NAJARIBU KUSAHAU kuwa NA MINYOO!
>> Friday, April 04, 2008
Ni kweli ulichosikia.
    Wanikumbusha kwa nini?
Najaribu kutoangalia.
    Unanionyesha kwa nini?
Ndio, inanuka na kunukia....
Mguso pia naustukia....
Huzuni, furaha na mashaka pia...
Najaribu kusau
 ....ladha chachu  na chungu pia
Sitaki kusahau
......ladha tamu, kuumizwa sina nia
Najaribu kusahau!
 Unanikumbusha kwanini?
--------------   -----------------
DUH!
Elewa uelewavyo hapo juu!
Nitapotea kidogo kwa siku kadhaa hapa kijiweni.
Hizi siku kadhaa ambazo hamtanisikia, nahisi wengine mtaenda kusali na kuswali.
Ngoja nikuache Ahmet Ozhan  akija na miondoko ya Wasufi katika wimbo wa swala
DUH!
Ngoja nikuache tu  pale Congo kanisani pia upate huu wimbo wadini uitwao KUMAMA YAHWE
 
  
 Posts
Posts
 
 




0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Post a Comment