Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

BINADAMU WOTE si sawaSAWA au NANI kakuhakikishia NI SAWA?

>> Thursday, April 10, 2008

Kuna mambo ni vigumu kukiri waziwazi maeneo fulani, kwa sababu za kidini, kisiasa(kuwa politically correct), kiungwana na hata kwa sababu unaweza ukaharibu ulaji pale.........


Kwa waungwana , sentensi kama binadamu wote ni sawa lakini si sawasawa inaweza kunoga masikioni kuliko kukubali BINADAMU WOTE SI SAWA.

Unaweza kubisha!

Lakini .....
.......katikati ya binadamu pamoja na usawa wote tuuteteao, kuna;

  • Wenye nguvu na wanyonge
  • Wenye koneksheni na ambao hawajui liendealo
  • Wasomi waliofanikiwa kupata vyeti na wale wasomi walioelimika
  • Wazuri machoni mwako na wale ambao unajaribu kukiri umewapendea tabia
  • Weusi na wale wengine waitwao weupe
  • Wanawake na wanaume
  • Pia wale........na ...........
....kitu ambacho ukichanganya , utastukia kuwa ni vigumu kukwepa kahisia kuwa hakuna usawa.

Swali:
  • Hivi wanawake na wanaume ni sawa au sawasawa?
  • Wakati unapigania usawa au sawasawa unauhakika wewe huchangii kuongeza si usawa au sawasawa hapo nyumbani kwako?
  • Unabisha kuwa kuna maeneo wasichana na wenye uume waitwao wazuri kufanikiwa kirahisi zaidi ya wenzangu na mimi?
Naamini kunatatizo la watu ambao ndani ya roho , moyo mpaka akilini mwao, hawaamini katika usawa ingawa waweza kuwakuta ndio wakomstari wa mbele katika kuonyesha jamii kuwa wao ni wapigania haki za wote na za usawa.

Vita vya kugombea usawa ambao unagusa maeneo yale tu yakufaidishayo na kusahau kuwa hata ndani ya nyumba yako kuna nanihiii na........pia mpaka yule hausigeli/hausiboi ambaye hasikilizwi hata mpaka na wewe , ni vigumu kushinda.

Lakini.....
......vita vya kugombea usawa vinatoa ajira zake.

  • Unaweza ukajikuta umeanzisha NGO fulani ikulipayo mshahara!


  • Vita vya kugombea usawa vinakuza status yako sehemu fulani kitu ambacho kitakufanya wewe uonekane si sawa na wengine.
Ukweli ni kwamba;

BINADAMU wengi hawapendi kuwa sawa na wewe.

Watapenda kuwa na uhusiano na wewe kama tu uhusiano wao na wewe unawasaidia kitu fulani(hata kama msaada ni jinsi wajisikiavyo vizuri wakati wana kusaidia)
Watakuzimia kama unafanya kakitu wakazimiako, ingawa kama ingeliwezekana , wangependa wawe katika viatu vyako na wewe ndio uwe unawazimia wao.
Usitishike lakini!
Nakubali kuwa kuna starehe pia katika shughuli ya kumzimia mtu fulani au hata NYERERE.

Unaweza kubisha!

Katika jamii , ukiangukia katika wale wakubalikao, waweza kustukia hata mambo yako yanakubalika kirahisi.

Watu watahakikisha wanatafuta sababu kuwa kwanini wewe na wao mnamahusiano kama inalipa na haiaibishi.

Swali:
  • Hivi kwani , BARRACK OBAMA , COLIN POWEL , JERRY RAWLINGS, au hata TIGERS WOODS ni weusi kama dunia ya sasa iwapavyo lebo?
  • Hivi kwani hustukii kuwa historia ya dunia ingetafsiriwa kivingine, ingekuwa kawaida kwa weusi kuwaita akina Malcom X, Spike Lee, Barrack Obama hata mpaka BOB MARLEY wazungu?
  • Unafikiri weye kama mjukuu wa Nyerere ni vigumu kupata UBUNGE?

Sikatai!

Katika mambo ambayo mpaka mwisho wa dunia yatakuwa bado yanafanyiwa kazi, ni hili la usawa.Lakini tafsiri zake zitakuwa zinageuka kufuata jicho la jamii litafsirivyo ni nani anapata ulaji kuliko mwenzake, kitu ambacho kitafanya kuwe na NGO za wanaume kugombea haki zao kutokana na wanawake kuzidi kuwabinya kunako.

DUH!
Naacha Basi!

Lakini sikubali kinamna ,Lord Kitchener asemavyo;




Wala sikubaliani na mtazamo wa PETER TOSH kuhusu kila mweusi hata awe Muaborijini, lazima ajitambue kuwa yeye ni Muafrika, katika:

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Anonymous 10:29 am  

MZEE SIMON KATIBU.UMESEMA HAUKUBALIANI NA NABII TOSH?KUMBUKA NA WAYAHUDI PIA WALIMKANA MFALEM WAO YESU KRISTO,NAMI SISHANGAI WEWE MWAFRIKA KUTO KUKUBALIANA NA NABII TOSH.KAMA WEWE SI MIMI NA MIMI HUWEZI KUELEWA NABII ANASEMA NINI.

AMANI.

RASTA HAPA.

Simon Kitururu 1:14 pm  

@Rasta: Ukisoma vizuri nilicho andika, utagundua nini nimesema sikubaliani naye. Kumbuka vile vile mimi sio Rasta. Ninamuheshimu Peter Tosh, lakini yeye si nabii wangu. Na naamini naruhusiwa kukataa chochote kutoka kwa yoyote kama sikubaliani nacho.Kama Bob Marley na hata Bunny Wailer ambao walikuwa marasta kama wewe na walifanikiwa pia kutokubaliana na Peter Tosh katika baadhi ya mambo, nahisi utastukia kuwa hata wewe kunaeneo ambalo laweza kukukumbusha ubinadamu wake.

I and I'ism nilipitia miaka ya nyuma .Kwa hiyo nakuelewa kwanini unafikiria ufikiriavyo.
Amani!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP