Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

WANAWAKE huoga TOFAUTI kwa sababu wana MAtiti. AU?

>> Thursday, April 17, 2008

Wanawake na wanaume ndio binadamu awaonao kila siku ya MUNGU ibadilikayo.
Binadamu anaweza akajisahau kuwa kuna maeneo yamuathiriyo binadamu mwenye uume na mwenye uke ambayo hayajabadilika sana kimawazo hata ki.....ndani ya asilimia kubwa ya idadi ya binadamu waishio katika duniani hii ibadilikayo.


NI RAHISI kusahau kuwa , bado katika dunia hii , haki za wanawake na watoto hazina kipaumbele sana machoni mwa wanaume na hata wanawake pia. Watoto sitawazungumzia sana hapa sana leo hii, ingawa naamini kuna wanawake ambao wamefikia kuamini kuwa wanaume wafikiriavyo na watakavyo, ndivyo watakiwavyo kufanya, kufanyiwa au hata kuonekana.

Wanaume wametawala maeneo mengi hapa duniani mpaka unaweza kusahau kwa nini bado ni watoto wakiume wanaopendelewa kielimu na kikuwezeshwa kujitegemea kuliko watoto wadada.

Watu husahau kuwa katika dunia hii, asilimia kubwa ya watu wako katika nchi masikini na asilimia kubwa ya watu bado wanaamini mafanikio katika watoto wa kiume na si katika watoto wa kike.

DONDOO:(Pamoja na wachina kusifiwa wana akili sana, NAFIKIRI unakumbuka wamefanikiwa kupendelea watoto wa kiume, na kuwa na watoto wa kiume mpaka wanaanza kuishiwa wanawake wa kuoa au kumimbisha hivi sasa.)

Sasaa......

Dunia inabadilika kila siku, na binadamu inabidi abadilike kukabiliana na mabadiliko kama anataka kuhakikisha kizazi chake kuendelea kuwepo hapa duniani.

Ushirikiano wa mwanakaka na mwanadada katika kufanikisha mridhiko wa maisha haya mafupi binadamu aishiyo, unahitajika sana, hasa kama nia ni kujaribu kuishi haya maisha kwa mafanikio na furaha.

Mafanikio ya binadamu hapa duniani , hutafsiriwa na mtu mwenyewe kutokana na jinsi alivyo athiriwa kimawazo na mambo mengi yamzungukayo tokea azaliwe , kuanzia aonje chuchu, apate au akose elimu , mpaka mara yake ya mwisho kupumua.
SAMAHANI KIDOGO........!

Swali:

  • Hivi maisha ya mafanikio ni lazima yawe ya furaha?
  • Hivi kujua kutokanako na elimu hakusababishi kumkosesha tu raha binadamu ambaye asingejua , asingetaka?
  • Unataka kujua una UKIMWI?
  • Hivi unataka mto wa kike au wakiume ukimimbisha au ukimimbishwa leo usiku?
DUH!

Cha ajabu ni KWAMBA, mafanikio ya binadamu JAMIII iyazungumziayo, ni mafanikio YATAFSIRIWAYO na jamiii kuwa NI MAFANIKIO .

JAMII itasifia na hata vitabu kuandika kuhusu yale JAMII itambuayo kuwa ni MAFANIKIO hata kama HAYO mafanikio huweza kuwa si MAFANIKIO kwa muhusika binafsi..

Swali:
  • Unafikiri maisha ya Rais NELSON MANDELA, ya kuachika mara mbili na watoto kukua bila baba, kwa mtazamo wa jamii ni mafanikio?
  • Unafikiri maisha ya MANDELA ya kutaka haki kwa kila mtu bila kuipendelea familia yake binafsi, JAMII kwa ujumla inatambua kuwa ni MAFANIKIO?

DUH!

WAKATI UNAMCHUNGULIA BINADAMU AKIOGA, kuna maeneo unayatolea macho kutokana kuvutiwa kwako wewe binafsi au kwa sababu yalikaa tu karibu na tundu la mchungulio.

Nakiri kuwa lazima utagundua zile tofauti uzionazo mbele yako na labda wakati huo huo , hautakuwa unafikiria au kujali binadamu umchunguliaye anawaza nini tofauti na wewe zaidi ya kugundua nini alicho nacho kilicho tofauti na wewe.

Kwa wanawake na wavulana , karibu kila mtu anakakitu kake ukitokea tu ,kanamsitua kuwa huyu jamaa mvuto wake divisheni ziro: lakini kwanini wengine wanampasisha mtihani?

Kwa wanaume pale kijiweni, kuna atakaye kuambia kuwa yeye ni mtu wa matako, macho , miguu , nywele au hata yule ambaye atasifiwa kwa busara zake na jamii, kwa sababu anasema anapenda tabia ya yule ampendaye kuliko yale macho ya gololi na mashavu ya kumimina.


Nahisi kwa wanawake pia unaweza kusikia kuwa anampenda jamaa kwa sababu anabomba la matege, ana macho kama bundi au hata kwa sababu ana kifua kama simba: si umecheki siksi paki zile?

Swali:
  • Unafanya nini kusaidia kuleta usawa wa haki za wanawake na wanaume?
  • Umejichubua kwa sababu unafikiri wanaume wanapenda au unakubali kuchunwa buzi kwa sababu wanawake kazi yao ni kupendeza na kukupikia chakula kabla ya kukupa kifuko cha dhambarau ukitoka kazini / kabla ya kulala?

DUH!

  • Naelewa mafanikio yako yanaweza yakawa ni kujinyima hapa duniani kwa sababu unafikiri utafaidi mbinguni ukishafariki.

  • Naheshimu kuwa wewe mwanamke ndio kungwi na mama ambaye unampeleka binti yako kutairiwa kinjegere, ili jamii ikukubali na wewe mwenyewe ufikie kukubali kuwa UMEFANIKIWA, kwa sababu umefikia katika uzani wa MAFANIKIO katika jicho la JAMII na umefikia JAMII itakavyo.

  • Nakubaliana na wewe pia kuwa umejichubua iliupendeze na unapendeza katika jicho lako na jicho la yule.

  • Nakubali kuwa , ukiniona sichani nywele , unafikiria kuwa nywele zangu chafu lakini ukisuka twende kilioni na kukaanazo wiki kadhaa bila kuziosha, wewe bado msafi.
NDIO!

Nakubali kuna wanawake na wanaume , wasenge na wasagwaji pia!
Nakubali hakuna binadamu wawili sawa!

Lakini.....

HUFIKIRII kuwa mimi , wewe, yule na yeye ambao tukotofauti , tunaweza tukawa katika ahueni zaidi kama WANAWAKE watapata nafasi sawa na wanaume katika dunia hii ya leo ya sayansi na tekinolojia ambayo haihitaji sana misuli kama enzi za ujima?

Hufikirii kuwa , ni mimi na wewe ambao tunachangia kutokuwepo kwa usawa wa binadamu wote kutendewa ubinadamu sawasawa bila kujali ni wanawake au wanaume?


Inawezekana unavyowaza ni sawasawa tu!
Si kuna MALIPO MBINGUNI?

Inawezekana unavyowaza ni sawasawa tu!
Si mwanamume ni kichwa cha familia halafu ana misuli uenye nguvu zaidi ya mwenye uke?

Inawezekana unavyofikiria ni sawa!
Kwani ni nani anataka au kuhitaji dume jike katika shughuli?

AU?

USITISHIKE!
Nawaza tu kibulicheka!

Hebu tuangalie jinsi wanawake na wanaume waogavyotofauti , kama maji yakitoka pale DAR-es-SALAAM, MOROGORO au pale SAME, MBAGA , Manka, KILIMANJARO kwa bibi, kama kuna bafu fulani.....


DUH!
Ngojea tu ni waachie Elana na KC wa Read My Hips dance troupe ,wazungumze kwa kutumia mwili....


BAADAYE BASI!

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP