USHAWAHI kumtazama KWA MAKINI binadamu akikimbiza MWENGE?
>> Sunday, April 13, 2008
Binadamu hupenda kuoanisha kitu na jambo.
Ndio maana binadamu anajioanisha mpaka yeye na jina lake.
Labda ndio maana anaitika ukimuita lile jina!
DUH!
Kuna vitu kibao binadamu anavioanisha na kakitu fulani.
Ukimchorea mistari miwili kinamna, atakuambia, huo ni msalaba, halafu atadai unamkumbusha Ukristo au hata YESU.
Ukimchorea kinusu mduara na mbwembwe fulani , atakuambia umemkumbusha MWEZI au hata UISLAMU.
Ukamuonyesha sanamu fulani, anaweza akakuambia huyo ni Rais Nyerere , yule rais bomba sana au hata akakuambia huyo ni BIKIRA Maria, ingawa anajua kuwa, hakuna aliyewahi kumchora au hata kumpiga picha Bikira Maria au yule mwanaye ajulikanaye kwa jina maarufu kama YESU, wakati wako hai .
Sasaaa.....!
Hivi vitu viwakilishavyo majambo muhimu kwa binadamu, labda ni vizuri sisi binadamu kuwa navyo na kuvishabikia.
Labda vinaleta mwamko wa maendeleo, vinatusababisha tujisikie tuko karibu na Mwenyezi Mungu, tuko karibu kama binadamu na binadamu au hata kujitambua kuwa sisi kabila letu ni Wagogo.
Sasaaaa........!
Narudia swali:
- Ushawahi kumtazama KWA MAKINI binadamu akimbizaye MWENGE?
- Unafikiri binadamu wakati anakimbiza mwenge, akilini mwake anafikiria nini?
- Ushajistukia unaweza ukapigwa butwaa ukiona Mdau anakojolea kaburi?
Naweza kumshangaa Muiraki alivyokuwa anapiga sanamu la Saddam Husein kama vile linasikia maumivu , wakati mimi mwenyewe nakubali, naweza kukasirika nikisikia jamaa wanakojolea sanamu ya Rais wetu mtukufu JAKAYA KIKWETE.
Sasaa.....
MWENGE wa OLIMPIKI , au hata ule MWENGE mwingine , twendeni tu tukaukimbize!
Lakini......, wakati naukimbiza MWENGE, naruhusiwa kuwaza ;` sijui watatulipa kweli baada ya mbio hizi?´ au `Nasikia baadaye kuna bomba la ubwabwa kwa wakimbizao mwenge´, na si lazima niwaze kuwa ni kweli tunahitaji umoja katika DUNIA hii.
Lakini....., wakati tunaukimbiza ule mwenge, tujiulize:
- Tofauti ya mwenge na kibatari pale nyumbani kwa bibi ,ni nini?
- Ushawahi kutupa,kuchoma au hata kuchambia gazeti lenye picha ya Mheshimiwa ,Mtukufu au Hata PAPA Mtakatifu?
JUMAPILI NJEMA!
Tulia na PM DAWN
0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Post a Comment