariki.

 • Naheshimu kuwa wewe mwanamke ndio kungwi na mama ambaye unampeleka binti yako kutairiwa kinjegere, ili jamii ikukubali na wewe mwenyewe ufikie kukubali kuwa UMEFANIKIWA, kwa sababu umefikia katika uzani wa MAFANIKIO katika jicho la JAMII na umefikia JAMII itakavyo.

 • Nakubaliana na wewe pia kuwa umejichubua iliupendeze na unapendeza katika jicho lako na jicho la yule.

 • Nakubali kuwa , ukiniona sichani nywele , unafikiria kuwa nywele zangu chafu lakini ukisuka twende kilioni na kukaanazo wiki kadhaa bila kuziosha, wewe bado msafi.
NDIO!

Nakubali kuna wanawake na wanaume , wasenge na wasagwaji pia!
Nakubali hakuna binadamu wawili sawa!

Lakini.....

HUFIKIRII kuwa mimi , wewe, yule na yeye ambao tukotofauti , tunaweza tukawa katika ahueni zaidi kama WANAWAKE watapata nafasi sawa na wanaume katika dunia hii ya leo ya sayansi na tekinolojia ambayo haihitaji sana misuli kama enzi za ujima?

Hufikirii kuwa , ni mimi na wewe ambao tunachangia kutokuwepo kwa usawa wa binadamu wote kutendewa ubinadamu sawasawa bila kujali ni wanawake au wanaume?


Inawezekana unavyowaza ni sawasawa tu!
Si kuna MALIPO MBINGUNI?

Inawezekana unavyowaza ni sawasawa tu!
Si mwanamume ni kichwa cha familia halafu ana misuli uenye nguvu zaidi ya mwenye uke?

Inawezekana unavyofikiria ni sawa!
Kwani ni nani anataka au kuhitaji dume jike katika shughuli?

AU?

USITISHIKE!
Nawaza tu kibulicheka!

Hebu tuangalie jinsi wanawake na wanaume waogavyotofauti , kama maji yakitoka pale DAR-es-SALAAM, MOROGORO au pale SAME, MBAGA , Manka, KILIMANJARO kwa bibi, kama kuna bafu fulani.....


DUH!
Ngojea tu ni waachie Elana na KC wa Read My Hips dance troupe ,wazungumze kwa kutumia mwili....


BAADAYE BASI!

Read more...

LABDA hutaki kuona MAJINI,MIZIMU, NDONDOCHA au hata KIDONDANDUGU!

>> Tuesday, April 15, 2008

SWALI:

 • Unataka kuona au KUTOSIKIA nini LEO?
Inawezekana tunalazimika kuona yatuzungukayo kwa sababu yametuzunguka.

Lakini...
....mwingine anaweza akawa na uhakika kuwa tunaona na kusikia mambo fulani kwa sababu tunawekea umuhimu mambo hayo au hata kuyatafuta kwa kutumia, jicho sikio au hata akili.

Inawezekana hata tukawa tunachagua jinsi ya kuona au kusikia jambo , ndio maana muziki mzuri kwangu , kwako makelele , na kitu kizuri kwangu, kwako kina sura mbaya na kinanuka kikwapa.

DUH!

Kutokana na utafiti mbalimbali, watu huona mpaka mizimu , majini au hata ndondocha kwa sababu tu walishaambiwa kuwa katika makaburi hayo, saa sita usiku , kuna jini na mizimu inacheza sindimba.

Hebu angalia hiki kideo uone jinsi kirahisi unavyoweza kutoona kitu mbele yako kama hutafuti kukiona....

Kisayansi pia wanadai kuwa sehemu iliyo na cabon monoxide nyingi, nguvu za elektro magneti kubwa, zinaweza kuingiliana na ufanyaji kazi wa ubongo, na kukukusababisha uanze kuhalusineti au kuona vitu ambavyo havipo.

Lakini....
.....kikubwa kikufanyacho uone au kusikia kile kitu, ukiondoa kuwa unataka kukiona au kusikia kutokana na yaliyojengeka akilini mwako tokea uzaliwe mpaka sekunde hii ya kukipigia chabo, ni kwa sababu jamaa washakuambia ukifika Makambako, usile nyama, kwa sababu zinaweza kuwa ni za kunguru.

Hebu cheki kideo hiki pia....


Unafikiri bila kusimuliwa kwenye kideo kuna nini, ungeona MBILIKIMO au WATOTO wanacheza MPIRA wa MIGUU?

Lakini....
...inawezekana unaona au kusikia pia vitu ambavyo vinaonekana na kusikika kutokana na kuwa vinaonekana na kusikika.

AU?

SIKU NJEMA!

Read more...

OMBI MAALUMU kwa WACHAWI!

Kabla sijaendelea.......
....tulia na picha hii ya mjamaa akipata NYAMA choma.....






Usitishike!
Inawezekana watu hawali watu.
Inawezekana picha hii si ya kweli.
Nimeitoa hapa









ILA...
...Ombi maalumu kwa WACHAWI!

Mchawi yeyote mzoefu , naomba dondoo za nini kinaendelea katika fani yako .
Unaweza kuanzisha blogu ya wachawi bila kujitambulisha au kutoa komentsi kama ma- anonymous watoavyo wakati wakitukana.

NINGEPENDA kukukumbusha kuwa FANI yako ya uchawi, ni miongoni mwa fani ambazo zina wataalamu wachache sana, ukilinganisha na idadi ya watu waathirikao na UCHAWI ,kifikira au hata kiimani na utendaji.

FANI yako ,inaathiri sana mamilioni ya watu katika nchi masikini, HASA KUTOKANA na usiriusiri wake .

JARIBU kusaidia kuelimisha watu KUHUSU FANI yako, ili yale yawatishayo ambayo ni danganya toto yajulikane.

ASANTE sana !

DUH!

Usitishike!
Lakini sitaniii hapa!

Unaweza kujitoa katika wazo la wachawi kwa kutulia na Kizomba. Mpate basi....

Read more...

KABLA HUJAWEKA MAUA KABURINI KWA UMFAHAMUYE.

>> Monday, April 14, 2008

Tunakutana, kuzozana, kupendana au hata kupigana, lakini wakati kila mmoja akianza kivyake, hatuchukulii kuwa ndio inaweza kuwa mara ya mwisho kuonana.

Hakuna ajuaye nini kitatokea sekunde ijayo, ila tunazungumzia kesho tutafanya nini.

Hakuna awezaye yote, lakini, kila siku tunategemewa kufanya yote.

Hakuna azikwaye na mali zake, lakini hatuachi ubahiri na kujilimbikizia.

Tunajua hakuna ajuaye yote, lakini hatuachi kumdharau asiyejua au aitwaye mjinga.

Swali:

 • Ushamwambia unayempenda kuwa unampenda ?
 • Ushamsamehe unayemchukia?
 • Unasubiri useme marehemu alikuwa mtu mzuri?


Lakini....
 • Hivi marehemu lazima asamehewe?
 • Kujilazimisha kumsamehe mtu hata kama moyo hautaki, imo?

DUH!

USITISHIKE!

Niko mawazoni tu!

JUMATATU NJEMA!
Msikilize kidogo Nina Simone akikuambia IF U KNEW

Read more...

USHAWAHI kumtazama KWA MAKINI binadamu akikimbiza MWENGE?

>> Sunday, April 13, 2008

Binadamu hupenda kuoanisha kitu na jambo.
Ndio maana binadamu anajioanisha mpaka yeye na jina lake.

Labda ndio maana anaitika ukimuita lile jina!

DUH!

Kuna vitu kibao binadamu anavioanisha na kakitu fulani.
Ukimchorea mistari miwili kinamna, atakuambia, huo ni msalaba, halafu atadai unamkumbusha Ukristo au hata YESU.

Ukimchorea kinusu mduara na mbwembwe fulani , atakuambia umemkumbusha MWEZI au hata UISLAMU.

Ukamuonyesha sanamu fulani, anaweza akakuambia huyo ni Rais Nyerere , yule rais bomba sana au hata akakuambia huyo ni BIKIRA Maria, ingawa anajua kuwa, hakuna aliyewahi kumchora au hata kumpiga picha Bikira Maria au yule mwanaye ajulikanaye kwa jina maarufu kama YESU, wakati wako hai .

Sasaaa.....!
Hivi vitu viwakilishavyo majambo muhimu kwa binadamu, labda ni vizuri sisi binadamu kuwa navyo na kuvishabikia.

Labda vinaleta mwamko wa maendeleo, vinatusababisha tujisikie tuko karibu na Mwenyezi Mungu, tuko karibu kama binadamu na binadamu au hata kujitambua kuwa sisi kabila letu ni Wagogo.

Sasaaaa........!

Narudia swali:

 • Ushawahi kumtazama KWA MAKINI binadamu akimbizaye MWENGE?
 • Unafikiri binadamu wakati anakimbiza mwenge, akilini mwake anafikiria nini?
 • Ushajistukia unaweza ukapigwa butwaa ukiona Mdau anakojolea kaburi?
Mtu na kielelezo chake , hataki mchezo!

Naweza kumshangaa Muiraki alivyokuwa anapiga sanamu la Saddam Husein kama vile linasikia maumivu , wakati mimi mwenyewe nakubali, naweza kukasirika nikisikia jamaa wanakojolea sanamu ya Rais wetu mtukufu JAKAYA KIKWETE.

Sasaa.....

MWENGE wa OLIMPIKI , au hata ule MWENGE mwingine , twendeni tu tukaukimbize!

Lakini......, wakati naukimbiza MWENGE, naruhusiwa kuwaza ;` sijui watatulipa kweli baada ya mbio hizi?´ au `Nasikia baadaye kuna bomba la ubwabwa kwa wakimbizao mwenge´, na si lazima niwaze kuwa ni kweli tunahitaji umoja katika DUNIA hii.

Lakini....., wakati tunaukimbiza ule mwenge, tujiulize:

 • Tofauti ya mwenge na kibatari pale nyumbani kwa bibi ,ni nini?
 • Ushawahi kutupa,kuchoma au hata kuchambia gazeti lenye picha ya Mheshimiwa ,Mtukufu au Hata PAPA Mtakatifu?
DUH!
JUMAPILI NJEMA!
Tulia na PM DAWN

Read more...

Maswala ya ,`HUYU demu asingekuwa AMEOLEWA, ningemtongoza!´

DONDOO:

 • Hapa siongelei swala lililo karibu na swala kama la Raisi Mandela kumuoa mke wa rafiki yake Samora , baada ya Rais huyo wa Mozambiki kufariki.
Inawezekana kabisa ukinyimwa ,ukataka zaidi!
Inawezekana kabisa unataka na kinakufikirisha kwa sababu huna!
Vile viatu ambavyo ushavisahau chini ya kitanda, inawezekana mwenzako anavitamani leo hii katika duka fulani.

DUH!

Unaambiwa, MAJANI huonekana yakijani zaidi kwenye bustani ya mwenzio.
Ulichonacho , inawezekana umekizoea mpaka hustukii ni jinsi gani kilivyo kikali.

Ukionacho mtaani , na haswa kile ambacho hukijui, kina weza kikawa kinakuvutia sana tu.
Ukweli ni kwamba ukitamanicho chaweza kukukinaisha hata kabla hujavuka dakika tano yakuwa nacho.

Cha mwenzako ambacho unauhakika huwezi kukipata kinabakia kama kipimo cha yale ambayo akilini mwako umependa kuyakubali kuwa ndio ukweli ukizungukacho hicho kitu ulicho amua kukiita kitu kizuri.

Naamini si kitu kibaya kutamani cha mwenzio kama kinakusababisha upige hatua fulani mbele , katika kujijua au hata katika kukufanya ujitume kufanya mambo vizuri zaidi ilikufikia mwenzako alipo.

Tatizo ni pale tu kama tamaa ya yale usiyonayo yatakujenga chuki kwa yule ufikiriaye anacho kukuzidi.

Swali:
 • Unauhakika ulichonacho si kizuri kuliko cha mwenzio ikiwa kinakutosheleza?



DUH NAACHA na moja kwa moja natoka nje ya TOPIKI!

Huu wimbo hapa chini ni kwa wale (hasa Marasta) wasionielewa nikisema mimi si Rasta , hasa kutokana na ukweli sichani Nywele (kama ionekanavyo pichani) , hata baada yakujieleza mara kedekede kwanini mimi si RASTA.
Photobucket

Tulieni basi na hawa MARASTA wanaojulikana zaidi katika PUNK ROCK kutokea miaka ya sabini, ambao wale MARASTA waaminio kuwa urasta unaendana na ROOTS REGGAE pekee, wanakwazika hata kwa kuwasikiliza.Wapate basi BAD BRAINS

DUH!
Usitishike!
Niko na ERIC BIBB (niliyenaye pichani) ....masikioni.
Photobucket
Tulia naye basi!

Kwa mara nyingine , ASANTENI MARAFIKI wote popote mlipo kwa yote!

Nawatakia kila la heri katika harakati za kuishi!

Asanteni pia marafiki ambao tumebahati kukutana hivi karibuni !

Mungu akipenda tutakutana tena!
Baadhi mnaweza kujistukia katika picha zangu hizi katika filmloop....

Tuko pamoja na BAADAYE basi!

Read more...

USHAWAHI kuiona au KUPIGA PICHA ya MUNGU?

>> Friday, April 11, 2008

Swali:

 • Mungu wako wa upendo , anaweza kuwahurumia wale ambao kwa uwezo wao dhaifu wa kibinadamu wamefanikiwa kufa bila kumstukia au kumuelewa na kumfuata?
 • Hivi Mungu wa mwenzio ni wa uongo eeh?


Ukiongelea maswala yahusuyo Mungu, kama unaimani fulani, utaamini kuwa Mungu haonekani.

Ukiongelea maswala ya Mungu, ni rahisi watu kuhisi unakufuru au unacheza mpakani na kupitiliza.

Lakini, ukimuongelea Mungu kinamna sikio la fulani linaamini kuwa ni Mungu atakiwavyo kuongelewa, huyo mtu fulani anaweza akawa mfuasi wako kama umenuia kuwania kuwa msikilizwaji katika maswala ya imani.

Binadamu karibu katika jamii zote duniani, huamini kuwa kuna kitu, vitu au........ ambayo ina/zina/..ana nguvu na uwezo kuliko binadamu yoyote yule.

Mara nyingi huyu/hiki/....huogopwa ,ingawa wengi huamini katika msaada wake kwa binadamu.

Swali:
 • Kwa nini hata yule Mungu wa upendo, anaogopwa?
Ukweli ni kwamba, wako watu wengi ambao utake usitake, wanamuona, kumpiga picha au hata kumchora Mungu wao.

Kuna werevu fulani ambao tunawasifia siku kibao kwa jinsi watumiavyo akili zao na kufanikisha mambo kibao ambao wanaweza kukufanya ushangae wakikuonyesha au kukusimulia kuhusu Mungu wao.

Nafikiri kwa kifupi unaweza kuwakumbuka Wamisri waliotuachia mpaka Mapiramidi jinsi walivyo kuwa wanamuabudu Farao wao kama yule Ramesses II

Nafikiri unaweza kukumbuka Wajapani wakati wanatawala Asia karibu yote , namaanisha mpaka China, walikuwa na Mungu Mfalme, kama vile huyu Emperor Shōwa aka Hirohito.

Au unaweza kumkumbuka yule mtoto aliyezaliwa juzi juzi India aka LALI ambaye anasura mbili asujudiwaye kama Mungu na watu ambao itakuwa vigumu kuwaita wajinga.

Hebu tujikumbushe baadhi ya Picha fulani ambazo zinaweza kukupa baadhi ya......:

 • Mtoto aitwaye Lali ambaye kashaanza kuabudiwa





Picha kwa hisani ya AP









 • Mungu Farao RamessesII




Picha kwa hisani ya Hajor







 • Yesu



Picha kwa hisani ya Google images







 • Mungu Jua


Picha kwa hisa ya Tinka Sloss







 • Mungu Mfalme Hirohito










Picha kwa hisani ya Google images







 • Hapa weka picha ya Msichana fulani aabudiwaye ( Unaweza kufuatilia hata mitaa ya Nepal kama humuabudu msichana fulani wewe)

 • Hapa weka picha ya mvulana fulani....
 • Unaukumbuka ule mbuyu fulani ambao unatambikiwa?


Picha kwa hisani ya ULI SEIT






DUH Naacha basi hii topiki!
Unajua niko mawazoni tu lakini!

Usitishike wala kuchukia, fikiria tu!

AU?

IJUMAA NJEMA!

Samahani kwa ambao nimewakwaza au kuwapa vibes za kufuru!

Msisahau kuniombea kwa Mwenyezi MUNGU wenu!



Pata wimbo wa Injili kutoka kwa Bob Marley!

Read more...

TANGAZO kwa WADAU walioko HELSINKI !

UNAKARIBISHWA katika ile PATI YA WAAFRIKA yaKILA mwezi
ndani ya HELSINKI.

Tarehe: 12.4.08

Saa: 21:00 mpaka 04.00

Mahali:Ravintola Kaisaniemi

Anuani ya sehemusehemu: Kaisaniementie 6

Kiingilio: 5 Euro

Kutunziwa Jacket: 2 Euro

DJS: EDDO the MAN akiwa na ALIKO aka Altunes














Karibu
Mmoja !Karibu Wote!
Kwa habari zaidi nenda
: www.africannight.org

DUH!
Haka kawimbo kamtajako mende aka Kaka ROACH (Kakaroach in meh petty coat), kamenikaa kweli kichwani mwangu leo....


Naona nimemzidisha LORD KITCH !

DUH!

Usisahau kuwa pati hii mpaka Msondo Ngoma ni mbele kwa mbele.
Basi tulia na mwanadada nimzimiaye aka Lady Jaydee akikuambia USIUSEME MOYO

Read more...

PAKA SHUME WEE!Lione lilivyo!

>> Thursday, April 10, 2008

Swala la wewe ni nani ni refu.
Watu tuna majina ili kurahisisha baadhi ya maeneo yajaribuyo kujibu wewe ni nani.

Wewe ni nani, lawezakujibiwa kuwa wewe ni,

 • Msichana au mvulana
 • dume au jibaba
 • Alufani au Zubeda
 • Kibaka au Msenge
 • Mlokole au Mpagani
 • Kichaa au Umezidiwa na akili ndio maana hatukuelewi.
 • Au hata......nk kadhaa fulani!
.....na yote yakawa yamelenga kunako kuhusu wewe ni nani.

DUH!

Wewe ni nani, ni swala binafsi na la jamiii pia.

Ndio maana ukimtukana SIMON KITURURU;`` embe DODO wee!´´, anaweza akakasirika kwa sababau unacheza na jinsi afikiriavyo jamii inamtambua.

Kuna maeneo ya SIRI na ya SWALA BINAFSI, ambayo jamii inaweza kutotambua, wakati wewe mwenyewe ukiwa kwenye kioo au pale bafuni unayakagua na kujaribu kufikiria ni jinsi gani ungekuwa bomba au umeula, kama usingekuwa hivyo ulivyo.

Sasa ukija kunitukana ; ``Muangalie SIMON KITURURU , meno KAMA NGIRI!´´,wakati pale chooni wakati najiangalia kiooni, nilikuwa sina uhakika na muonekano wa meno yangu, tusi lako lazima litanigusa kunako , kuliko kama sina udhaifu na kamuonekano kangu.

DUH!

Swala binafsi noma!

Unaweza mpaka kujishuku kuwa hapa nakuandika wewe kumbe hata sijawahi kustukia kuwa titi lako moja dogo kuliko jingine au hata.......

Swala la `` Paka shume wee!´´, ukilifikiria, huwezi kukasirika hata kama litageuka herufi na kutamkika ; MBWA WEE!Sana sana litakuchekesha!

Fikiria swala la wewe ni nani!

Inawezekana mimi naandika hapa bloguni kwa sababu binafsi , kama vilevile wewe usomaye nachoandika , usomavyo kwa sababu zako binafsi

Basi bwana!
Nakubaliana
nawe kuwa, mimi mwenyewe niko safari moja nawe , ya kujaribu kujua mimi ni nani.

DUH!

Swala binafsi ni binafsi na tumuachie mtu binafsi!

Swali:
 • Wewe ni nani?
Siku njema!

Lakini kama unanafasi unaweza kutulia bado na Soca Chutney kama iletwavyo na Shurwayne Winchester -akikuambia Don't Stop

Read more...

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP